Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Alikuwa anajibu maswali katika mazungumzo marefu. Ukitafuta kwenye Twitter ya Kumekucha utayapata yote.Chande anaposema watumiaji wengi wa umeme wanalipia kuanzia 33% mpaka 50% ya matumizi ya umeme anataka kusema nini?
Jaribu Clubhouse na Twitter. Ile ya Twitter ilikuwa more succinct.
#Kumekucha with Maharage Chande, Managing Director, #TANESCO
With Kumekucha Tanzania, Mrusha Jones and 10 others
Sitaki kumuwekea maneno mdomoni. Maharage Chande alijitahidi sana kusema ukweli, lakini kwa heshima na diplomasia isiyovunjia heshima uongozi wa nchi, wa sasa na uliopita.
Ukweli ni kwamba, mfumo wetu wa kijamaa umeshindwa. Na pengine si Ujamaa wenyewe, ni utekelezaji wetu.
Tunataka wananchi walipe umeme kwa bei ya chini ambayo haiwezi kuendesha shirika, halafu umeme ukiwa hautoshi, unakatika, shirika linashindwa kuongeza mitambo, linahitaji ruzuku sana serikalini, tunalalamika.
Naelewa hoja ya kijamaa ya kufanya umeme uwe "public good", na kufanya umme uwe bei ya chini kwa watu.
Mpango huu unaweza kufanikiwa kama hawa watu wanainuliwa kiuchumi eventually waweze kulipa umeme kwa bei halisi, sio kila siku wabebwe tu. Au kama mnataka kuwabeba watu, kuwe na maendeleo makubwa ya viwanda, watumiaji wa umeme wa kawaida wasaidiwe na viwanda vikubwa. Nchi nyingi zinafanya hivi, hata za kibepari. Nafikiri hata Marekani sehemu nyingi wanafanya hivi.
Lakini, sisi tatizo letu, kwanza hatuinui watu kiuchumi vya kutosha, hivyo wanaobebwa kwa kupewa bei za chini ni wengi, na wanazidi kuongezeka mwaka hadi mwaka. Wanaoondoka kwenye umasikini na kuingia tariffs za juu ni wachache kitakwimu.
Pili, hata tukitaka kufanya viwanda vibebe mzigo, viwanda vyenyewe ni vichache, nchi imekuwa ya ku import kila kitu, na hata hivyo vichache, haya matatizo ya umeme na maji yanavifanya vipunguze zaidi uzalishaji, katika vicious cycle ya "upungufu wa umeme unasababisha upungufu wa uzalishaji, upungufu wa uzalishaji unasababisha upungufu wa ulipaji wa umeme, ambao unasababisha upungufu wa bajeti ya TANESCO kushughulikia tatizo la upungufu wa umeme".
Hivyo, TANESCO, licha ya kuwa monopoly, inategeme aruzuku. Kwa sababu watu hawalipi market price/ production cost. Wanaobebwa hawapungui, ndiyo kwanza wanazidi. Viwanda vya kusaidia kuwabeba hawa watumiaji masikini navyo vinapungua au kupunguz auzalishaji.
There is no free lunch, at some point someone has to pay.
Serikali haina mkakati. Yani serikali siyo tu inataka free lunch.They want to eat their free lunch and still have it too.
Serikali inaweza kuwa na ajenda ya kisiasa ya kuwapa watu umeme nafuu, au inaweza kuwa na nia ya kumaliza umasikini kwa kuwatoa watu gizani na kuwapa umeme bure.
Lakini, kama haina mkakati wa kuwatoa kwenye umasikini na kuwajengea purchasing power ya kununua umeme kwa bei halisi, tutabaki kuwa na matatizo tu.
Shirika litazidi kuomba ruzuku, serikali yenyewe haina pesa inakwenda kwa mikopo, mitambo itahitaji kutengenezwa.
Hatuwezi kwenda kijamaa jamaa sana katika ulimwengu ambao mitambo inanunuliwa kwa pesa za kigeni.