Muungano: Maalim Seif aipa tume ya jaji Warioba masharti

Muungano: Maalim Seif aipa tume ya jaji Warioba masharti

Sasa ninyi majasiri si mjiondoe kabisa, vunjeni Muungano hata mimi nitakuunga mkono. Ninyi masema tunawanyonya na tunawazibia neema zenu lakini kwa nini hamtaki kutoka na sasa hivi manataka Jamhuri za Tanzania?

Halafu usituite waoga, hivi kuna muoga gani anaweza kumdhulumu mtu jasiri?

Kwa mtazamo wako (na Wazanzibar wenzako).

1. Tunawanyonya rasilimali zenu (kama zipo)
2. Tunawazibia neema zenu
3. Tunawachagulia viongozi nk nk

Sasa hapo nani jasiri!! Anayedhulimiwa ama anayedhulumu?

Mimi naona mnasuburi yule Baba yenu afufuke ili aje awasemee , kama alivyokua muda wote wa maisha yake. Sasa kwavile mnatatizo hilo, sisi tutauvunja Muungano kipande baada ya kipande. Sasa hapo utamjua nani jasiri na nani muoga?
 
Kiongozi mzuri ni yule anayeonyesha njia hata kama wafuasi wake hawataki. Ni yule anayesimamia kile kilicho sahihi na wala si kura. Seif si kuwa anafuata wanachosema wznz, anawadanganya kwa kutowaeleza ukweli.

Tume ya Warioba ilimpa fursa ya kutoa maoni yake nyumbani kwake.
Seif akaulizwa kwanini tusivunje muungano na tukutane huko EAC?

Jibu la Maalim ni kuwa muungano wetu ni bora kuliko ule wa EAC kwasababu una umri na umepitia misuko suko mingi.
Ukisoma taarifa ya link hapo juu ni Seif huyo huyo anasema kuwa muungano hauna faida na umedhoofisha znz.

Sasa hapa lazima mtu mwenye akili ajiulize, hivi huyu kiongozi anajua anachosema?
Tulitarajia angemwambia Warioba muungano uvunjwe na wala asingeshtakiwa. Hakufanya hivyo.

Wakati akiwa kibanda maiti Seif alisema muungano umedhoofisha sana upande mmoja ambao ni Zanzibar.
Wakati huo huo anataka kuwe na Jamhuri za muungano wa Tanzania.
Kwamba dakika hii anasema hiki, next minute anakanusha alichokisema.

Hapa ndipo tunashangaa kama Uliberali ndio huo basi kuna tatizo.
Huyu si kiongozi ni mtafuta masilahi tu, kwamba awe rais hata kama mzanzibar wa kawaida ataumia.

Kwa shida iliyopo znz hivi sasa chini ya Muungano huu wa kidhalimu ,sitegemei kama kutakuwa na shida zaidi ya baadaya znz kuwa na mamlaka kamili. Kwa wale wenye umri mkubwa wanaeleza kuwa hakukua na shida ya maisha kama hii kabla ya Muungano. Hata miaka ya mwanzo ya Muungano hakukua na shida kama ya leo.

Kila kukicha mnanyofoa uwezo wa serikali ya Mapinduzi na kupeleka kwa Muungano kwa manufaa ya Tanganyika. Makosa yale waliyoyafanya wazee wetu , sisi watu wa leo hatutokubali. Zile zama zidumu fikra za mwenyekiti "zidumu" zimekwisha. Ulimwengu wa leo kila mtu ana uhuru wa kimawazo na fikra zake.
 
Chanzo cha habari hii ni kutoka katika gazeti la Habari leo
(http://www.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/12645-makamu-wa-rais-atikisa-muungano)

Makamu wa Rais wa Zanzibar bw Seif Sharif Hamada ametoa masharti ya mambo 10 yanayopaswa kuondolewa katika mambo ya muungano. Amesema tume ya maridhiano ya Wazanzibar imeamua yafuatayo yasiwe ndani ya katiba mpya.
Ufuatao ni muhtasari wa habari hiyo

1.Zanzibar kuwa na uraia
2.Kubadili jina la muungano kutoka Jamhuri ya watu wa Tanzania na kuwa muungano wa Jamhuri za Tanzania
3.Znz kuwa na sarafu yake na benki kuu yake
4.Zanzibar kuwa na ushirika wa mambo ya kimataifa pekee
5.Zanzibar kuwa na baraza lake la mitihani
6.Kuwa na jeshi lake la Polisi
7.Kuwa na mamlaka zake za kodi zisizofungamana na upande mwingine
8.Usajili wa vyama vya siasa kila upande usiotegemeana
9.Hati za kusafiria
10. Bendera ya znz kule New York, Adis Ababa na Commonwealth.

Maalim ametoa masharti kuwa katiba mpya lazima iwe na marekebisho makubwa katika mambo ya muungano.
Amesema Wazanzibar wataiangalia rasimu ya katiba kwa masharti yaliyotolewa na tume ya maridhiano
.

Angefupisha maoni yake kwamba hautaki Muungano.
Zaidi ya hapo anajidhalilisha maana mambo hayo kumi hapo juu ndiyo yanayojenge na kutambulisha kitu kinaitwa Nchi .Kama hiyo haitoshi Bora arudi kwao Pemba na adai Uhuru wa nchi itakayoitwa Pemba naye atakuwa Raisi wa Kwamba wa Pemba Huru.
 
Chanzo cha habari hii ni kutoka katika gazeti la Habari leo
(http://www.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/12645-makamu-wa-rais-atikisa-muungano)

Makamu wa Rais wa Zanzibar bw Seif Sharif Hamada ametoa masharti ya mambo 10 yanayopaswa kuondolewa katika mambo ya muungano. Amesema tume ya maridhiano ya Wazanzibar imeamua yafuatayo yasiwe ndani ya katiba mpya.
Ufuatao ni muhtasari wa habari hiyo

1.Zanzibar kuwa na uraia
2.Kubadili jina la muungano kutoka Jamhuri ya watu wa Tanzania na kuwa muungano wa Jamhuri za Tanzania
3.Znz kuwa na sarafu yake na benki kuu yake
4.Zanzibar kuwa na ushirika wa mambo ya kimataifa pekee
5.Zanzibar kuwa na baraza lake la mitihani
6.Kuwa na jeshi lake la Polisi
7.Kuwa na mamlaka zake za kodi zisizofungamana na upande mwingine
8.Usajili wa vyama vya siasa kila upande usiotegemeana
9.Hati za kusafiria
10. Bendera ya znz kule New York, Adis Ababa na Commonwealth.

Maalim ametoa masharti kuwa katiba mpya lazima iwe na marekebisho makubwa katika mambo ya muungano.
Amesema Wazanzibar wataiangalia rasimu ya katiba kwa masharti yaliyotolewa na tume ya maridhiano
.

My take:
Maalim seif sina hana uelewa wa kile anachozungumzia. Kama anao,atakuwa anafahamu kuwa hadhra''audience'' yake haina uelewa na anaweza kuongea atakavyo na kupigiwa makofi.

Kwanza, Maalim Seif lazima atambue katiba ni chombo cha umma na si kwa ajili ya kundi au sehemu moja ya jamii.
kusema anaweka masharti ni dharau kwa wananchi wa Taifa hili.

Pili,tume ya Jaji Warioba ilipoundwa(wengine tulikataa), maalim na wabunge wake wa CUF waliridhia na chama chake kuwa sehemu ya wajumbe wa tume
Alikubalina na taratibu zilizopo na hawezi kuiwekea masharti tume alioridhia kwa kila hali.

Tatu, tume ya maridhiano ya wzn haina nguvu za kisheria.Kama ina nguvu zinaishia huko visiwani.
Haina mamlaka ya kuzungumza kama au Watanganyika hivyo maoni ya tume yanabaki kuwa maoni ya maskani au vijiweni.

Nne,Kubadili jina la JMT kuwa muungano wa jamhuri za Tanzania. Ni dhahiri anautaka muungano kwa kujificha.
Uwepo wa uraia na hati za kusafiria za znz hauna sababu za kuwa na Muungano wa Jamhuri za Tanzania anazodai.

Tano;Kuondoa jeshi la Polisi katika muungano.Polisi ni sehemu ya majeshi ya ulinzi na usalama yenye Amir jeshi mkuu mmoja tu.

Laukana anataka ulinzi na usalama viondolewe, Seif asema Jeshi na Polisi viondolewe ili kuwa na dola kamili.
Jeshi la Tanzania lina Amir jeshi mmoja tu ambaye ni wa majeshi ya ulinzi na usalama ikiwemo Polisi.

Sita,Baraza la mitihani la znz. Hilo limeshafanyika. Anachopaswa kufanya ni kuwashawishi wajumbe wa znz ndani ya NECTA kujitoa
Atake wizara ya elimu ya juu iondolewe pia

Saba, Mafuta na gesi, vimeshaondolewa kwa kutumia BLW.Mafuta yanachimbwa ardhini,hivyo anapaswa kutamka kuwa Ardhi isiwe katika muungano. Na ili kulinda mafuta na ajira zitokanazo, Maalim aseme kuwa ajira na shughuli za utumishi ziondolewe katika muungano.

Nane,Mamlaka za kukusanya kodi zipo znz (TRA na ZRA) Ushahidi upo mapato ya TRA yanabaki huko.
Znz inapokea pesa za bure kwa kupitia ofisi ya makamu wa Rais wa JMT(Mwaka huu bilioni 32).
Anapaswa azikatae kwanza kabla ya kuongelea mamlaka za kodi.

Tisa,Bendera ya JMT haimpendezi, Seif anatakiwa aache kutumia kitu chenye nembo ya JMT asiyotaka

Kumi, Maalim anapaswa kuwaeleza watu kuhusu mgao wa BoT znz inayoupata.
Na aangalie pengo la bajeti ya znz linavyozibwa na pesa za Muungano.

Kumi na moja,Uraia na hati za kusafiri na mambo ya nje,kwanza awaamuru wznz walioko bara akiwemo makamu wa Rais waache warudi kwenye Uraia. Arudishe kile kitambulisho cha JMT alichochukua Karimjee chini ya jina la JMT

Kumi na mbili,Vyama vya siasa, Maalim alikuwa Morogoro kuzindua kampeni za chama chake juzi.
Ili awe serious na anachosema tunamtaka apige marufu kukanyaga Tanganyika katika mambo ya kisiasa.

Madai ya Seif ni wazi anataka kuvunja muungano. Upo umuhimu wa kumsaidia afikie malengo yake ya kisiasa

kwanza, aache kuogopa kutamka 'vunja muungano''.Adai znz huru bila mkataba au kujibanza katika baadhi ya maeneo

Pili,Apige marufuku wabunge wa kiliberali(CUF) wasije Dodoma na wafanyakazi wa serikali ya muungano waondoke

Tatu,apeleke mswada wa kunja muungano BLW na BLM yeye akiwa makamu wa Rais kwa kushirikiana na Rais ambaye ni mwenyekiti wa baraza la mapinduzi

Nne,amshauri Rais ili kauli zake ziwe za SMZ na si za viunga vya minazi.

Muhimu:Maalimu aheshimu maoni ya wananchi juu ya katiba hana sababu za kuifanya ZNZ iweke masharti ya kisiasa kwa Tanzania.

Maalim aseme kama ni msemaji wa SMZ, kuongelea katika viunga vya minazi hakutaleta suluhu.

Maalim Watanganyika hawapo tayari kuburuzwa na wazanzibar kwa makundi au watu wa nje.
Tanganyika si sehemu na haijawahi kuwa sehemu ya sultan na haitakuwa sehemu ya Sultan

cc. Mwanakijiji, JokaKuu, Jasusi, Mag3, Wickama, Mkandara,EMT,Kichuguu,Mchambuzi,Kigwangalla, Zitto, Jusa,Tundu Lisu, AshaDii, Prishaz,Ngongo, Ms Judith, Ghibuu, Barubaru,Ngambo,Nonda, Ngali,Mwalimu,Nape,Bongolander,Invisible,Mwakalinga Y.R,
Watanganyika na Wanajamvi wote

huwa napata shida sana kumwelewa maalimu seif....ni kirusi cha ajabu.....all he is thinking about is power.....

kwa nini asiseme pia wawe na jeshi lao....

nataki chama kiwepo bara na visiwani.....pamoja na kupewa serekali yao....kimsingi hapa tunaona ule ukweli kwamba CUF ililenga zanzibar tu...kwingine haawana haja napo.... hata simwelewi gaidi huyu...laba mwale wa mbagala wanamwelewa....
 
Let it go. Hatuwezi sema kuna muungano,wkt mzanzibari tanganyika anajiachia anavyotaka lkn mtanganyika akiwa znz anakosa amani(kama kaenda nje ya nchi). Wazanzibari wanapaswa wawe wazi kwa kinachowasibu na si kuwa wanafiki.
Viongozi wanaona faida ya muungano lkn wanashindwa kuelimisha watu wao...wana maslahi binafsi,mtawaua waznz wenzenu...labda cjui kwa haraka haraka ni kitu gn tanganyika inahitaji toka znz, mm sioni labda mniambie nyie waznz mnaosema tunawanyonya, labda matiti.
Mnatakiwa mkae chini mtafakari hili na serikali iwe moja na si tatu km anavyotka mzeemwanakijiji,maana mimi sioni kitu cha kujivunia nje ya muungano nyinyi waznz.
 
Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni ! Hivi ule muafaka wa CCM na CUF huko Zanzibar ulikuwa wa nini?Basi warudi mezani
 
MAALIM SEIF ALALAMIKA KUHUSU IDADI YA WABUNG\

Mara baada ya rasimu kutangazwa maalim seif amekimbilia kuhoji idadi ya wabunge wa bunge la Jamhuri ya muungano.
Amehoji kuwa ni kwanini znz ipewe wabunge 20 na Tanganyika 30.
Hizi ni nchi mbili ambazo zina usawa na hivyo zinatakiwa ziwe sawa katika uwakilishi.

Haya ndiyo mawazo aliyokuwa nayo hadi kukimbilia idadi ya wajumbe wa tume kuwa sawa badala ya kuangalia muundo na taratibu za kupata katiba.

Kinachoshangaza maalim Seif yupo bize kuhesabu watu wangapi watapata ulaji.
Nilitegemea makamu wa rais aangalie na kuhoji gharama za uendeshaji na zitagawanwa vipi.

Kwa vile yeye na wznz wana hulka ya kudai lakini hawajui kutoa tayari malalamiko ya kipuuzi kama haya yameanza.
Ni upuuzi kuhoji wabunge bila kuhoji gharama za kuendesha bunge zitapatikanaje

Ndiyo maana tunasisitiza kuwa maalim Seif kachoka kifikra, apunzike na hafai.
Mungu asadie na nina uhakika hataweza kuwa rais katika ardhi ya Tanganyika maisha yake yote.
Ni hatari sana .
 
Nadhani huenda ZNZ hawajui with certainity wanataka nini. Na kama wanajua basi hawajui wakipateje. Maana kila kitu kiko wazi lakini hawachukui hatua kutimiza matakwa yao badala yao kutwa kulalama tuu bila kuchukua hatua madhubuti kama mara zote walivyokuwa wanashauriwa hapa. Wanachoonesha hapa ni kuwa wao ni 'nataka sitaki' kama huyu dada kwenye hii comedy hapa Kansiime Anne is divorcing her man on minibuzz - YouTube. Hawataki kukubali kuwa wao kama hawautaki muungano kwa dhati kabisa na wakaamua kuchukua hatua muuungano utavunjika.

Lakini hauhitaji kuwa na Phd kujua kwamba waznz wanautaka sana muungano (and they seem they can't live without it) na ndo maana wanaongeza vipengele lukuki kwa ajili yao tu as if sisi ni watawala wao na ndio wafaidika wakuu wa muungano huu ilhali the opposite is true kwamba wao ndio main beneficiaries wa huu muungano.

Msimamo wango mara zote utabakia, ama tuwe nchi moja, taifa moja au znz waachwe kwa amani waende zao.
 
Serikali 3 ni kuvunja muungano. CUF waseme moja ama wavumilie mfumo uliopo wa muungano au watamke wazi kwamba muungano uvunjike. Zingine zote ni porojo na kuuma maneno! Wanafiki Wakubwa!
 
huyo ndo simbaaa.. maalim seif sio wewe jingakubwa..... ndo mwenyewake mzanzibari halisi anaebura milioni kibao nyinyi.... wewe kasirikaaaaaa..
mtoto umekula kungu nini? naona umelegealegea, au ndo ulibelali?
 
Njia rahisi ni kuifufua tanganyika ikae meza moja na z'br ijadili muungano,kinyume na hapo ni magumashi tu.
Nyie watu mbona mnatusumbua, kwani nini mnachotaka. Tanganyika ikae meza moja na hiyo Wilayat wajadili muungano upi na ili iweje? Tanganyika haina haja na majadiliano juu ya muungano yeye ni "price taker"; nyinyi na "price maker" majadiliano huwa hakuna. Kwa hivyo nyie kaeni Kibandamaiti kubalianeni maazimio yenu wekeni enforcement kwa watu wenu kisha wasilisheni rasmi kupitia serikali yenu ambayo na nyie cuf mmo, then mtaona kinachofuata

Ndicho kinachotakiwa, tatizo Watanganyika wamelala fofofo.
Kinachotakiwa na nani? "kulala fofoffo" kwa watanganyika si ndio fursa yenu kufanya mtakayo sasa mnataka kujadiliana nini na Tanganyika. Nchi yenu, watu mnao, serikali mnayo, kila kitu mnacho; mnataka majdiliano na tanganyika juu ya muungano ili iweje? mbona hamko wazi? mkataba mmeshaambiwa NO! kama hamna fall back position ya mkataba, so timueni- Ndio njia rahisi kwenu ya kuondoa 'kero za muungano'
 
c matakwa ya maalim ni matakwa ya waz'br,na ndio maoni ya waz'br yaliyotolewa kwenye tume ya warioba.

kweli waliberali waarabu walishawachokonoa zamani! Kila kitu wanachotaka mnawatekelezea!
 
Nyie watu mbona mnatusumbua, kwani nini mnachotaka. Tanganyika ikae meza moja na hiyo Wilayat wajadili muungano upi na ili iweje? Tanganyika haina haja na majadiliano juu ya muungano yeye ni "price taker"; nyinyi na "price maker" majadiliano huwa hakuna. Kwa hivyo nyie kaeni Kibandamaiti kubalianeni maazimio yenu wekeni enforcement kwa watu wenu kisha wasilisheni rasmi kupitia serikali yenu ambayo na nyie cuf mmo, then mtaona kinachofuata

Kinachotakiwa na nani? "kulala fofoffo" kwa watanganyika si ndio fursa yenu kufanya mtakayo sasa mnataka kujadiliana nini na Tanganyika. Nchi yenu, watu mnao, serikali mnayo, kila kitu mnacho; mnataka majdiliano na tanganyika juu ya muungano ili iweje? mbona hamko wazi? mkataba mmeshaambiwa NO! kama hamna fall back position ya mkataba, so timueni- Ndio njia rahisi kwenu ya kuondoa 'kero za muungano'
Kiukweli viongozi wengi wa Tanganyika hawaoni tatizo kwani ndio wanaoyafaidi matunda ya mfumo huu wa muungano, wananchi wake hawana pa kusemea zaidi ya vyama vyao vya upinzani ambavyo nao viongozi wao (wachache) wakivutwa mkono hunyamaza, lakini si Maalimu Seif bwana, huyu ni jembe.
 
Hebu rudia kusoma, ndio umeandika nini hapa?
 
ni fikira potofu ujinga na uroho wa madaraka, wazanzibar wanaruhusiwa kwenda zao, mtumwa anamkumbuka bwanake sultan ni kipindi kirefu hajamtia bakora,tutakuwa tunaendeleza lile tamasha la pasaka hasa soka mpaka pale uhamsho watakapoiteka zanzibar completely.

Hahahahahaaaa, yaani waTanganyika mnakerwa sna na Zanzibar Kuwa huru, mansahau Kuwa Mwisho wa Ubaya Huwaaa..............., nyinyi mnapaswa kutafakari ya Tanganyika yenu ndani ya muungano nasio Zanziabar Ndani ya muungano, plz keep Quart for the Zanzibar freedom maana hayakuhusu na wala huhusiki katika maisha ya waZanzibari.
 
Serikali 3 ni kuvunja muungano. CUF waseme moja ama wavumilie mfumo uliopo wa muungano au watamke wazi kwamba muungano uvunjike. Zingine zote ni porojo na kuuma maneno! Wanafiki Wakubwa!

Unajua maan ya selfish, naona unayo ww maan si CUF wala CCM & chama chengine chochote hapa Zanzibar, wanaodai uhuru wa Zanzibar ni waZanzibari nasio vyma vya siasa na hata hao Uamsho ni waZanzibari kwani waZanzibari wengi hapa ni waislamu so sioni tatizo kuungana na kudai haki yao, waZanzibari wanachodai ni mkataba au kuvunjika kabisaaaa kwa huo muungano, ninani alie tafuna maneneo hapo?, au huo uselfish ndio unaokusumbua?, wew huijui Zanzibar basi hata kusikiliza vyombo vyahabari kwaumakini?.... Inasikitisha sna km hujui bora kaakimya hutopunguz kitu!!.
 
Kumbe! sasa akina Shein, Vuai,Balozi Idd Seif, wale wa masikani ya kisonge, michenzani wao sio wznz? Tume ya watu 15 kutoka znz ilimwakilisha nani katika tu ya warioba kama si wznb?

Inaposemwa 66 % je 34% siyo wznz? Mbona CCM wanasema tofauti na CUF au!

Hapa huwa tunauliza mkataba mnaotaka ni wa kitu gani?
Yapo mambo 7 hayo siyo mkataba kweli? ninyi mngetaka yabaki yapi ! maana mkataba una mambo sasa ni yapi hayo?

Kama humuwezi kusema, basi kamwambieni Maalim muda wake kisiasa sasa basi, kete aliyo nayo ni kuvunja muungano ambayo tunaiunga mkono na tumeshawashauri sana namna ya kufanya. Hamtaki kwasababu ya woga!
Msipofanya sasa Gavana anakuja muda si mrefu.
 
Wenye Muungano wanasema: https://www.jamiiforums.com/katiba-mpya/467037-ccm-wapinga-serikali-tatu.html
 
Back
Top Bottom