WEWE ni mjuzi hebu naomba nieleze Waziri Mkuu atatoka wapi na atafanya kazi gani ? Tafadhali usinyofoe sehemu za Katiba na badala yake chukuwa Katiba nzima. Sasa nasubiri wewe muelewa ili nithibitishe mark ya100 unayostahiki.

Sasa amii kama ni hivyo si ukasome katiba yote wewe mwenyewe? naona Nyerere alikupa ilim bure na unaweza kuisoma!

Na kama huijui kwanini una jadili kitu husichokijua?
 

Samahani, Mkuu lakini heri ungeandika kwa kiswahili maana hii lugha uliyoitumia ni ngumu kidogo! Ushauri tu!
 

Nasemaje kama wa kulaumiwa ni viongozi wako na sio upiga kelele kwani wao si wanalijuwa hili sasa kwa nini wasichukue hatua kama ni kosa? Mbona Jumbe walimchukulia hatuwa?

Msichofahamu wenzangu kuwa huu Muungano hauko wazi sasa kwanini usijadiliwe na kuuweka sawa kama inawezekana na ispowezekana na uende arijojo kama ulivyokwenda Ujamaa.
Nafikiri wenzetu mnatupinga kwa sababu ya Utanganyika na Uzanzibari tu lakini bila shaka mmeshabaini kuwa kuna kasoro nyingi zinazotaka kufanyiwa kazi na sio kuweka viraka.
 
1. walichosema Zanzibar ni mfumo wa ulinzi sio jeshi .
2. Pinda ni Waziri Mkuu wa Tanganyika na mambo ya Muungano sio Waziri Mkuu wa Zanzibar na hilo limeshathibitishwa na serikali ya Zanzibar yenyewe.


We Ami waziri mkuu wa Tanganyika ndo nani tena? Nchi gani hiyo inaitwa Tanganyika? Au ulikuwa na maana ya mkoa wa Tanga?. Na hakuna aliyesema Pinda ni waziri mkuu wa Zanzibar.

Duh kaazi kweli kweli ami

Sijakuelewa ami
 
Tatizo lako roho yako ina pepo wa ubaya . Ivo wewe unajiringia kuwa Muisrael nafikiri Watanganyika ni watu wasiopenda dhuluma. Pengine wewe ni exceptional.

Ngekewa,

Uelewa ...uelewa amii. Waisrael waliporudi kwao waliwakuta Wapalestine wapo pale wameshajiendeleza sana kiuchumi na kwa kila kitu. Wao wakaanza from zero. Wapalestine wao wakajibweteka tu wenzao wakawa wanafanya kazi kwa bidii sana.....

Miaka kama sitina na baadaye (leo) wapalestina wamezidiwa mara mamilioni na Israel na wanatawaliwa.

Acheni kubweteka na kukaa MASKANI na kunywa gahawa na halua. DO something!
 

Ni ufinyu wa mawanzo kuipima nchi kwa population na area. Ivo kuna daraja ngapi za nchi hapa duniani na hupimwa na nyenzo gani. Mbona kuishiwa kwa hoja kunakufanya uonekane kama si wale mnaojitapa kwa elimu? Hivyo hapo mlipoamuwa kuungana mlifanya hesabu ya watu na ukubwa wa ardhi na kuutiya kwenye Katiba na sio Tanganyika na Zanziba?
 
Ngekewa, unaweza kusoma sana shule za darasani na USIELIMIKE.

Ni exposure tu ya mambo ndo inasaidia.

Yale maswali yamekushinda. Pole sana nitamuuliza mwanangu anaesoma darasa la nne changanyikeni primary school, kisha nitakupa majibu yake kesho au leo jioni.
 

Nimeshakujibu na badala yake nimekupa wewe suala ambalo lingesibitisha ualimu wako bado hujanijibu. Nafikiri mwalimu usiniache kwa kukuuliza masuala nawe ndio nami nazidi kupata hako kashule nilichokikosa.
 
Sasa amii kama ni hivyo si ukasome katiba yote wewe mwenyewe? naona Nyerere alikupa ilim bure na unaweza kuisoma!

Na kama huijui kwanini una jadili kitu husichokijua?

AIsee Brother, wacha kuniacha njiani, ivo darasa lako haliwezi kujibu masuala bali kuuliza tu ? Umwalimu wa namna gani wewe na unategemea mimi mwanafunzi wako nitakuwa vipi?
 
Mh. Zitto,

Kwa maoni yangu, maswala ya muungano yanahitajika kuelezewa kwa kutumia current, active act or consitution as ammended from time to time.

Haya mambo ya kusema article za association, sijui sheria ya mwaka 1965... they are misleading! kwa kuwa kuna mengi yamebadilika na kwa kufuta sheria ile ya 2/3 Zanzibar na Bara.

Nasema hivyo kwa sababu... article of association mimi naziona kama MOU ambazo zinakuwa zinafanya kati mpaka pale tu ambapo sheria husika itakuwa enacted... sheria ikishakuwa enacted ... MOUs etc zinakufanya natural death.

Kwa maana hiyo basi, sio sahihi kuletewa quote yoyote ambayo sio sheria ambayo ni uptodate...

Otherwise wazanzibar wataturudisha kwenye Article of Association ambako... ndio kama vile tunajadili kuungana... hizi zilikufaya pale katiba ya muungano ilivyotungwa na kutumika... na katiba inayotumika kwa sasa ni ile ya latest version with ammendments.

Pia nina uhakika hakuna siku katiba ya muungano ilibadiliswa bila kuhusisha Zanzibar... hata makamu wa pili alivyoondolewa kuwa Rais wa Zanzibar ... walihusika na walipitisha...

Kuna viongozi ambao majukumu yao yamewashinda na sasa wanatafuta agenda za 2010 election.
 

Oh my GOD. Kaka akili zote hizo kumbe ziko katika kuketua mahesabu tu? Eti Wapalestina walibweteka? Hivi unajua kweli historia ya kuanzishwa kwa nchi ya Israel katika 73 ya iliyokuwa ardhi ya taifa la Palestina? Hivi kweli unajua hata kuanzishwa kwake na madhila yaliyowapata wapalestina katika kuanzishwa, Kuendelezwa na hata kulindwa kwa Taifa la Palestina?

Hivi unajua utajiri wa wapalestina ulimwenguni?

Kwa kweli ndugu yangu umenitisha sana na muono finyu ulionao katika suala la Palestine-Israel......

Fikiria kuwa una nyumba yako halafu anakuja mtu anayedai kuwa alikuwepo hapo mika 2000 iliyopita na anachukua asilimia 73 ya nyumba yako hiyo na ukipinga anaendelea kuchukua zaidi na zaidi na hata kufikia kukuzungushia wigo kuzunguka vijieneo viwili mlivyojazana wewe na familia yako ambao. Halafu anatumia huo wigo uhakikisha kuwa kila kiingiacho na kitokacho ni lazima kipate ruhusa yake. Kumbuka bado anahitaji watoto wako wamfanyie kazi ngumu kwa ujira kiduchu. Halafu baadae anakuja anakudhihaki kuwa umasikini wako ni kwa sababu wewe ni mzembe umebweteka....

Yaani kama vile mafisadi wetu wanaofikia jeuri ya kusema tuache kupiga soga (yaani kupinga ufisadi wao) ili tuendelee wakati UFISADI wao ni chanzo kikuu cha kuzungukwa na umasikini tulionao......

Fikiria, tafiti na elimika kabla ya kujenga taswira....

Tanzanianjema
 
AIsee Brother, wacha kuniacha njiani, ivo darasa lako haliwezi kujibu masuala bali kuuliza tu ? Umwalimu wa namna gani wewe na unategemea mimi mwanafunzi wako nitakuwa vipi?

Ningependa sana nikujibu "mwana funzi" wangu. Ila umeniwekea condition, unanifanya nisiwe huru (independent) ndo maana nikasema bora ukajisomee mwenyewe.

Hivi Ngekewa, Tanzania Bara tunafaidika na nini hasa kiuchumi (sio kisiasa kwa kuogopa msije danganywa na Uarabuni) kutoka kwenu?
 

Huyo Karume ana bytime hivi sasa.Unafikiri atasema nini wakati amewekwa na ccm bara! Ulitegemea aseme zanzibar si nchi! Naona patakuwa hapatoshi huko visiwani.
 
Mh. Zitto,

Pia nina uhakika hakuna siku katiba ya muungano ilibadiliswa bila kuhusisha Zanzibar... hata makamu wa pili alivyoondolewa kuwa Rais wa Zanzibar ... walihusika na walipitisha....

Uhakika huu unatokana na kuwa ulikuwepo wakati bunge linapitisha hilo ama umepitia handsard ya kikao hiko?

Tanzanianjema
 

Tanzania njema. Nashukuru. Unahaki kuandika utakalo na kufikiri kuwa unavyofikiri ndo sahihi HULIPII KODI kuandika unavyofikiri.

Nami naomba nifikiri (silipii kodi), nauliza swali: Nina nyumba yangu, huyo mtu anapokuja anaingiaje wakati milango nimefunga (nipo makini)?

Pili nina kiwanja changu jamaa wameniomba niwagawie robo (usiniambie waisrael walirudi wengi kuliko wa Pelestina; itakuwa kicheko cha mwaka) nimewapa robo ya kiwanja changu; inakuwaje baada ya miaka 60 hawa wageni wananizidi mimi ardhi, utajiri na nguvu?

Ngugu yangu utake usitake ukweli unabakia kuwa wapelestine wamebweteka sana Mtoto akizaliwa (wengi wao) wanapelekwa madrassa na kuambiwa adui yako ni Israel.......Je hiyo itawaendeleza kweli? kwanini wasiwapeleke formal school?. - Elimu inadidimia hapo. Ndo kujibweteka huko.

Natanguliza shukrani kwa majibu
 
Ubavu Anao Au Hataki Kurejea 2010?

Haya mtumeni wa kumtuma akaadhibu viongozi wa Zanzibar ,kama Mtandao wa Kikwete haukupigwa na chini na kubaki kutumbilia macho kiti cha Uraisi.
Viongozi wa Zanzibar au wahafidhina wanaweza kuwambia lolote waliopo serikali ya Muungano ,maana Zanzibar Block votes ni kama veto kwa kumpata mgombea wa Uraisi wa Tanzania .je hamuoni kama Zanzibar nayo ipo juu ya Serikali ya Muungano ,ichambueni kwa kina sehemu hiyo na vipi kunapotokea kivumbi ndqani ya mchakato wa kumpata mgombea wa CCM ,ndio nikasema Muungano umekwisha.
 
Sorry nilisahau.

Hata Wazanzibar pia wana utajiri mkubwa tu huku bara na wengine ukitaka kuwajua vizuri wamejilipua wengi tu Uingereza!
 
Huyo Karume ana bytime hivi sasa.Unafikiri atasema nini wakati amewekwa na ccm bara! Ulitegemea aseme zanzibar si nchi! Naona patakuwa hapatoshi huko visiwani.

Kwa nini yeye aseme wakati ana wakumsemea.......hata bila ya kutumwa....

Karume kwake yeye hii ni gear ya kumblackmail JK asilazimishe ajenda yake ya serikali ya mseto. Ofcourse with a presure from mafashisti na maafisadi wake wanaojiita wahafidhina.

CUF kwao ni muendelezo wa ajenda yao ya "ukombozi wa zanzibar" na kuhakikisha wanatengeneza mazingira ya "state of urgency" wakitegemea CCM watalazimika kucompromise na pia kuongeza ombwe la mahusiano kati ya CCM-Tanganyika na CCM/ASP Zanzibar.

Mwisho wa siku kitakachopatikana ni mauaji ya kimbari yanayonukia......

Tanzanianjema
 


Aisee naona hutakii mema nchi hii. Hakuna mauaji ya kimbari yatakayotokea.
 
Uhakika huu unatokana na kuwa ulikuwepo wakati bunge linapitisha hilo ama umepitia handsard ya kikao hiko?

Tanzanianjema

Tanzanianjema,

Acha kuwatusi waZanzibar, hakuna hata siku moja ambapo kiongozi wa Zanzibar awe waziri, Rais au hata wajumbe wa baraza la wawakilishi aliwahi kusema kuna kifungu cha katiba kibadilishwa kinyemela.

Ambalo linawezekana ni aidha waliwahi kupiga kura bila kujua wanapigia kura kitu gani?... hili ni jambo la kawaida hata pale Dodoma.

Lakini hakuna hata kiongozi mmoja ambaye amewahi kusema katiba imebadilishwa kinyemela, na wewe pia unajua vizuri sana kwamba serikali ya jamhuri haina maslahi yoyote ya kufanya hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…