omarilyas
JF-Expert Member
- Jan 24, 2007
- 2,130
- 150
Tanzania njema. Nashukuru. Unahaki kuandika utakalo na kufikiri kuwa unavyofikiri ndo sahihi HULIPII KODI kuandika unavyofikiri.
Nami naomba nifikiri (silipii kodi), nauliza swali: Nina nyumba yangu, huyo mtu anapokuja anaingiaje wakati milango nimefunga (nipo makini)?
Pili nina kiwanja changu jamaa wameniomba niwagawie robo (usiniambie waisrael walirudi wengi kuliko wa Pelestina; itakuwa kicheko cha mwaka) nimewapa robo ya kiwanja changu; inakuwaje baada ya miaka 60 hawa wageni wananizidi mimi ardhi, utajiri na nguvu?
Ngugu yangu utake usitake ukweli unabakia kuwa wapelestine wamebweteka sana Mtoto akizaliwa (wengi wao) wanapelekwa madrassa na kuambiwa adui yako ni Israel.......Je hiyo itawaendeleza kweli? kwanini wasiwapeleke formal school?. - Elimu inadidimia hapo. Ndo kujibweteka huko.
Natanguliza shukrani kwa majibu
Kaka kodi unalipia sana ingawa utaalamu wako hutumika sana katika kusaidia waajiri/wawekezaji/wachukuaji wetu kutolipia.....
Mimi nina imani na kichwa chako na pia natambua kuwa siasa wala historia sio profession yako. Hata hivyo haitakuwa vibaya kujisomea zaidi kuhusiana na masuala haya.
Naamini ukifungua kichwa chako, ukajiuliza, ukatafiti na ukajielimisha kuhusiana na suala la Palestine-Israel utang'amua mengi na kukusaidia kujua facts......
Tanzanianjema