Masatu said:Jamani mbona jazba? haya ni mawazo ya mtu mmoja tu naona yanachukiwa kama ndio msimamamo wa kila Mzanzibar kupelekea wengine kuanza kunyosha chuki zao siji tumewachoka, wabaguzi, wanachagua hewa nk.
Jamani mbona jazba? haya ni mawazo ya mtu mmoja tu naona yanachukiwa kama ndio msimamamo wa kila Mzanzibar kupelekea wengine kuanza kunyosha chuki zao siji tumewachoka, wabaguzi, wanachagua hewa nk.
The issue hapa ni kuwa huyu mwakilishi kachemka na kwa kuwa ni mwakilishi kutoka upinzani ( cuf ) one can see the motives as kuvutia wapiga kura na kupata publicity. Huyu ni wa kudharauliwa tuu na kama walivyosema wachangiaji wengine kama wanataka kuanzisha huo mpango wa passport then there should be two way traffic na wao wakija Bara waje na pass na tuende mbele zaidi kuwe na resident permit/work permit vilevile.
Tatizo kubwa la hawa wazanzibara ni ubaguzi tu!
wamekuwa wakibaguana sana kwa misingi ya upemba na uunguja mara uCUF na uCCM. Wameona hiyo haitoshi sasa wanataka sisi twende kwao kwa passport???!!!mbona hawasemi na wao waje kwetu kwa passport???wao wanapenda vya bure tu, kweli hawa mdebwedo wameishiwa sasa wanalazimisha mambo.
Karaha waliyonayo wazanzibara ni ile ya kuwabeba wazanzibari wasio na shukrani. Kila leo wanakuja na demands mpya. Yaani wanawataka wasiende bila karatasi mkononi. Huku wao naishi na kujenga majengo yao huku bara.Sijaelewa Karaha gani mojawapo. Ile ya kulazimishwa kukubali kila kitu au ile ya shida ya Muungano kusababishwa na viongozi walafi wa Visiwani? Ikiwa hii ya pili si kweli kwani hao viongozi wanaojipendekeza kwa Muungano ndio walafi wakitegemea kunufaika na hongo za Bara ili kuzidi kuikandamiza Zanzibar.
Kwa nini mnashindwa kuelewa kuwa Wazanzibari wanataka uhuru wa kujiendeleza na iwapo huo Muungano utabadilika na kuwa na mwelekeo huo basi hakutokuwa na tatizo.
Polls zenyewe zinajisema. Polls zilizohukuliwa Zanzibar zinaonyesha 80% hawataki muungano. Tunalazimishana nini?.
Karaha waliyonayo wazanzibara ni ile ya kuwabeba wazanzibari wasio na shukrani. Kila leo wanakuja na demands mpya. Yaani wanawataka wasiende bila karatasi mkononi. Huku wao naishi na kujenga majengo yao huku bara.
Na kwa taarifa yako muungano wetu unawafaidia zaidi wazanzibarikuliko wazanzibara.
Hata tukivunja ndoa nina hakika kwa asilimia mia moja hatuna hasara hata chembe. Ila wazanzibari lazima wakatane mapanga, maana chuki zao kisiasa kati ya kafu na sisiemu lazima bila sisi wafike huko.
Karaha waliyonayo wazanzibara ni ile ya kuwabeba wazanzibari wasio na shukrani. Kila leo wanakuja na demands mpya. Yaani wanawataka wasiende bila karatasi mkononi. Huku wao naishi na kujenga majengo yao huku bara.
Na kwa taarifa yako muungano wetu unawafaidia zaidi wazanzibarikuliko wazanzibara.
Hata tukivunja ndoa nina hakika kwa asilimia mia moja hatuna hasara hata chembe. Ila wazanzibari lazima wakatane mapanga, maana chuki zao kisiasa kati ya kafu na sisiemu lazima bila sisi wafike huko.
Shabash u sound very good. Ukweli ni kuwa mfumo wa huu Muungano ndio unaohitaji marekebisho. Lazima Tanganyika na vyombo vyake vitolewe katika Vyombo vya Muungano na vitengwe kama vile Zanzibar na vyombo vyake vilivyotengwa. Au vyombo vyote vya Zanzibar lazima viwe "intergrated " katika Vyombo vya Muungano kama vile vyombo vya Tanganyika vilivyokuwa "intergrated". Kinyume cha hayo uliopo sasa ni usanii. Serikali ya Tanganyika haiwezi kuwa ndiyo hiyo hiyo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. It is just as simple as that. Kama wa-tanganyika wa kawaida hata hawana habari na kinachoendelewa Zanzibar- Wazanzibari wa kawaida wana habari tosha na kubinywa na Serikali ya Muungano katika kupata maslahi yao. It is just as simple as that.
Niliwahi kusema huko nyuma tatizo tuliangalia sisi wenywe kwa nini hawa jamaa wakule zanzibar wapo hivyo walivyo mimi binafsi nikagunduwa tatizo lipo kwetu kwa nini nikasema hivyo Tumekuwa tunaonekana tupo DESPERATE na kuwa na hawa watu na hata watowa maoni hapa utangalia wanatowa hayo maoni katika hali inayoonesha hivyo kwa nini leo sisi tusiwe na mawazo kupigania yanayo tuhusu sisi wa bara badala tumekuwa tunangangania na kupigia kelele nini wazanzibar wanataka kukifanya kule kwao ni mamuzi yao na kwaupande wetu tufanye mamuzi yetuWajumbe Zanzibar wataka Wabara watumie pasipoti
Na Ali Suleiman
BAADHI ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamepinga sera ya vitambulisho vya Mzanzibari mkazi na kusema suala hilo linafanywa zaidi kisiasa na kutaka kurudishwa kwa hati ya kusafiri kati ya Tanzania Bara na Zanzibar ambayo iliondoshwa mwaka 1995.
Hayo yalisemwa jana na Waziri Kivuli Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Bw. Abdalla Juma, wakati akisoma maoni ya kambi ya upinzani katika suala la sera ya vitambulisho vya Mzanzibari mkazi.
Alisema haiwezekani Wazanzibari kuitwa wakazi katika nchi yao na kuongeza kwamba vitambulisho hivyo havifai.
"Vitambulisho hivi kwa kweli havifai, sera hii haifai isipitishwe, kwa sababu inaonekana wazi kuwadhalilisha Wazanzibari katika nchi yao," alisema Bw. Abdalla.
Wajumbe wengine wa Baraza walitaka kurudishwa kwa utaratibu wa zamani wa kuwapo hati za usafiri wakati wa kuingia katika visiwa vya Unguja na Pemba.
Mwakilishi wa Magomeni, Bw. Salmin Awadh, alitaka kurudishwa kwa hati za usafiri na kusema kuondoshwa kwake kwa kiasi kikubwa kumesababisha kasi ya ujambazi na uhalifu.
"Tunataka kurudishwa kwa hati za usafiri kati ya Zanzibar na Tanzania Bara...tunataka kuwepo kwa udhibiti katika eneo la bandari pamoja na uwanja wa ndege'alisema Awadh.
awadh alisema sera ya vitambulisho vya uzanzibari ukazi lengo lake ni ulinzi kwa wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba na kuweza kuwatambuwa hasa Wazanzibari na wageni.
mwakilishi wa viti maalumu kutoka katika chama cha wananchi CUF Zakia Omar naye alitaka kurudishwa kwa utaratibu huo ambao alisema ulisaidia sana kudhibiti vitendo vya uhalifu.
alisema kuondoshwa kwa hati za kusafiria kati ya Tanzania Bara na Zanzibar kwa kiasi kikubwa kumerudisha wimbi la vitendo vya uhalifu.
hati ya kusafiri kati ya Tazania Bara na Zanzibar pasipoti iliondolewa katika miaka ya 1995,baada ya kubainika kuwepo kwa vikwazo vya usafiri katika nchi moja ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na kuonekana kwenda kinyume na katiba.
source: majira
Wabara watengwa Z`bar
2008-10-21 10:09:30
Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar
Lile chokochoko la kutaka Zanzibar itambuliwe kama nchi kamili sasa limepiga hatua zaidi baada ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kuwasilisha sera ya vitambulisho vya Mzanzibari mkaazi ikilenga kuwaengua wananchi kutoka Tanzania Bara kuruhusiwa kuajiriwa Zanzibar.
Msimamo huo tata uliwekwa bayana jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ, Suleiman Othman Nyanga, alipokuwa akiwasilisha sera ya vitambulisho vya Mzanzibari mkaazi katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea mjini hapa.
Kwa kauli hiyo, wenye vitambulisho vya Uzanzibari ndio watapewa kipaumbele cha ajira ili kudhibiti nafasi za kazi kuchukuliwa na wageni kutoka nje ya Zanzibar, wakiwamo watu kutokaTanzania Bara.
Waziri Nyanga alisema kwamba waajiri wote katika sekta binafsi watatakiwa na Wizara ya Kazi, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na watoto kuhakikisha wanatoa kipaumbele kwa Wazanzibari kabla ya kuwafikiria watu wengine kutoka nje ya Zanzibar.
``Taasisi zisizokuwa za Serikali zitakuwa na majukumu ya kutumia vitambulisho vya Mzanzibari katika kutoa kipaumbele kwa Wazanzibari katika kutoa ajira, mikopo na misaada ya kimaendeleo,`` alisema Waziri Nyanga.
Alisema kwamba mpango huo endapo utatekelezwa itasaidia vijana wengi wa Kizanzibari kunufaika na ajira na hivyo kufanikisha mpango wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini kwa Wazanzibari.
Alisema kwamba Serikali itahakikisha kila Mzanzibari anasajiliwa na kupatiwa kitambulisho hicho na atatakiwa kutembea nacho wakati wote kama alama ya Mzanzibari.
Aidha, alisema kwamba kitambulisho hicho cha Uzanzibari mkaazi pia kitatumika kutoa kipaumbele kwa Wazanzibari wanaohitaji kunufaika na udhamini wa mikopo ya elimu ya juu kupitia mfuko maalum wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri Nyanga alisema kwamba sera hiyo mpya itahakikisha kwamba inadhibiti uingiaji na utokaji wa watu katika maeneo ya Bandari na Uwanja wa Ndege kwa kutumia vitambulisho vya Mzanzibari mkaazi ili kupunguza tatizo la uhalifu na mmonyoko wa maadili Zanzibar.
Waziri huyo alisema kwamba vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi vitatumika katika ugawaji wa ardhi, viwanja na nyumba za serikali ili kuepusha kupatiwa umiliki wa ardhi kwa watu wasiokuwa na sifa kwa mujibu wa sheria ya Zanzibar.
Aliwaeleza Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwamba watumishi wote wa serikali watalazimika kuonyesha vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi kabla ya kupokea mishahara ili kudhibiti vitendo vya wafanyakazi hewa.
Waziri Nyanga alisema kwamba serikali itahakikisha wanatoa vitambulisho maalum kwa wageni wanaoishi kwa ruhusa maalum za kazi ambayo itafanywa na Ofisi ya Msajili wa vitambulisho Zanzibar.
Alisema kwamba vitambulisho hivyo vimelenga kuimarisha usalama, kulinda haki za kiuchumi na kuongeza kasi ya maendeleo ya jamii kwa wananchi wake.
``Lengo kubwa ni kuwatambua Wazanzibari wote waliopo nchini na shughuli zao kwa lengo la kupanga vyema mipango ya maendeleo,`` alisema Waziri Nyanga.
Alisema kwamba vitambulisho hivyo vitasaidia kuwatambua watu walioko Zanzibar ambao wameingia bila ya kufuata utaratibu na kuhakikisha wananchukuliwa hatua za kisheria.
Alisema miongoni mwa matatizo yaliyojitokeza kutokana na kukosekana kwa vitambulisho vya Mzanzibari ni kushindwa kuthibiti vyema wimbi la uhalifu kutokana na kushindwa kuwatambua wale sugu pamoja na kushindwa kugawanya mapato na rasilimali zake kama vile ardhi kwa ajili ya mashamba, viwanja vya kujenga nyumba na hivyo rasilimali hizo kuangukia mikononi mwa watu wasiohusika kupata haki hizo.
``Kutokana na kushindwa kumtambua nani Mzanzibari, serikali hushindwa kutoa huduma kama vile elimu, matibabu na maji bila ya malipo na hivyo serikali hubeba mzigo mkubwa wa kutoa huduma kwa watu wasio Wazanzibari ambao wangesitahiki kuchangia huduma hizo,`` alisema Waziri Nyanga.
Alisema kwamba kwa msingi huo kitambulisho cha Mzanzibari mkaazi ndiyo kitakachotumika katika utoaji wa ajira na leseni za vyombo vya baharini na angani.
Vilevile, alisema vitambulisho hivyo vitatumika kama alama ya Mzanzibari ndani na nje ya nchi na wale ambao ni wageni watakuwa na sifa ya kupewa vitambulisho hivyo baada ya kuishi Zanzibar kwa miaka kumi na kuomba kupewa Uzanzibari ukaazi kupitia Serikali za Mitaa na baadaye Mkuu wa Wilaya.
Hakuna kosa wazanzibari kudai paasport kwani kila mtu anaangali interest zake. Lazima tukumbuke muungano ni wa nchi mbili. Muungano haukuwa wa kuimeza Zanzibar. Zanzibar ina kila sura ya kuwa ni nchi kwa hivo tunapozungumzia suala la muungano, hatuzngumzi kama zanzibari ni mkoa kama Mara. Sababu ya kero la Muungano ni kuwa wenzetu mumesahau kuwa paliunganishwa nchi sio mikoa.
Matatizo ni kuwa kuanzai 1995 pasi ya kwenda na kurudi iliondoshwa na ujambazi umezidi Zanzibar. Ndani ya wiki mbili zilizopita, watu 13 wameuawa zanzibar hala hao wauwaji wamekimbilia bara na hawajulikani wamepotelea wapi. Ikiwa patakuwa na udhibiti wa aina fulani itakuwa rahisi kuwatafuta wahalifu wanao kimbilia bara au visiwani kujificha.
sasa hivi tuna serikali mbili (yaani ya bara na visiwani) na NIA ni kwenda kwenye serikali moja. Sisi wazanzibari hatuwezi kukubali kupoteza "IDENTITY" yetu. Sisi tuna historia ndefu na kubwa hapa duniani na kuipoteza Zanzibar kwa kisingiio cha muungano ni kama kuwaua wazanzibari wote.
Jengine, muungano wenyewe pia hautambuliki unaanza wapi na unaishia wapi. Hakuna makaratasi ya mikataba kwa ufupi ni USANII mkubwa huu mungano. Mikataba ya kimataifa huwa ina makubaliano halafu wahusika wanatia "seal" au sinature zao. Mkataba wetu ulisainiwa na NANI?. Nyinyi ndugu zangu mumeona waraka wowote ulio tiwa saini ya NYERERE na KARUME?. Hakuna na kwa kuwa hakuna, mumetukalia KIKOLONI.
Munaweza muka very emotional on this issue but remember, FACTS are FACTS. Hayo mengine tunaweza kuyazungumzia lakini tukubalini kuwa koloni la Tanganyika ni Zanzibar.