Muungano ni kati ya nchi ya Tanganyika na Zanzibar, kama Zanzibar ipo Tanganyika ipo wapi?

MKWEAMINAZI

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2023
Posts
930
Reaction score
1,304
Mwaka 1964 nchi ya Tanganyika iliungana na nchi ya Zanzibar na kuzaa nchi ya Tanzania.

Nilitarajia muungano ule ungezifuta nchi zote mbili yaani nchi ya Zanzibar na nchi ya Tanganyika ili kuwe na nchi moja tu ya Tanzania. Kinachoshangaza kwa muungano huu ni uwepo wa nchi ya Zanzibar na kutoweka kwa nchi ya Tanganyika.

Je kwanini nchi ya Tanganyika itoweke na nchi ya Zanzibar iwepo?

Kwanini nchi ya tanzania iwe kwenye ardhi ya nchi ya Tanganyika bila kuijumlisha ardhi ya nchi ya Zanzibar wakati udongo wa Tanganyika na Zanzibar ulichanganywa?

Au huu muungano ulikuwa wa kubadili jina la Tanganyika na kuwa tanzania maana jina la zanzibar lipo?

Nauliza tena, Nchi ya tanganyika ipo wapi?

 
Japo Tanganyika haijulikani ilipo, lakini Dodoma peke yake inatosha kuwatawala wazanzibari, sasa mimi sijui na hiyo Dodoma iko wapi!.
 
Wazanzibar ndo wanatutawala sisi hatuna uwezo wa kuwatawala,huu ni muungano wa hovyo kuwahi kutokea duniani
Na wala hatuna uwezo wa kujitawala. Bora wao kukiwa na Rais wa Tanzania kutoka bara,still Zanzibar wanajitawala.Inauma eti hatuna haki ya kufanya kazi hospital za Zenj za Serikali na Taasisi zozote zile za Serikali ya Zenj ila wao haki wanayo.#Tanganyikaexit
 
Na hiki ndicho Wazanzibari wanakipenda kwenye huu muungano. Wanufaike zaidi kuliko Watanganyika. Very selfish people.
 
Tanganyika ipo lakini wameivalisha koti hilo koti alovishwa Tanganyika linaitwa muungano kwa hiyo Tanganyika ndio Muungano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…