Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

Sisi watanganyika tupo tayari hata serikali moja ila sasa upande wa pili ndo balaa lilipo, ndo maana kwa sasa tunataka serikali tatu ili mmoja akisusa muungano tunautupilia mbali, muungano ni kama koti tu, likikubana unalivua!
 
Hakuna cha balaa sisi hatutaki muungano na Tanganyika, katu wazanzibar hatukubali kumezwa
 

Unaonaje Serikali ya Tanzania ikafa kabisa na kuwepo Zanzibar peke yake? Kumbuka Tanzania ni nchi ya kusadikika lakini Zanzibar imekuwepo tangu na tangu. Kuwepo na Serikali moja tu SMZ na makao ya serikali yawe Zanzibar.
 
Sisi watanganyika tupo tayari hata serikali moja ila sasa upande wa pili ndo balaa lilipo, ndo maana kwa sasa tunataka serikali tatu ili mmoja akisusa muungano tunautupilia mbali, muungano ni kama koti tu, likikubana unalivua!

Sisi Wazanzibari tuko tayari kuwa na serikali moja tu SMZ yaani Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Tanzania ife kwa vile Tanzania ni muungano ambao utaleta gharama huku Zanzibar ipo na ilikuwepo haikuhitaji kuungwa.
 
Nyie wanafiki wakubwa siku zote mmeimba wimbo wa serikali 3 leo mna kuja na wazo ka serikali 1. Nchi hii ina tatizo la watu kufikiria kwa wakati
 
Kiukweli hayo yoote, 2, 3 ni uzushi tuu, Binafsi napeda kon NCHI MOJA SERIKALI MOJA!
 

Wazee wetu walipigania uhuru wa Tanganyika ili kuungana na Zanzibar? Kwani kodi zetu zinahudumia watu wa nje? Tumefika hata Hazina ya nchi inaongozwa na mgeni!
 
Kiukweli hayo yoote, 2, 3 ni uzushi tuu, Binafsi napeda kon NCHI MOJA SERIKALI MOJA!

Unataka Dsm ilipuliwe na mabomu ya kujitoa mhanga kutoka wapigania uhuru wa Jamhuri ya Zanzibar??
 

Naheshimu mawazo yako, lakini huoni mawazo haya kama ni sawa na kusema Kenya, Uganda, Burundi zote zisarenda mamlaka yake na kujenga taifa jipya ? Inaingia akilini kweli ? Kwa mawazo yangu muungano wenyewe ninaotaka ni serekali mbili 2 - Tanganyika na Zanzibar period !
 
Nakubaliana na mtoa mada ila kwa angalizo kuwa sera ya majimbo ndo ituongoze, kila jimbo litaruhusiwa kuwa na sharia zake na kujiamulia mambo yake yenyewe! ZnZ iwe ni jimbo ambalo likitaka sharia za kiislam wapewe ruksa! Kaskazini wakitaka kuingia mikataba ya uwekezaji bila ya kuingiliwa waruhusiwe ila kiasi cha mapato kiwe kinapelekwa serikali kuu!...
 
Sijakuelewa ndugu! Nikiota niko na Profesor wa ccm maana yake nini? Nani huyo Profesa wa ccm?

Bila shaka anamanisha profesa majimarefu wa Korogwe, Prof. Mahalu, Prof. Mwandosa, Prof. Tibaijuka au pengine Prof. Mparamagamba.
 
Mh Samweli sitta mwenyekiti wa kudumu wa bunge la katiba nakupongeza kwa kuchaguliwa kuliongoza bunge la katiba ili kupata katiba bora ya watanzania wote bila kujali itikadi za kidini, vyama au ukanda.

Mh sitta sis watanzania tunataka katiba mpya bora na sio bora katiba kama hii iliyopo sasa. kwenye swala la muungano tuwe na serikali moja au tatu hatutaki mbili, mwenyekiti wa chama asiwe raisi, viongozi wote wanaowagusa wananchi kwa ujumla wachaguliwe kwa kura na sio kuteuliwa kama wabunge maalumu, ma dc, ma rc, mawaziri na wakuu wa majeshi ya ulinzi wachaguliwe na bunge na wawajibishwe na bunge badala ya rais.

pawepo na kifungu cha kudhibiti wa utitiri wa vyama vya siasa, mapato ya kila mkoa yabaki mikoani kwa aslimia 70%, 10% iende serikali kuu na 20% yaende kwenye mikoa yenye rasilimali chache.

Nawasilisha.
 
Nataka serikali moja ili znz iwe kama lindi kwa au serikali tatu ili tanganyika iwepo nadhani huo utakuwa muafaka kamili

'Kama' kwenye lugha ya Kiswahili maana yake "sio yenyewe" kwa hivyo matakwa yako ni kutaka kitu kisichowezekana!
 


serikali 1 ndo mpango mzima
 

Watanganyika ni watu wa ajabu sana,kwanini munajilazimisha kuwabeba waznzibr wakati mshaelewa kuwa wazanzibr hawataki kubebwa?kwanini musiwabee wauganda au wakenya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…