Kinadharia serikali moja ndiyo njia ya maana ya kujenga muungano imara. Lakini kiuhalisia ni jambo lisilowezekana. Kwa hiyo kudai serikali moja ni kutaka kuvunja muungano tu sawa na wale wanaotaka muungano wa mkataba.
Tumedai serikali tatu kwa miongo mitatu sasa na tunashukuru tume imeliona hili. Njia ya kupunguza gharama ni kumfanya Rais wa Muungano awe mkuu wa nchi bila kuwa mkuu wa serikali na achaguliwe na Bunge badala ya kuchaguliwa kwenye kura ya jumla. Hivi walivyopendekeza itakuwa ni maajabu kwa sababu kutakuwa na serikali tatu lakini zitakazokuwa na nguvu ya maana kiutendaji ni mbili tu za bara na visiwani. Mwisho wa yote Rais wa Muungano ambaye kimsingi hana nchi atapwaya vibaya sana, na wale wawili wanaweza kumzira na kuachana naye na hao mawaziri wake 15!
Kwa mfumo waliopendekeza walipaswa kuruhusu utawala wa majimbo kwa bara wakati Zanzibar wangeendelea na serikali yao. Sioni namna ambavyo Rais wa Muungano atafanya kazi huku kukiwa na Rais kamili wa Tanganyika.
Sisi tuliopata nafasi ya kuingia kwenye mabaraza ya katiba itabidi jambo hili tulidadavue vyema.
Sijui kwa nini bado tuna "flip flop" na suala la Muungano. Wote tunajua kuwa huu Muungano ni kikwazo kikubwa sana katika ku-design a good, an effective and a responsible governing system.
Kama siyo huu muungano wala tusingekuwa na system, au kujaribu hata kupendekeza system, ya utawala isiyoeleweka, even kufikia extent ya kupendekeza kuwa na ceremonial president.
Watanzania wapewe haki ya kujiamualia through a referendum. Waulizwe kama bado wanapenda kuendelea kuwepo kwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Kama hawapendi, basi na Muungano uvunjwe, kila mtu achukue times zake. Kama bado wanapenda Muungano uwepo, basi waulizwe wanapendelea Muungano wa aina gani.
Personally, kuendelea kupendekeza kuwepo Muungano wa serikali tatu, tena with a ceremonial president, ni kukwepa ku-address the core problems za Muungano wa sasa na kuendelea kuendeleza kiini macho cha Muungano.
Najaribu kufikiria idea ya kuwa na ceremonial president kwenye nchi ambayo viongozi wake waliochaguliwa kuwa accountable kwa wananchi, lakini wanafanya kazi zao in a ceremonial way. Sasa itakuwaje kama wakipewa full title ya kuwa ceremonial leaders?
Kwa nchi kama Tanzania, we need a responsible and accountable President, not a ceremonial president. Hatutaki kuwa na Rais ambaye kazi yake itakuwa ni kutembea na mikasi mfukoni kwa ajili kukata utepe kama anavyofanya Makamu wa Rais.
Kama vipi na tusiwe na rais wa aina hiyo kabisa. We aren't that rich to pay for someone simply for doing nothing.