Muungano ni kati ya nchi ya Tanganyika na Zanzibar, kama Zanzibar ipo Tanganyika ipo wapi?

Muungano ni kati ya nchi ya Tanganyika na Zanzibar, kama Zanzibar ipo Tanganyika ipo wapi?

Wakuu napenda kuuliza swali la kipuuzi, hii inaendaje aisee

Zanzibar Ina raisi wake tena ni mzawa ,viongozi wote wa Zanzibar ni wazawa na haitakaa itokee raisi wa Zanzibar asiwe mzawa.

Zanzibar inawimbo wake wa taifa pamoja na bendera yake.

Pia vilivyopo na vipatikanavyo Zanzibar nivya Zanzibar na havitakiwi kuhusishwa na Muungano.

Hiyo Inathibitisha kuwa Zanzibar sio mkoa Bali ni taifa lenye taratibu zake.

Haya twende TANZANIA.
Ni muungano wa nchi mbili nazo ni TANganyika na ZANzibar.

TANZANIA Ina raisi wake ambaye anaweza kuwa mzawa wa Tanganyika au Zanzibar, hivohivo kwa makamu wake pamoja na viongozi wengne.

TANZANIA Ina wimbo wake wa taifa pamoja na bendera yake.

Pia Kila kitu kuanzia mapato na vitu vitu vingine ambavyo ni Mali ya TANZANIA vyenyewe ni ruksa kwa nchi ya TANganyika na ZANzibar.

Swali langu ni je Iko wapi nchi ya Tanganyika?

Kwann nchi ya Zanzibar ipo na inatambulika lakini Tanganyika haijulikani ilipo?

Kuna umuhimu gani na faida gani za kimuungano kwa TANZANIA pamoja na nchi zake yaan TANganyika na ZANzibar?

Je kinashindikana kipi kiuvunja huu muungano kama Hauna maana?

Iko wapi nchi ya Tanganyika?

Wajuvi na wadau mbalimbali karibun.

NB: Huu Uzi usifutwe wala kuhamishwa nmemaliza.
 
Wapo viongozi kibao ambao sio wazawa wa Zanzibar na kuhusu muungano mbona Kodi za TRA Hadi Zanzibar zinakusanywa licha yakua tuna ZRA yetu mnatakaje sasa
 
Mwaka 1964 nchi ya Tanganyika iliungana na nchi ya Zanzibar na kuzaa nchi ya Tanzania.
Mkuu MKWEAMINAZI, kwanza kwa ruhusa yako, naomba kulitumia bandiko lako hili, kama mbegu ya kuoteshea bandiko langu fulani.

Pili nikurekebishe hii opening statement yako ya "Mwaka 1964 nchi ya Tanganyika iliungana na nchi ya Zanzibar na kuzaa nchi ya Tanzania", it should be "Mwaka 1964 nchi iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika, iliungana na nchi iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na kuzaa nchi ya Tanzania", kwasababu nchi hizi zote mbili sasa hazipo!.
Nilitarajia muungano ule ungezifuta nchi zote mbili yaani nchi ya Zanzibar na nchi ya Tanganyika ili kuwe na nchi moja tu ya Tanzania.
Hii ni kweli, na ndicho kilichopo!. Watanzania wanahitaji sana kuelimishwa kuhusu muungano now, than any other times, kwasababu ni Mama Samia, ndiye aliyetoa ruhusa watu waachwe huru kujadili muungano "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza
Kinachoshangaza kwa muungano huu ni uwepo wa nchi ya Zanzibar na kutoweka kwa nchi ya Tanganyika.
Baada ya muungano, nchi zote mbili zilitoweka, hakuna nchi ya Tanganyika, wala nchi ya Zanzibar, kilichopo ni nchi moja tuu ya Tanzania!. Zanzibar sio nchi!.
Je kwanini nchi ya Tanganyika itoweke na nchi ya Zanzibar iwepo?
Nchi zote mbili zilitoweka, hakuna nchi ya Tanganyika wala hakuna nchi ya Zanzibar, bali nchi ya Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara iliyokuwa Tanganyika na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar iliyokuwa Zanzibar.
Zanzibar hii iliyopo sio nchi, ni sehemu ya Tanzania yenye utawala wake wa ndani!.
Kwanini nchi ya tanzania iwe kwenye ardhi ya nchi ya Tanganyika bila kuijumlisha ardhi ya nchi ya Zanzibar wakati udongo wa Tanganyika na Zanzibar ulichanganywa?
Sii kweli nchi ya Tanzania iko kwenye ardhi ya iliyokuwa Tanganyika, nchi ya Tanzania ni eneo lote la iliyokuwa Tanganyika na eneo lote la iliyokuwa Zanzibar!.
Na ni kufuatia kitendo kile cha kuchanganya udongo, ndio kuizi fuse nchi zote mbili kuwa nchi moja, hivyo muungano wetu ni muungano wa milele!, hauwezi kuvunjwa kwa namna yoyote, kwasababu ili kuuvunja huu muungano wetu adhimu, ni lazima kuuchukua ule udongo ulio changanywa na kuutenganishe, kitu ambacho haiwezekani!.

Ndio maana hata ule unaitwa ni mkataba wa muungano, The Articles of the Union between Tanganyika and Zanzibar, ule sio mkataba, ni makubaliano ya kuungana milele!, Je, Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano?. Kilichopo ni Makubaliano Tuu ya Muungano?
Au huu muungano ulikuwa wa kubadili jina la Tanganyika na kuwa tanzania maana jina la zanzibar lipo?
Hapana, Tanganyika ilibadili jina na kuwa Tanzania Bara, ila jina la Zanzibar lilibaki kwasababu ya utawala wake wa ndani tuu lakini Zanzibar sio nchi!.
Nauliza tena, Nchi ya tanganyika ipo wapi?
Usiendelee kuuliza tena, nchi ya Tanganyika haipo!, na nchi ya Zanzibar pia haipo, kilichopo ni nchi moja ya Tanzania!.

Elimu ya Uraia Kuhusu Muungano wetu adhimu!.

Duniani kuna miungano ya aina mbili Kuu,
1. Miungano ya union, nchi mbili au zaidi zinaungana kuunda nchi moja. Zile nchi zote zinakufa na inazaliwa nchi moja mpya.
2. Miungano ya federation, ni nchi mbili au zaidi zinaungana na kuunda nchi moja, ila zile nchi zote zinakuwa na serikali ya muungano, Federal Government na State Government, kila nchi ina utawala wake wa ndani.

Muungano wetu ni very unique, kwasababu ni muungano pekee duniani ambao on one side ni muungano wa union kwa nchi mbili kuungana kuunda nchi moja ya JMT, at the same time ni muungano wa federation wenye serikali mbili.

Muungano wetu kimataifa ni muungano wa union, Tanzania kimataifa ni nchi moja ya JMT, yenye serikali moja ya JMT, chini ya rais mmoja wa JMT, ambaye ni head of state, head of the government and CinC.

Lakini Kitaifa, nchi ya Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar, yenye katiba mbili, katiba ya JMT, na katiba ya Zanzibar, yenye serikali mbili, serikali ya JMT na serikali ya Zanzibar, SMZ, yenye marais wawili, rais wa JMT na rais wa Zanzibar.

Mkanganyiko wa Katiba.
Kama nilivyosema kimataifa Tanzania ni nchi moja ya JMT, hakuna mkanganyiko wowote wa kimataifa kuhusu Tanzania.

Lakini Kitaifa kuna mkanganyiko wa katiba kati ya katiba ya JMT na katiba ya Zanzibar.

Kwa mujibu wa katiba ya JMT, ya mwaka 1977, Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar. Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani.

Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, inaiita Zanzibar ni nchi, ni moja ya nchi mbili zinazounda JMT!. Kitendo cha katiba ya Zanzibar kuuita Zanzibar ni nchi, kinawakanganya Watanzania kudhani kuwa nchi ya Tanganyika ndio pekee iliyokufa ila nchi ya Zanzibar ipo haikufa!.

Naomba niwahakikishie Tanzania ni nchi moja ya JMT, ile nchi inayotajwa na katiba ya Zanzibar kuwa ni nchi ya Zanzibar, sii kweli kuwa Zanzibar ni nchi, bali ni jina tuu, hayo mabadiliko ya katiba ya Zanzibar kujiita nchi, ni kwaajili ya Zanzibar tuu, lakini mabadiliko hayo hayatambuliwi na katiba ya JMT.

Kwa vile Rais Samia, anakwenda kutupatia katiba mpya, hili pia litarekebishwa, na kwa maoni yangu, dawa pekee na ya kudumu ya kuondoa kero zote za muungano, ni kwenda kwenye serikali moja!.

P
 
Hawa jamaa itikadi zao na infiriolity complex waliokuwa nayo, Pasco, serikali moja haitawezekana
 
katiba ya JMT, na katiba ya Zanzibar, yenye serikali mbili, serikali ya JMT na serikali ya Zanzibar, SMZ, yenye marais wawili, rais wa JMT na rais wa Zanzibar.
Hapo naona Kuna raisi wa muungano wa Tanganyika na Zanzibar na raisi wa Zanzibar je Yuko wapo raisi wa Tanganyika????
 
Baada ya muungano, nchi zote mbili zilitoweka, hakuna nchi ya Tanganyika, wala nchi ya Zanzibar, kilichopo ni nchi moja tuu ya Tanzania!. Zanzibar sio nchi!.
Zanzibar sio nchi?? Em nenda ukawaulize wapemba kama Zanzibar ni nchi au ni Nini
Uwasikie watasemaje.
 
Back
Top Bottom