Nonda, Nguruvi3, Jasusi, Mwanakijiji, Kichuguu, zomba, takashi,
..kuhusu hizi tuhuma au shutuma za "kumezwa" na muungano.
..hivi kweli wa-Tanganyika hatujamezwa na huu muungano?
..manake sisi ndiyo tume-sacrifice utaifa wetu na kuchukua utaifa wa Tanzania.
..pia hatuna serikali yetu wenyewe, na zaidi ikitokea Raisi wa muungano akawa Mzanzibari, basi huwa na mamlaka ya kutuingilia mpaka ktk zile wizara zisizohusu muungano.
..pia imetokea, na siyo mara moja, kwa wa-Zanzibari kuteuliwa kuongoza wizara ambazo zinahusiana na masuala ya wa-Tanganyika. wakati huohuo sisi hatuna ruksa ya kuongoza wizara ktk serikali ya wa-Zanzibari.
..hivi wanaostahili kulalamika kwamba wamemezwa na muungano ni wa-Tanganyika au wa-Zanzibari??
Baru baru, kelele unazosikia si kelele za watu ni kelele za vikundi cha watu. Watanganyika wengi bado ni wamoja na wanaamini katika maisha ya kuvumiliana.Mimi naamini wazi kama Mtaunda muungano wa Serikali moja tu basi automatic Zanzibar lazima itajitoa na hivyo muungano kufa. Kwa waZnz hawatakubali kuwa mkoa ndani ya Serikali moja.
Lakin kwa upande wa Tanganyika kama Znz ikijitoa katika Muungano wenu lazima kuna haya yatawatokea.
Pitia link hii ya TTB Religion » Tanzania Tourist Board
Hapo utagundua lazima kutakuwa na kupokezana madaraka kwa dini kuu zilizotajwa na kubainishwa na Serikali ya JMTz. Kwani kwa sasa pengo hilo linafichwa na waZnz kwa upande wa dini moja.
Sasa sijui wa Tanganyika mnalionaje hilo ambalo sasa lipo dhwahiri shahir halina siri tena.
[/QUOTE]Mwisho, wako wa-ZNZ wanaoamini kwamba Tanganyika ni mali ya ZNZ. Watu hao hukumbushia na kutaka kurudisha dola ya Sultani wa ZNZ iliyostawi kutokana na biashara ya watumwa na pembe za ndovu toka Tanganyika and beyond.........
Takashi, Sina uhakika kama uliandika kitu ulichokusudia au uliamua kuandika kila neno lilipokuja kichwani.JokaKuu,
Huu ulaghai ndio wanzanzibari wamechoka nao. Hatuwezi kuwa na Muungano ambao nyinyi (Tanganyika) muwe "partner" na hapo hapo muwe "master". Hapa hapatakuwa na haki. Lazima kuwe na Tanganyika ,Zanzibar na Muungano.
Huwezi kuwanyima watu haki zao za msingi na kuwatawala ki-dikteta halafu utegemee mapenzi kutoka kwao.
Huwezi kuwanyima watu uhuru wa kujiunga na OIC halafu utegemee mapenzi kutoka kwao.
Hakuna mzanzibari anaetaka kuitawala Tanganyika , bali ni kinyume chake. Mznz anataka aachiwe apumue..
We need them they dont need us tunawapotezea time, they need to plan their own thing we are obstacle
Serikali moja, na ni sisi watanganyika ndiyo tunavyotaka. Kama wazanzibari hawataki serikali moja, basi waishie hukohuko. Sijui kwa nini hii mizee yetu inawabembeleza hawa wazanzibari, wana nini? Get'em out of our way, wanatujazia miinzi tu na misamaki yao.
Mkuu Joka kuu, siyo tu bei rahisi bali pia hawalipi kabisaaa! hawajui bei ya umeme kama mwananchi wa Kidatu au Ruaha.@Nguruvi3,
..wewe endelea kuwaelimisha hawa mabwana.
..unajua imefika wakati "kero za muungano" zimekuwa kama entitlement ya wa-ZNZ.
..its about time na sisi wa-Tanganyika tuwe na kero zetu.
..umeme unazalishwa Tanganyika, lakini tunaupata kwa bei kubwa kuliko wenzetu wa-ZNZ. katika mazingira hayo nani mkoloni, na nani mtawaliwa???
Mimi naamini wazi kama Mtaunda muungano wa Serikali moja tu basi automatic Zanzibar lazima itajitoa na hivyo muungano kufa. Kwa waZnz hawatakubali kuwa mkoa ndani ya Serikali moja.
Lakin kwa upande wa Tanganyika kama Znz ikijitoa katika Muungano wenu lazima kuna haya yatawatokea.
Pitia link hii ya TTB Religion » Tanzania Tourist Board
Hapo utagundua lazima kutakuwa na kupokezana madaraka kwa dini kuu zilizotajwa na kubainishwa na Serikali ya JMTz. Kwani kwa sasa pengo hilo linafichwa na waZnz kwa upande wa dini moja.
Sasa sijui wa Tanganyika mnalionaje hilo ambalo sasa lipo dhwahiri shahir halina siri tena.
Nguruvi3Takashi, Sina uhakika kama uliandika kitu ulichokusudia au uliamua kuandika kila neno lilipokuja kichwani.
Hapo mwanzo umesema, tunataka serikali ya Tanganyika, Zanzibar na Muungano. Ukimaanisha kuwa uwepo wa serikali 2 na ile ya muungano. Hadi hapo unataka muungano uwepo.
Kwenye aya hiyo hiyo ya kwanza umesema 'huwezi kuwanyima watu haki zao na kuwatawala kidikteta'
Aya ya pili unasema '' huwezi kuwanyima watu haki yao ya kujiunga na OIC'' na katika aya hiyo hiyo unasema ''Hakuna Mznz anayetaka kuitawala ZNZ bali kinyume chake'' ukimaanisha Tanganyika wanataka kuitawala ZNZ.
Aya ya tatu unasema 'we need them, they don't need us'' ukaongezea ''they need to plan their own thing we are the obstacles''.
Wakati aya ya kwanza ukisema kuwepo muungano aya zingine zinakataa uwepo wa muungano. Umeona jinsi ulivyojichanganya kwa kuanzia tu. Huwezi kutaka muungano wakati unalalamikia udikteta na kunyimwa haki.
Kwa vile umeeleza na kuonyesha wazi kuwa ZNZ inaonewa na kunyima haki zake basi ZNZ haihitaji kuwa na muungano ili ipate haki zake zote na ku-plan bila obstacles. Hilo litawezekana ZNZ ikijitoa katika muungano. Ni haki yao.
Usichokielewa kabisa ni kuwa ZNZ inatapa tapa, wamegoma kuvunja muungano na wanataka muungano tena kwa mbinu na nguvu. Wanataka muungano kupitia serikali 3 au mkataba. Wameshindwa kuandika mswada wa kuvunja muungano.
Maoni ya WZN kwenye tume wote wanataka muungano akiwemo Maalim Seif, Jusa na wachochezi wengine wenye hadhi kubwa sana ZNZ. Maana yake ni kuwa, ZNZ needs Tanganyika.
Kwa kutambua kuwa ZNZ inayimwa haki zake Watanganyika wamesema hivi;
Hawataki serikali 3
Hawataki mkataba
Tunawataka WZNZ nao waseme hivyo ili wapate ZNZ itakayojiunga na OIC kupata mikate, asali na maziwa bila bughudha.
Kama WZNZ hawatkubali kuvunja muungano, Watanganyika waliowabeba watauvunja;
1. Kudai serikali 1 ambayo ZNZ hawatakubali
2. Kukataa mkataba au serikali 3
3. Kuwatimua kwa kubana milango muhimu huku bara.
Ikishindikana basi ZNZ itabaki kuwa koloni na hapo watalazimika kutii amri kutoka Dodoma. Mna chaguo !
Nguruvi3
Nadhani kumefanyika usanii au makosa katika ku-quote maneno yangu. Hiyo sentensi nyekundu sio maneno yangu .Nadhani kuna mchangiaji ali-quote maneno yangu lakini akachanganya na yake. (Kidzude)
Mimi msimamo wangu uko pale pale , SITAKI MUUNGANO NATAKA NI(TU)ACHIWE TUPUMUWE. Niliposema huwezi kuwa na Muungano ambao Tanganyika ,iwe partner na hapo hapo iwe Master. Hii ni kujaribu kuelezea moja ya sababu ambazo mtu kama mimi naukataa Muungano. Kutokuwepo kwa Tanganyika ni chanzo cha ulaghai na uwongo wa Muungano. Nia yenu sio Muungano bali ni utawala...(Ukoloni).
Kuna pesa zinagaiwa mitaani Zanzibar kwa mtu yeyote atakae toa maoni ya kukubali Muungano kama ulivyo kwa Tume ya Katiba.
Pesa hizi zimetoka Tanganyika , kwavile wemeshaona msimamo wa waznz ni tishio kwa Ukoloni wao. Sasa Bw,Nguruvi3, JokaKuu, Mkandara, MM kijiji n,k. Zuwieni rushwa hii ,MZNZ hanunuliwi tena kwa 5,000 Tsh.
Aibu aibu, wabunge wanatembeza bahasha za hela...Kweli hamjiamini.
Mimi naunga mkono harakati zenu za LET ZNZ GO ! ila ninacho waomba muwe na nia dhati.