Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

Hili la serikali tatu ni sawa kwa kuwa muda si muda tutakuwa na akina Yeltsin watakaowaacha akina Gorbachev bila nchi ya kutawala na hivyo Tanganyika kuwa nchi peke yake bila unyonyaji wa Zanzibar na Zinzibar kubakia peke yake bila unyonyaji wa Tanganyika. Juzi nimewasikia wakililia kiti chao UN basi tukimpata Yeltsin wetu nao watakuwa na kiti chao huko UN. Wacha zije lakini tatu hazitadumu.
 
Kwa mtazamo wangu uwezekano wa Wazanzibar kuridhika without zanzibar being sovereignty state haupo, si ni juzi tu tumesikia Maalima anaomba sarafu yao, mambo ya nje yao?? so siungi mkono serikali tatu mbili wala moja naona tukubali tu kwamba Muungano umefika mwisho! kila mmoja ajikate kivyake.
 
I agree with you Mzee Mwanakijiji mzigo wa kuendesha hizi unatushinda elimu duni afya duni huduma duni yote hii ni uhaba wa fedha sasa serikali tati tena jamani hii tuseme hapana tuungane na ccm kuukataa
 
ndumyana; Unataka muungano uvunjwe kama ambavyo mkoa wenu wa Mbeya utavunjwa vipande viwili, then what???
 
Last edited by a moderator:
Tangu jana ilipotolewa hii rasimu nimepiga kelele sana juu ya muundo wa serikali tatu. Haijaniingia akilini ilikuwaje wanasheria wetu wabobezi kwenye hii tume wakaja na rasimu ya namna hii. Kwanza wamewachanganya wananchi kwa kudhani serikali sasa itakuwa ndogo, wakati huo wananchi wameshindwa kuelewa kwamba rasimu hii ni mzigo mzito na ni namna ya ulevi wa kisiasa kujitengenezea madaraka.

Jana tayari wenzetu wametoa matamko, kwamba wao wanataka serikali yenye madaraka kamili, kwamba hata hayo mambo saba yaliyobaki wataendelea kuyadai hadi watakapopata madaraka kamili. Maana yake ni kwamba, kelele za muungano zitaendelea hata baada ya hii rasimu kama itapitishwa (serikali tatu) wanataka serikali yao yenye madaraka kamili.

Hawa wanatoka kwenye chama ambacho most likely kinaweza kushika madaraka zanzibar wakati wowote (rejea historia za chaguzi zilizopita) kwa hiyo hawataacha kudai, wataendelea na kelele zao, na kwa hakika kama watakuwa madarakani, watashinikiza kujiondoa kwenye muungano ili wawe na madaraka kamili.

Inawezekana tume ya jaji haikuzingatia maoni halisi ya wazanzibar wengi, badala yake maoni yao yalimezwa na yale ya wabara ambao siku zote wamekuwa wakitaka serikali tatu. Ikaonekana wengi wanataka serikali tatu.

Mtanzania yeyote anayeitakia mema nchi yetu hawezi kutetea mfumo wa serikali tatu. Binafsi maoni yangu ni kwamba, ama serikali moja, au tuuvunje muungano tubaki na mahusiano ya kawaida ya undugu.

Najua wanasiasa wetu hili limewafurahisha sana maana fursa za kisiasa zitaongezeka sambamba na kuendeleza mashindano ya kutafuna nchi. Maana sasa kutakuwa na majogoo matatu pale juu huku kila moja likining’inia juu ya watendaji wake.
 
Hivi, katika hizo serikali tatu ina maana kila mojawapo ya hizo serikali itakuwa na rais wake, makamu wake, pamoja na mabaraza yake ya mawaziri au inakuwakuwaje hasa?
 
liwalo naliwe serikali moja,taifa moja,nchi moja,rais mmoja,huo ndo muungano
 
Pole sana Mwanakijiji kwa kuyarudia matapishi yako! Yapo wapi yale madharau na kejeli ulizozielekeza kwa Wazanzibari? Naona ile sitizai niliyokwambia imekuumbuwa.
Mbona umeshachelewa kwani kalamu zenu zimeshafanya kazi ambayo hamkuitarajia?

Leo Iwapi ile Zanzibar bye bye
yako ya siku tatu nyuma?
 
  • Thanks
Reactions: lum
Mzee Mwanakijiji
utaandika sana mwaka huu,nilitaka kushangaa usipinge serikali tatu,ningestaajabu sana.Msimamo wa viongozi wa imani yako ni huu wa serikali moja au muungano uvunjike.Msimamo huu umekuja baada ya wznz kujitambua na kustukia hila zenu.Sasa hakuna upenyo wa kupeleka mambo yenu kule.Rasimu ya katiba itaendelea vizuri na hatimaye tutapata katiba tuitakayo.Endelea kuandika utakavyo lakini maoni ya wengi yataamua.Pole mfia dini
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: lum
Nadhani sasa umefika wakati wa kuwaacha Wanzanzibar wadai nchi yao wenyewe. Hata sisi Watanganyika tunataka nchi yetu, full stop. Hatutaki muungano...

Tatizo lenu mmezoea kupata na kuona aliyekosa hana haki ya kudai nae apate. Sasa onjeni kile wenzenu kilikuwa kikituuma.
Wazanzibari hatuna hofu wala hautudundi mshipa ni nyie mtakaoamua kusuka au kunyowa!
 
Hii misemo ya kizenji siielewi hata. Nitamtafuta Joti anifafanulie...
 
rasimu hii sijui warioba alijifungia chumbani na mkewe akaitunga au alizingatia maoni yetu? kifupi hii rasimu ni upuuzi na ushuzi wa warioba sio maoni ya wananchi.
 
Back
Top Bottom