Kaka kodi unalipia sana ingawa utaalamu wako hutumika sana katika kusaidia waajiri/wawekezaji/wachukuaji wetu kutolipia.....

Mimi nina imani na kichwa chako na pia natambua kuwa siasa wala historia sio profession yako. Hata hivyo haitakuwa vibaya kujisomea zaidi kuhusiana na masuala haya.

Naamini ukifungua kichwa chako, ukajiuliza, ukatafiti na ukajielimisha kuhusiana na suala la Palestine-Israel utang'amua mengi na kukusaidia kujua facts......

Tanzanianjema
 
Sorry nilisahau.

Hata Wazanzibar pia wana utajiri mkubwa tu huku bara na wengine ukitaka kuwajua vizuri wamejilipua wengi tu Uingereza!


Fairplayer,

Tuliza munkari, thread iliyoko mbele yetu inahitaji kuelimishana zaidi kuliko kitu chochote.

Alafu acha kuweka mifano ya Israel na Palestina... itatufikisha mbali mkuu wangu.
 
Kasheshe,

kweli.

Tanzania Njema,
Asante. Tujadiliane kuhusu hili sehemu nyingine. Acha nibaki na msimamo wangu na wewe ubaki na wako kuhusu hili suala la Palestine-Israel. Maswali yako nimekujibu nadhani.

Asante

Fairplayer
 
Sorry,

By the way tulikuwa tunatoka nje ya mada.

Tuendelee,

Tanzania njema, Mizengo Pinda na Shamsi Vuai nani yupo juu ya mwingine? na je Zanzibar wana majeshi ya ulinzi?
 

Hivi mimi ninayekuuliza unapopata uhakika wako na wewe unayedai kuwa kuwa wazanzibariwaliwahi kupiga kura bila kujua wanapigia kura kitu gani?... hili ni jambo la kawaida hata pale Dodoma, nani anayewatusi ndugu zangu wanaotoka visiwa vya zanzibar?

Kutosema wakati ule haina maana kuwa halijafanyika na haina maana kuwa hawajalisema pembeni. Na una uhakika gani kuwa hawakulisema hilo? hukumbuki kuwa wakati huo hakukuwa na live broadcasting na hata printing media haikuwa kama ilivyo sasa.......

Tanzanianjema
 
5) Without prejudice to the application of the Constitution
of Zanzibar in accordance with this Constitution concerning all
matters pertaining to Tanzania Zanzibar which are not Union
Matters

HAYO NDIO YALIYOTANGULIA NAWE UNAJARIBU KUYAACHA


Tunaelemishana tu... ngoja nikupe lingine hapa!

Serikali ya Muungano imekuwa inatekeleza nia yake ya ku-empower local government kuhakikisha zinajiamulia mambo mengi zaidi.

Mfano...
Elimu ya Msingi hadi ya Sekondari itaratibiwa na Halmashauri... kama ilivyo kule Zanzibar.

Elimu ya Juu ni Mambo ya Muungano (hivyo mkoa ya Tanzania na Zanzibar ziko at per)

Mambo ya Kilimo yataratibiwa na Serikali za Mitaa.

Kama ilivyo mambo ya kilimo kule Zanzibar inayaratibu.

Mambo ya maji etc. the same.

Lakini pamoja na yote haya hizi serikali za mitaa (local government) they will never claim kwamba ni independent states... hapana..
 
Aisee naona hutakii mema nchi hii. Hakuna mauaji ya kimbari yatakayotokea.

Well kama unapoona mtoto anachezea kibiriti karibu na mtungi wa gezi ukasema kuwa nyumba inaelekea kuwaka moto ni kutotakia mema wenye nyumba basi kwa hilo utanisamehe lakini sitaacha kusema.

Kwa tunaofuatilia siasa na hali ilivyo Zanzibar wa miaka mingi kuna kila aina ya dalili na uwezekano wa mauaji ya kimbari kutokea haswa katika kisiwa cha unguja. Yapo makundi na hata watu binafsi ambao wapo tayari kwa kutekeleza hilo mara tu itakapowezekana. Wapo wanaotoka ndani ya Zanzibar lakini pia wapo wali nje ya Zanzibar wakiwa tayari kutekeleza hilo. Usiniulize kina nani lakini tambua hilo. Zanzibar is ripe for genocide...........as there are all signs and structures ready for such.......

Tatizo kaka kile uendapo visiwani huko unaenda kama mtalii kujivinjari na huchukui hatua za kuchunguza hli ya mambo kule......

Kumbuka kuwa hiyo haotakuwa mara ya kwanza.....

tanzanianjema
 

Du kumbe live coverage ndio kigezo cha kuhusishwa watu! nimechoka... kumbuka wanaotakiwa kuhusishwa ni wajumbe wa baraza la mapinduzi ambao wakati huo wanakuwa kwenye hilo baraza, hawahitaji live coverage.

Kuona live au kwenye magazeti ni mazungumzo baada ya habari.

No more comments
 
Kasheshe,

kweli.

Tanzania Njema,
Asante. Tujadiliane kuhusu hili sehemu nyingine. Acha nibaki na msimamo wangu na wewe ubaki na wako kuhusu hili suala la Palestine-Israel. Maswali yako nimekujibu nadhani.

Asante

Fairplayer

Haina haja ya kuwa na msimamo, ni suala la mtazamo na ukweli wa mambo na sio prejudices zilizojengeka kutokana na propaganda za wenye nguvu dhidi ya wanyonge....

Huwezi kuchukua kinachoitwa habari kuhusu CHADEMA kutoka katika RAI ya MAFISADI ama MAJIRA ya MTANZANIA fisadi na kuchukua msimamo kuhusu kile kiitwacho "madhambi" ya CHADEMA.....

Alamsik kaka

Tanzanianjema
 


Suala la makamu wa rais wa jamhuri ya muungano ni suala la Bunge la Tanzania na sio baraza la wawakilishi wa watu wa Zanzibar.....na linahitaji robo tatu ya kura za wabunge kutoka Zanzibar kitu ambacho hakikufanyika na hata records zinaonyesha hivyo.....tabia ya kudharau vitu tunavyoona vidogo kama hivyo ndio hufikisha mataifa mengi pabaya......

Tanzaninjema
 

Ngekewa,

Usitafune mawe hapa! Kama Wazanzibari wameuchoka Muungano kwa nini wasijitoe? mbona mwanyoosha vidole ati?

Kama mmedhulumiwa na kudhalilishwa, kinaashinda nini kuamka sikumja na kusema Muungano sasa basi na kutoa talaka? kwa nini ubabaishaji wa maneno?
 
Zitto,
Mkuu maelezo yako ni mazuri na yanalingana na asili ya Muungano kama ulivyosema lakini kuna mambo ambayo nataka kuyazungumzia hapa...
Kama kweli Waziri mkuu hana madaraka na Mawaziri wa Visiwani inakuwaje Waziri wa Visiwani amjibu PM ktk swala ambalo halimhusu yeye ama wizara yake..
Nasema hivi kwa sababu swali aliloulizwa waziri mkuu liliulizwa na Mbunge wa Jamhuri ya Muungano! Katika bunge ambalo hata wawakilishi kutoka Zanzibar walikuwepo ikiwa na maana swali zima lilihusu Muungano.

Mkuu hata Chuo Kikuu hapo Mlimani kuna vitengo na inawezekana kabisa Profesa wa kitengo fulkani hana madaraka ktk kitengo kingine lakini inapofikia swali linalohusu Chuo kizima na swali likaelekezwa kwa mmoja wa Maprofesa kuhusiana na Kitengo ambacho wao wanafikiri hahusiani nacho ni UNAFIKI fulani kwa sababu Wa Zanzibar pengine walifahamu nini litakuwa jibu la huyo kiongozi...
Sasa tazama basi turudi kwenye issue nzima hii.. Ikiwa kweli Zanzibar ni nchi na Wao wenyewe wamesema Tanganyika ndio sio nchi inakuwaje vitu vyote walivyosema kama ni sababu ya kuifanya Zanzibar kuwa nchi Vipo Bara pia!..I Mean kama Bara ingekuwa sio nchi basi ingekuwa na upoungufu wa vitu ambavyo Zanzibar wanavyo kama walivyozungumza..
Hivyo basi ikiwa kuwepo kwa vitu hivyo bara khakuifanyi kuwa nchi inakuwaje vitu hivyo hivyo viifanye Zanzibar kuwa nchi!..
Binafsi naamini kabisa kuwa Kama Zanzibar ni nchi basi hata Bara ni nchi na kama hakuna Zanzibar vilevile hakuna Bara. Yaliyotokea yote ni utaratibu tu wa kiutawala ili kuweka mipaka ya ki territorial ambayo Bara pamoja na ukubwa wake bado ina mamlaka sawa na Zanzibar ktk Muungano.
Shamhuna amekosea sana kumjibu PM wetu hasa kwa kusema hana Madaraka Zanzibar kwa sababu Ya mabaduiliko makubwa yaliyopitishwa ktk mfumo mzima wa Uongozi nchini. Kwa jinsi majibu ya Shmhuna yalivyotolewa ni sawa kabuisa na kupinga kuwepo kwa hoja ya Zanzibar ktk bunge la Muungano..Jambo ambalo binafsi linanifanya nijiulize hao Wabunge wa Zanzibar huwa wanafanya nini Dodoma ktk Bunge ambalo linaongozwa kikatiba na PM wa bara!
PM ambaye hawahusu!
 
Kiboko yenu katika mambo haya ni CUF ,kwa jinsi nionavyo CUF hivi sasa imetulia inajaribu kutafuta kulikoni ?
Ila wakiibuka safari hii mtasikia mliyokuwa hamjawi kuyasikia na mtakaa midomo wazi na hizi valange valange.
Sera ya CUF ni serikali tatu ,hilo halina mjadala ni jambo linaloeleweka au sio ?
Sasa chukulia CUF imetwaa madaraka Zanzibar na sera yao ni serikali Tatu na imesajili sera yake hiyo na kukubaliwa na msajili wa Vyama,CUF imesikika ikisema kama Raisi wa Zanzibar atatokana na CUF basi hatoingia kwenye vikao vya Serikali ya Muungano au kwenye baraza la mawaziri kama raisi asiena wizara maalum ,hilo hawatolikubali hata sekunde moja , kwa maana hiyo watataka Raisi wa Zanzibar awe ni makamo wa kwanza wa Raisi wa Muungano ,kumbuka sera ni serikali tatu ,hivyo Tanganyika itabidi iwepo ni kitu cha lazima , kwa ulimbo huo Tanganyika itarudi na Zanzibar itarudisha hadhi yake ya Kitaifa na Kimataifa ,malumbano yanayokwenda hivi sasa kati ya serikali ya Muungano na serikali ya Zanzibar yanaashiria ushindi kwa CUF ,fahamu kwamba serikali ya Zanzibar inatume yake ya Uchaguzi unaohusika na Uchaguzi wa huko, malumbano tumekwenda nayo mpaka inafikia siku ya uchaguzi wahafidhina wataweza kuikomoa timu ya Butiama vile vile wataweza kuikosesha ushindi CCM kwa upande wa Zanzibar kukiwa na nia ya kuikomboa Zanzibar ,hivyo ni lazima CUF waachiwe ushindi wa che ili kuzidi kuiweka matatani timu ya Butiama na hapo ndipo itakapokuwa mwisho wa mafisadi ,ndio nikasema Kikwete hana ubavu wa kupinga wanalolitaka wahafidhina na huyo Mwakiyembe huenda akaonywa na kupigwa na chini. Ili CCM ibakie madarakani maisha inawalazimu timu ya Butiama iridhie kila linalotakiwa na timu ya wahafidhina ,hivyo Serikali ya Kikwete japo inajilabu kuwa na hapa mnaisifia eti ipo juu ,kuna mambo inabidi iiname ili kupata cha uvunguni ,Sijui mmenifahamu ?
 
Unajua kwa mfumo wa sasa na jinsi CCM ilivyo, Uraisi wa Zanzibar hauna maana yeyote kama NEC na CC zitakaa na kumshurtisha unless aamue kuvunja Muungano.

Huku kudinda kwa Karume, Shamhuna na wengine wafanyie kelele Serikalini wakifika katika chama, kende zitasinyaa. Sasa hapo ndipo mujiulize ni nani mwenye nguvu!
 

Tunapingana lakini penye point na ukweli nakubali.

Salute mkuu kwa hii post
 
Sasa kule Butima ni kina nani walisinyaa mitako ? Wacha kusema maneno yasio na maana ule msemo wa kiswaili usemao ukinyooshea kidole kimoja kwa mwenzako kuna vingine vitatu vinakuelekea wewe mwenyewe ,sasa huko butiama ndio hivyo tena.
 

Reverend,

You are spot on.

This Zanzibar issue is being unduly procrastinated. CMM walijijengea utamaduni mbaya wa "Zidumu fikra", ndani ya mikutano yao hawawezi kuambiana haya waziwazi, wanaogopana. Angalau siku hizi kuna baadhi wamegundua njia, wanatoa japo machozi. Hata huku kwenye kadamnasi pia hawana uwezo wa kutamkiana waziwazi, wanapindisha maneno na kuzunguka mbuyu. Sasa wanamalizana magazetini.

Ukifuatialia mjadala huu utagundua akina nani ni wa Tanganyika, muungano kwao sio kipaumbele. Tatizo ni hao wanaotaka kujitoa. Badala ya kujenga hoja zilizo wazi, wanaanza kiuchokozi. Mtu makini angegundua kwamba Muungano hauna mvuto kwa Watanganyika, ni mzigo, na hivyo angeibuka na hoja makini, zisizojiumauma, zinazoeleweka badala ya kuanza kwa kunyea kambi. Hakuna mtu anayependa hewa chafu na kudharauliana.

Unguja na Pemba wanaonekana wameungana katika hili. Unguja ni CCM, Pemba ni CUF. Tegemeo la CCM ni bara. CCM Unguja wanajichimbia kaburi, bila ubavu wa bara hawana kitu... wamesahu hilo, wao wako "busy" wakichafua hewa. Ndiposa watakapojikuta wamegalagazwa na CUF ikichukua ushindi wake iliodhurumiwa tangu zamani. Hapo ndio penye... sipati picha.

Kuna kitu Wazanzibar wamegundua kwenye muungano...they were fixed, bahati mbaya hawana upeo wa namna ya kukitatua, ndio sababu ya hewa kuchafuka namna hii. I feel sorry for them, tuwasaidie, tuwaachie Zanzibari yao.
 


Mbona mzee unaniweka juu namna hiyo? Zenji nikienda ni kusalimia marafiki tu, Kutalii wapi na wapi mie?.

Najua kuwa sio mara ya kwanza. Ila tunaomba Mungu aepushilie mbali!
 
Hapa ni Referendum tu, suala kubwa kama hili halihitaji maamuzi ya chama ya kukaa kwenye meza kula kuku na kutia saini, ni suala la wananchi. Suala hili lirudishwe kwa wananchi wa bara na visiwani waamue muungano ama la.
 
Hapa ni Referendum tu, suala kubwa kama hili halihitaji maamuzi ya chama ya kukaa kwenye meza kula kuku na kutia saini, ni suala la wananchi. Suala hili lirudishwe kwa wananchi wa bara na visiwani waamue muungano ama la.

Sorry lakini unaonekana kama mfanyakazi mkongwe serikalini, maamuzi ya tuunde tume, tuwarudishie wananchi, yaani unatoa general statement isiyotoa suluhu.

Samahani ni mtazamo tu naweza kukosea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…