Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

Tulikosea tangu mwanzo wakati ToR zinatolewa. Tume ya Warioba kimsingi ilikuwa inafungwa na yafuatayo:​
 
mimi nadhani mtoa mada bila kumung'unya maneno ungesea tu kwa kifupi "TUVUNJE MUUNGANO HUU KILA MMOJA AWE KIVYAKE TUTAKUTANA kwenye shirikisho la EAC " .hiyo tu ingetosha usisumbuke kutokwa mapovu kuandika riwaya.
 
mimi nadhani mtoa mada bila kumung'unya maneno ungesea tu kwa kifupi "TUVUNJE MUUNGANO HUU KILA MMOJA AWE KIVYAKE TUTAKUTANA kwenye shirikisho la EAC " .hiyo tu ingetosha usisumbuke kutokwa mapovu kuandika riwaya.
Uenda haujanielewa vizuri ndg yangu


“Muungano ni tunu na tukijaribu kuuvunja
dunia nzima itatushangaa, mimi sitajali
zikiwa serikali tatu, moja au mbili lakini
ninachotaka ni kwamba muungano
uendelee kuwepo, athari za kuvunja
Muungano ni kubwa sana tusithubutu hata
kujaribu kuuvunja,”


“Muungano ni tunu kama vile amani,
mshikamano wa kitaifa, undugu, kama
kuujadili tujadili muundo wake uweje ila si
vyema tukaanza kufikiria kuuvunja, wenzetu
huko nje watatuona watu wa ajabu”

“Mwananchi anayetaka serikali moja
aachwe aseme sababu zake, anayetaka
serikali mbili na wanaotaka serikali tatu
waachwe wazungumze sababu za kutaka
hivyo ila mwisho wa siku Muungano huu
lazima tuhakikishe upo na uzidi kuimarika,”


Mgawanyo wa madaraka ni kitu
kingine muhimu na uwepo utaratibu wa
kuhakiki kama mfumo uliopo unafanya kazi
au la (check and balance)lengo likiwa ni
kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa na
wananchi wanapata huduma kwa wakati.
 
sasa huo muungano wa mkataba ukatolea mfano EAC huo ni muungano au mashirikiano?hapo muungano utakuwa haujavunjika na yamebaki mashirikiano?
 
Katika swala la bunge umekosea, wabunge hawatokuwa 400, watakua 75. Majimbo yatapunguzwa!

Nashukuru kwa taarifa mkuu but vp kwa mtazamo wako we unadhani ni sawa kuweka huu utaratibu wa wabunge wawili ni sawa?
 
Wapeni Mamlaka yao utajuwa wanafaida gani Wazanzibari, Mbona hamjaweka kipengele cha anaetaka kuvunja muungano ruhuksa.
 
Yakitokea ya Kenya au Zimbabwe ya kuunda serikali ya mseto ( vyama viwili kuunda serikali)!! hii ni balaa lingine!!

Kama vile Warioba alivyoshindwa kuwa na maamuzi kwenye tume ya Rushwa amekuja na balaa lingine!!
 
I agree with you Mzee Mwanakijiji mzigo wa kuendesha hizi unatushinda elimu duni afya duni huduma duni yote hii ni uhaba wa fedha sasa serikali tati tena jamani hii tuseme hapana tuungane na ccm kuukataa
Hatushindwi vitu kwa sababu ya ukosefu wa fedha. Tunashindwa kwa sababu ya kuongozwa na punda. Muhimu kwa punda ni kula, kunywa na ikiwezekana kutobebeshwa mizigo, basi. Mengine hayamhusu. Na ndivyo viongozi wetu wa 'Chama Cha Zamani' walivyo.
 
Kitu cha kijinga zaidi ni uwepo wa mawaziri zaidi ya kumi wakishughulikia mambo saba. Mambo saba wizara 15? Haiwezekani.

Hapo sasa mkuu na hapo bado watataka kuweka na manaibu waziri, kiuhalisia balaza la mawaziri linabidi lisizidi mawaziri 10 pamoja na manaibu.
 
kama zanj wakiwa na serikali yao, na sisi Wadanganyika tukawa na serikali yetu hivi kuna muungano hapo? ni bora kuwe na one government yenye mawaziri wakuu wawili wa bara na wa zanj...huku chini kuwe na serikali za majimbo ambazo zitakuwa zinawajibika kwa serikali kuu..
 
Swali lango dogo. Baada ya kuzikataa options tatu za mwanzo kuna haja gani ya kuingia Muungano wa Mkataba ambao kusema ukweli hautakuwa muungano bali ni uhusiano wa kimataifa. Kwa nini kila upande usiende zake badala ya kuanzisha nchi ya kufikirika? Zanzibar haitahama hapo ilipo. Pamoja na kelele zote za kujitegemea bado watakuja Dar kutafuta chakula. Soko lao dogo mno. Mfanyabiashara wa Zanzibar anayetaka kupanuka kibiahsara atakuja Dar, n.k. Zanzibar kama ina kitu cha kuuza nje, hasa nchi za maziwa makuu, italazimika kupitisha Dar. Tatizo ni kwamba wazanzibari wanadhani Muungano ukivujika watafanya biashara na waarabu. Hizo ni ndoto. Mtawauzia nini? LET THE MIDGETS GO.
 
Wengi wanaeza wasikubaliane na mm kwa sasa. Ila mambo yakishaenda kombo watankumbuka. Badala ya kupoteza muda kwenye kutunga katiba tungeanza process za kuvunja muungano coz hata tukwepe vp ndko tuelekeako. Tofaut ni hapo baadae unaeza ucvunjke kwa aman.

Hebu fikiria
Kama tukikubaliana serikal 3,ya tanganyika itaundwa lini akat katba inaisha 2014 na haijaainisha juu ya serikal hyo?
Katiba ya tanganyika itatungwa lini?
Hv itakuaje vyama tofaut vikishka serkal?
Kwani kuna sababu gan ya kuungana ya msing ambayo itakosekana tukiungania ktk afrka mashark?
Vyanzo vya mapato vya serikal ya muungano vitakuaje?
Wabara hawawez kubal serikal 2, na waznz hawawez kubal serkal 1.
So either way (nw kwa aman/baadae kwa harakat na maandamano na fujo) muungano utavunjika tena kwa 7bu hakuna serikal 1,2 au 3 itakayokubaliwa.

Tufahamu hata hzo option zngne za majimbo au mkataba haziwezekani au sio salama kwa sasa, ukizingatia wananchi wa kila upande wanataka kuvutia kwao, xo kuweka kitu kama serikal za majimbo inaweza kuwa hatari, ukifahamu baadhi ya vyama vya siasa vina misimamo kinyume na muungano. Na mkataba ni hatari coz a slight mistake inaweza kuharibu kila jambo!

Badala ya kupoteza muda kutafuta katiba ya muungano, tungeandaa refferendum ili tuwe na uhakika wa idadi ya wananch kila upande wanaoutaka huo muungano na uweje, kama sio kila nch isimamiwe na serikal iliyopo kufanya michakato ya kujitenga na kupata viongoz wao, ila hakuna kulilia asset au resource iliyo kwa mwenzako. Na wakati huo baadhi ya shughul kama vitambulisho vya uraia zisimame etc. Ila mpaka kwa options zilizopo sasa na hali, tunapoteza muda.
 
Hawa wazanzibari hamjawaelewa hizo serikali tatu wamesema kwa sharti la muungano wa mkataba.serikali tatu hawataweza kulipia gharama za muungano,umeme na mishahara ya wafanyakazi inawahenyesha hadi fedha zitoke bara tuwaache waende zao kwa amani.kuna muungano uliojulikana sana hapa duniani kama wa urusi na bado ukavunjika sembuse huu wa kwetu usio na kichwa wala miguu??Waasisi walilazimisha tu huu muungano bila kuwauliza wananchi kama wanautaka au la,lazimisha ndoa halafu uone kama itadumu ni sawa na huu muungano,na hizi ndio athari zake ni suala la muda tu muungano utakuwa ni historia.
 

Mwanakijiji, Jaji Warioba na Tume yake wamekubali kucheza muziki wa wimbo wasioujua. Na ijulikane rasmi ya kwamba SERIKALI TATU NI NJIA RAHISI NA SAHIHI YA KUUVUNJA MUUNGANO.
 
Serikali moja sawa. Je wazanzibari wako tayari kwa hilo? Maana wazenji wana uelekeo mkubwa sana wa kutaka kujitawala nje ya muungano.
 
Kwa nini viongozi wa CCM wanang'ang'ania muungano?

wanaong'ang'ania muungano ni watanzania sio viongozi wa ccm.. tume ya katiba ina wajumbe wa vyama vyote akiwemo baregu wa chadema na ile iliyosomwa na warioba ni taarifa ya tume ya katiba mpya..acha uzuzu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…