Muungano: Maalim Seif aipa tume ya jaji Warioba masharti

Muungano: Maalim Seif aipa tume ya jaji Warioba masharti

Ukisoma vizuri utaona kuna njia panda. CCM inasema itajadili katika ngazi zote na wanachama wakikubali hawana ujanja.

Labda nisema hapa hakiangaliwi chama kinasema nini, yanyoangaliwa ni maoni ya wananchi.

Lakini iwe iwavyo, bado siwaelewi WAZANZIBAR kwasababu wao ndio waliokuwa wanalilia Tanganyika irudi, sasa inarudi wanataka kitu kingine. Hata Waliberali w CUF sera ya chama chao ni serikali 3.

WaznZ wamelalamika wanaonewa katika mambo 22 yamepunguzwa hadi 7 bado wanataka kitu kingine.

Swali kubwa ni kuwa hivi kwanini kuwe na mkataba ambao tunajua unaweza kufa kesho?
Kwanini tusiwe na mkataba kupitia EAC.

Na kwamba, mkataba anaousema Maalim ni wa mambo gani? Hakuna upuuzi kama kusema tunataka bila kusema ni kitu gani unataka. Nini mkataba uwe na kwanini mkataba na tusiende Kule rahisi kabisa wa EAC ambao kila nchi ni dola kamili.

Ndio maana nauliza hivi Seif anajua anachosema? Kwanini kama hataki muungano asiwahamasishe wznz wakatae rasimu yoyote ile ili tujue yameisha anabaki kubabaika na mkataba?

Mkataba una masilahi gani na Tanganyika?
Hapa wznz wamebanwa kuchomoa hawawezi kubaki wanaona chungu.
Kule Arusha wanasema ni ngumu kumesa.

TangAnyika ipo huru kwa uamuzi wa wzn.
 
MAALIM SEIF ALALAMIKA KUHUSU IDADI YA WABUNG\

Mara baada ya rasimu kutangazwa maalim seif amekimbilia kuhoji idadi ya wabunge wa bunge la Jamhuri ya muungano.
Amehoji kuwa ni kwanini znz ipewe wabunge 20 na Tanganyika 30.
Hizi ni nchi mbili ambazo zina usawa na hivyo zinatakiwa ziwe sawa katika uwakilishi.

Haya ndiyo mawazo aliyokuwa nayo hadi kukimbilia idadi ya wajumbe wa tume kuwa sawa badala ya kuangalia muundo na taratibu za kupata katiba.

Kinachoshangaza maalim Seif yupo bize kuhesabu watu wangapi watapata ulaji.
Nilitegemea makamu wa rais aangalie na kuhoji gharama za uendeshaji na zitagawanwa vipi.

Kwa vile yeye na wznz wana hulka ya kudai lakini hawajui kutoa tayari malalamiko ya kipuuzi kama haya yameanza.
Ni upuuzi kuhoji wabunge bila kuhoji gharama za kuendesha bunge zitapatikanaje

Ndiyo maana tunasisitiza kuwa maalim Seif kachoka kifikra, apunzike na hafai.
Mungu asadie na nina uhakika hataweza kuwa rais katika ardhi ya Tanganyika maisha yake yote.
Ni hatari sana .
Hafai na hatari kwa lipi?!
Yule ni Mzanzibari kiongozi wa Wazanzibari! kutaka wabunge wawe na idadi sawa ni kwa maslahi yao Wazanzibari hivyo hakuna ajabu hapo kwa vile anaweka mbele na kujali maslahi yao Wazanzibari kwanza, kukiita anachofanya kuwa ni upuuzi siyo sahihi hata kidogo!

...ajabu ni viongozi wa Tanganyika wanaushupalia muungano ambao hauna manufaa yoyote ya maana kwa Watanganyika.
 
Hafai na hatari kwa lipi?!
Yule ni Mzanzibari kiongozi wa Wazanzibari! kutaka wabunge wawe na idadi sawa ni kwa maslahi yao Wazanzibari hivyo hakuna ajabu hapo kwa vile anaweka mbele na kujali maslahi yao Wazanzibari kwanza, kukiita anachofanya kuwa ni upuuzi siyo sahihi hata kidogo!

...ajabu ni viongozi wa Tanganyika wanaushupalia muungano ambao hauna manufaa yoyote ya maana kwa Watanganyika.
Sideeq, kuna sababu za kusema kuwa kuna upuuzi.
Sisemi hivyo kwa kashfa bali kwa maana ya neno. Upuuzi ni neno na tendo ni kupuuza.
Kwa kiingereza wanasema ignore. Kwa maneo mengine ni puuza au usitilie manani.

Maalim Seif kusema hakuna tatizo kama mwananchi na kama kiongozi. Tatizo ni kuwa kile anachokisema hakilingani na hadhi yake hasa ukizingatia kuwa ni katibu mkuu wa chama na pia makamu wa rais.

Mfano, anaposema kuwa Tanzania haijawahi kuwa na mkuu wa majeshi mznz, sijui hilo unaliweka katika kundi gani.
Huko nyuma alishawahi kusema kuwa nafasi za ubalozini wznz ni wachache. Sasa kama mkuu wa majeshi ni mzanzibar na tuna balozi 33 kila ubalozi ukaajiri wznz watupu 20 jumla tutakuwa na wznz 667. Je hili litakuwa limemuondolea dhiki yule mshona nyavu za samaki asiyeweza kulipa sh 10,000 kama ada ya mtoto?

Ni mwaka wa tatu nadhani Maalim na wenzake akina Ahmed Rajab wamekuja na kitu kinaitwa Mkataba.
Hakuna anayeeleza jambo gani liwe la mkataba na huo mkataba ni wa nini na maana yake ni nini.

Alichowahi kusema ni kuwa kukiwa na mkataba kama mmoja haridhiki anajitoa. Leo tunatengeneza katiba ya miaka 50 kwanini tuishi tukiwa na mashaka kuwa kesho katiba inaweza kubadilika kwasababu kuna mmoja hajaridhika?

Aliulizwa kwanini kama ni mkataba tusikutane EAC ambako kila mmoja atakuwa dola kamili?
Jibu lake ni kuwa muungano wetu ni mzuri kuliko EAC. Alaa sasa basi anachokitaka nini tena kwasababu tayari keshasema ni mzuri, je ni yeye kuvunja au kuwa na mkataba?

Kungekuwa na mantiki kama basi angesema tuwe na mkataba wa kitu kadha wa kadha kwa manufa ya nchi zetu.
Hilo halisemi yeye anaimbisha wznz kwaya kwa maneno waisyoyajua.

Hapa jamvini nani amewahi kueleza kuhusu mkataba zaidi ya mitusi?
Hao wznz wanaosoma hapa hawajui, narudia hawajui mkataba uwe wa nini sasa mtu anayeweza kuyumbisha akili za wanadamu kama hawa ni wa kumfanya nini kama si kumpuuza kwa upuuzi.

Kama hasemi maktaba wa nini atulie maana hana hoja. Habari ya kugawana madaraka aache maana hajui gharama za madaraka hayo.

Lini uliwahi kumsikia Seif akihimiza wznz walipe bill za umeme!
yeye ni ajira tu hata kama halipii hata senti tano.
Kwanini tuendelee kumsikiliza huyu mtu na tusimpuuze.
 
Back
Top Bottom