JokaKuu,
Huu ulaghai ndio wanzanzibari wamechoka nao. Hatuwezi kuwa na Muungano ambao nyinyi (Tanganyika) muwe "partner" na hapo hapo muwe "master". Hapa hapatakuwa na haki. Lazima kuwe na Tanganyika ,Zanzibar na Muungano.
Huwezi kuwanyima watu haki zao za msingi na kuwatawala ki-dikteta halafu utegemee mapenzi kutoka kwao.
Huwezi kuwanyima watu uhuru wa kujiunga na OIC halafu utegemee mapenzi kutoka kwao.
Hakuna mzanzibari anaetaka kuitawala Tanganyika , bali ni kinyume chake. Mznz anataka aachiwe apumue..
We need them they dont need us tunawapotezea time, they need to plan their own thing we are obstacle
Takashi, Sina uhakika kama uliandika kitu ulichokusudia au uliamua kuandika kila neno lilipokuja kichwani.
Hapo mwanzo umesema, tunataka serikali ya Tanganyika, Zanzibar na Muungano. Ukimaanisha kuwa uwepo wa serikali 2 na ile ya muungano. Hadi hapo unataka muungano uwepo.
Kwenye aya hiyo hiyo ya kwanza umesema 'huwezi kuwanyima watu haki zao na kuwatawala kidikteta'
Aya ya pili unasema '' huwezi kuwanyima watu haki yao ya kujiunga na OIC'' na katika aya hiyo hiyo unasema ''Hakuna Mznz anayetaka kuitawala ZNZ bali kinyume chake'' ukimaanisha Tanganyika wanataka kuitawala ZNZ.
Aya ya tatu unasema 'we need them, they don't need us'' ukaongezea ''they need to plan their own thing we are the obstacles''.
Wakati aya ya kwanza ukisema kuwepo muungano aya zingine zinakataa uwepo wa muungano. Umeona jinsi ulivyojichanganya kwa kuanzia tu. Huwezi kutaka muungano wakati unalalamikia udikteta na kunyimwa haki.
Kwa vile umeeleza na kuonyesha wazi kuwa ZNZ inaonewa na kunyima haki zake basi ZNZ haihitaji kuwa na muungano ili ipate haki zake zote na ku-plan bila obstacles. Hilo litawezekana ZNZ ikijitoa katika muungano. Ni haki yao.
Usichokielewa kabisa ni kuwa ZNZ inatapa tapa, wamegoma kuvunja muungano na wanataka muungano tena kwa mbinu na nguvu. Wanataka muungano kupitia serikali 3 au mkataba. Wameshindwa kuandika mswada wa kuvunja muungano.
Maoni ya WZN kwenye tume wote wanataka muungano akiwemo Maalim Seif, Jusa na wachochezi wengine wenye hadhi kubwa sana ZNZ. Maana yake ni kuwa, ZNZ needs Tanganyika.
Kwa kutambua kuwa ZNZ inayimwa haki zake Watanganyika wamesema hivi;
Hawataki serikali 3
Hawataki mkataba
Tunawataka WZNZ nao waseme hivyo ili wapate ZNZ itakayojiunga na OIC kupata mikate, asali na maziwa bila bughudha.
Kama WZNZ hawatkubali kuvunja muungano, Watanganyika waliowabeba watauvunja;
1. Kudai serikali 1 ambayo ZNZ hawatakubali
2. Kukataa mkataba au serikali 3
3. Kuwatimua kwa kubana milango muhimu huku bara.
Ikishindikana basi ZNZ itabaki kuwa koloni na hapo watalazimika kutii amri kutoka Dodoma. Mna chaguo !