Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
Chanzo cha habari hii ni kutoka katika gazeti la Habari leo
(http://www.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/12645-makamu-wa-rais-atikisa-muungano)
Makamu wa Rais wa Zanzibar bw Seif Sharif Hamada ametoa masharti ya mambo 10 yanayopaswa kuondolewa katika mambo ya muungano. Amesema tume ya maridhiano ya Wazanzibar imeamua yafuatayo yasiwe ndani ya katiba mpya.
Ufuatao ni muhtasari wa habari hiyo
1.Zanzibar kuwa na uraia
2.Kubadili jina la muungano kutoka Jamhuri ya watu wa Tanzania na kuwa muungano wa Jamhuri za Tanzania
3.Znz kuwa na sarafu yake na benki kuu yake
4.Zanzibar kuwa na ushirika wa mambo ya kimataifa pekee
5.Zanzibar kuwa na baraza lake la mitihani
6.Kuwa na jeshi lake la Polisi
7.Kuwa na mamlaka zake za kodi zisizofungamana na upande mwingine
8.Usajili wa vyama vya siasa kila upande usiotegemeana
9.Hati za kusafiria
10. Bendera ya znz kule New York, Adis Ababa na Commonwealth.
Maalim ametoa masharti kuwa katiba mpya lazima iwe na marekebisho makubwa katika mambo ya muungano.
Amesema Wazanzibar wataiangalia rasimu ya katiba kwa masharti yaliyotolewa na tume ya maridhiano.
My take:
Maalim seif sina hana uelewa wa kile anachozungumzia. Kama anao,atakuwa anafahamu kuwa hadhra''audience'' yake haina uelewa na anaweza kuongea atakavyo na kupigiwa makofi.
Kwanza, Maalim Seif lazima atambue katiba ni chombo cha umma na si kwa ajili ya kundi au sehemu moja ya jamii.
kusema anaweka masharti ni dharau kwa wananchi wa Taifa hili.
Pili,tume ya Jaji Warioba ilipoundwa(wengine tulikataa), maalim na wabunge wake wa CUF waliridhia na chama chake kuwa sehemu ya wajumbe wa tume
Alikubalina na taratibu zilizopo na hawezi kuiwekea masharti tume alioridhia kwa kila hali.
Tatu, tume ya maridhiano ya wzn haina nguvu za kisheria.Kama ina nguvu zinaishia huko visiwani.
Haina mamlaka ya kuzungumza kama au Watanganyika hivyo maoni ya tume yanabaki kuwa maoni ya maskani au vijiweni.
Nne,Kubadili jina la JMT kuwa muungano wa jamhuri za Tanzania. Ni dhahiri anautaka muungano kwa kujificha.
Uwepo wa uraia na hati za kusafiria za znz hauna sababu za kuwa na Muungano wa Jamhuri za Tanzania anazodai.
Tano;Kuondoa jeshi la Polisi katika muungano.Polisi ni sehemu ya majeshi ya ulinzi na usalama yenye Amir jeshi mkuu mmoja tu.
Laukana anataka ulinzi na usalama viondolewe, Seif asema Jeshi na Polisi viondolewe ili kuwa na dola kamili.
Jeshi la Tanzania lina Amir jeshi mmoja tu ambaye ni wa majeshi ya ulinzi na usalama ikiwemo Polisi.
Sita,Baraza la mitihani la znz. Hilo limeshafanyika. Anachopaswa kufanya ni kuwashawishi wajumbe wa znz ndani ya NECTA kujitoa
Atake wizara ya elimu ya juu iondolewe pia
Saba, Mafuta na gesi, vimeshaondolewa kwa kutumia BLW.Mafuta yanachimbwa ardhini,hivyo anapaswa kutamka kuwa Ardhi isiwe katika muungano. Na ili kulinda mafuta na ajira zitokanazo, Maalim aseme kuwa ajira na shughuli za utumishi ziondolewe katika muungano.
Nane,Mamlaka za kukusanya kodi zipo znz (TRA na ZRA) Ushahidi upo mapato ya TRA yanabaki huko.
Znz inapokea pesa za bure kwa kupitia ofisi ya makamu wa Rais wa JMT(Mwaka huu bilioni 32).
Anapaswa azikatae kwanza kabla ya kuongelea mamlaka za kodi.
Tisa,Bendera ya JMT haimpendezi, Seif anatakiwa aache kutumia kitu chenye nembo ya JMT asiyotaka
Kumi, Maalim anapaswa kuwaeleza watu kuhusu mgao wa BoT znz inayoupata.
Na aangalie pengo la bajeti ya znz linavyozibwa na pesa za Muungano.
Kumi na moja,Uraia na hati za kusafiri na mambo ya nje,kwanza awaamuru wznz walioko bara akiwemo makamu wa Rais waache warudi kwenye Uraia. Arudishe kile kitambulisho cha JMT alichochukua Karimjee chini ya jina la JMT
Kumi na mbili,Vyama vya siasa, Maalim alikuwa Morogoro kuzindua kampeni za chama chake juzi.
Ili awe serious na anachosema tunamtaka apige marufu kukanyaga Tanganyika katika mambo ya kisiasa.
Madai ya Seif ni wazi anataka kuvunja muungano. Upo umuhimu wa kumsaidia afikie malengo yake ya kisiasa
kwanza, aache kuogopa kutamka 'vunja muungano''.Adai znz huru bila mkataba au kujibanza katika baadhi ya maeneo
Pili,Apige marufuku wabunge wa kiliberali(CUF) wasije Dodoma na wafanyakazi wa serikali ya muungano waondoke
Tatu,apeleke mswada wa kunja muungano BLW na BLM yeye akiwa makamu wa Rais kwa kushirikiana na Rais ambaye ni mwenyekiti wa baraza la mapinduzi
Nne,amshauri Rais ili kauli zake ziwe za SMZ na si za viunga vya minazi.
Muhimu:Maalimu aheshimu maoni ya wananchi juu ya katiba hana sababu za kuifanya ZNZ iweke masharti ya kisiasa kwa Tanzania.
Maalim aseme kama ni msemaji wa SMZ, kuongelea katika viunga vya minazi hakutaleta suluhu.
Maalim Watanganyika hawapo tayari kuburuzwa na wazanzibar kwa makundi au watu wa nje.
Tanganyika si sehemu na haijawahi kuwa sehemu ya sultan na haitakuwa sehemu ya Sultan
cc. Mwanakijiji, JokaKuu, Jasusi, Mag3, Wickama, Mkandara,EMT,Kichuguu,Mchambuzi,Kigwangalla, Zitto, Jusa,Tundu Lisu, AshaDii, Prishaz,Ngongo, Ms Judith, Ghibuu, Barubaru,Ngambo,Nonda, Ngali,Mwalimu,Nape,Bongolander,Invisible,Mwakalinga Y.R,
Watanganyika na Wanajamvi wote