Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 64,960
- 111,265
Inawezekana vipi mabadiliko ya kisiasa Tanzania kutokea kabla ya muundo wa muungano kushugulikiwa?
Kwa tabaka tawala na state machinery suala la muungano ni kufa na kupona, kwao haiyumkiniki muungano kuvunjika kwa hiyo hata kama wangekuwa wanademokrasia vya kutosha wakubali ushindi wa upinzani suala la muungano linakuwa shida kubwa zaidi kwa sababu CHADEMA kinaweza kushinda Tanganyika ila Zanzibar hakiwezi kushinda, uwepo wa vyama tofauti madarakani Tanganyika na Zanzibar itakuwa msumari wa mwisho kwenye jeneza la muungano.
Katika hali itawezekanaje watawala ndani na nje ya CCM bara na visiwani kukubali chama chochote cha upinzani kushinda?!