Mkuu
Nguruvi3 ,
Maalim Seif anawazuga tu kwa haya anayoyaongea kwa sababu hata ukidadavua neno kwa neno utagundua contradiction nyingi tu.
He's a liability siyo tu kwa Watanganyika, bali hata kwa Wazanzibari kama watapewa hiyo nchi wanayoipigia kelele kila siku. He's gonna sell them.
I can't agree more Ng'wamapalala.
Huyu anataka kuwauza wazanzibar kwasababu ya Urais.
Ukisoma maoni ya tume ya Warioba, wznz wengi wamedai kubadilishwa muundo wa muungano, hawajasema kuvunja. Katika link hapo juu makamu wa rais Seif Idd amesema wazi kuwa wao wanafaidika na muungano.
Vuai aliyekuwa waziri kiongozi alisema wazi kuwa znz inanufaika na muungano.
Rais Shein kasema hayo na hata mznz wa kawaida kabisa anafahamu hivyo.
Seif anadhani kuwa na passport na Uraia wa znz kunatosha kuwa suluhu ya matatizo ya wznz.
Anawauza kwasababu kwa hali yoyote, znz itabaki kuitegemea Tanganyika.
Ni kanuni za asili na wala siyo suala la kisiasa.
Kuwaondoa wznz katika mahusiano kwa kiburi, matusi na kejeli kutawaumiza wznz wa kawaida kabisa.
Seif hatambui kuwa ziaidi ya nusu ya wzn inaishi Tanganyika.
Hatambui kuwa hakuna taifa lolote duniani lililobeba wznz wengi kama Tanganyika.
Anawauza wenzake kwa kusema kuwa baraza la mitihani liondolewe na limeondolewa.
Sasa wale wafanyakazi wa znz NECTA ni lazima waondoke.
Kibaya zaidi ni kuwa hilo baraza lao ambalo halitambuliwi na vyuo vya elimu ya juu Tanganyika litaondoa ule ubwete wa nafasi za upendeleo.
Hapa nifafanue kidogo, wakati wa kuchagua wanafunzi wa kuingia elimu ya juu, mwanafunzi wa znz mwenye div 4 anayonafasi kubwa kuingia elimu ya juu Tanganyika kuliko mwanafunzi wa Tanganyika mwenye div 2.
Hii ni kwasababu wao wanatakiwa wajaze nafasi kadhaa hata kama wataleta mwenye div 4 yenye D moja.
Kwasasa hali itabadilika, wanafunzi wa znz lazima wapimwe kama wale wa Rwanda au Malawi.
Hakuna nafasi za upendeleo wala malipo ya bure kama sasa kwasababu wanatahiniwa na bodi tofauti.
Seif hajaliona hilo anaangalia Urais tu.
Kuhusu contradictions, soma habari nzima ya Kibanda maiti.
Kwa mantiki ya katiba ni kuwa Seif anataka kuvunja muungano. Hilo ni sawa na sisi tunamsaidia iwe hivyo.
Mwisho wa hotuba anasema hataki jina la JMT anataka Muungano wa Jamhuri za Tanzania.
Haa! sasa huyu hataki muungano halafu anataka muungano tena
Anasema bendera ya Tanzania ni kinyaa. Juzi akiwa Morogoro alisindikizwa na ving'ora vya bendera hiyo hiyo.
Ndege anayopanda ina bendera hiyo hiyo asiyoitaka. Sasa hapa anakataa nini na anataka nini.
Anataka Uraia wa kila nchi. Miezi michache alikuwa Karimjee kachukua chake mapema sasa anauza wenzake.
Hajawahi kuwaambia kwanini alichukua kitambulisho cha JMT asiyoitaka to begin with!!
Kuhusu vyama vya siasa, anadai kuwe na separation kila sehemu iwe na chama chake.
Mwezi wa pili sasa anzunguka Tanganyika kuanzia Singida, Arusha, Morogoro n.k. kuimarisha uliberali.
Huyu ndiye asiyetaka kuwe na vyama vya siasa pamoja.
Hoja kubwa hapa si kusema eti wznz wasikatae muungano, in fact hapa tulipo tumeshafanya kila jitihada za wao kujinasua. Kinachowashinda wznz ni ukweli kuwa maisha bila Tanganyika ni maumivuy makali sana.
Wanafikiria hivi nusu ya nchi ikirudi kwao ni kitu gani kitatokea?
Wanafikiria,hivi shughuli zao za uchumi ambazo asilimia 90 inategemea soko la bara zitakuwaje baada ya kutengana?
Na wale walioko bara wanajiuliza, wakirudi znz wataanzia wapi maana wengine wanawajukuu,warudi kufanya nini na kwa kuanzia wapi.
Hayo yanawatisha ndio maana utasikia wakisema hawataki muungano kwenye viunga vya minazi, wakija Tanganyika wanataka serika 3 au mkataba.
Wakiambiwa mkataba uwe wa EAC wanasema tuna undugu.
Wakiulizwa undugu wa vipi wanasema kuoleana.
Mbona kuna watu wa Kenya, Uganda, Norway na filipine wameoleana bila muungano. Yote hayo ni uoga tu.
Ni kweli Sief si kiongozi wa kumchukulia serious kwa watu wenye akili zao.
Kwabahati mbaya si wote kundi lake linazidi kupiga kelele hovyo.
Eti Tanganyika inanyonya znz! hayo ndiyo Seif anapita akihubiri.
We don't need that, tuna matatizo mengi sana ya kushughulikia, hawa ni kuwaacha waondoke.
Nasikitika hawakupa uhuru juzi kama redio zao zilivyosema, lakini tupo bega kwa bega na wao hadi wapate uhuru.
Uhuru huo ni pamoja na kuiacha Tanganyika ipumue.
Hakuna cha Jamhuri za Tanzania wala wizara fulani iwe au isiwe.
Tuacheni tupumue miaka 50 ya kubeba mtoto inatosha, sasa tunawatua chini.
This time around hakuna ujanja, lazima kila kitu kiwekwe mezani.
Natoa wito hiyo rasimu ikitoka, kama kuna kipenegele cha kuwabeba ipigwe chini haraka sana.
Mtanganyika lazima kwanza ujiulize, kitu ABCD kinakusaidiaje wewe. Ukikubali bila kufikiri utaishia kulipa bill ya umeme elfu 50 kwa mwezi kumbe elfu 20 unamlipia mznzibar.
Ukikubali bila kufikiri utashangaa huna zahanati, kumbe bilioni 32 zimepelekwa tu kwasababu kuna sehemu inaitwa znz
Ukikubali bila kufikiri, baba yako na mama yako watakatwa kodi za mshahara, wadogo zako washinde na njaa kumbe pesa hizo ni kumsomesha mtoto wa kizanzibar.
Ukikubali bila kutafakari, utapita barabarani na bahasha za khaki ukitafuta ajira, kumbe ajira yako kapewa mtu kwasababu tu ni mnzanzibar.
Tafakari