Mkuu
Nguruvi3 ,
Hivi bado huwa mnazichukua kauli za Maalim Seif serious?
Mimi nilishamfuta katika ulimwengu wa wanasiasa wanasema na kutenda. Huyu jamaa anatumia ujinga wetu katika siasa zake za kitapeli. He stands only for his own skin. Maslahi na nafsi yake ni zaidi ya maslahi ya wananchi wake. He's a political prostitute. He's willing to prostitute himself for his political personal gain. Karagabaho!.
Wazee wetu walioleta hili "dudu" linaloitwa muungano pamoja na kufanya hivyo kwa nia nzuri, madhara yake yamekuwa makubwa na yanaendelea kuwa makubwa zaidi ya jinsi walivyotegemea.
CCM wako kwenye matope na hili "dudu" na ninaamini wengi wanapenda sana kuachana nalo lakini kivuli cha Mwl. Nyerere kinawaogopesha kuchukua maamuzi. MwanaCCM gani yuko tayari kuingia kwenye historia kama aliuvunja muuungano ambao kwa mujibu wa katiba iliyopo ni usaliti katika kiapo?.
Hotuba ya Mwl. Nyerere pale kilimanjaro hotel tarehe 14th March 1995 kuhusu kumpata Rais bora ilipigilia nyundo historia ya nchi kuhusiana na hili "dudu" muungano. Maneno yake hayo yamekuwa kama zimwi kwa CCM. Watakaoweza kupambana na hili ZIMWI na kulitupilia mbali ni watu kutoka nje ya nyumba ya CCM peke yake.
Ninaamini kitakachopatikana katika katiba hii mpya ni serikali tatu kwa vile kuna wanaCCM wengi ambao wanapenda iwe hivyo na hata mapendekezo ya CCM katika tume kuhusiana na hili "dudu" yalikuwa VAGUE.
Maalim Seif anawazuga tu kwa haya anayoyaongea kwa sababu hata ukidadavua neno kwa neno utagundua contradiction nyingi tu.
He's a liability siyo tu kwa Watanganyika, bali hata kwa Wazanzibari kama watapewa hiyo nchi wanayoipigia kelele kila siku.
He's gonna sell them.