nahavache
JF-Expert Member
- Apr 3, 2009
- 871
- 247
kwa nchi ndogo kama tz kuwa na serikali 3 ni kunyonya nguvu za wanyonge na kuwanufaisha wachache,coz serikali zote hz zitahitaji mawazir ambao watakuwa wanalipwa pesa nying bila kufanya kaz na pia umaana wa muungano pia utakuwa umetoweka kabsaa!!!!
Kwa mahesabu yasiyochambuliwa kwa makini, mtu anaweza akadhani kuwa serekali tatu zitaongeza mzigo kwa mwananchi wa kawaida kwa sababu tulikuwa na mbili lakini sasa tunaenda tatu. Ila ukiwa mwangalifu utakuta kuwa serekali tatu zitakuwa zimepunguza sana gharama zinazomuangukia mwananchi. Serekali ya sasa tuliyo nayo ni mzigo. Tuchukulie tu suala la bunge, kwa sasa kuna wabunge zaidi ya 50 kutoka Zanzibar ambao kimsingi sioni kazi yao kwenye bunge la jamhuri ya muungano kwa sababu 90% ya mijadala ya bunge la jamhuri ya muungano inahusu masuala ya Tanganyika. Kwenye serekali tatu, tutakuwa na wabunge 20 tu kutoka Zanzibar kwenye bunge la muungano ambao watajadili mambo machache kwa muda mfupi kwa sababu mambo ya muungano ni machache kama bunge la Africa Mashariki vile. Kama serikali tatu zinaonekana ni mzigo, mbona basi hata hizo mbili zilikuwa mzigo, ingefaa iwe moja kabisa.
Uchumi huwa unakuwa kisaikolojia zaidi. Kwa mfano, mtu akiwa na uhakika kuwa atapata hela, anafanya expenditure. Na hivyo hivyo, serekali tatu zitaondoa dukuduku la wengi kwa sababu wengi na hivyo kufanyakazi kwa bidii wakijua wanafanya kwa ajili ya serekali yao. Kule Zanzibar wanadhani mapato yao yanaenda bara, lakini serekali tatu zitawafanya wajue kuwa mapato yao hayaendi kokote. Ni mapato kidogo tu watakayochangia kwenye muungano.
In fact kama ni wizara, zitakuwa zile zile au zipungue. Ni vile tu wizara za mambo ya nje, ulinzi zitakuwa kwenye serekali ya muungano na serekali ya Tanganyika itakuwa na wizara zake nyingine kama za elimu, fedha nk
Tutazoea tu, LET ZANZIBAR GO