Mkuu Mkandara,
Hapa ndipo watu wengi mnachanganya madesa. Sawa Zanzibar haitaki Mfumo wa serikali moja lakini nia yetu ni kuiridhisha Zanzibar au kujiridhisha wadau wote wa Muungano juu ya Mfumo wanaoupenda? Alafu hii ishu ya kumezwa Zanzibar ni Propaganda tu ya wanazi wachache wanaohofia Mfumo wa serikali moja kuwatoa nje ya ulingo wa kisiasa. Kwani nikuulize kwenye Mfumo wa serikali moja Serikali ya Bara haitamezwa? Itaendelea kuwepo?
Tatu, ishu ya Uongozi wa kiutawala itamuliwa na wadau wote kama wakishakubaliana Mfumo wa Serikali moja. Kama wataamua iwe Rotation au otherwise hiyo siyo ishu.
Unasema mawazo ya serikali moja ni mawazo ya Ubinafsi zaidi na yasiyotakiwa hata kupendekezwa kwa sababu ndio kichochezi cha Ubaguzi huu uloanzishwa na Wazanzibar. Mi nakukatalia ndugu yangu. Nikuulize tu leo rafiki yako mmoja akija akikuambia tuchange pesa tununua kiwanja tujenge ghorofa tuishi pamoja alafu mwingine akakuambia kila mtu atafute pesa zake ajenge ghorofa lake kivyake. Ni wazo lipi ni la kiubinafsi? Kujenga nyumba moja pamoja au kujijengea nyumba kivyako vyako?
Pia unasema swala la serikali tatu au moja halihusiani kabisa na cost lakini kwa bahati mbaya umeshindwa kudemonstrate ni jinsi gani serikali tatu haitaleta impact in terms of Operation Cost.
Hata hivyo nakubaliana na wazo lako la kuvunja ndoa hii kati ya Tanganyika na Zanzibar maana kwa sasa tunalazimishana tu.
TUMBIRI (PhD, University of HULL - UK),
tumbiri@jamiiforums.com
Kwanza nitakujibu swali lako la Ubinafsi ktk kujenga Nyumba. Mtu yeyote anayetaka mimi tuchange fedha ili tununue nyumba wakati najua fika yeye ndiye atafaidika zaidi ktk nyumba hiyo kwa sababu ana watoto 40 wakati mimi nina watoto 2 anipe vyumba vitatu ilihali yeye atachukua vyumba 41.. Mbinafsi ni yule anayekazania kuchanga na kuishi nyumba moja ili kukidhi interest zake bila kujali kwamba miye pia nina mke na watoto nahitaji Uhuru fulani sio wa kupewa chumba cha kulala. UBinafsi sii kuishi pamoja bali ni ubinafsi ni pale mtu anapoweka interest zake mbele ya mtu mwingine. kama unataka utishi pamoja unaweza kuwa mbinafsi usipotaka kusikia mawazo ya mwenza.. Ubinafsi pamoja na kusema it's My way or the highway! - Hakuna mjadala.
Kuhusu swala la Operating cost, mkuu wangu lazima kwanza unielewe. nachosema mimi sababu ya kufikia maamuzi ya kuwa na nyumba moja, mbili au mbili katika uzio mmoja ni kutokana na kutoelewana kwetu. Swala la cost ni secondary maaa the prime thing ni kutafuta suluhu ya mahusiano kwa sababu kama ingekuwa rahisi tungejenga nyuma ya nyumba sita tu badala ya ghrofa. Minimum cost, choo ya kiswahili, kutumia mkaa na kadhalika ingetu gharimu kidogo zaidi ya kujenga ghorofa...
Ubishi wetu sio aina gani ya nyumba tunataka kuijenga bali ni mahusiano gani baina yetu yanayoweza kudumisha uhuru, haki na usawa wa wananchi wa pande mbili.
Sjui kama umewahi kuishi na watu as roommate, kuishi na hata ndugu mkiwa watu waizma mnaojitegemea kimaisha ukaona ugumu wake. Siku zote sisi miafrika tumeshindikana hata ndugu wawili hawawezi kuishi nyumba moja..lazima ugonvi utatokea na wengine urafiki huvunjika wanapoishi pamoja na sababu siku zote huwa ni mmoja wao kujifanya mtawala wa nyumba na mwenye mdomo mchafu wa kumsema mwenzake mchafu, haogi, haoshi vyombo na kadhalika japokuwa huyu mwenye mdomo anayasema haya kwa sababu ya kutazama interest zake na mambo gani yanamkwaza yeye..
Na mara zote ktk hali hii huwa hakuna salama baina yao isipokuwa kutengana ama huyu mmoja awe babu jinga kukubali matusi yote na wala kutoweka madai lakini akipiga mahesabu yake. Hapa hakuna Urafiki wala undugu mkuu wangu ni kuzidanganya nafsi..HIVI NDIVYO TULIVYO na tulivyokuwa muda wote wa muungano wetu japokuwa watu wengi wanachanganya sana kati ya MUUNGANO na JUMUIYA maana hii tulonayo sio ushirika amajumuiya ila ni NDOA baina ya nchi mbili hufungwa kwa mkataba na huachika kwa mkataba na sababu ya kuvunja ndoa..Unaweza kulivua koti ukisikia joto, lakini huwezi kulitupa koti maana utalihitaji siku nyingine ya baridi.
Ujenzi wa nyumba moja ulitushinda kwa sababu tuligawana vyumba, mamlaka na hata tuligawana hadi ujenzi wa msingi isipokuwa kushiriki pamoja ktk kufunika paa na kuta za ujenzi wa gate la kuingia wageni. Tatizo lipo kwenye finishing ya nyumba hii, Living room bara tumeweka furniture, Jikoni tumenunua vyombo hadi majiko tukisema ni ya bara japokuwa chakula tunakula wote. Zanzibar wanajitazama wanasema what do we own ndani ya nyumba hii?.. hawana kitu sasa imetokea kuna uwezekano wa wao kununua gari, bara tunasema hilo gari litakuwa letu sote maana tuna share kila kitu ndani, unakula, kupika na hata kunakalia makochi yangu na kadhalika.
Wazanzibar wenzetu wanataka nao wawe na chao, makochi yao, vuyombo vyao maana hii habari ya mali ni ya mnunuzi aloanza hawaikubali.. Tusiwachagulie marafiki wanaokuja watembeklea kwa sababu tu tuna shre nyumba wakati sisi hatutaki wageni ambao pengine wanaweza kuwa wezi ama wahuni wavuta Bangi wenye malengo ya kuchafua nyumba hii.
Hivyo hizi hitilafu zinazojitokeza ktk muungano wetu ndizo zinazo tuonyesha UBINAFSI wa mtu (nchi) maana tunatoka ktk kushare nyumba. Madai ya Zanzibar ktk mfano wako ni ndivyo Zanzibar wanafikiri ya kuwa tunashare nyumba tu..Wakati ukweli ni kwamba Muungano ni NDOA yetu sio uhsirikiano wa kushare au roomate.. Wanadai ktk nyumba hii wamepewa tu chumba lakini living room kuna TV ya MTanganyika, picha za ukoo wa Mtanganyika, furniture za Tanganyika hadi chooni kila kitu kinahesabuka ni cha Mtanganyika, Mzanzibar hana kitu ndani ya nyumba hii, kiasi kwamba hata akitaka kuleta mgeni wake ni lazima umuombe huyu Tanganyika ruksa!. Katika ndoa mali ya bwana ama mke ni mali ya mwenza pia, hili hawaliafiki kutokana na tabia ya bara kudai hizi ni mali zake sio za muungano wakati hakuna serikali ya bara - hapa kuna ukweli fulani.
Haya ndio madai ya zanzibar sasa wewe unapotaka ifikie hata kile chumba sio chake tena ni nyumba yetu wote ilihali Utaweka masharti ya kugawa kwa kutazama watoto wako. Wewe una watoto 40 mwenzako ana mmoja ama wawili, halafu unataka nyumba hii iwe yenu wote. Mkuu watoto 40 lazima watapunguza kipato cha huyu mtoto mmoja ambaye aliingiza mtaji ktk ujenzi wa nyumba hii..Na njia pekee inayoweza kutufaa ni kila mmoja wetu ajikate tu.
Aidha ni BORA sana kama mna uwezo kila mtu ajenge nyumba yake kivyake (Let Zanzibar Go) ama Ujamaa wa Kikafrika pale nyumba mbili za familia zinajenga ndani ya uzio mmoja - Ukienda kwa Mkandara (Tanzania) utakuta nyumba kadhaa za wazazi na watoto wakiishi na familia zao..(serikali tatu)