Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Jinsi hii thread ilivyoandikwa kwa munkari, inaifanya kuwa biased na kuonyesha chuki binafsi na siasa za MAJITAKA ( Kitchen sink politics)
 
Now I do confirm that "light travels faster than sound.....until you hear them speak".Ha,ha,haaa!
 
The ishu hapa sio what Mwakyembe amesema au hakusema, tatizo hapa ni Muungano na matatizo yake, na huku muafaka, sisi bara we could care less kama hivi vyote viwili vipo au havipo,

Kama una akili ya kutukana kiasi hiki kwa nini usirushie matusi viongozi wako huko visiwani waliokufikisha hapa, yaani kukubali taifa lako liwe mkoa wa Bara, maana you can jump and cry lakini ukweli unaosimama kisheria ni kwamba nchi yako ni mkoa tu wa bara, na rais wako hana tofauti yoyote na RC, ndio maana hata asipokuwepo kwenye mikutano ya cabinet huwa hasubiriwi kwa sababu rais wa jamhuri hawezi subiri RC,

Hatuipendi sana hiii lugha lakini ni wewe mwenyewe unai-provoke na maneno yako ya ubara na uvisiwani, yaani untaka na sisi bara tuanze kutanganza kwenye radio na TV ya taifa maneno ya kuwaomba watoto wasichezee mchanga wa mbele ya nyumba ya Mzee Jang'ombe kama huko kwenu? na viongozi kuanza kuitana kwenye madirisha huko Ikulu kama vile wako mtaaani?

Huko visiwani mnahitaji ku-grow up! sisi Bara tunaondoka hivyo hatuna muda wa kuwasubiri kwanza mpaka mbebane kwenye mikokoteni!
 
Mkuu FMES

Hapa mbavu sina umemkoma nyani Giladi na sifikirii kama atarudi, Du! ubarikiwe tu hizi dana dana nyingine hazina hata mkia.
 
SASA NIMEELEWA, NILIDHANI NAJIBIZANA NA MWIBA, KUMBE MWIBA HUYO NINAYEDHANIA NI MTU NI KITENGO CHA PROPAGANDA CHA CUF NA MJAHIDINA. MIMI SIENDELEI TENA. HAPA HAKUNA HOJA, HAKUNA MANTIKI WALA HAKUNA MAUDHUI - NI CHUKI BINAFSI TUPU NA UDINI. HATUTAFIKA, KWAHERINI! Lazaros
 
...........Kama una akili ya kutukana kiasi hiki kwa nini usirushie matusi viongozi wako huko visiwani waliokufikisha hapa, yaani kukubali taifa lako liwe mkoa wa Bara, maana you can jump and cry lakini ukweli unaosimama kisheria ni kwamba nchi yako ni mkoa tu wa bara, na rais wako hana tofauti yoyote na RC, ndio maana hata asipokuwepo kwenye mikutano ya cabinet huwa hasubiriwi kwa sababu rais wa jamhuri hawezi subiri RC,.........

asta.............Mkuu pole pole mkuu.......hapo hapo inatosha mkuu......maana unaua.........duuh
 
Spika Sitta ni mzushi mwengine ,hivi ni nani aliemuambia kuwa Mzee wa Mikasi ni mwakilishi wa Zanzibar ,jamani naona MiCCM imekuja juu lakini ,mtakufa kifo Nyani au kima.
Kijana Lazaro huna kina hata kimoja unachokijua,usibabaishe na kutaka kuuuficha ukweli ,Mwakiyembe amekosea na amekwenda mbali sana kusema hadharani chuki zake binafsi kwa viongozi wanaoitetea Zanzibar kuwa ni Nchi eti waadhibiwe ati hawana adabu ,eti wamedharau.
Mwakiyembe amechonga fitna ndani ya CCM na ndio mpaka leo CCM hawaelewani,na kama Mwakiyembe na kamati yake kama sio majungu na chuki nini kimefanyika hadi leo.
Mtamtetea sana na nyie mnaomtetea hamumtakii heri huyu jamaa kila mkizidi kumtetea ndio mnamuingiza ndani ya shimo ambalo hataweza kutoka.
Ikiwa Serikali ya Zanzibar itaamua kumshitaki Mwakiyembe kwa kuwaita mwanasheria Mkuu wa Zanzibar na Waziri Shamhuna hawana adabu basi atakuwa matatani ,hao wenzake anaowaona marafiki watamgeukia na hapo ndipo atakapoifahamu chungu ya CCM.
Hivi Ndugu Lazaro kati ya Shamhuna na Mwakiyembe nani alitoa ujeuri na kukosa adabu na kuvuka mipaka ya uzungumzaji.
Napenda kama utakariri aliyosema Shamhuna na aliyosema Mwakiyembe halafu tupime kwa kipimo utakacho wewe.
Hapa usilete mambo ya itifaki kwani hiyo itifaki ni moja ya mambo yasiyokubaliwa na WaZanzibari ,hilo ni katika mipango yenu ya kuimeza Zanzibar.
Makamo wa kwanza haiwakilishi Zanzibar kama inavyosema Hati ya Muungano ila Sitta spika anaesimamia hoja za Chama chake anataka kulilazimisha, haijulikani wazo hilo amelitoa wapi.
Halafu Ndugu Lazaro siku hizi usilete mambo ya Katiba kwani imeshagundulika hiyo Katiba unayoitegemea imetungwa na CCM kwa manufaa yao ,haifai tena tunaweza kusema imekwisha expire tokea kuundwa kwa mfumo wa Vyama vingi ,sasa hao wasomi unaowataja kama watakwambia ukweli basi watakubaliana kuwa Katiba iliyopo haifai hata kunakiliwa katika hoja za siku hizi kwani mambo yamebadilika siku hizi ni kasi na ari mpya sasa utaleta Katiba iliyotungwa kuendeleza Ujamaa ,hayo ni mambo mbali mbali kabisa.
Wameambiwa na kila mtu wabadilishe KATIBA wanasema wakati haujafika, maana CCM haijaondoka madarakani ,ndio maana yake.
Hao MaDr. hawana msimamo ni watu wa kutumiwa tu na wanajali maslahi yao binafsi kwa kuwa wanaposema hivyo watu kama akina Lazaro mnawaona MaDr. wamesema ukweli na mnawapenyezea vijisenti au kuwafagilia, wakati watu hao wanshindwa kuwatetea WaTanzania kwa kuogopa kumhoji Raisi ,kwa kuogopa Kumhoji waziri Mkuu au waziri yeyote yule ,si mnamuona Sitta siku hizi anazima masuali ya papo kwa papo ,wanataka kuiga mambo wakati hawayawezi. Na nyinyi kina Lazaro mnaona hawa ndio viongozi wa kuwategemea.


Sema sema sema !!!!! kaka usiposema tutajuaje ulivyo, tutathibitishaje kuwa hata watu wa dini fulani wakiwa wasomi bado elimu haiwasaidii!!!! sema kaka ili uwe wa mfano humu JF wote tukiwa na akili walimu na viongozi watapatikana vipi??
 
Yaani mkuki kwa nguluwe au sio ,pale Shamhuna alisema hakuna selikali ya Mseto wala choloko ,akina Mwakiyembe walipiga makofi,sasa inakuwaje leo aombe lazi.tamko rasmi kutoka serikalini SMZ mmelisikia ni majibu kutoka CCM kisiwa ndui Zanzibar(Wahafidhina wakiitaka timu ya Butiama iombe razi)

Jee kuna kipengere kwenye Katiba kinachosema kuwa kumpinga Waziri Mkuu ni KOSA? Na jee Mwakyembe au Bunge linauwezo gani juu ya Shamuhuna na nini adhabu ya"kosa" la Shamuhuna kwa kanuni za Bunge?
Usipoyajibu hayo basi Mwakyembe ni fyongo.

Halafu huyu Mwakiyembe ni mchochezi na hajui maana halisi ya neno Fedheha kwa taifa kama ni fedheha basi Tanzania ilipata fedheha kwa kutoa wakimbizi waliokimbilia shimoni baada ya unyama wa dictator nduli Benyamin kuyapeleka majeshi Zanzibar na kwenda kuuwa na kufanya ushenzi wa kupindukia kule Pemba , mnaoulinda Muungano haya ndio mnayoyaunga mkono na hamna jingine ,kusema Muungano hauna kasoro unafaida zaidi kwa Zanzibar ni kwa haya ya akina Mwakiyembe kusimama kifua mbele kusema Shamhuna kakosa adabu , mwakiyembe amepata mdomo kwa sababu ya kuwazamisha wenziwe na hivyo hapo alipo anatumiliwa tu na muda wake ukiisha atatupwa jalalani kama wengine ,msemo wa Kiswahili husema kila ngoma ivumapo ndipo inapokalibia kupasuka wako wapi magogo ya CCM ambayo yakisifika ,na yakitembea bega kwa bega na Nyerere ,leo hii si tumeona wamepigwa buti kwenye kinyang'anyiro cha Uraisi ,na wengine wowote wale huwa wanatumiliwaga tu ,yupo wapi Mangula ? hata humsikii mtu ambae alikuwa ni mtetezi wa CCM kwa hali na roho,Mwakiyembe fahamu tu Waziri Pinda alishaliona kosa lake na hadi hii leo hakurupuki tena kujibu masuala yanayohusu Muungano ,na kila siku tunasikia Sitta anavyomukinga.Imeonekana Waziri Mkuu hakupata mafunzo ya kujibu masuala ya papo kwa papo kitu ambacho kiongozi wa juu ni lazima akutane na usalama wa Taifa wamfundishe namna ya kujibu.
Mimi Mwiba kama suala aliloulizwa Pinda ningeulizwa basi ningelijibu kwa ufasaha kabisa tena kwa maneno mafupi na watu wa pande zote mbili wangeliridhika.
Ila Muheshimiwa Pinda ameteleza na hili halina mjadala ,hasa ukiichukulia maana ya kuteleza.

Wana JF
Ninavyoona mimi Hoja za mwakyembe hazina mashiko hata kidogo, kama sikumnukuu vibaya amesema kuwa ilikuwa shamhuna afikirie dhana ya collective responsibility na asipinge kauli ya PM Mizengo Pinda ,OKAY. Sasa hapa ninapata kigugumizi..... collective responsibility ipi aliyoikusudia Harison Mwakyembe kwa sababu kama ni utendaji wa Baraza la Mawaziri Shamhuna hahusiki na baraza la mawaziri la T/bara au pengine kuna mantiki mengine yaliyiojificha. ......... Sijui, lakini nafikiri kama Mwakyembe hataki kuelewa mipaka ya kiutendaji kati ya SMZ/ SMT/bunge/ baraza la wawakilishi hio ni kasoro kubwa akiwa yeye ni mwanasherisa wa kuheshimika.

La pili, Kwa mtazamo wa haraka hoja hii ya znz ninchi, wilaya au handeni, biharamulo, haipewi nguvu si tu ndani ya bunge au kwenye vyombo vya habari. Inaonekena wazi wazi kuwa Spika anamlinda PM pinda asijibu hoja yoyote ile inayohusiana na sakata hii. Kwa nini? Hapana jawabu ya mkato lakini ni mkakati tu wa SMT(Serikali ya Muungano) kukandamiza uhuru wa mawazo kwa wabunge wetu kule bungeni. Je hili Mwanasheria Mwakiyembe ameliona na kulikemea ?????

Ukifuatilia ktk media za bara, utaona kuwa vyombo vyote vya habari haviko objective and neutral katika kuielezea sakata hii ya znz ikielekea kuwa ni wilaya ya handeni / babati. Wahariri wanaendeleza ajenda ya kutulaumu sisi wazanzibari eti hatutaki muungano na hawataki kuandika makala za kiuchambuzi ambazo zingeeleza mambo mengine ambayo yako nje ya boksi na hayapewi nafasi.

Lililobaki, ni sisi wananchi kuja na activism ya hali ya juu na tuoneshe wazi kuwa hatutaki muungano kabisa na sio tu ufanyiwe marekebishao. Wanasiasa wamejitahidi na wanaendelea kujitahidi kuunda jukwaa la kueleza maoni yao na inapasa tuwaunge mkono kwa juhudi zao.

Haya yote yangekuwa kuzungumzia umaskini Zanzibar,miundo mbinu mibovu,elimu duni, makazi duni, umeme, hospitali, maji n. tungekuwa mbali sana.Great mind discuss idea.Awe Mwakyembe amekosea awe hajakosea mambo yote ya muungano yana maswali ambayo kuyajibu kwake ni kuvunja muungano.wakati wenzetu ulaya wanaungana Afrika wanagawanyika.JAMANI TUJIONEE HURUMA NCHI YETU IMO KATIKA NCHI ZINAZOONGOZA KWA UMASKINI.KUMBUKENI NYERERE ALISEMA TUKIVUNJA MUUNGANO HUKO VISIWANI NA NYIE LAZIMA MGAWANYIKE. BARA WATAKUWA STABLE.

BADALA YA MWIBA KUFIKIRI MJINASUE KWENYE HALI MLIYONAYO WEWE UNAPIGA KELELE NA MWAKYEMBE HAYA...WAKATI WENZENU WANAWAZA KUFUNGUA SHULE WEWE UNAHIMIZA MADRASA!!!!

MIAKA YOTE HII TANGU 60s Mwiba unagundua leo kuwa muungano una matatizo, mwakyembe amekosea POLE SANA!!!!!!!!!!!!!
 
Watu wenye nguvu nyingi sana za kiuchumi duniani( Ulaya) wanaungana.
Sisi watu duni wa mawazo na tulio nyuma kiuchumi tunataka kugawana vipande vya ardhi ili kila mtu awe Sultan.

Hoja ya msingi inayopelekea Wazanzibari kulalama imefichama kwenye imani yao na asili ya kundi fulani la watu huko visiwani.

Muungano una matatizo hakuna anayebisha, lakini wenzetu wanang'ang'ania suluhisho la namna moja tu.

Mkifanikiwa kuachana na wanabara mtaanza kuwasaka wazanzibara wote visiwani na kuwatimua, wazanzibara wakimalizika wanguja wataambiwa damu yao nao si ya asili ya huko, wanguja wakiisha wapemba wataambiwa kwao ni somalia kismayu, wapemba wakiisha watabakia waarabu wenye damu ya asili ya Omani.

Mwendo huo mie nauita "kwenda Kisengere nyuma" kama Kifulukombe.
 
It is obvious to me that the ill-equipped Shamhuna is either a hopeless zealot, almost Zionistic in nature, or positing himself to be flung into a higher office.It is obvious that Mwakyembe is one of the "Defenders of The Faith" stressing on collective responsibility, a concept I doubt Shamhuna knows the smell of, let alone its intricacies, philosophy and history.

Like a Catholic Cardinal or a Swiss Guard, Mwakyembe faithfully lays down the rules and reminds jokers that you cannot be against your own government. If you do not believe in the leadership of the pontiff and the Pontifex Maximus you cannot be Catholic by definition.Anybody seeing this position as contradictory to his Lowassa indictments misses the important fact that he was acting in a capacity as a Chairman of a presidential Commitee.

While this does not mean he was right in all aspects of his prosecution, if not persecution, of Lowassa, it clearly disqualifies the analogy presented by Mkuu Mwiba.

The big question is, with Shamhuna being a hazy but aspiring pawn in SMZ, is he bound to the concept of collective responsibility to the Union Government?

When the central question is Zanzibari autonomy, this becomes a vicious cycle of two arguments.

Shamhuna believes, or forwards the impression anyway, that Zanzibar is sovereign [sic], Mwakyembe obviously does not subscribe to that.Mwakyembe's criticism is inherently self serving and insufficient as he is imposing collective responsibility on a person disputing the legality of the stated status quo without addressing the facts of the disputed hierarchy.

I call on the article(s) of the Union and their possible ratifications, What are the facts?
 
Kwi kwi kwi chi chi chi!!! heri mimi njomba nisiseme kitu kwenye hii thread.
 
Pundit, there you are! This is the right kind of interaction we need, sober, sound and articulate - not the diatribe we are subjected to by people suffering from paranoia like Mkuu Mwiba and company who see in Dr. Mwakyembe a devil incarnate simply because he did a historical wonderful job of showing Lowassa the door. Wengine tutaendelea kumheshimu kwa hilo, aendelee kufanya hivyo tena na tena!
The question you raise here is pertinent: are the Shamhunas bound by collective ministerial responsibility to the Union Government? My answe is in the affirmative, YES, on grounds which Dr. Mwakyembe may not necessarily subscribe to. I wish he comes forward to elaborate his position as we are doing here.
Let me begin by saying that although the constitutional set up in Tanzania provides for a central government and a regional government for Zanzibar (Wazanzibari msiniue kwa kutumia neno regional, hiyo ni lugha ya kikatiba isiyo na maana ya mkoa), that set-up does not make the system confederal in which the regional government "alone operates directly" upon Zanzibaris. The situation we have is that the central government also operates directly upon Zanzibaris on matters singled out as "union" by the Union Constitution, hence the federal element in the set-up. It is this interactive nature of government operations in Tanzania and Zanzibar in particular which makes the two governments not mutually exclusive, contrary to Shamhuna's thinking.
Wananchi wa Zanzibar wanajua kuwa wanaunda Serikali mbili zinazowahusu moja kwa moja na zenye madaraka tofauti. Hivyo basi Katiba inaweka mazingira kuhakikisha kuwa wananchi hawapewi maagizo yanayokinzana; hawapelekewi ujumbe unaotofautiana na serikali hizi mbili! Hence, Articles 6,8(1)(c),8(2),47(1)(a),126 - 128 etc of the Union Constitution.
Nitoe mfano wa Art.6 inasema: "Katika Sehemu hii ya sura hii, isipokuwa kama maelezo yahitaji vinginevyo neno "Serikali" maana yake ni pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar..." Art.8(1)(c) nayo inasema:"Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo Serikali itawajibika kwa wananchi".
Hivi akina Shamhuna wanadhani wanawajibika kwa wananchi gani? Wanawajibika kwa wananchi wa Zanzibar kupitia wawakilishi wao walioko Baraza la Wawakilishi na walioko Bunge la Jamhuri ya Muungano! Wawakilishi wa wapigakura wa Zanzibar walioko Bungeni hushiriki katika mchakato wa uteuzi wa Waziri Mkuu. Hivyo Pinda ni waziri Mkuu wa Wazanzibari na Waziri Mkuu wa Watanzania bara! Shamhuna akimtia kidole machoni, anawatia kidole machoni wananchi wake waliomchangua hata yeye kuingia BLW!
Let me end here by thinking aloud on one other aspect. Hivi Shamhuna akija bara, anadhani kwa nini anapokewa kwa ving'ora vya Serikali ya Jamhuri ya Muungano (pamoja na kwamba nafasi yake haiko hata kwenye Katiba ya Zanzibar)? Kwa nini mawaziri wa Zanzibar wakitembelea Tanzania Bara wanatetemekewa na vyombo vya Muungano? It is simply because they are part of the Union set-up, broadly thinking
Nilimsoma juzi Dk. Mwakyembe kwenye gazeti la The African akisema kuwa Katiba imempa Waziri Mkuu madaraka makubwa ya kuwaongoza mawaziri wote wa Jamhuri ya Muungano. Sasa akina Shamhuna hawajui kuwa wanawapa taabu sana mawaziri wenzao kuwapokea wakija bara kutokana na wao kuonyesha kiburi cha kipuuzi kabisa kwa mtu aliyewazidi madaraka?
Niwaombe Wabunge wetu waendelee kuhoji kila kitu kwa uwazi na ukweli. Mambo ya kufichaficha na kuoneana aibu hayatusaidii. Akina Mwakyembe endeleeni na kazi hiyo, hata kama mtatukanwa na akina Mwiba. Ningependa mhoji faida ya kuendelea na structure hii ya Muungano wakati Wazanzibari (akiwemo Karume mwenyewe, ingawa anawatumia akina Shamhuna) waziwazi wanaonyesha hawataki. Hawasemi moja kwa moja kutokana na unafiki na ubabaishaji walionao viongozi tulionao. Siku moja nakumbuka Shamhuna alitamka: "Muungano gani mnauongelea, hivi nyie watu wa bara hamuioni bahari?" Kazi tunayo!
 
Inabidi wakuu wa nchi wakubali kurekebisha kasoro zilizopo. Acheni ubabaishaji bwana. Kama yamewashinda, tuambieni kuliko mara hivi mara vile. Usanii mtupu.
 
Wazanzibar tunawabembeleza mno, waacheni waende zao, kama hawataki waache malumbano na bara waseme wazi. Waziri mkuu amenukuu katiba kwamba Zenj sio nchi, sasa wanataka aseme nchi wakati aliapa kuilinda katiba? Acheni ubabaishaji. Basi semeni katiba ifanyiwe marekebisho ili zanzibar iwe nchi kwa mujibu wa katiba na sio kulalamika kwa mambo yasiyo na msingi. mbona wabara wamepoteza Tanganyika yao na hawalalamiki. Ina maana nyie Zanzibar yenu ni muhimu sana kuliko Tanganyika yetu_
 
Mkumbuke nyie Wazenj bila Muungano mnaoubeza kwa sasa mziki wa Pemba kutaka kujitenga hamtaweza kuuzima. Muwe makini sana msije juta baadae.
 
Tutabaki kulumbana na akina Shamhuna wakati tatizo hasa ni namna RAIS wa Zanzibar anavyopatikana. Sote tumekuwepo na tumeshuhudia jinsi chaguzi za Zanzibar zimekuwa na utata mwingi tangu mwaka 1990.
Kwa jinsi Karume alivyoupata Uraisi, mtu mwenye AKILI timamu hawezi kusema kuwa Zanzibar ni NCHI! Hawa aloowateua wanaelekea KUSAHAU na kuendelea kuropokaropoka tu. Tukiacha uchaguzi HURU ufanyike Zanzibar, wote hawa kesho yake wataihama Zanzibar.
 
1.

Mkuu heshima yako kwanza, in the future jaribu kuelewa hoja kwanza kabla hujakurupuka, hoja yangu ni kwamba kwenye katiba yetu ya Jamhuri cheo cha Deputy Prime Minister hakipo, hii ni fact sio opinion yangu,

However: Toka tupate uhuru kumekuwa na tabia kutoka kwa baadhi ya viongozi wetu wakuu kujaribu kuwabembeleza wapambe wao kwa kulazimisha kuwepo hiyo nafasi temporaly, kwa mfano:-

1. kiongozi wa kwanza kufanya hivyo alikuwa ni Mwalimu, alipoona Salim amekataliwa kuwa rais, akamtengenezea hiki cheo ili kumfariji kwa the expense of us wananchi.

2. Wa pili alikuwa Malecela, akiwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza Wa Rais, alipoona Mrema anakuwa threat kwenye mbio za kugomeba urais wa 1995, akamtengenezea hii nafasi ili kumshawishi apunguze mbio za urais.

3. Na this time naye Muungwana, baada ya kuona Shamuhuna amekosa umakamu wa rais, naye akamtengenezea hako ka-nafasi kumfariji.

Ahsante Mkuu.

Mkuu mwenzangu kwa hapa sikukurupuka kwani ulichosema wewe ni kuwa ni matakwa ya Karume tu kutengeneza nafasi iliyo nje ya katiba kwa makusudi ya Shamuhuna. Nashukuru kuwa umeeleza mwenyewe kuwa kitendo hichi kilishafanywa kabla na hivyo Karume alikuwa akifuata na wala sio utashi wake.
 
Back
Top Bottom