sometimes sikuelewi Mwanakijiji... wewe ni mmoja wanaobwabwaja sana kuhusu zanzibar lakini huna idea inayosimama wima, unayumba kama shamba la mpunga tu
Hakuna haja ya muungano... PERIOD!
Mimi nafikiri Warioba na Tume yake wameamua" kummaliza" Mwanakijiji kwa shinikizo la damu na vidonda vya tumbo.
Tokea juzi Mzee wetu hali vizuri,hajisikii vizuri.
Mwanakijiji angeelekeza nguvu zake na kalamu yake katika kudai serikali ya Tanganyika, Period.
Hakuna haja ya muungano wala nini. Mwalimu Nyerere alisharidhia kufa kwa muungano. Kitabu cha Mwalimu cha 1994 kina maneno haya:
Kwa kweli hata kesho Nchi za Afrika ya Mashariki zikiamua kuungana, na Tanzania ikawa ni mshiriki, naamini kuwa ni rahisi zaidi kushirikisha Tanzania yenye Serikali Mbili - ya Zanzibar na ya Tanganyika - kuliko Tanzania yenye Serikali Mbili, ya Tanzania na ya Zanzibar.Uk 11-12 link http://www.scribd.com/doc/28203083/Uongozi-Wetu-Na-Hatma-Ya-Tanzania-by-Nyerere
Hatuhitaji serikali ya Muungano wala katiba ya Muungano. Tunahitaji kurudi tulipoanzia,unaweka reverse gear.Turudishe nchi mbili huru ambazo zitakwenda katika hatua ya kuunda Shirikisho la Afrika Mashariki kila moja kivyake.
Tunachokihitaji ni serikali ya Tanganyika na katiba ya Tanganyika tu.
Mwalimu alisharidhia kuuvunja muungano kwa njia ya kistaarabu.Au kuna utata katika kauli yake hiyo hapo juu?
Kwa nini tunaendelea na usanii,kupoteza muda na fedha za walalahoi kwa kujadili Katiba ya Muungano ambayo haina umuhimu wowote?
Jumuia ya Afrika Mashariki ina nia ya kuwa Shirikisho la Afrika Mashariki. Sijui ni kwa nini hatuelekezi nguvu zetu huko.
Ni wazi baada ya hatua ya ukusanyaji wa maoni kuhusu katiba Mpya, Kwa kuzingatia maoni ya wazanzibari ya kudai "waachiwe wapumue" na muungano wa mkataba(asilimia 66), Tume ya Warioba ilikuwa na kazi ndogo tu ya kupendekeza mchakato wa kuandika Katiba ya Tanganyika na kuunda serikai ya Tanganyika na kuasisi Taasisi za Tanganyika.
Badala yake Tume imeona itoe msaada kwa CCM kwa kuleta Rasimu tata. Ni wazi kuwa lengo ni kuibeba na kuipa muda CCM ijiandae vizuri katika maigizo ya kisiasa.
Mchakato wa kuunganisha Afrika Mashariki unasema hivi:
Kuhusu hatua ya mwisho ya shirikisho la kisiasa, katika Mkutano Usio wa Kawaida mwaka 2004 Wakuu wa Nchi wa Kenya, Tanzania na Uganda waliazimia kuunda Kamati ya Kuharakisha Shirikisho la Afrika Mashariki. Kamati hiyo inayoongozwa na Amos Wako iliwasilisha taarifa yake kwa Wakuu wa Nchi mwezi November mwaka huo huo katika Mkutano wa Sita wa Wakuu wa Nchi.
Miongoni mwa mambo mingine, kamati hiyo ilitengeneza ratiba iliyotaka mambo yafuatayo:
a. Rasimu ya katiba ya shirikisho la Afrika Mashariki ifi kapo Desemba 2007
b. Kupitishwa katiba na mkutano wa Wakuu wa Nchi mwezi Januari 2009
c. Kura ya maoni kuhusu katiba ifi kapo Desemba 2009
d. Shirikisho la kisiasa lenye urais wa mzunguko ifi kapo 2010 na uchaguzi wa rais ifi kapo 2013
Mkutano wa Wakuu wa Nchi Usio wa Kawaida uliofanyika Dar es Salaam mwezi Mei 2005 ulielekeza kuundwa kwa utaratibu wa mashauriano ya kitaifa kukusanya maoni kutoka kwa Waafrika Mashariki juu ya Shirikisho la Afrika Mashariki na kuharakisha mchakato huo. Uk 90 -92
Link http://www.kituochakatiba.org/index2.php?option=com_docman&task=doc_view&gid=1208&Itemid=27