Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa kweli ni upuuzi; as a matter of fact ni kana kwamba hawajui hesabu za seti! Hivi Mbunge mwanamke atakuwa anawakilisha wanawake tu kwenye hilo jimbo na Mwanaume atawakilisha wanaume watupu?
liwalo naliwe serikali moja,taifa moja,nchi moja,rais mmoja,huo ndo muunganoTangu jana ilipotolewa hii rasimu nimepiga kelele sana juu ya muundo wa serikali tatu. Haijaniingia akilini ilikuwaje wanasheria wetu wabobezi kwenye hii tume wakaja na rasimu ya namna hii. Kwanza wamewachanganya wananchi kwa kudhani serikali sasa itakuwa ndogo, wakati huo wananchi wameshindwa kuelewa kwamba rasimu hii ni mzigo mzito na ni namna ya ulevi wa kisiasa kujitengenezea madaraka.
Jana tayari wenzetu wametoa matamko, kwamba wao wanataka serikali yenye madaraka kamili, kwamba hata hayo mambo saba yaliyobaki wataendelea kuyadai hadi watakapopata madaraka kamili. Maana yake ni kwamba, kelele za muungano zitaendelea hata baada ya hii rasimu kama itapitishwa (serikali tatu) wanataka serikali yao yenye madaraka kamili.
Hawa wanatoka kwenye chama ambacho most likely kinaweza kushika madaraka zanzibar wakati wowote (rejea historia za chaguzi zilizopita) kwa hiyo hawataacha kudai, wataendelea na kelele zao, na kwa hakika kama watakuwa madarakani, watashinikiza kujiondoa kwenye muungano ili wawe na madaraka kamili.
Inawezekana tume ya jaji haikuzingatia maoni halisi ya wazanzibar wengi, badala yake maoni yao yalimezwa na yale ya wabara ambao siku zote wamekuwa wakitaka serikali tatu. Ikaonekana wengi wanataka serikali tatu.
Mtanzania yeyote anayeitakia mema nchi yetu hawezi kutetea mfumo wa serikali tatu. Binafsi maoni yangu ni kwamba, ama serikali moja, au tuuvunje muungano tubaki na mahusiano ya kawaida ya undugu.
Najua wanasiasa wetu hili limewafurahisha sana maana fursa za kisiasa zitaongezeka sambamba na kuendeleza mashindano ya kutafuna nchi. Maana sasa kutakuwa na majogoo matatu pale juu huku kila moja likininginia juu ya watendaji wake.
Nadhani sasa umefika wakati wa kuwaacha Wanzanzibar wadai nchi yao wenyewe. Hata sisi Watanganyika tunataka nchi yetu, full stop. Hatutaki muungano...
Hii misemo ya kizenji siielewi hata. Nitamtafuta Joti anifafanulie...Tatizo lenu mmezoea kupata na kuona aliyekosa hana haki ya kudai nae apate. Sasa onjeni kile wenzenu kilikuwa kikituuma.
Wazanzibari hatuna hofu wala hautudundi mshipa ni nyie mtakaoamua kusuka au kunyowa!