Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Watanganyika wanaoishi ZNZ ni wangapi sheikh na wao kama wataamua kubaki huko hiayari yao, lakini sidhani kuwa wanafiki 1000.
Mimi nawaunga mkono UAMSHO na WZNZ wanapaswa kuwaunga mkono UAMSHO. Njia bora ya kuwaunga mkono ni kuacha kuongelea serikali 3 au mkataba. Hadi hapo kutakuwa hakuna chaguo ila kuvunja muungano.
. Kuna CUF na CCM, kuna Spika kuna mwanasheria mkuu, wana bendera na wimbo wa taifa, mahakama kuu. HakunKuhusu vyama vya siasa na usajili hilo si kweli kwasababu ZNZ ina BLWa mtu yoyote yule aliyejaribu kufikisha mswada wa kuvunja muungano kwa njia za kisheria kama walivyoleta mswada wa GNU au mabadiliko ya katiba.
Nani aliwazuia WZN Kuanzisha SUK au kubadili katiba yao? Jusa hajawahi kushtakiwa kwa kusema anachodhani ni sahihi.
Wazanzibar wanatumia mwanya tu kukwepa ukweli kuwa hawataki kuvunja muungano.
Ndiyo maana leo tunasikia serikali 3 au mkataba. Sasa kama hutaki muungano unataka serikali 3 au makataba wa nini.
Sisi Tanganyika tumeshaona hatuna manufaa na huu muungano na sasa hatutaki serikali 2, 3 au mkataba tunataka ZNZ iondoke zake kwa amani.
Tusaidieni basi ili tuvunje hili dudu kwa amani kwa kukaa kimya ili asijetokea mtu na kusema upo uwezekano ABC.
LET ZNZ GO!
[SIZE=3 said:MAMMAMIA;4255533]Hapo kwenye RED - Kuwakataza wananchi kujadili maslahi ya taifa lao ni KULAZIMISHANA na pia kung'ang'ania serikali tatu ni kulazimishana. Kwa nini kulazimishana huku? Kwa faida ya nani?
[/SIZE]
Kuna waliotoa rai ya kura ya maoni, matokeo yake yatakuwa kwa kasima gani - Tanzania Bara 50+1 na Zanzibar 50+1 iwe ndio uamuzi wa wengi juu ya kile watakachoamua au Tanzania yote wakiamua 50+1 iwe ndio imepita?
Kwa mtazamo wangu ni kuwa MUUNGANO UMESHAKUA KIROBA CHA MISUMARI, hakibebeki tena. Uamuzi wowote utakaoamuliwa sasa - iwe serikali 1,2,3...au kanda 7 au serikali 30 (yaani kila mkoa na serikali yake)...bado kero za Muungano zitazidi na hivyo kuzidi kutobebeka.
Kwa maoni yangu, suluhisho pekee la kutatua kero za Muungano ni kuvunja Muungano.
kwenye signature hapo kwanini hao washauri wasimshauri amwache mkewe, kwangu mimi kikwete aligombea urais kama zamu tu lakini hana hata hadhi ya kuwa monitor wa darasa,bogus ni bogus tu.wanatenganishwa mapacha nini vinchi hivi viwili vibovu.naunga mkono hoja asilimia mia.Tusikubali kwenda serikali tatu. Kwa vile tumekatazwa kutaka kuvunja Muungano - japo waliotukataza hawana uwezo huo - na kwamba tunaweza kujadili "muundo" bora wa Muungano. Ninawasihi watu wa bara kudai "Serikali moja, taifa moja, na nchi moja". Haya mambo ya serikali mbili nchi mbili au serikali tatu nchi mbili hayaingii kichwani na ni jitihada za kujaribu kuibeba Zanzibar. Wakati umefika tudai uwepo wa serikali moja tu ya kitafa kwenye nchi moja. labda yeye hana akili kwa sababu nionavyo mimi raisi wetu hana hata hadhi ya kuwa monitor wa darasa yeye aligombea uraisi kama zamu mbona hao washauri hawamshauri amwache mkewe bogus ni bogus tu.
Ninafahamu kabisa matokeo ya watu wa bara kutaka hili. Jambo pekee ambalo tusikubali kuuziwa (CCM na upiinzani wanataka hili) ni serikali tatu. Serikali tatu ni mzigo ambao hatuwezi kuubeba na wala hatupaswi kuubeba. Nawasihi wenzangu tukate kuongezewa mizigo. Tuwe na serikali moja, taifa moja na nchi moja. Sasa kama hili lina maana Zanzibar iwe "serikali moja, taifa moja na nchi moja" na bara iwe "serikali moja, taifa moja na nchi moja" basi na iwe.
Tuwasaidie Zanzibar watoke kwenye Muungano kama hawataki serikali moja kwani mbili hawataki na tatu tutajipa mzigo zaidi!
SAY NO TO SERIKALI TATU!!
Iambie tume ya Warioba - hatutaki serikali tatu!!
wamepata fursa ya kuujadili muungano kwa amani wanalazimisha matakwa yao we waache hakuna kitu kitakachodumu milele kwa kulazimishana.tatizo lao wanaamini katika jeshi na polisi na kwa uchache mahakama lakini naamini kwa dhati kabisa ipo siku watu wataudai kwa mapanga hawatojali bunduki wala singe we kaka subiri **** hawi **** milele na siku akishtuka anayejihisi mjanja hutafuta sehemu ya kujificha.na hii sio kwa muungano tu bali kwa yote ambayo wanayatekeleza kwa kuwakandamiza wengine.
Mkuu nakupa big up uko juu ya mstari
Takashi, nadhani kuna jambo umelielewa vibaya tena vibaya sana.Naona umesahau kama msajili wa vyama vya siasa ni Bw, TENDWA, sio BLW au spika KIFICHO. Chama cha siasa ili kisajiliwe lazima kiwe na wanachama waanzilishi kutoka Tngka na ZNZ. Ingelikuwa rahisi kama kusingekuwa na ulazima huo, ili znz wawe na vyama vyao bila kuhusisha wtngka.
Usisubiri kauli kutoka katika chama chochote kile cha siasa ya kuvunja Muungano. Halita tokea mpaka hapo katiba mpya ikiruhusu hivyo. Hata CHADEMA hawataki Muungano, ila kwa sasa hivi wanaishia serikali 3 au majimbo.
Vile vile sijakusikia kuwasakama CHADEMA kwa kutaka serikali 3 ila umekuwa ile hanagaiko la moyo"obsessed with Zanzibar" .
Wewe tena unakimbilia kuharibu hali ya hewa tena! una shida katika ubongo uende MIREMBE! Wenzako wanajadili kuukataa muungano nawe unakimbilia ROME!! psychiatric case!!In your dreams that will never happen hadi Vatican itapobadilika na kua mkoa pia u know what i mean
Ukidai serikali moja ni sawa tu na kuuvunja Muungano, Nadhani unawatania wazanzibari.Tusikubali kwenda serikali tatu. Kwa vile tumekatazwa kutaka kuvunja Muungano - japo waliotukataza hawana uwezo huo - na kwamba tunaweza kujadili "muundo" bora wa Muungano. Ninawasihi watu wa bara kudai "Serikali moja, taifa moja, na nchi moja". Haya mambo ya serikali mbili nchi mbili au serikali tatu nchi mbili hayaingii kichwani na ni jitihada za kujaribu kuibeba Zanzibar. Wakati umefika tudai uwepo wa serikali moja tu ya kitafa kwenye nchi moja.
Ninafahamu kabisa matokeo ya watu wa bara kutaka hili. Jambo pekee ambalo tusikubali kuuziwa (CCM na upiinzani wanataka hili) ni serikali tatu. Serikali tatu ni mzigo ambao hatuwezi kuubeba na wala hatupaswi kuubeba. Nawasihi wenzangu tukate kuongezewa mizigo. Tuwe na serikali moja, taifa moja na nchi moja. Sasa kama hili lina maana Zanzibar iwe "serikali moja, taifa moja na nchi moja" na bara iwe "serikali moja, taifa moja na nchi moja" basi na iwe.
Tuwasaidie Zanzibar watoke kwenye Muungano kama hawataki serikali moja kwani mbili hawataki na tatu tutajipa mzigo zaidi!
SAY NO TO SERIKALI TATU!!
Iambie tume ya Warioba - hatutaki serikali tatu!!
Kumbuka mwaka jana December (9/December 2011) tulisherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania (for the majority of people and media, and me included) AND THAT WAS OFFICIAL! - 50TH ANNIVERSARY OF TANZANIA INDEPENDENCE (watu wachache walisherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara). Sikumsikia aliyesherehekea miaka 50 ya uhuru wa tanganyika.
Jiulize kwa nini tulisherehekea miaka 50 ya UHURU WA TANZANIA au UHURU WA TANZANIA BARA, wakati Tanzania iliasisiwa mwezi April mwaka 1964 kwa muungano wa mataifa huru mawili - Hiyo miaka 50 ilitokea wapi?. Kwa nini tusherekee Uhuru wa Tanzania nchi ambayo haikupata/haikuwahi kutawaliwa? Jibu ni rahisi, TANGANYIKA ndio TANZANIA ndio MUUNGANO, na SERIKALI YA TANGANYIKA ndio SERIKALI YA MUUNGANO. kwa mfano, Tanzania yajipanga kuiadabisha malawi kwa kadhia ya ziwa Nyasa, jee zanzibar inashirikishwa kwenye kadhia hiyo - hapana. Jee ni nini msimamo wa zanzibar juu ya hilo? utasikilizwa? TANGANYIKA NDIO TANZANIA. Na muungano si lolote zaidi ya ukoloni wa wa tanganyika kwa zanzibar. Tanganyika yaweza kuiingiza Tanzania kwevye vita, dhidi ya Amini, au Malawi (mungu apitishie mbali), zanzibar haiwezi jambo kama hilo. Haiwezi hata kujiunga na OIC hadi siku Tanganyika watapopenda.
Kwa hali hiyo basi Mfumo wa serikali moja hautakuwa na jengine zaidi ya kuitumbukiza/kuimeza/kuiyeyusha zanzibar katika Tanganyika. Tanganyika wont have nothing to lose. BASI IWE KWA CONSENT YAO wazanzibari.
Mwanakijiji si kweli kwamba serikali tatu ni ghali kuliko serikali 2 tuliyo nayo sasa,
Chadema wakichukua nchi kutakuwa na mawaziri wa muungano wasiozidi watano (ulinzi, mambo ya nje, fedha, nimesahau nyingine) Kwa hiyo utakapokuwa na mawaziri 12 na manaibu mawaziri ni 24 na 10 wa Tanganyika = 34. Sasa linganisha mawaziri tulio nao. Just an example kwa kuwa hoja yetu ni lazima serikali iwe ndogo.
Pili, ukipunguza wizara maana yake unapunguza watumishi waliojazwa ktk wizara hizo. Mabilioni yanaokolewa.
kama hukubaliani na mimi lete calculation hapa.
Samahani Mwanakijiji, Unaweza kunambia ni mzigo gani zaidi utawapata Bara kukiwa na serikali tatu?..P. Aweda, kwanza huwezi kuwa na wizara tano tu za Muungano; na hata kama inawezekana utaoa kuwa wizara tano za Muungano zitakuwa ndio za muhimu zaidi na zenye gharama zaidi.
Mkuu Mikael P Aweda,
Lakini tukiwa na serikali moja maana yake ni kwamba hatutakuwa na haja ya kuwa na duplicate Ministries in both sides of Union. Tutakuwa na Wizara ya Moja ya Mambo ya Afya, Wizara moja ya Kilimo, Wizara moja ya Maji, Nishati, Michezo nk. Sasa sijui ni vipi gharama zitapungua ikiwa tutakuwa na serikali tatu contrary na serikali moja ikizingatiwa kwamba possibilities ya kupunguza na kumerge Wizara ipo hata kwa kuwa na Serikali moja.
Samahani Mwanakijiji, Unaweza kunambia ni mzigo gani zaidi utawapata Bara kukiwa na serikali tatu?..
Lakini Utaweza vipi kuwa na serikali Moja ikiwa mnajua hili haliwezi kukubaliwa na zanzibar amabo watakuwa wamemezwa haswa na serikal ya bara?..Mnafikiri kweli zanzibar inaweza kubali kuwa mkoa tu ktk Utaifa wa nchi yetu au hilo bunge litakuwa vipi maana ni nchi mbili zilizoungana kuunda Moja. Je ni 50/50 kutoka bara na visiwani, Uongozi wa kiutawala utakuwa vipi 50/50 au ule alioanzisha Nyerere wa rais akitoka bara makamu atoke visiwani, sijui uwwiano. jamani mnatazama vitu kwa picha gani haswa kushauri hata hii serikali moja ikiwa tumeshindwa ktk ushirika huu uliopo..
Mkandara,
Kukiwa na serikali tatu maana yake ni kwamba kila nchi (Tanganyika na Zanzibar) zitapaswa kuchangia pato lao fulani kila mwaka kuiweka Serikali ya Muungano in Operation. Under One Government hakutakuwa na hicho kitu. Kwa hiyo huo mzigo hautakuwa tu kwa Wabara bali hata kwa Wazanzibari
Nakala: Mzee Mwanakijiji.
TUMBIRI (PhD, University of HULL - UK),
tumbiri@jamiiforums.com
Aaaah mkuu wangu, mimi ni pro serikali tatu pia ukiondoa hii ya kuvunja muungano kuliko hiyo serikali moja, lakini najua haiwezekani kutokana na kwamba Zanzibar hawatapenda hii kabisa. Serilkali tatu, kuna serikali za states ambayo zitakuwa mbili na hiyo ya Republic itakuwa na majukumu ktk maswala yote YATAKAYOKUWA YA MUUNGANO kama unavyoona serikali ya Obama au ya Cameron.Kuna swali halijibiwi na pro-serikali 3.
Hivi hiyo serikali ya tatu itashughulikia mambo gani? Tukipata jibu hapo tunaweza kuanza na hesabu, bila jibu unapataje hesabu za gharama za kuendesha kwa kuanzia tu.