Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

kwa nchi ndogo kama tz kuwa na serikali 3 ni kunyonya nguvu za wanyonge na kuwanufaisha wachache,coz serikali zote hz zitahitaji mawazir ambao watakuwa wanalipwa pesa nying bila kufanya kaz na pia umaana wa muungano pia utakuwa umetoweka kabsaa!!!!

Kwa mahesabu yasiyochambuliwa kwa makini, mtu anaweza akadhani kuwa serekali tatu zitaongeza mzigo kwa mwananchi wa kawaida kwa sababu tulikuwa na mbili lakini sasa tunaenda tatu. Ila ukiwa mwangalifu utakuta kuwa serekali tatu zitakuwa zimepunguza sana gharama zinazomuangukia mwananchi. Serekali ya sasa tuliyo nayo ni mzigo. Tuchukulie tu suala la bunge, kwa sasa kuna wabunge zaidi ya 50 kutoka Zanzibar ambao kimsingi sioni kazi yao kwenye bunge la jamhuri ya muungano kwa sababu 90% ya mijadala ya bunge la jamhuri ya muungano inahusu masuala ya Tanganyika. Kwenye serekali tatu, tutakuwa na wabunge 20 tu kutoka Zanzibar kwenye bunge la muungano ambao watajadili mambo machache kwa muda mfupi kwa sababu mambo ya muungano ni machache kama bunge la Africa Mashariki vile. Kama serikali tatu zinaonekana ni mzigo, mbona basi hata hizo mbili zilikuwa mzigo, ingefaa iwe moja kabisa.
Uchumi huwa unakuwa kisaikolojia zaidi. Kwa mfano, mtu akiwa na uhakika kuwa atapata hela, anafanya expenditure. Na hivyo hivyo, serekali tatu zitaondoa dukuduku la wengi kwa sababu wengi na hivyo kufanyakazi kwa bidii wakijua wanafanya kwa ajili ya serekali yao. Kule Zanzibar wanadhani mapato yao yanaenda bara, lakini serekali tatu zitawafanya wajue kuwa mapato yao hayaendi kokote. Ni mapato kidogo tu watakayochangia kwenye muungano.
In fact kama ni wizara, zitakuwa zile zile au zipungue. Ni vile tu wizara za mambo ya nje, ulinzi zitakuwa kwenye serekali ya muungano na serekali ya Tanganyika itakuwa na wizara zake nyingine kama za elimu, fedha nk
Tutazoea tu, LET ZANZIBAR GO
 
Watu wote MIOYONI mwetu TUNATAMANI kuona Tanganyika kivyake na Zanzibar Kivyake. Shida ni huyo wa kusema na IWE hivyo.

Viongozi wangependa kuona kero za muungano Zimefika MWISHO. Wananchi tuko wazi kabisa kuwa kero hazitokani na kero bali kero hizi zinatokana na MUUNGANO wenyewe. Tusingeungana tungekuwa huru sana kuliko huu UTUMWA wa sasa.

Siungi mkono nchi moja maana hapo zitazaliwa kero mpya kabisa. Kwamba Zenj yenye Rais wake sasa iwe mkoa na Shain awe RC ni kichekesho! Huko tusiende.

Suruhu yetu ni moja tu kuwa tuwe kama ilivyokuwa March 1964. Tanganyika huru na Zanzibar huru kila mtu amtakie heri mwenzake.
Ni kwa nini hawataki uvunjike?
Hii inasababisha wapemba watupigie kelele kila kukicha
 
Tume ya Warioba walipaswa kutuachia maamuzi wananchi kwani tulitaka katiba ambayo itawapa madaraka wananchi lakini wametuletea rasimu ya katiba ambayo inawazungumzia wanasiasa na kuwapa madaraka zaidi swala la muungano wangekuja na mapendekezo matatu muungano wa serikali tatu,mbili au moja na wananchi wakaamua wachague ipi wanataka.siyo kutuletea upuuzi wao kwa sababu bado wanataka waendelee kutawala hivi wanajua ni gharama kiasi gani zinahitajika kuendesha serikali tatu au kwa sabaubu wanaishi kwa kodi zetu,wameacha maswala muhimi kama ya ardhi,uraia wa nchi mbili,kinga ya rais tukatae serikali tatu ama moja au tuvunje muungano
 
Serikali Moja ama hakuna Muungano.
NOoo to serikali tatu.

MAMBO MANNE serikali moja; serikali mbili; serikali tatu na kuvunja muungano Hakuma lililo rahisi kimjadala. nafuu ni serikali mbili au tatu kwa maana ya kukubaliana lakini uhaalisia ni serikali moja. jambo la kushangaza ni kwanini hatuwezi kukubaliana hili la serikali moja. watanganyika wakilazimisha serlikai moja ni mgogoro na wazanzibari. uwezekano ni kuachana na muungano na kuanza upya
 
Isaac JK

Kama ulifuatilia utoaji wa maoni kuhusu Katiba mpya hawa watu walisema "waachiwe wapumue".

Kwa sababu hadidu rejea alizopewa Warioba na Tume anayoingoza ni kuwa "Muungano ujadiliwe kwa nia ya kuuboresha tu" na sio uwepo wake au kutokuwepo kwake. Wazanzibari waliuona mtego wa JK na walibuni kitu walichokiita "Muungano wa Mkataba".
Walipendekeza mamlaka kamili kwa Zanzibar , mamlaka kamili kwa Tanganyika na Muungano wa mkataba.

Tume ya Warioba wamekuja na rasimu ambayo haizingatii maoni hayo na walitoa angalizo kuwa Tume itakuja na mapendekezo ya Rasimu ya Katiba mpya inayoangalia masilahi ya taifa na sio inayotokana na maoni ya wananchi.

Katika upokeaji wa maoni kutoka kwa wananchi, Tume ya Warioba ilipata wakati mgumu ilipofanya kazi zake kule Zanzibar na Wajumbe wa Tume walionekana kukerwa na maoni yaliyodai Zanzibar huru,Zanzibar yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa,kufufuliwa kwa Tanganyika na muungano wa mkataba.

Kama Tume ingeyafanyia kazi maoni yaliyotolewa na wazanzibari (kitakwimu inasemwa ni asilimia 66) basi Tume ya Warioba ingekuja na mapendekezo ya kuifufua katiba ya Tanganyika na serikali ya Tanganyika na bila ya kupoteza muda, mchakato wa kuandika katiba mpya ya Tanganyika ungeanzishwa.

Tunawalazimisha wazanzibari wawe ndani ya muungano lakini hawautaki muungano, hawataki serikali tatu,mbili au moja. Wameshasema sana wanataka nchi yao na uhuru kamili wa kujiamulia mambo yao.

Tunalazimisha serikali tatu lakini kama ni muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar tu, hautadumu. Kama nchi za Malawi, Zambia, Burundi, Rwanda zitaruhusiwa kujiunga, huenda Zanzibar watajifunza kitu na kutamani kubakia katika muungano.

Wakati watu wanajadili "usanii" wa Tume ya Katiba mpya, CCM wanacheka sana, wanachekelea sana. Muda wa kuandika Katiba ya Tanganyika na kuiunda na kuisimika serikali ya Tanganyika utafanya uchaguzi mkuu usogezwe mbele au itatumika katiba ya 1977.

Kwa kweli kinachoendela ni kituko/maigizo tu. Kama Tume imetoa pendekezo la kuanzisha serikali tatu. Hatua ya kwanza ilikuwa ni kuandika katiba ya Tanganyika na kuunda serikali ya Tanganyika. Baadae serikali ya Tanganyika ikae mezani na serikali ya Zanzibar kujadili Muungano kama vile wabia hawa wa muungano walivyofanya 1964.

Tunatengeneza utata na maumivu tu ya muungano badala ya kuamua kulishughulikia tatizo la muungano na mfumo/muundo wake lililopo mbele yetu kwa ujasiri na kwa kujiamini. Tunateketeza fedha za kodi za walalahoi na pia tunatengeneza matatizo mingine mapya na mazito zaidi.

Tanzania ni nchi ya mazingaombwe!

i lyk this
 
Mie nakubaliana nawe lakini ili kupunguza manung'uniko hasa ya Wazanzibar ndiyo maana Tume imekuja na mapendekezo hayo. Nashauri serikali za Tanganyika na ile ya Zanzibar iongozwe na Magavana ili Rais abaki mmoja tu yaani Rais wa Muungano. Iwapo Wazanzibar hawatakubali hilo basi wakubali kuchangia nusu ya gharama za kuendesha serikali ya shirikisho kwa muundo wa serikali tatu. Napenda kutoa taadhali kwa serikali kuhusu suala la muungano wahakikishe kwa gharama yoyote unaendelea kuwepo. Tujifunze namna nchi Tajiri zinavyohaha kuleta muungano wa mataifa yao sasa kwanini sisi watanzania turudi nyuma hatua moja badala ya kusonga mbele kwenye muungano wa serikali moja. Tanzania ni nchi moja na hivyo tuwe na serikali moja tu pamoja na serikali za jimbo la Tanganyika na Zanzibar.
 
Hivi, waliopendekeza serikli tatu ni nani? Si wananchi? Ina maana wakati wananchi wengine wanatoa maoni yao wengine walikuwa viti virefu?

Halafu hili suala la kusema kuwa serikali itakuwa ndogo gunajidanganya. Ukiacha mawaziri 15, bado bara wstakuwa na mawaziri wao na serikali yao. Hayo ya warioba ni ya muungano zaidi. Tutaendelea kuwa na wabunge 350 pamoja na wale 75 wa muungano. Kazi ipo
 
watanganyika wakilazimisha serlikai moja ni mgogoro na wazanzibari. uwezekano ni kuachana na muungano na kuanza upya
Let them go!
kwani tunawataka?
Wao wazenji ndo wanatung'ang'ania.
Kila siku wanadai wawe nchi huru ukiwapa option waondoke hawataki.
Eti wanataka Tanganyika ikae mezani na wao! Tanganyika iko wapi inayowataka.
 
kwel tz nch ya kamasi ukipewa mkate unatatja jiwe, ukiomba samaki unapewa nyoka!
 
Muungano ni kuungana inakuje mnaungana na kua na maamuz binafsi kila 1 na yake,kwa mfn umeoa thn kila mtu analala kwake anapikia vyombo vyake anakula peke yka anatembea pek yake hyo cio NDOA, Angalien kwa umakin hiyo jaman hapa hakuna kuna kitu kigen kitakuja........................!!!!!(.................)
 
kwa maana kila serikali na raisi wake,makamu wa raisi,waziri mkuu,.........
 
Toka lini BOGA na punje la mchele vikaungana?,hapo ni lazima punje ya mchele itamnyonya BOGA(kama tunavyonyonywa sasa),hivyo basi ni punje ya mchele iingizwe kwenye BOGA tu,na jina linaweza badilishwa kidogo...BOGAM=TANZANIA...Nchi mmoja,serikali mmoja,rais mmoja,bunge moja na mfumo mmoja wa mahakama..THATS ALL!
 
Jaji Warioba kaniangusha kweli kweli! Eti Muungaano wa serikali tatu? Kusema kweli huo haufai kuitwa muungano labda tuutafutie jina lingine muafaka...three presidents, three Governments, three Parliaments, three, three...? Eti katika kuimarisha Muungano? From two to three? What a joke! Are we serious? Maybe only in Tanzania! If having two Presidents and two governments has not proved workable, this new idea is sheer madness...it is just like jumping from the frying pen into the fire! Somebody somewhere somehow has his maths upside down!

Imagine this...Rais wa Tanganyika anakula kiapo kuilinda na kuitetea katiba ya nchi ya Tanganyika (Tanzania bara!), Raisi wa Zanzibar anakula kiapo kuilinda na kuitetea katiba ya nchi ya Zanzibar...je, Raisi wa Muungano anakula kiapo kuilinda na kuitetea katiba ya nchi gani? Je, huo unaoitwa Muungano ni wa serikali au wa wananchi wa nchi hizi mbili. Je, kwa kuwa ni wananchi ndio wanaoichagua serikali yao, serikali isipowatimizia matakwa yao, Raisi yupi awajibike, serikali ipi iwajibike na wawakilishi gani wawajibike?

Nawaomba Watanzania wenzangu, tuache ushabiki wa kitoto katika jambo zito kama katiba ya nchi. Kama Muungano wa serikali mbili umeshindikana na sababu zipo za wazi kabisa na kama Muungano wa serikali moja nao unashindikana kwa sababu yoyote ile, dawa ni moja tu, Muungano uvunjwe na kila mmoja ajiendee zake...Mafahali wawili hawakai zizi moja! Matatizo yote yanayoukabili Muungano kama ulivyo sasa yanasababishwa na ubinafsi ambao kwa udhaifu wetu tumeulea na sasa umeota mapembe.

Naanza kuwa na wasiwasi na watu wanaoutetea mfumo wa serikali tatu kuwa ni ubinafsi ule ule uliotufikisha hapa ndio unaosukuma ajenda yao...kuficha uovu wao na udhaifu wao chini ya mwamvuli wa Muungano. Kamwe hawa watu hawasukumwi na maslahi ya taifa na watu wake bali wanajua fika kuwa Serikali moja itawaumbua na kuwaacha uchi wasipate pa kuficha hila zao za kuendelea kuvuna wasichopanda huku wananchi wakibaki kwenye sintofahamu ya kuamua lawama atupiwe nani. Serikali tatu ni ajenda isiyo na nia njema, tusiikubali kamwe!

Hapana kwa serikali tu, ni serikali moja au Muungano kwishnei, period.
 
Nakubaliana nawe na ndo msimamo wangu one government .Hizo nyingine ni tamaa tu.
 
Kutolewa kwa rasimu ya katiba mpya ambayo imetoa mwelekeo wa kuwa na serikali tatu na hivyo kutoa mwanya wa kuundwa kwa Taifa la Tanganyika, huenda kukawa ndio mwanzo wa wanzanzibar kuonja machungu ya kuishi kwa kujitegemea kiuchumi.

Ni muungano wa serikali mbili uliokuwa unawasitiri wazanzibar wengi kiuchumi kuliko raia wa Tanganyika.

Wazanzibar karibu wote walikuwa wanahudumiwa kiuchumi na serikali ya Tanzania ambayo inakusanya kodi kubwa kutoka kwenye biashara ya pombe, Sigara, Kitimoto, madini, Pamba, nk kutoka upande wa Tanganyika.

Sasa tunapoelekea wazanzibar itabidi waishi kwa kutegemea serikali yao zaidi ambayo inapata mapato kutoka kwenye kilimo cha karafuu(ambacho kipo duni sana) na bandari(ambayo kwa sasa imefifia sana). Zipo ndoto za mafuta Zanzibar, hizi si za kutegemea sana kwa sababu rasilimali hii huwa inawindwa na mataifa tajiri duniani na kichocheo cha vita popote duniani.

Zanzibar imebebwa sana kiuchumi na Tanganyika, sasa ni wakati wake kujibeba, mtoto akililia wembe mpe!!!
 
Toka lini BOGA na punje la mchele vikaungana?,hapo ni lazima punje ya mchele itamnyonya BOGA(kama tunavyonyonywa sasa),hivyo basi ni punje ya mchele iingizwe kwenye BOGA tu,na jina linaweza badilishwa kidogo...BOGAM=TANZANIA...Nchi mmoja,serikali mmoja,rais mmoja,bunge moja na mfumo mmoja wa mahakama..THATS ALL!

si wananch ndio wametaka au ni warioba ndio anataka!
 
Back
Top Bottom