Muungano: Maalim Seif aipa tume ya jaji Warioba masharti

Muungano: Maalim Seif aipa tume ya jaji Warioba masharti

Nguruvi3,
Kati ya mambo muhimu yanayoratibu shughuli za kimataifa ni swala zima la makubaliano(consent). Kabla ya kuundwa ka Jamhuri ya Muungano zilikuwepo nchi mbili. Inaaminika nchi hizi(kupitia viongozi wake) zilikubaliana kuungana. Kama ndivyo basi zinaweza kukubaliana kutengana! Sioni kwanini swala la muungano lipelekwe kwa mivutano na usiri kama vile ni maswala ya waganga wakienyeji! Wafuate utaratibu na wajitoe kabisa! Kinachowasumbu wazanzibari ni sitaki nataka! Ningeona wapo makini zaidi kama kweli wanataka wavunje kabisa Muungano. Hata mimi natamani sana Tanganyika iwe dola huru. Kuna mambo mengi sana tutasolve tukiachana na hawa ndugu!
 
Last edited by a moderator:
Mimi ni Mtanganyika na ninasubiri kwa hamu hiyo siku Tanganyika yetu itakaporejea. Kwa mantiki hiyo, ninamuunga mkono Maalim na Wazenj wote na Walibelari wote kudai Zanzibar huru. jamani tuwaunge mkono maana siku Zanzibar itakapopata uhuru wake, moja kwa moja na Tanganyika itakuwa imerejesha uhuru wake. Ushauri wa bure kwa akina Maalim na Walibelari: vunja ndoa na CCM, unga mkono harakati za ukombozi wa pili wa Tanzania zinazoendeshwa chini ya uongozi wa CDM na M4C yake mtakuwa mmejihakikishia uhuru wenu. Muungano kama ulivyo leo hii ni mradi wa CCM kuendelea kuhodhi utawala. As long as mnaendelea na ndoa ya CUF + CCM (sijui kama ni ya jinsia moja au tofauti), basi hizo ngonjera zitabakia hapo hapo Kibanda maiti!!!

Ila watu wachokozi jamani!
 
kuna kosa lilifanyika kwa kufikiri kumpatia wadhifa kunaweza kumaliza kiu yake ya kuwa Kiongozi mkuu ndani ya ZNZ,sasa kiu hiyo imekuzwa zaidi!Ninavyo fahamu mimi kwa uelewa wangu mdogo Vyama vinavyo iendesha ZNZ haviwezi kuwa na itikadi sawa kwa 100%.Kwa sababu hao waZNZ 66% niwale tu waliopata bahati ya kuonana na TUME ya Warioba na si 66% ya waZNZ wote.Sasa anapotaka kusema 66% ya WaZNZ ni Upotoshaji!!Mimi kama Mtanganyika sijaona nimepata nini kwa kuwa nao,napia nitakosa nini kwa Seif kuvunja huo Muungano.Tumsaidie huyo Maalim auvunje haraka huo Muungano kwasababu itatugharimu zaidi kwa kuwa na watu ambao unafikiri mkokwenye msafara mmoja kumbe wao wamepanga kukutosa njiani!Maana anajua kabisa kwa Muungano kuwepo hawezi kufikia kilele cha matamanio yake kisiasa,Jamani tumwache! Tusikuze sana tufanye kama tumegawa mkoa mpya kama tulivyo pata mikoa ya Njombe Simiyu n.k
 
Maalimu Seif ni sehemu ya Serikali ya Zanzibar,Kwanini hakuzungumza kiserikali na badala yake anazungumza kichama?Watanganyika tunataka muungano uvunjwe kabisa sio marekebisho,Zanzibar iwe huru tena hata leo, angalau tutapumua
Tena watoke wote huku bara warudi kwao... wanadeka sana na tumewabeba vya kutosha
 
KAuli aliyotoa angekuwa makamu rais usa kesho tungesikia kafukuzwa hv cuf wanakaaje na hili bomu khaaa
 
Kitu kinachoshangaza ni kuona kuwa Maalim hana kitu alichokisimamia na kukiamini kwa dhati.
Anabadilika kila uchao

Yeye na chama chake cha Uliberali walitaka serikali 3
Mara akabadilika anataka mkataba bila kukubaliana na Waliberali
Sasa hivi anataka dola huru ya znz kwa kutumia kamati ya maridhiano na wala si BLW au BLM
Ukisoma vizuri anataka federalism kwa hilo la Muungano wa Jamhuri za Tanzania
Maudhui ya habari zake ni kuwa hataki muungano.
Wakati hataki muungano, yupoo bize Morogoro na Singida akiimarisha CUF
Haieleweki anaSema kama MaaliM, Makamu wa Rais au Katibu mkuu wa CUF.
Maneno na majungu huyasema viungani Znz, akija Tanganyika ni muumini wa muungano.
Hataki Tanzania na bendera zake ni mbaya hazimpendezi, mfukoni anakitambulisho cha Tanzania.

In short huyu jamaa anayumba yumba sana.
Watanganyika tuwaunge mkono hawa jamaa haraka sana.
Wakishakuwa na Passport zao maana yake ni kuwa hawa ni raia wa nje hakuna mkataba wala mashiriikiano kila mtu kivyake
 
Maalim seif ni kirusi hatari sana kilichojaa nyongo ya unafiki ndani yake!wazanzibar wajiulize what next baada ya Maalim seif kushinikiza muungano uvunjike?wajinga ndo waliwao na madevu yao,kwanza ni bora kubeba gunia la misumari kuliko kuendelea kuwakumbatia hao wasiokuwa na shukrani akina yakhe!

Kama Maalimu Seif hata pigwa risasi nchi haita tawalika .Mtu huyu ni hatari kuliko faida zake za kuishi hapa hana tofauti na Wahaini wegine anachochea vuruguna Waislamu wana aangamia kwa yeye kutaka madaraka ambayo hawezi kudumu nayo!!!!!!!
 
Nguruvi3,

..wa-Znz wameweka ya kwao mezani.

..na sisi wa-Tanganyika tuweke ya kwetu mezani.

..suala la ardhi, Maalim Seif amelielezea ktk taarifa waliyotoa baada ya kongamano lao.

..kwa upande wangu madai ya kina Maalim yanabeba 90% ya matamanio yangu.

..naunga mkono msimamo wa Maalim Seif na wenzake.

cc: Barubaru, THE BIG SHOW, takashi, GHIBUU, Nonda

JokaKuu,

Kumekuwa na kampeni za kumchafua Maalim hapa JF, hasa kutoka kwa wale waabudu Nyerere. Lakini ukweli wa mambo Tz inahitaji viongozi kama Maalim Seif. Kiongozi anaejiamini na kutamka hadharani yale anayo yaamini katika ulimwengu huu wa siasa. Tanganyika inahitaji kiongozi kama Maalim , atamke hadharani msimamo wa Tanganyika katika Muungano.

Tanganyika na Tanzania zitofautishwe, huu uhuni wa kutumia mali za Muungano kwa maslahi ya Tanganyika umalizike. Tunako elekea ni kubaya simba wa Uamsho wamemaliza kazi yao ya kuamsha wznz, sasa wanajitayarisha kwa hatua ya pili ya Ukombozi.
 
Kama Maalimu Seif hata pigwa risasi nchi haita tawalika .Mtu huyu ni hatari kuliko faida zake za kuishi hapa hana tofauti na Wahaini wegine anachochea vuruguna Waislamu wana aangamia kwa yeye kutaka madaraka ambayo hawezi kudumu nayo!!!!!!!

Mtu mzembe kama wewe mwenye mawanzo finyu na ndoto za mchana...Siku aki uwawa Maalim ,hio ndio itakuwa siku ya mwisho ya muungano. Vile vile ,pengine hata wewe mwenyewe unaweza kuwa katika hao watakaoangamia baada ya kuuwawa kwa Maalim Seif.

Hiyo ndio itakuwa siku ya mwisho kengele za kanisa kusikika ndani ya ZNZ. Hiyo ndio itakua siku ya maafa makubwa ndani ya Tanganyika,vile vile. Yamemshinda Mungu wako NYERERE ,sitegemei kama yupo mwengine mwenye uthubutu huo.
 
Chanzo cha habari hii ni kutoka katika gazeti la Habari leo
(http://www.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/12645-makamu-wa-rais-atikisa-muungano)

Makamu wa Rais wa Zanzibar bw Seif Sharif Hamada ametoa masharti ya mambo 10 yanayopaswa kuondolewa katika mambo ya muungano. Amesema tume ya maridhiano ya Wazanzibar imeamua yafuatayo yasiwe ndani ya katiba mpya.
Ufuatao ni muhtasari wa habari hiyo

1.Zanzibar kuwa na uraia
2.Kubadili jina la muungano kutoka Jamhuri ya watu wa Tanzania na kuwa muungano wa Jamhuri za Tanzania
3.Znz kuwa na sarafu yake na benki kuu yake
4.Zanzibar kuwa na ushirika wa mambo ya kimataifa pekee
5.Zanzibar kuwa na baraza lake la mitihani
6.Kuwa na jeshi lake la Polisi
7.Kuwa na mamlaka zake za kodi zisizofungamana na upande mwingine
8.Usajili wa vyama vya siasa kila upande usiotegemeana
9.Hati za kusafiria
10. Bendera ya znz kule New York, Adis Ababa na Commonwealth.


Maalim ametoa masharti kuwa katiba mpya lazima iwe na marekebisho makubwa katika mambo ya muungano.
Amesema Wazanzibar wataiangalia rasimu ya katiba kwa masharti yaliyotolewa na tume ya maridhiano
.

My take:
Maalim seif sina hana uelewa wa kile anachozungumzia. Kama anao,atakuwa anafahamu kuwa hadhra''audience'' yake haina uelewa na anaweza kuongea atakavyo na kupigiwa makofi.

Kwanza, Maalim Seif lazima atambue katiba ni chombo cha umma na si kwa ajili ya kundi au sehemu moja ya jamii.
kusema anaweka masharti ni dharau kwa wananchi wa Taifa hili.

Pili,tume ya Jaji Warioba ilipoundwa(wengine tulikataa), maalim na wabunge wake wa CUF waliridhia na chama chake kuwa sehemu ya wajumbe wa tume
Alikubalina na taratibu zilizopo na hawezi kuiwekea masharti tume alioridhia kwa kila hali.

Tatu, tume ya maridhiano ya wzn haina nguvu za kisheria.Kama ina nguvu zinaishia huko visiwani.
Haina mamlaka ya kuzungumza kama au Watanganyika hivyo maoni ya tume yanabaki kuwa maoni ya maskani au vijiweni.

Nne,Kubadili jina la JMT kuwa muungano wa jamhuri za Tanzania. Ni dhahiri anautaka muungano kwa kujificha.
Uwepo wa uraia na hati za kusafiria za znz hauna sababu za kuwa na Muungano wa Jamhuri za Tanzania anazodai.

Tano;Kuondoa jeshi la Polisi katika muungano.Polisi ni sehemu ya majeshi ya ulinzi na usalama yenye Amir jeshi mkuu mmoja tu.

Laukana anataka ulinzi na usalama viondolewe, Seif asema Jeshi na Polisi viondolewe ili kuwa na dola kamili.
Jeshi la Tanzania lina Amir jeshi mmoja tu ambaye ni wa majeshi ya ulinzi na usalama ikiwemo Polisi.

Sita,Baraza la mitihani la znz. Hilo limeshafanyika. Anachopaswa kufanya ni kuwashawishi wajumbe wa znz ndani ya NECTA kujitoa
Atake wizara ya elimu ya juu iondolewe pia

Saba, Mafuta na gesi, vimeshaondolewa kwa kutumia BLW.Mafuta yanachimbwa ardhini,hivyo anapaswa kutamka kuwa Ardhi isiwe katika muungano. Na ili kulinda mafuta na ajira zitokanazo, Maalim aseme kuwa ajira na shughuli za utumishi ziondolewe katika muungano.

Nane,Mamlaka za kukusanya kodi zipo znz (TRA na ZRA) Ushahidi upo mapato ya TRA yanabaki huko.
Znz inapokea pesa za bure kwa kupitia ofisi ya makamu wa Rais wa JMT(Mwaka huu bilioni 32).
Anapaswa azikatae kwanza kabla ya kuongelea mamlaka za kodi.

Tisa,Bendera ya JMT haimpendezi, Seif anatakiwa aache kutumia kitu chenye nembo ya JMT asiyotaka

Kumi, Maalim anapaswa kuwaeleza watu kuhusu mgao wa BoT znz inayoupata.
Na aangalie pengo la bajeti ya znz linavyozibwa na pesa za Muungano.

Kumi na moja,Uraia na hati za kusafiri na mambo ya nje,kwanza awaamuru wznz walioko bara akiwemo makamu wa Rais waache warudi kwenye Uraia. Arudishe kile kitambulisho cha JMT alichochukua Karimjee chini ya jina la JMT

Kumi na mbili,Vyama vya siasa, Maalim alikuwa Morogoro kuzindua kampeni za chama chake juzi.
Ili awe serious na anachosema tunamtaka apige marufu kukanyaga Tanganyika katika mambo ya kisiasa.

Madai ya Seif ni wazi anataka kuvunja muungano. Upo umuhimu wa kumsaidia afikie malengo yake ya kisiasa

kwanza, aache kuogopa kutamka 'vunja muungano''.Adai znz huru bila mkataba au kujibanza katika baadhi ya maeneo

Pili,Apige marufuku wabunge wa kiliberali(CUF) wasije Dodoma na wafanyakazi wa serikali ya muungano waondoke

Tatu,apeleke mswada wa kunja muungano BLW na BLM yeye akiwa makamu wa Rais kwa kushirikiana na Rais ambaye ni mwenyekiti wa baraza la mapinduzi

Nne,amshauri Rais ili kauli zake ziwe za SMZ na si za viunga vya minazi.

Muhimu:Maalimu aheshimu maoni ya wananchi juu ya katiba hana sababu za kuifanya ZNZ iweke masharti ya kisiasa kwa Tanzania.

Maalim aseme kama ni msemaji wa SMZ, kuongelea katika viunga vya minazi hakutaleta suluhu.

Maalim Watanganyika hawapo tayari kuburuzwa na wazanzibar kwa makundi au watu wa nje.
Tanganyika si sehemu na haijawahi kuwa sehemu ya sultan na haitakuwa sehemu ya Sultan

cc. Mwanakijiji, JokaKuu, Jasusi, Mag3, Wickama, Mkandara,EMT,Kichuguu,Mchambuzi,Kigwangalla, Zitto, Jusa,Tundu Lisu, AshaDii, Prishaz,Ngongo, Ms Judith, Ghibuu, Barubaru,Ngambo,Nonda, Ngali,Mwalimu,Nape,Bongolander,Invisible,Mwakalinga Y.R,
Watanganyika na Wanajamvi wote

Umesahau kumi na tatu; kwanini viongozi wa ki-tanganyika waoga kupita kiasi. au ndio kile tunacho kiamini kuwa wao ndio wanaonufaika na Muungano huu wa kidhalimu.
 
naona kasema wakati wakuu wako masafa. je wamemwachia? nilimsikia alikuwa na hisia kali. kama vile tume ya warioba imeyapiga chini.. nasubiri rasmu kama maoni tumetoa sana
Mungu ilinde nchi na watu wako.
 
Sijui kwa nini CCM haitakiwa watu tupige kura kama tunautaka huu Muungano au la! Manake Wazanzibar wanafikiri wametuchoka, sisi ndo tumewachoka mbaya!. Hamna hata faida!
 
muungano ulipatikana kwa sababu flani na kwa sasa zile sababu hazina mashiko. sisi watanganyika muungano umekuwa mzigo kwetu na kero nafikiri niwakati wa kuwaacha hawa jamaa wabaki na zanziba yao nasisi tubaki na tanganyika yetu
 
Hapa naomba usome tena kwa utulivu. Sijazunguka, msome The Big show ameeleza kwa ufasaha nilichokusudia.

Hakuna anayetaka kung'ang'ania znz. Lakini basi znz isijibanze kwa kuchagua mambo.
Hivi anatakaje awe na jeshi la Polisi na wala si Jeshi la ulinzi na usalama. Kwanini asikatae JWT

Kwanini asiseme ardhi siyo sehemu ya mambo ya muungano lakini gesi na mafuta amesema.

Kwavile anataka kuvunja muungano, je anataka muungano wa Jamhuri za Tanzania kwa mambo gani.

sokwe ukijibu haya hata mie ntaelewa!juzi bungen wabunge wa Zanzibar walitaka zanzibar inufaike na gesi ya mtwara (correct me if I am wrong) hapo hapo wao wanasema mafuta sio mambo ya muungano!je Zanzibar inataka kuinyonya Tanzania/Tanganyika?kinachopatikana Zanzibar ni Chao lakini kinachopatikana Bara ni Chetu sote!ndio hivo Mwataka?kama ndio hivo then nafikir hata sie Tanganyika hatuhitaji muungano na nyie!mjikalie na mafuta yenu na sisi tujikalie na tabu zetu!
 
Last edited by a moderator:
Yericko, wala hakuzungumza kichama. Amezungumza kwa kutumia tume ya maridhiano ambayo haina nguvu za kisheria, kikatiba au vyovyote.
Alichokifanya ni kujificha katika dema na kutema alichokitaka yeye.

Hakuna sababu za makamu wa rais kuongelea mambo mazito kama haya katika viunga vya minazi. Shame!

Haya ndo matatizo ya Ndoa Mseto...mwenzie juzi tulimuona kaenda kujibanza msikitini na kutamka yake ya kumoyo...naam haswaa yale anayoyataman kutoka moyon mwake...Hamad naye huyo kajibanza maali kusema yake!
 
Mkuu Nguruvi3 ,

Hivi bado huwa mnazichukua kauli za Maalim Seif serious?

Mimi nilishamfuta katika ulimwengu wa wanasiasa wanasema na kutenda. Huyu jamaa anatumia ujinga wetu katika siasa zake za kitapeli. He stands only for his own skin. Maslahi na nafsi yake ni zaidi ya maslahi ya wananchi wake. He's a political prostitute. He's willing to prostitute himself for his political personal gain. Karagabaho!.

Wazee wetu walioleta hili "dudu" linaloitwa muungano pamoja na kufanya hivyo kwa nia nzuri, madhara yake yamekuwa makubwa na yanaendelea kuwa makubwa zaidi ya jinsi walivyotegemea.

CCM wako kwenye matope na hili "dudu" na ninaamini wengi wanapenda sana kuachana nalo lakini kivuli cha Mwl. Nyerere kinawaogopesha kuchukua maamuzi. MwanaCCM gani yuko tayari kuingia kwenye historia kama aliuvunja muuungano ambao kwa mujibu wa katiba iliyopo ni usaliti katika kiapo?.

Hotuba ya Mwl. Nyerere pale kilimanjaro hotel tarehe 14th March 1995 kuhusu kumpata Rais bora ilipigilia nyundo historia ya nchi kuhusiana na hili "dudu" muungano. Maneno yake hayo yamekuwa kama zimwi kwa CCM. Watakaoweza kupambana na hili ZIMWI na kulitupilia mbali ni watu kutoka nje ya nyumba ya CCM peke yake.

Ninaamini kitakachopatikana katika katiba hii mpya ni serikali tatu kwa vile kuna wanaCCM wengi ambao wanapenda iwe hivyo na hata mapendekezo ya CCM katika tume kuhusiana na hili "dudu" yalikuwa VAGUE.

Maalim Seif anawazuga tu kwa haya anayoyaongea kwa sababu hata ukidadavua neno kwa neno utagundua contradiction nyingi tu.

He's a liability siyo tu kwa Watanganyika, bali hata kwa Wazanzibari kama watapewa hiyo nchi wanayoipigia kelele kila siku.

He's gonna sell them.
 
Hadidu rejea za tume ilikuwa marufuku kutoa maoni ya kuuvunja,wazenj wanataka mkataba ili kuuboresha na 66% wametaka hivyo,je watanganyika mlitoa maoni gani kwenye tume kuuboresha?

Mkataba wa nini?hebu niambie wewe unaona mimi kama mtanganyika nafaidika vipi na uwepo wa Zanzibar kama sehemu ya Muungano?hakuna sababu ya mkataba,daini nchi yenu na muondoke jumla.
 
Kwa kifupi hayo masharti hayako sahihi maana anachagua vitu vinavyofaidisha wazanzibari tu....hii ni sawa na wale wanaosema wanataka kula pande zotehilo tatizo la muungano ni kubwa kuliko watu wanavyodhani....na unaendelea kwa shinikizo la nchi za nje hasa za magharibi (sipendi kuzizungumzia kwenye discussion hii ila kila mtu anajua ni za kiusalama na kiuchumi pia) na shinikizo la ndani (CCM)ukiangalia tanzania bara ilivyo sasa....ukiondoa muungano ni sawa na kupunguza nguvu ya CCM na kuongeza nguvu ya CHADEMA....hili CCM hawawezi kukubali anayebisha anaweza angalia idadi ya wabunge na kura CCM na CHADEMA walipata zanzibar!hata kama CHADEMA hawataipiku CCM karibuni ila trend inaonesha kuwa umaarufu wao unazidi kuongezeka bara, kwa hiyo watakua na nguvu ya kuinfluence decisions nyingi muhimu.kwa tanzania visiwani, kuvunja muungano ni sawa na kuikabidhi nchi hiyo kwa CUF kwa sababu kila mtu anafahamu nguvu kubwa ya kiutawala ambayo CCM imeweka pale kutokea bara....imefikia wakati wanasema rais wa zanzibar anachaguliwa dodoma.kwa hiyo sidhani kama huu muungano utavunjwa karibuni....na matatizo yake yatazidi kuongezeka ili CCM iweze kubaki madarakani
 
Back
Top Bottom