Muungano unatutafuna! Iweje bara Umeme uwe shilingi 350 kwa unit wakati Zanzibar ni shilingi 130?

Chande anaposema watumiaji wengi wa umeme wanalipia kuanzia 33% mpaka 50% ya matumizi ya umeme anataka kusema nini?
Alikuwa anajibu maswali katika mazungumzo marefu. Ukitafuta kwenye Twitter ya Kumekucha utayapata yote.

Jaribu Clubhouse na Twitter. Ile ya Twitter ilikuwa more succinct.


Sitaki kumuwekea maneno mdomoni. Maharage Chande alijitahidi sana kusema ukweli, lakini kwa heshima na diplomasia isiyovunjia heshima uongozi wa nchi, wa sasa na uliopita.

Ukweli ni kwamba, mfumo wetu wa kijamaa umeshindwa. Na pengine si Ujamaa wenyewe, ni utekelezaji wetu.

Tunataka wananchi walipe umeme kwa bei ya chini ambayo haiwezi kuendesha shirika, halafu umeme ukiwa hautoshi, unakatika, shirika linashindwa kuongeza mitambo, linahitaji ruzuku sana serikalini, tunalalamika.

Naelewa hoja ya kijamaa ya kufanya umeme uwe "public good", na kufanya umme uwe bei ya chini kwa watu.

Mpango huu unaweza kufanikiwa kama hawa watu wanainuliwa kiuchumi eventually waweze kulipa umeme kwa bei halisi, sio kila siku wabebwe tu. Au kama mnataka kuwabeba watu, kuwe na maendeleo makubwa ya viwanda, watumiaji wa umeme wa kawaida wasaidiwe na viwanda vikubwa. Nchi nyingi zinafanya hivi, hata za kibepari. Nafikiri hata Marekani sehemu nyingi wanafanya hivi.

Lakini, sisi tatizo letu, kwanza hatuinui watu kiuchumi vya kutosha, hivyo wanaobebwa kwa kupewa bei za chini ni wengi, na wanazidi kuongezeka mwaka hadi mwaka. Wanaoondoka kwenye umasikini na kuingia tariffs za juu ni wachache kitakwimu.

Pili, hata tukitaka kufanya viwanda vibebe mzigo, viwanda vyenyewe ni vichache, nchi imekuwa ya ku import kila kitu, na hata hivyo vichache, haya matatizo ya umeme na maji yanavifanya vipunguze zaidi uzalishaji, katika vicious cycle ya "upungufu wa umeme unasababisha upungufu wa uzalishaji, upungufu wa uzalishaji unasababisha upungufu wa ulipaji wa umeme, ambao unasababisha upungufu wa bajeti ya TANESCO kushughulikia tatizo la upungufu wa umeme".

Hivyo, TANESCO, licha ya kuwa monopoly, inategeme aruzuku. Kwa sababu watu hawalipi market price/ production cost. Wanaobebwa hawapungui, ndiyo kwanza wanazidi. Viwanda vya kusaidia kuwabeba hawa watumiaji masikini navyo vinapungua au kupunguz auzalishaji.

There is no free lunch, at some point someone has to pay.

Serikali haina mkakati. Yani serikali siyo tu inataka free lunch.They want to eat their free lunch and still have it too.

Serikali inaweza kuwa na ajenda ya kisiasa ya kuwapa watu umeme nafuu, au inaweza kuwa na nia ya kumaliza umasikini kwa kuwatoa watu gizani na kuwapa umeme bure.

Lakini, kama haina mkakati wa kuwatoa kwenye umasikini na kuwajengea purchasing power ya kununua umeme kwa bei halisi, tutabaki kuwa na matatizo tu.

Shirika litazidi kuomba ruzuku, serikali yenyewe haina pesa inakwenda kwa mikopo, mitambo itahitaji kutengenezwa.

Hatuwezi kwenda kijamaa jamaa sana katika ulimwengu ambao mitambo inanunuliwa kwa pesa za kigeni.
 
Muungano wa mchongo, tanganyika mikononi mwa wageni. Nani aliyetuloga?.
 
Mbara kupata ajira zanzibar sio rahisi, mbara kupata kiwanja Zanzibar sio kitu rahisi, umeme tunawauzia sisi lkn wao gharama kwa mwananchi ni ndogo kuliko unakotoka, petrol kwao ni bei ya chini sana, sukari nk.
 
 
Aisee?? Mbona huu ni unyonyaji Sasa?... Haiwezekani....
Sio unyonyaji. Ni jukumu letu kuhakikisha Zanzibar haizami. Ni eneo dogo lenye uchimi mdogo na science na technolojia bado hazijaendelea sana. Ukubwa jalala, lazima tuhakikishe Zanzibar haizami. Ikiparaganyika na sisi hatuko salama
 
Yani unakaa unamuamini Maharage?
 
Wacha owongo mchenzi wee! Yaani tangu ujuzi unaleta maada hazina vichwa wala miguu.. Yaani upuuzi mtupu!
 
mm nikinunua wa 2000 napata unit 16:7 umeme wa buku unit 8:
 
Yani unakaa unamuamini Maharage?
Si kwamba namuamini Maharage.

Huu ukweli naujua hata Maharage alivyokuwa shule ya sekondari Azania.

Nilikuwa namsikia Mkuregenzi Mtendaji wa TANESCO wa wakati huo na yeye alisema hivyohivyo.

Kama hujui kwamba umeme wa majumbani Tanzania unauzwa bei ya chini sana kulinganisha na bei halisi, basi una mengi sana ya kujifunza.

Do your research.Kama unabisha, bisha kwa facts and figures.

Linganisha Tanzania na nchi jirani zetu hapa kwenye hii link. Bei ya umeme wa nyumbani Kenya ni mara mbili ya ile ya Tanzania. Nchi zilizotupita kwa unafuu wa umeme karibu zote ni zinazozalisha mafuta.

Na wengine tayari wanaongeza bei za umeme ili kufikia bei za uhalisia kulingana na production cost.


Unaendeleza tabia ya wabongo wengi ya kubisha bila data.

 
Zanzibar(ZECO) yupo Tariff 3-HV kama mteja wa Tanesco na wenzie kina Bulyanhulu Gold Mine na Twiga Cement - TPCC wote wako bei moja/unit

punguzeni malalamiko
Ndiyo sera ya shirika letu la tanesco: masikini na wanyonge kama sisi kutozwa sh 350 kwa unit, matajiri na mabwanyenye sh 130 kwa unit, wafanyakazi wa tanesco sh 000 kwa unit. Wazanzibari wamelistukia hilo, wakalala nalo mbele na kufanikiwa kuwa kundi la sh 130 kwa unit. Wabara nao wanapaswa kupambana kuingizwa tarrif kama ya wazanzibari. Sh 350 per unit ni bei kubwa sana. Ulaya unit moja ni sh 30 tu. Hata tutakapoanza kuuza umeme nje ya nchi, bei haitazidi sh 130 kwa unit.
 
mkuu, ZECO ndiyo inayouziwa 130 per unit, ZECO then inasambaza kwa wananchi za wazanzibar na kuwauzia 480 kwa unit

ikumbukwe kwamba 130 ( nakumbuka ilikua kama 156 miaka ya nyuma ) per unit, ni kwa wateja wa msongo mkubwa wa tanesco (Tariff 3-HV), ikiwemo mgodi Bulyanhulu, kiwanda cha Twiga Cement na ZECO
 
Ukifanya hizi comparisons unaconsider pia uchumi wa hiyo nchi na thamani ya hela yao?
Au ndio ni zile zile za Nape na Vifurushi.

Au bei ya Apple marekani ni shngapi na Tz ni shingapi?

Au Zimbabwe wanauziwa umeme shingapi?
 
Ukifanya hizi comparisons unaconsider pia uchumi wa hiyo nchi na thamani ya hela yao?
Au ndio ni zile zile za Nape na Vifurushi.

Au bei ya Apple marekani ni shngapi na Tz ni shingapi?

Au Zimbabwe wanauziwa umeme shingapi?
Hizo comparison ni kwa standardized currency.

Inaonekana hujasoma hata heading.

"Household electricity prices in Africa as of December 2021, by country(in U.S. dollars per kilowatt hour)"

Vifaa vya kutengeneza umeme vinanunuliwa nje, mostly kwa US dollars.

Kama unaongelea Purchasing Power Parity, you are making a case against yourself.

Kwa sababu, hapo katika nchi chache ambazo zimetushinda kwa unafuu, zenyewe zina Purchasing Power Parity zaidi yetu.

Maana yake ni kwamba, Tanzania ina tatizo zaidi ya bei ndogo ya umeme tu.

Tanzania ina tatizo la bei ndogo ya umeme katika nchi ya watu wasio na uwezo wa kulipia umeme. Wenzetu, hususan wenye mafuta na idadi ndogo za watu, wameweza kuwa nd bei ndogo zaidi hata kama watu wao wana uwezo zaidi. Lakini wengine wasio na mafuta wala idadi ndogo sana ya watu, kama Zimbabwe, ambao wameendekeza kufanya umeme uwe wa bei rahisi sana, wamelazimika kupandisha bei. Inaonekana kupandisha bei ni kitu kisichoepukika, kwa sababu tumekopa kujenga mabwawa, kuna maintenance inahitajika, kuna inflation katika soko la kimataifa.

Bila kuongeza bei ya umeme tutaendelea kuwa na matatizo tu.

Na hapo ndipo ninaposema kwamba, naelewa falsafa ya kufanya umeme uwe public good na kuu subsidize, lakini falsafa hii inabidi itekelezwe kwa mtizamo wa kufanyika kwa muda tu kuwatoa watu katika umasikini, waweze kulipia market rate/ production cost eventually.

Ttaizo letu tunafanya bei iwe ndogo, lakini hatuwaondoi watu kwenye umasikini kama inavyotakiwa.

Worse still, tunazaliana sana na kuongeza watu masikini kuliko uwezo wa kuwahudumia.

Kwa hivyo sioni tunavyoweza kukabiliana na haya matatizo kirahisi.
 
Mkuu,

Ukipigania kila mtu alipe bei ya chini, mitambo ikiharibika ikahitaji kununuliwa mipya at market rate in US dollars, mtanunuaje wakati wote mnagombania kulipia bei ya chini?

Huoni kwamba mnagombania kumkamua maziwa ng'ombe ambaye hamtaki kumlisha?

Kwa nini usipiganie hao wasiolipa inavyotakiwa walipe inavyotakiwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…