BARUA YA WAZI KWA RAIS WA DOLA YA ZANZIBAR DR. ALI MUHAMMED SHEIN
BISMILLAHI ‘RRAHMANI ‘RRAHIM
Kila sifa njema zinamstahikia Allah, Subhanah wa Taala, isofichika kwake dhulma wala harudishi dua ya mwenye kudhulumiwa. Rehma na amani zimshukie Mtume Muhmmad (s.a.w) kipenzi chake na cha umma, mtetezi wa waliodhulimiwa hata kabla ya kupewa Utume
Sheikh amechagua maneno kutoka aya ili kukidhi haja yake ya kuweka maneno dhulma na kudhulumiwa katika jitihada za kujenga hoja ya kudhulumu au kudhulumiwa na Tanganyika.
Amefanya hivyo kwasababu hoja yake haiwezi kusimama yenyewe bila kuingiza kipengele cha udini.
Anamtaja Mtume Muhhamada (S.A.W) kama mtetezi wa wliodhulumiwa kwa maana aliyokusudia yeye ingawa ukweli ni kuwa Mtume Muhhammad(S.A.W) alipewa utume kwa minajadili ya kuwalingania wanadamu kwa yale mema yaliyoamrishwa na mabaya yaliyokatazwa.
Mh. Rais;Ni kweli nchi yeti ya Zanzibar imechafuliwa jina lake kuwa ni nchi ya amani kama ilivyogeuzwa nchi yetu na ndugu zetu na kufanywa kuwa ni koloni lao baada ya mkoloni Mwingereza kutupa uhuru mwaka 1963 na kuwa na kiti chetu Umoja wa Mataifa huku walimwengu wote wakishuhudia; kiti ambacho kwa uwezo wake Allah atakirejesha karibuni na wewe ukiwa rais wa Zanzibar au uliyemwakilisha kuweza kuketi juu yake Insha'allah na sisi wananchi wako wa Zanzibar tukifurahikia jambo hilo adhimu
Hapa anaonyesha chuki dhidi ya Watanganyika kwa kuwahusisha na upotevu wa amani. Baada ya kupata uhuru kilichofuata ni mapinduzi kabla ya muungano.
Mapinduzi yenyewe yaliyomwaga damu ni kielelezo kuwa hakukuwa na amani kabla ya hapo. Kama ingekuwepo mapinduzi yalikuwa na ulazima gani? Sheikh ameruka ukweli kuwa mapinduzi yalitokana uonevu wa Sultan na hoja zake ni za kukataa mapinduzi kwanza na hapo kuna maswali, je mapinduzi ni halali?
Sheikh anamchagiza Rais aone ufahari wa kukalia kiti UN, hakika hilo ni haki kabisa kama ndivyo wanavyoamua na kupenda iwe. Tatizo ni tafsiri itokanayo, kwasababu kwa kuwa na kiti tu UN ni ushahidi anataka kuuvunja muungano. Hilo pia ni jambo jema ubaya wake ni kujificha wakati analisema.
Hapa Sheikh anawakana wenzake wanaotaka serikali 3 au mkataba kwasababu uwepo wa vitu hivyo hautaruhusu kuwa na Marais wawili ndani ya UN. Hakuna Rais wa Puerto Rico au Quebec ndani ya UN wala kiti cha England wala Walace. Kipo kiti cha United Kingdom.
Mh.Rais;Ni kweli nchi yetu inatiwa dosari lakini si kweli kuwa wananchi wa Zanzibar ndio wanaosababisha dosari hiyo na doa hilo la uvunjifu wa amani; ushahidi wa maneno haya tutaupata tukirejea na kutizama kwa jicho la uadilifu na insafu katika matukio tafauti. Kwa hakika tukifanya hivyo tutagundua bila ya taabu kuwa Jeshi la Polisi la Tanzania ndio wahusika wakuu na waanzilishi wa vurugu na uvunjifu wa amani ya nchi yetu ya Zanzibar kwa mara zote tatu, nikimaanisha machafuko yaliyotokea tarehe 25-26/5/2012 mjini Zanzibar na yale ya kuhujumu waumini na kunajisi misiskiti tarehe 17/6/2012, Donge, Mahonda na Mkokotoni pamoja na hujuma ya tarehe 20/7/2012 msikitini pia dhidi ya Waislamu walokusanyika msikiti wa Mbuyuni kuwasalia ndugu zao waliofariki kwa ajali ya meli ya Mv. Skaget. Waislamu tulihujumiwa ndani ya msikiti. Jeshi la polisi halikusita hapo bali liliwaingilia wananchi wanyonge mpaka ndani ya nyumba zao na kuwatendea matendo haramiya ya chuki na uhuni na katika waliotendewa matendo hayo maovu walikuwa wanawake na watoto wachanga. Polisi hao wakhalifu wa sharia waharibifu wa amani walifika hadi ya kutupa mabomu ya madawa makali ndani ya majumba ya raia bila ya kujali athari zitakazowasibu watoto wachanga na wanawake wenye kunyonyesha. Iwapo jeshi la polisi lililopewa jukumu la kulinda sharia, kuweka amani na kuwahami wananchi na mali zao ndio wenye kuvunja shariakwa kuwahujumu watu bila ya sababu, wananchi na haki zao zitalindwa na nani?
Sheikh anasema nchi inatiwa dosari akimaanisha na Watanganyika. Amesahau kuwa dosari zilikuwepo kuanzia enzi za UMMA party, ZPP,ZPP na ASP. Ugomvi wa mwaka 2001 uliopelekea wao kutozikana ulisababishwa na Maalimu Seif na Salimin Amour.
Kama dosari ingeletwa na Watanganyika iweje Maalimu na Komandoo washindwe kuliona hilo na kama wznz walikubali kufitinishwa kwanini Mtanganyika alaumiwe kwa upumbavu wa mtu mwingine?
Sheikh analitaja jeshi la Polisi la Tanzania kuleta vurugu nchini Zanzibar. Halafu mbele anasema ikiwa jeshi la Polisi ndilo lenye dhama ya kuleta amani.... Kwa maneno mengine jeshi lililopo Zanzibar ambalo commissioner wake na askari ni wznz, waziri wa mambo ya ndani ni mznz ni la Tanzania, lipi la visiwani tusilolijua?
Lakini pia kwanini atarajie jeshi la Tanzania kulinda amani wakati ameshasema ni la Tanzania linalopeleka vurugu? Kuna majeshi mangapi na kwanini kwanza asianze kulikana jeshi la Tanzania ambalo anaomba lilinde amani?
Hapa alikusudia kujenga hoja kuwa jeshi ni la Tanzania ambayo ZNZ si sehemu yake na hivyo ni mamluki.
Anasema Polisi ni wahalifu wa sharia akisahau kuwa wapo waliochoma wenzao moto na majengo moto ambao ni wahalifu wa kwanza wanaolazimu uwepo wa jeshi la Polisi liwe la ZNZ au Tanzania.
Sheikh anasema jeshi la Polisi limehujumu wanawake na watoto wachanga.
Alichokusudia ni kuonyesha na kuchochea hasira kuwa watoto wachanga walihujumiwa.
Asichokijua sheikh wetu ni kuwa wapo watoto wachanga (infants 0-6month), watoto (children; 1-6 years) watoto wakubwa (6-12years) na watoto (kids;12-17 years),hawa kwa pamoja tunasema ni watoto na hakika sheria na taratibu haziruhusu wao kuwa victims wa jambo lolote.
Sheikh hakutakiwa kusema watoto wachanga kwasababu kusema hivyo ni kuwaondoa wengine kwenye ulinzi (immunity) ya hatia. Kama Polisi walifanya uhalifu basi walioathirika ni watoto kwa ujumla na siyo wachanga peke yao. Ijulikane tu neno wachanga ameliweka kuamsha hisia na hili linaomuondolea sifa yake ya usheikh ya kuwa mkweli, asiye mchochezi, mfitini wala muungo.
Mh.Rais;Matokeo ya ukiukwaji wa sharia na haki za binadamu yaliyopelekea kuiharibia nchi yetu ya Zanzibar sifa yake ya amani na utulivu yamesababishwa na jeshi la polisi la Tanzania lililoacha kutekeleza wajibu wake wa kutunza amani ya nchi yetu Zanzibar . La kusikitisha zaidi ni kuwepo baadhi ya watendaji wako wa karibu wanaopotosha ukweli na kuifanyia khiyana nchi yetu ya Zanzibar kwa kufikisha kwako taarifa za uongo zilizopelekea kuitia doa na kuiharibu khutuba yako ilojaa maneno matukufu ya Allah Subhanah wa Taala pamoja na mafunzo kutoka Sunna za Mtume (s.a.w), khutuba ambayo ilitarajiwa kukemea dhulma za jeshi la polisi dhidi ya Waiislam na nyumba tukufu za Allah (S.w.T) iliyohujumiwa pamoja na wanawake na watoto wachanga ndani ya majumba kama ulivotetea makanisa na kubainisha hatari na ubaya wa walioyachoma makanisa hayo kwa lengo la kutaka kuanzisha fitna baina ya Waislam na jirani zao Wakristo waliokaribishwa nchini Zanzibar na kuishi pamoja nao miaka mingi kwa amani kiasi ambacho haijawahi kutokea Muislamu kulitusi kanisa licha kulichoma moto, kwani hayo ni kinyume na mafunzo ya dini yetu tukufu ya Kiislamu
Sheikh anasema wapo watu wanampelekea taarifa za uongo akimaanisha kuwa kile anacokisema yeye ndio ukweli. Anasahau ukweli kuwa kusema watoto wachanga tu ni fitna kwasababu endapo wapo walioathrika basi ni pamoja na wagonjwa, wazee, watoto na akina mama. Hapa anawatuhumu watendaji kwa uongo ule ule anaousema. Taarifa anayomplekea Rais ina ufitini wa kiwango kizuri tu, sasa ushujaa wa kusema wengine ni waongo anaupata wapi?
Anasema waislam wameishi na jirani zao wakristo miaka mingi. Si
ndugu zao hata kama ni mznz bali jirani.
Anasema kuna njama za kuhujumu Uislam ZNZ, hapo amesahau kuwa ZNZ ni ya wote na alipaswa kusema kuna njama za kuihujumu ZNZ na siyo waislam pekee kwasababu jeshi analolituhumu likirusha mabomu halichagui dini au kabila.
Sheikh anasema hakuna mwislam aliyetusi ukristo kwa maana yakuwa hujuma ni za kutunga. Ameshau kuwa ni wznz waliwachoma moto Watanganyika si kwa ukristo bali kwa utanganyika seuze ukristo!
Sheikh hakumbuki kuwa asiye mwislam znz anaitwa kafir, je neno kafir ni jema kwa watu wanaoishi kama jirani.
inapojikariri khiyana hiyo inajenga hisiya kwa wenyeji wa nchi hii ambao wengi wao ni Waislamu kuwa wanabaguliwa, na sio wao tu bali hata kudharauliwa nyumba zao tukufu za ibada na kuthaminiwa makanisa peke yake. Sisi Waislamu hatutaki nyumba zozote za ibada zidharauliwe. Nyumba zote za ibada lazima ziwekewe hishima zinazostahi
Wangechoma moto makanisa! ufahamu kuwa misikiti na makanisa ni sehemu takatifu zizsizopaswa kuwa maskani za wahalifu kujificha. Anachotuambia ni kuwa midhali kuna mznz kachoma moto mwenzake akikikmbilia msikitini huyo aachwe. Kwamba miskiti itumike kuhifadhi wahalifu hivyo ndiivyo dini inasema! Ufahamu wa sheikh unatia wasi wasi sana
Mh.Rais;Kwa heshma zote naomba zichunguzwe sana sifa mawe na . bili kwa watu wote wa karibu na viongozi, sifa mbazo ni hatari kuzikosa tena zinaweza kuiangamiza nchi yetu tukufu ya Zanzibar . Sifa hizo si nyengine illa ni ukweli na uaminifu ambazo ni kinyume na uwongo na khiyana. Yarabbi Muumba Mbingu na Ardhi, usieshindwa na jambo, tunakuomba muhifadhi Rais wetu, turejeshee nchi yetu kwa salama na amani, DOLA HURU YA ZANZIBAR, wastiri wanawake na watoto wachanga majumbani na Wazanzibari wote tunaodhulumiwa kwa kudai uhuru wa nchi yetu ya Zanzibar uloporwa na jirani zetu, ndugu zetu baada ya kutoka kwa wakoloni.Amir Mkuu, Jumuiya ya Maimamu Zanzibar
Farid Hadi Ahmed
Sheikh anasema warejeshewe nchi yao, nami nakubaliana naye kabisa.
Alichoshindwa kuelewa ni kuwa alipaswa awashawishi wabunge, wawakilishi, mwanasheria mkuu wairudishe nchi yao. Tena kasema dola huru ya ZNZ, nakubaliana naye lakini hakuna dola isiyo na jeshi kwahiyo alipaswa kuwashawishi wzn waanzishe jeshi kwanza.
Sheikh anasaidia kuondoa uwezekano wa serikali 3 au mkataba kwasababu tayari ameshadai kiti UN na jeshi, sasa mkataba utahusu mambo gani au serikali ya mkataba itahusu nini.
Wakati akisema hayo Maalimu Seif naye anasema tuwe na umoja kama wa ulaya, sijui kwanini umoja huo usiwe ndani ya EAC bali Tanganyika na ZNZ tu.