Pinda amepinda kweli,maana Hapa mpaka kieleweke. Mmelikoroga kwa kibri na jeuri sasa mtalipa ghali sana.
...........Kama una akili ya kutukana kiasi hiki kwa nini usirushie matusi viongozi wako huko visiwani waliokufikisha hapa, yaani kukubali taifa lako liwe mkoa wa Bara, maana you can jump and cry lakini ukweli unaosimama kisheria ni kwamba nchi yako ni mkoa tu wa bara, na rais wako hana tofauti yoyote na RC, ndio maana hata asipokuwepo kwenye mikutano ya cabinet huwa hasubiriwi kwa sababu rais wa jamhuri hawezi subiri RC,.........
Spika Sitta ni mzushi mwengine ,hivi ni nani aliemuambia kuwa Mzee wa Mikasi ni mwakilishi wa Zanzibar ,jamani naona MiCCM imekuja juu lakini ,mtakufa kifo Nyani au kima.
Kijana Lazaro huna kina hata kimoja unachokijua,usibabaishe na kutaka kuuuficha ukweli ,Mwakiyembe amekosea na amekwenda mbali sana kusema hadharani chuki zake binafsi kwa viongozi wanaoitetea Zanzibar kuwa ni Nchi eti waadhibiwe ati hawana adabu ,eti wamedharau.
Mwakiyembe amechonga fitna ndani ya CCM na ndio mpaka leo CCM hawaelewani,na kama Mwakiyembe na kamati yake kama sio majungu na chuki nini kimefanyika hadi leo.
Mtamtetea sana na nyie mnaomtetea hamumtakii heri huyu jamaa kila mkizidi kumtetea ndio mnamuingiza ndani ya shimo ambalo hataweza kutoka.
Ikiwa Serikali ya Zanzibar itaamua kumshitaki Mwakiyembe kwa kuwaita mwanasheria Mkuu wa Zanzibar na Waziri Shamhuna hawana adabu basi atakuwa matatani ,hao wenzake anaowaona marafiki watamgeukia na hapo ndipo atakapoifahamu chungu ya CCM.
Hivi Ndugu Lazaro kati ya Shamhuna na Mwakiyembe nani alitoa ujeuri na kukosa adabu na kuvuka mipaka ya uzungumzaji.
Napenda kama utakariri aliyosema Shamhuna na aliyosema Mwakiyembe halafu tupime kwa kipimo utakacho wewe.
Hapa usilete mambo ya itifaki kwani hiyo itifaki ni moja ya mambo yasiyokubaliwa na WaZanzibari ,hilo ni katika mipango yenu ya kuimeza Zanzibar.
Makamo wa kwanza haiwakilishi Zanzibar kama inavyosema Hati ya Muungano ila Sitta spika anaesimamia hoja za Chama chake anataka kulilazimisha, haijulikani wazo hilo amelitoa wapi.
Halafu Ndugu Lazaro siku hizi usilete mambo ya Katiba kwani imeshagundulika hiyo Katiba unayoitegemea imetungwa na CCM kwa manufaa yao ,haifai tena tunaweza kusema imekwisha expire tokea kuundwa kwa mfumo wa Vyama vingi ,sasa hao wasomi unaowataja kama watakwambia ukweli basi watakubaliana kuwa Katiba iliyopo haifai hata kunakiliwa katika hoja za siku hizi kwani mambo yamebadilika siku hizi ni kasi na ari mpya sasa utaleta Katiba iliyotungwa kuendeleza Ujamaa ,hayo ni mambo mbali mbali kabisa.
Wameambiwa na kila mtu wabadilishe KATIBA wanasema wakati haujafika, maana CCM haijaondoka madarakani ,ndio maana yake.
Hao MaDr. hawana msimamo ni watu wa kutumiwa tu na wanajali maslahi yao binafsi kwa kuwa wanaposema hivyo watu kama akina Lazaro mnawaona MaDr. wamesema ukweli na mnawapenyezea vijisenti au kuwafagilia, wakati watu hao wanshindwa kuwatetea WaTanzania kwa kuogopa kumhoji Raisi ,kwa kuogopa Kumhoji waziri Mkuu au waziri yeyote yule ,si mnamuona Sitta siku hizi anazima masuali ya papo kwa papo ,wanataka kuiga mambo wakati hawayawezi. Na nyinyi kina Lazaro mnaona hawa ndio viongozi wa kuwategemea.
Yaani mkuki kwa nguluwe au sio ,pale Shamhuna alisema hakuna selikali ya Mseto wala choloko ,akina Mwakiyembe walipiga makofi,sasa inakuwaje leo aombe lazi.tamko rasmi kutoka serikalini SMZ mmelisikia ni majibu kutoka CCM kisiwa ndui Zanzibar(Wahafidhina wakiitaka timu ya Butiama iombe razi)
Jee kuna kipengere kwenye Katiba kinachosema kuwa kumpinga Waziri Mkuu ni KOSA? Na jee Mwakyembe au Bunge linauwezo gani juu ya Shamuhuna na nini adhabu ya"kosa" la Shamuhuna kwa kanuni za Bunge?
Usipoyajibu hayo basi Mwakyembe ni fyongo.
Halafu huyu Mwakiyembe ni mchochezi na hajui maana halisi ya neno Fedheha kwa taifa kama ni fedheha basi Tanzania ilipata fedheha kwa kutoa wakimbizi waliokimbilia shimoni baada ya unyama wa dictator nduli Benyamin kuyapeleka majeshi Zanzibar na kwenda kuuwa na kufanya ushenzi wa kupindukia kule Pemba , mnaoulinda Muungano haya ndio mnayoyaunga mkono na hamna jingine ,kusema Muungano hauna kasoro unafaida zaidi kwa Zanzibar ni kwa haya ya akina Mwakiyembe kusimama kifua mbele kusema Shamhuna kakosa adabu , mwakiyembe amepata mdomo kwa sababu ya kuwazamisha wenziwe na hivyo hapo alipo anatumiliwa tu na muda wake ukiisha atatupwa jalalani kama wengine ,msemo wa Kiswahili husema kila ngoma ivumapo ndipo inapokalibia kupasuka wako wapi magogo ya CCM ambayo yakisifika ,na yakitembea bega kwa bega na Nyerere ,leo hii si tumeona wamepigwa buti kwenye kinyang'anyiro cha Uraisi ,na wengine wowote wale huwa wanatumiliwaga tu ,yupo wapi Mangula ? hata humsikii mtu ambae alikuwa ni mtetezi wa CCM kwa hali na roho,Mwakiyembe fahamu tu Waziri Pinda alishaliona kosa lake na hadi hii leo hakurupuki tena kujibu masuala yanayohusu Muungano ,na kila siku tunasikia Sitta anavyomukinga.Imeonekana Waziri Mkuu hakupata mafunzo ya kujibu masuala ya papo kwa papo kitu ambacho kiongozi wa juu ni lazima akutane na usalama wa Taifa wamfundishe namna ya kujibu.
Mimi Mwiba kama suala aliloulizwa Pinda ningeulizwa basi ningelijibu kwa ufasaha kabisa tena kwa maneno mafupi na watu wa pande zote mbili wangeliridhika.
Ila Muheshimiwa Pinda ameteleza na hili halina mjadala ,hasa ukiichukulia maana ya kuteleza.
Wana JF
Ninavyoona mimi Hoja za mwakyembe hazina mashiko hata kidogo, kama sikumnukuu vibaya amesema kuwa ilikuwa shamhuna afikirie dhana ya collective responsibility na asipinge kauli ya PM Mizengo Pinda ,OKAY. Sasa hapa ninapata kigugumizi..... collective responsibility ipi aliyoikusudia Harison Mwakyembe kwa sababu kama ni utendaji wa Baraza la Mawaziri Shamhuna hahusiki na baraza la mawaziri la T/bara au pengine kuna mantiki mengine yaliyiojificha. ......... Sijui, lakini nafikiri kama Mwakyembe hataki kuelewa mipaka ya kiutendaji kati ya SMZ/ SMT/bunge/ baraza la wawakilishi hio ni kasoro kubwa akiwa yeye ni mwanasherisa wa kuheshimika.
La pili, Kwa mtazamo wa haraka hoja hii ya znz ninchi, wilaya au handeni, biharamulo, haipewi nguvu si tu ndani ya bunge au kwenye vyombo vya habari. Inaonekena wazi wazi kuwa Spika anamlinda PM pinda asijibu hoja yoyote ile inayohusiana na sakata hii. Kwa nini? Hapana jawabu ya mkato lakini ni mkakati tu wa SMT(Serikali ya Muungano) kukandamiza uhuru wa mawazo kwa wabunge wetu kule bungeni. Je hili Mwanasheria Mwakiyembe ameliona na kulikemea ?????
Ukifuatilia ktk media za bara, utaona kuwa vyombo vyote vya habari haviko objective and neutral katika kuielezea sakata hii ya znz ikielekea kuwa ni wilaya ya handeni / babati. Wahariri wanaendeleza ajenda ya kutulaumu sisi wazanzibari eti hatutaki muungano na hawataki kuandika makala za kiuchambuzi ambazo zingeeleza mambo mengine ambayo yako nje ya boksi na hayapewi nafasi.
Lililobaki, ni sisi wananchi kuja na activism ya hali ya juu na tuoneshe wazi kuwa hatutaki muungano kabisa na sio tu ufanyiwe marekebishao. Wanasiasa wamejitahidi na wanaendelea kujitahidi kuunda jukwaa la kueleza maoni yao na inapasa tuwaunge mkono kwa juhudi zao.
wewe Kila Kitu "shamhuna Hiki" "shamhuna Hivi" "shamhuna Vile". Au Wewe Ndiyo Shamhuna Mwenyewe?? Unaboa Sana Aisee!
1.
Mkuu heshima yako kwanza, in the future jaribu kuelewa hoja kwanza kabla hujakurupuka, hoja yangu ni kwamba kwenye katiba yetu ya Jamhuri cheo cha Deputy Prime Minister hakipo, hii ni fact sio opinion yangu,
However: Toka tupate uhuru kumekuwa na tabia kutoka kwa baadhi ya viongozi wetu wakuu kujaribu kuwabembeleza wapambe wao kwa kulazimisha kuwepo hiyo nafasi temporaly, kwa mfano:-
1. kiongozi wa kwanza kufanya hivyo alikuwa ni Mwalimu, alipoona Salim amekataliwa kuwa rais, akamtengenezea hiki cheo ili kumfariji kwa the expense of us wananchi.
2. Wa pili alikuwa Malecela, akiwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza Wa Rais, alipoona Mrema anakuwa threat kwenye mbio za kugomeba urais wa 1995, akamtengenezea hii nafasi ili kumshawishi apunguze mbio za urais.
3. Na this time naye Muungwana, baada ya kuona Shamuhuna amekosa umakamu wa rais, naye akamtengenezea hako ka-nafasi kumfariji.
Ahsante Mkuu.