Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

sometimes sikuelewi Mwanakijiji... wewe ni mmoja wanaobwabwaja sana kuhusu zanzibar lakini huna idea inayosimama wima, unayumba kama shamba la mpunga tu

Hakuna haja ya muungano... PERIOD!

Mimi nafikiri Warioba na Tume yake wameamua" kummaliza" Mwanakijiji kwa shinikizo la damu na vidonda vya tumbo.

Tokea juzi Mzee wetu hali vizuri,hajisikii vizuri.

Mwanakijiji angeelekeza nguvu zake na kalamu yake katika kudai serikali ya Tanganyika, Period.

Hakuna haja ya muungano wala nini. Mwalimu Nyerere alisharidhia kufa kwa muungano. Kitabu cha Mwalimu cha 1994 kina maneno haya:

Kwa kweli hata kesho Nchi za Afrika ya Mashariki zikiamua kuungana, na Tanzania ikawa ni mshiriki, naamini kuwa ni rahisi zaidi kushirikisha Tanzania yenye Serikali Mbili - ya Zanzibar na ya Tanganyika - kuliko Tanzania yenye Serikali Mbili, ya Tanzania na ya Zanzibar.Uk 11-12 link http://www.scribd.com/doc/28203083/Uongozi-Wetu-Na-Hatma-Ya-Tanzania-by-Nyerere

Hatuhitaji serikali ya Muungano wala katiba ya Muungano. Tunahitaji kurudi tulipoanzia,unaweka reverse gear.Turudishe nchi mbili huru ambazo zitakwenda katika hatua ya kuunda Shirikisho la Afrika Mashariki kila moja kivyake.

Tunachokihitaji ni serikali ya Tanganyika na katiba ya Tanganyika tu.
Mwalimu alisharidhia kuuvunja muungano kwa njia ya kistaarabu.Au kuna utata katika kauli yake hiyo hapo juu?

Kwa nini tunaendelea na usanii,kupoteza muda na fedha za walalahoi kwa kujadili Katiba ya Muungano ambayo haina umuhimu wowote?

Jumuia ya Afrika Mashariki ina nia ya kuwa Shirikisho la Afrika Mashariki. Sijui ni kwa nini hatuelekezi nguvu zetu huko.

Ni wazi baada ya hatua ya ukusanyaji wa maoni kuhusu katiba Mpya, Kwa kuzingatia maoni ya wazanzibari ya kudai "waachiwe wapumue" na muungano wa mkataba(asilimia 66), Tume ya Warioba ilikuwa na kazi ndogo tu ya kupendekeza mchakato wa kuandika Katiba ya Tanganyika na kuunda serikai ya Tanganyika na kuasisi Taasisi za Tanganyika.

Badala yake Tume imeona itoe msaada kwa CCM kwa kuleta Rasimu tata. Ni wazi kuwa lengo ni kuibeba na kuipa muda CCM ijiandae vizuri katika maigizo ya kisiasa.

Mchakato wa kuunganisha Afrika Mashariki unasema hivi:

Kuhusu hatua ya mwisho ya shirikisho la kisiasa, katika Mkutano Usio wa Kawaida mwaka 2004 Wakuu wa Nchi wa Kenya, Tanzania na Uganda waliazimia kuunda Kamati ya Kuharakisha Shirikisho la Afrika Mashariki. Kamati hiyo inayoongozwa na Amos Wako iliwasilisha taarifa yake kwa Wakuu wa Nchi mwezi November mwaka huo huo katika Mkutano wa Sita wa Wakuu wa Nchi.
Miongoni mwa mambo mingine, kamati hiyo ilitengeneza ratiba iliyotaka mambo yafuatayo:


a. Rasimu ya katiba ya shirikisho la Afrika Mashariki ifi kapo Desemba 2007
b. Kupitishwa katiba na mkutano wa Wakuu wa Nchi mwezi Januari 2009
c. Kura ya maoni kuhusu katiba ifi kapo Desemba 2009
d. Shirikisho la kisiasa lenye urais wa mzunguko ifi kapo 2010 na uchaguzi wa rais ifi kapo 2013
Mkutano wa Wakuu wa Nchi Usio wa Kawaida uliofanyika Dar es Salaam mwezi Mei 2005 ulielekeza kuundwa kwa utaratibu wa mashauriano ya kitaifa kukusanya maoni kutoka kwa Waafrika Mashariki juu ya Shirikisho la Afrika Mashariki na kuharakisha mchakato huo. Uk 90 -92

Link http://www.kituochakatiba.org/index2.php?option=com_docman&task=doc_view&gid=1208&Itemid=27
 
Pole sana Mwanakijiji kwa kuyarudia matapishi yako! Yapo wapi yale madharau na kejeli ulizozielekeza kwa Wazanzibari? Naona ile sitizai niliyokwambia imekuumbuwa.
Mbona umeshachelewa kwani kalamu zenu zimeshafanya kazi ambayo hamkuitarajia?

Leo Iwapi ile Zanzibar bye bye
yako ya siku tatu nyuma?
Sasa si ndio tunataka kuwasaidia mtoke vizuri; najua tukianza kudai serikali moja Zanzibar hawatokubali.. tukidai serikali tatu bado tutakuwa tunajaribu kuwaappease Zanzibar...
 
Thank you Nonda!!! nimependa sana ulivyoiweka... as i said before, i dont care what it takes kuvunja muungano, na hata ikiwa serikali ya tatu ndio avenue yenyewe ya nchi ya ahadi, NA IWE HIVYO

I HATE MUUNGANO WETU, NI MZIGO, UNAFIKI NA UPUUZI KWA WATANGANYIKA
 
Sasa si ndio tunataka kuwasaidia mtoke vizuri; najua tukianza kudai serikali moja Zanzibar hawatokubali.. tukidai serikali tatu bado tutakuwa tunajaribu kuwaappease Zanzibar...

MKUU HATA TALAKA HUANZA NA SEPARATION... ndio tunahama chumba kwa serikali ya tatu

ila kusema ukweli kabisa, WE DONT NEED HUU MUUNGANO... TUTAHESHIMIANA ZAIDI KILA NCHI ITAKAPOKUA HURU
 
Rasimu ya katiba kuhusu serikali tatu kwa maoni yangu hiki kiini macho, rasimu inataja kutakuwa na serikali ya Tanzania Bara (Tanganyika) lakini rasimu yenyewe haitaji muundo wa hiyo serikali kama ilivyo ya Zanzibar, Je Tanzania bara itakuwa na Rais wake, Mawaziri,Bunge lake, na mengineyo ya utawala?? Kwenye rasimu anatajwa rais wa Muungano (Shirikisho), mawaziri, bunge, mahakama na kadhalika; pia inataja serikali ya zanzibar na uongozi kamili rais, baraza la wawakirishi (bunge la zanzibar) lakini mbona sioni kutajwa kwa muundo wa utawala wa Tanzania Bara?? Hii inabaki tu kama ilivyo saa serikali mbili (hapa ndugu zangu ni kiini macho). Kuhusu wabunge wawili kwenye jimbo moja huu nao ni upuzi wa hali ya juu, je ikitokea hawa wabunge wakatoka vyama tofauti pinzani; hapa si kuongeza vurugu tu jimboni, kila mbunge atakuja na sera za chama chake au zake binafsi sasa hapo kweli kutakuwa na utulivu. Rasimu imewadhalilisha wanawake kuwapa upendeleo kuwa hawawezi kugombea na wanaume; hili inabidi tulikatae.
 
Hatutaki serikali tatu ata bure huyu mzee warioba ajue kua yeye ni mzee mda wowote anaweza akafa ila mzigo mzito atatuachia sisi vijana eti wabunge wawili kila jimbo nani atawalipa kwanini hizo hela zisitumike katika kuendesha shughuli nyingine za kimaendeleo mi nasema rasimu hii HAPANA HATA BUREE.
 
Sasa si ndio tunataka kuwasaidia mtoke vizuri; najua tukianza kudai serikali moja Zanzibar hawatokubali.. tukidai serikali tatu bado tutakuwa tunajaribu kuwaappease Zanzibar...



Serikali mbili. Budget inategemea mataifa ya nje, je itakuwaje kwa serikali tatu! Ukichaaa mkubwa tu wa kulinda viposho vyao na kutuletea Rasmu ya ajabu!

Suruhisho NI serikali moja ILI Kama wazanzibar hawataki waondoke, tena haraka!

Viva serikali moja viva mawazo ya mwanakijiji, tanganyika lazima Irudishwe na tunahitaji katiba yetu! Tutabembele- wazanzibar hadi lini?a mitano, then tutaandika katiba upya! Warioba Warioba!!!!! Nyerere anakuona!??


genious Nyerere alisema mwelekeo NI serikali moja, hii ya tatu, haitadumu HATA kwa miak
 
MMK watanganyika hatuna shida juu ya kuunda serikali moja lakini wenzetu ni wasumbufu mno, na huwa hawaelewi hii lugha. mimi nadhani rasimu hii ikipita na kuwa katiba kamili kama ilivyo ni daraja zuri la kuelekea serikali moja. lakini pia nadhani kwa kuangalia vichwa vya akina Jusa, serikali moja itakuja baada ya kwanza kuuvunja muungano, wazanzbari wakapata experience ya kuishi wenyewe kwenye tuvisiwa twao huku wakizidi kuzaliana na akina Jussa wakapata PBL(problem based learning)
 
Mwanakijiji mbona haukuonekana kutoa maoni kwenye tume ya katiba unaonekana saizi umechelewa.
 
Mkuu mwanakijiji acha kupotosha watu mawazo yako si mawazo yao,peleka shambani hizi ishu,badala ya kuchangia maendelea kwa ushauri mzuri bado umekaa kiuongo.
 
Kwenye hili suala la katiba limeishaingia siasa ni muelekeo ule ule wa Chadema na CCM.

Mwanakijiji Watanzania tupo zaidi ya milioni 40 cha kuchekesha unataka kuwa msemaji wao umechelewa kaka.
 
Kwenye hili suala la katiba limeishaingia siasa ni muelekeo ule ule wa Chadema na CCM.

Mwanakijiji Watanzania tupo zaidi ya milioni 40 cha kuchekesha unataka kuwa msemaji wao umechelewa kaka.


Mbona wazanzibar ni chini ya mil mbili wamekuwa wasemaji wakubwa wa kuwasemea wadanganyika mil 43 wanaoendelea kulala, ila wanakaribia kuamka!



Wewe una maslahi binafsi na wala si ya ccm, utawala aw baba yako ukipita HATA wewe na yeye mtagundua mfumo wa serikali tatu NI MZIGO kwa LENGO tu la kuwafurahisha viongozi Zanzibar na si wananchi wa zenji!endelea kufiri kwa kutumia tumbo!!

Wajitenge tu!serikali tatu ZA nini!
 
Mbona nyie wazanzibar. Mop chini ya mil mbili natala Mendeleev kusemea wadanganyika mil 43 wanaoendelea kuala, ila wanakaribia kuamka!


mjitenge Kabila serikali tatu ZA nini!

Ritz, tena kawa Mzanzibar? mimi siwezi kushikiwa akili mtu anaishi Marekani aniamlishe eti sema hapana serikali tatu, sema ndiyo serikali moja kwa kumfurahisha yeye.

Mimi natumia akili yangu napima mambo kama wewe na wenzako mnashikiwa akili siyo mimi.

Kila mmoja ana haki yake tusipangiane mambo.
 
Last edited by a moderator:
Kwa asilimia kubwa ni maoni Yao binafsi hususani la serikari tatu


Bila jimbo kuwa na wabunge wawili Wanawake wote au mwanamke na mwanaume je mama...... anaejipanga kuwa mbunge wa jimbo la mtama ILI baadaye awe waziri 2016 angeupataje!!!!!!!!!!! Rasmu NI mawazo tu ya hao, historia itawahukumu, ila wengi kwa umri wao they can hardly live kwa miongo miwili!
 
Kilicholetwa na tume ya Warioba ni mapendekezo ya Serikali ya Ccm,katika hali tulionao wa Muungano, kua na Serikali tatu ni kutaka kuuvunja muungano wenyewe,lakini haya maoni hayajaletwa kwa bahati mbaya ni mpango mahsusi wa ccm na Serikali yake kuhakikisha Nchi hii haitawaliki wakishinda CDM 2015,kwa sababu hapatakua na Tanzania tena Bali Tanganyika na Zanzibar.
 
Kinadharia serikali moja ndiyo njia ya maana ya kujenga muungano imara. Lakini kiuhalisia ni jambo lisilowezekana. Kwa hiyo kudai serikali moja ni kutaka kuvunja muungano tu sawa na wale wanaotaka muungano wa mkataba.

Tumedai serikali tatu kwa miongo mitatu sasa na tunashukuru tume imeliona hili. Njia ya kupunguza gharama ni kumfanya Rais wa Muungano awe mkuu wa nchi bila kuwa mkuu wa serikali na achaguliwe na Bunge badala ya kuchaguliwa kwenye kura ya jumla. Hivi walivyopendekeza itakuwa ni maajabu kwa sababu kutakuwa na serikali tatu lakini zitakazokuwa na nguvu ya maana kiutendaji ni mbili tu za bara na visiwani. Mwisho wa yote Rais wa Muungano ambaye kimsingi hana nchi atapwaya vibaya sana, na wale wawili wanaweza kumzira na kuachana naye na hao mawaziri wake 15!

Kwa mfumo waliopendekeza walipaswa kuruhusu utawala wa majimbo kwa bara wakati Zanzibar wangeendelea na serikali yao. Sioni namna ambavyo Rais wa Muungano atafanya kazi huku kukiwa na Rais kamili wa Tanganyika.

Sisi tuliopata nafasi ya kuingia kwenye mabaraza ya katiba itabidi jambo hili tulidadavue vyema.
 
Kilicholetwa na tume ya Warioba ni mapendekezo ya Serikali ya Ccm,katika hali tulionao wa Muungano, kua na Serikali tatu ni kutaka kuuvunja muungano wenyewe,lakini haya maoni hayajaletwa kwa bahati mbaya ni mpango mahsusi wa ccm na Serikali yake kuhakikisha Nchi hii haitawaliki wakishinda CDM 2015,kwa sababu hapatakua na Tanzania tena Bali Tanganyika na Zanzibar.

Tutoe maoni yetu bila kuipakazia tume. Kwa nini tunakiwa na akili za kutumwatumwa namna hii? Kwamba watu wazima wale zaidi ya 30 hawawezi kufikiria jambo hadi watumwe na CCM? Wale watu wana akili kuliko hao CCM na ni matusi kusema kwamba walitumwa na CCM. Shughulikia hoja sio ku-label watu!!
 
Back
Top Bottom