Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Masatu said:
Jamani mbona jazba? haya ni mawazo ya mtu mmoja tu naona yanachukiwa kama ndio msimamamo wa kila Mzanzibar kupelekea wengine kuanza kunyosha chuki zao siji tumewachoka, wabaguzi, wanachagua hewa nk.

Masatu,

..sidhani kama ni busara kuendelea kupuuza chokochoko kama hizi.

..kama wa-Zanzibari wangekuwa hawakubaliani na hoja za huyo mwakilishi basi ungewasikia[shamhuna,raza,nahodha,..] wakimpinga kwa nguvu zote.
 
Hakuna kosa wazanzibari kudai paasport kwani kila mtu anaangali interest zake. Lazima tukumbuke muungano ni wa nchi mbili. Muungano haukuwa wa kuimeza Zanzibar. Zanzibar ina kila sura ya kuwa ni nchi kwa hivo tunapozungumzia suala la muungano, hatuzngumzi kama zanzibari ni mkoa kama Mara. Sababu ya kero la Muungano ni kuwa wenzetu mumesahau kuwa paliunganishwa nchi sio mikoa.
Matatizo ni kuwa kuanzai 1995 pasi ya kwenda na kurudi iliondoshwa na ujambazi umezidi Zanzibar. Ndani ya wiki mbili zilizopita, watu 13 wameuawa zanzibar hala hao wauwaji wamekimbilia bara na hawajulikani wamepotelea wapi. Ikiwa patakuwa na udhibiti wa aina fulani itakuwa rahisi kuwatafuta wahalifu wanao kimbilia bara au visiwani kujificha.
sasa hivi tuna serikali mbili (yaani ya bara na visiwani) na NIA ni kwenda kwenye serikali moja. Sisi wazanzibari hatuwezi kukubali kupoteza "IDENTITY" yetu. Sisi tuna historia ndefu na kubwa hapa duniani na kuipoteza Zanzibar kwa kisingiio cha muungano ni kama kuwaua wazanzibari wote.
Jengine, muungano wenyewe pia hautambuliki unaanza wapi na unaishia wapi. Hakuna makaratasi ya mikataba kwa ufupi ni USANII mkubwa huu mungano. Mikataba ya kimataifa huwa ina makubaliano halafu wahusika wanatia "seal" au sinature zao. Mkataba wetu ulisainiwa na NANI?. Nyinyi ndugu zangu mumeona waraka wowote ulio tiwa saini ya NYERERE na KARUME?. Hakuna na kwa kuwa hakuna, mumetukalia KIKOLONI.
Munaweza muka very emotional on this issue but remember, FACTS are FACTS. Hayo mengine tunaweza kuyazungumzia lakini tukubalini kuwa koloni la Tanganyika ni Zanzibar.
 
Polls zenyewe zinajisema. Polls zilizohukuliwa Zanzibar zinaonyesha 80% hawataki muungano. Tunalazimishana nini?.
 
Jamani mbona jazba? haya ni mawazo ya mtu mmoja tu naona yanachukiwa kama ndio msimamamo wa kila Mzanzibar kupelekea wengine kuanza kunyosha chuki zao siji tumewachoka, wabaguzi, wanachagua hewa nk.

The issue hapa ni kuwa huyu mwakilishi kachemka na kwa kuwa ni mwakilishi kutoka upinzani ( cuf ) one can see the motives as kuvutia wapiga kura na kupata publicity. Huyu ni wa kudharauliwa tuu na kama walivyosema wachangiaji wengine kama wanataka kuanzisha huo mpango wa passport then there should be two way traffic na wao wakija Bara waje na pass na tuende mbele zaidi kuwe na resident permit/work permit vilevile.

Tafadhali rejea habari na utaona kuwa hii haikuwa kauli ya mwakilishi mmoja bali ni wawili, mmoja kila upande hivyo usilete uCuf wala Uccm. Mwakilishi hakuchemka bali ni mtizamo wa wengi kati ya Wazanzibari kuwa kuingia holela kwa wageni kumesababisha matatizo. Wawakilishi mnaowashutumu wametowa mapendekezo yao ya kutatuwa tatizo na iwapo mpo wenye fikira bora zaidi za hawa Wawakilishi ni heri kuzitowa ili tujenge.
 
Tatizo kubwa la hawa wazanzibara ni ubaguzi tu!
wamekuwa wakibaguana sana kwa misingi ya upemba na uunguja mara uCUF na uCCM. Wameona hiyo haitoshi sasa wanataka sisi twende kwao kwa passport???!!!mbona hawasemi na wao waje kwetu kwa passport???wao wanapenda vya bure tu, kweli hawa mdebwedo wameishiwa sasa wanalazimisha mambo.

Tujaribu kutofautisha UZANZIBARI na sera za vyama...kinachoendelea hapa ni kupigia upatu sera kuu ya CUF. Tunakosea tukisema kuwa huu ni uzanzibari....

Kwani kuwezesha, kutetea na kulinda UFISADI ni utanganyika na sio U-CCM?

Tanzanianjema
 
Sijaelewa Karaha gani mojawapo. Ile ya kulazimishwa kukubali kila kitu au ile ya shida ya Muungano kusababishwa na viongozi walafi wa Visiwani? Ikiwa hii ya pili si kweli kwani hao viongozi wanaojipendekeza kwa Muungano ndio walafi wakitegemea kunufaika na hongo za Bara ili kuzidi kuikandamiza Zanzibar.
Kwa nini mnashindwa kuelewa kuwa Wazanzibari wanataka uhuru wa kujiendeleza na iwapo huo Muungano utabadilika na kuwa na mwelekeo huo basi hakutokuwa na tatizo.
Karaha waliyonayo wazanzibara ni ile ya kuwabeba wazanzibari wasio na shukrani. Kila leo wanakuja na demands mpya. Yaani wanawataka wasiende bila karatasi mkononi. Huku wao naishi na kujenga majengo yao huku bara.
Na kwa taarifa yako muungano wetu unawafaidia zaidi wazanzibarikuliko wazanzibara.
Hata tukivunja ndoa nina hakika kwa asilimia mia moja hatuna hasara hata chembe. Ila wazanzibari lazima wakatane mapanga, maana chuki zao kisiasa kati ya kafu na sisiemu lazima bila sisi wafike huko.
 
Kazi ipo...bahati mbaya huu ni mfano wa muono wa watanganyika walio wengi kuhusiana na muungano na Zanzibar.....

Tanzanianjema
 
Karaha waliyonayo wazanzibara ni ile ya kuwabeba wazanzibari wasio na shukrani. Kila leo wanakuja na demands mpya. Yaani wanawataka wasiende bila karatasi mkononi. Huku wao naishi na kujenga majengo yao huku bara.
Na kwa taarifa yako muungano wetu unawafaidia zaidi wazanzibarikuliko wazanzibara.
Hata tukivunja ndoa nina hakika kwa asilimia mia moja hatuna hasara hata chembe. Ila wazanzibari lazima wakatane mapanga, maana chuki zao kisiasa kati ya kafu na sisiemu lazima bila sisi wafike huko.

Ukiona mwanamke haishi maneno kwenye nyumba basi ujue keshakuchoka.
Utabakia kila siku kusema mwanamke haishi maneno kama hujui ishara za ndoa kuvunjika.

Mwanaume anayeujua unyumba ataamua kutoa talaka ili watengane.

Sisi watanganyika tunashindwa kutoa talaka mpaka tutukanwe hadharani au mwanamke huyo azae mtoto wa nje ya ndoa, ndio tutoe talaka tatu.

Moja ya sera za Seif nikwamba kila mzanzibari awe na passport na apate ruhusa ya kusafiri anakotaka kwenda kama atakubaliwa na nchi anayokwenda.

Sisi watanganyika ukipata pass labda umealikwa nchi za kigeni wakati pass ni haki ya kila raia
 
Shabash u sound very good. Ukweli ni kuwa mfumo wa huu Muungano ndio unaohitaji marekebisho. Lazima Tanganyika na vyombo vyake vitolewe katika Vyombo vya Muungano na vitengwe kama vile Zanzibar na vyombo vyake vilivyotengwa. Au vyombo vyote vya Zanzibar lazima viwe "intergrated " katika Vyombo vya Muungano kama vile vyombo vya Tanganyika vilivyokuwa "intergrated". Kinyume cha hayo uliopo sasa ni usanii. Serikali ya Tanganyika haiwezi kuwa ndiyo hiyo hiyo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. It is just as simple as that. Kama wa-tanganyika wa kawaida hata hawana habari na kinachoendelewa Zanzibar- Wazanzibari wa kawaida wana habari tosha na kubinywa na Serikali ya Muungano katika kupata maslahi yao. It is just as simple as that.

,,,,,,,,yaan ukisema hivyo tu,kesho watakuambia tanganyika wesha ongeza jambo la 23 katika muungano,mimi sijui hata tufanye nini??Manake Bwana Jussa anasema turudi kulee katika mambo 11,embu yacheki hayo mambo yake 11,utaona kama yaliongezeka kutokana na muda na maendeleo,kwani nchi inakua na inaendelea,Mfano ni suala la Elimu ya Juu,Nia ni nzuri kwamba watu wawe na standard moja katika elimu ya juu kama nchi,huwezi kuwa na watu wanaotofautiana ki mitaala,na ukasema wapo katika paa la nchi moja etc.
Ukweli ninao uona mimi ni kwamba,wanasiasa wameiharibu zanzibar sana,watu wote wamekua Brain Washed na hizi Siasa Uchwara,Unapoamua kuingia kwenye Muungano,basi uoneshe nia kweli ya muungano huo,sio unakua UKITIA UKITOA,gharama ya kuendesha serikali ya sehemu ndogo kama hii,inabebwa na Masikini sisi wa zanzibari,Mfano,Katika yale mambo anayo yasema Bwana JUSSA,moja wapo ni Ushuru wa forodha,hilo ilikubaliwa lisimamiwe na muungano,Watawala wetu hawa katika kujitutumua na kuoneshana jeuri,wakaanzisha ya kwao ZRB,wakati TRA ilikuwepo na inatambuliwa toka ktk yalee 11(hata kama ilikua inaitwa Income Tax,by that tym),kodi inayokusanywa na TRA na ZRB ni mzigo,mwisho wa siku wanachi wanaona ni MUUNGANO,Embu tuwe wa kweli jamani,tushachoka na kila siku oooh Muunganoo,ooh Zanzibar tunaonewaaa,tuchague moja tu basi.
 
Wajumbe Zanzibar wataka Wabara watumie pasipoti

Na Ali Suleiman

BAADHI ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamepinga sera ya vitambulisho vya Mzanzibari mkazi na kusema suala hilo linafanywa zaidi kisiasa na kutaka kurudishwa kwa hati ya kusafiri kati ya Tanzania Bara na Zanzibar ambayo iliondoshwa mwaka 1995.

Hayo yalisemwa jana na Waziri Kivuli Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Bw. Abdalla Juma, wakati akisoma maoni ya kambi ya upinzani katika suala la sera ya vitambulisho vya Mzanzibari mkazi.

Alisema haiwezekani Wazanzibari kuitwa wakazi katika nchi yao na kuongeza kwamba vitambulisho hivyo havifai.

"Vitambulisho hivi kwa kweli havifai, sera hii haifai isipitishwe, kwa sababu inaonekana wazi kuwadhalilisha Wazanzibari katika nchi yao," alisema Bw. Abdalla.

Wajumbe wengine wa Baraza walitaka kurudishwa kwa utaratibu wa zamani wa kuwapo hati za usafiri wakati wa kuingia katika visiwa vya Unguja na Pemba.

Mwakilishi wa Magomeni, Bw. Salmin Awadh, alitaka kurudishwa kwa hati za usafiri na kusema kuondoshwa kwake kwa kiasi kikubwa kumesababisha kasi ya ujambazi na uhalifu.

"Tunataka kurudishwa kwa hati za usafiri kati ya Zanzibar na Tanzania Bara...tunataka kuwepo kwa udhibiti katika eneo la bandari pamoja na uwanja wa ndege'alisema Awadh.

awadh alisema sera ya vitambulisho vya uzanzibari ukazi lengo lake ni ulinzi kwa wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba na kuweza kuwatambuwa hasa Wazanzibari na wageni.

mwakilishi wa viti maalumu kutoka katika chama cha wananchi CUF Zakia Omar naye alitaka kurudishwa kwa utaratibu huo ambao alisema ulisaidia sana kudhibiti vitendo vya uhalifu.

alisema kuondoshwa kwa hati za kusafiria kati ya Tanzania Bara na Zanzibar kwa kiasi kikubwa kumerudisha wimbi la vitendo vya uhalifu.

hati ya kusafiri kati ya Tazania Bara na Zanzibar pasipoti iliondolewa katika miaka ya 1995,baada ya kubainika kuwepo kwa vikwazo vya usafiri katika nchi moja ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na kuonekana kwenda kinyume na katiba.

source: majira
Niliwahi kusema huko nyuma tatizo tuliangalia sisi wenywe kwa nini hawa jamaa wakule zanzibar wapo hivyo walivyo mimi binafsi nikagunduwa tatizo lipo kwetu kwa nini nikasema hivyo Tumekuwa tunaonekana tupo DESPERATE na kuwa na hawa watu na hata watowa maoni hapa utangalia wanatowa hayo maoni katika hali inayoonesha hivyo kwa nini leo sisi tusiwe na mawazo kupigania yanayo tuhusu sisi wa bara badala tumekuwa tunangangania na kupigia kelele nini wazanzibar wanataka kukifanya kule kwao ni mamuzi yao na kwaupande wetu tufanye mamuzi yetu
 
Wabara watengwa Z`bar

2008-10-21 10:09:30
Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar

Lile chokochoko la kutaka Zanzibar itambuliwe kama nchi kamili sasa limepiga hatua zaidi baada ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kuwasilisha sera ya vitambulisho vya Mzanzibari mkaazi ikilenga kuwaengua wananchi kutoka Tanzania Bara kuruhusiwa kuajiriwa Zanzibar.

Msimamo huo tata uliwekwa bayana jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ, Suleiman Othman Nyanga, alipokuwa akiwasilisha sera ya vitambulisho vya Mzanzibari mkaazi katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea mjini hapa.

Kwa kauli hiyo, wenye vitambulisho vya Uzanzibari ndio watapewa kipaumbele cha ajira ili kudhibiti nafasi za kazi kuchukuliwa na wageni kutoka nje ya Zanzibar, wakiwamo watu kutokaTanzania Bara.

Waziri Nyanga alisema kwamba waajiri wote katika sekta binafsi watatakiwa na Wizara ya Kazi, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na watoto kuhakikisha wanatoa kipaumbele kwa Wazanzibari kabla ya kuwafikiria watu wengine kutoka nje ya Zanzibar.

``Taasisi zisizokuwa za Serikali zitakuwa na majukumu ya kutumia vitambulisho vya Mzanzibari katika kutoa kipaumbele kwa Wazanzibari katika kutoa ajira, mikopo na misaada ya kimaendeleo,`` alisema Waziri Nyanga.

Alisema kwamba mpango huo endapo utatekelezwa itasaidia vijana wengi wa Kizanzibari kunufaika na ajira na hivyo kufanikisha mpango wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini kwa Wazanzibari.

Alisema kwamba Serikali itahakikisha kila Mzanzibari anasajiliwa na kupatiwa kitambulisho hicho na atatakiwa kutembea nacho wakati wote kama alama ya Mzanzibari.

Aidha, alisema kwamba kitambulisho hicho cha Uzanzibari mkaazi pia kitatumika kutoa kipaumbele kwa Wazanzibari wanaohitaji kunufaika na udhamini wa mikopo ya elimu ya juu kupitia mfuko maalum wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Waziri Nyanga alisema kwamba sera hiyo mpya itahakikisha kwamba inadhibiti uingiaji na utokaji wa watu katika maeneo ya Bandari na Uwanja wa Ndege kwa kutumia vitambulisho vya Mzanzibari mkaazi ili kupunguza tatizo la uhalifu na mmonyoko wa maadili Zanzibar.

Waziri huyo alisema kwamba vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi vitatumika katika ugawaji wa ardhi, viwanja na nyumba za serikali ili kuepusha kupatiwa umiliki wa ardhi kwa watu wasiokuwa na sifa kwa mujibu wa sheria ya Zanzibar.

Aliwaeleza Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwamba watumishi wote wa serikali watalazimika kuonyesha vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi kabla ya kupokea mishahara ili kudhibiti vitendo vya wafanyakazi hewa.

Waziri Nyanga alisema kwamba serikali itahakikisha wanatoa vitambulisho maalum kwa wageni wanaoishi kwa ruhusa maalum za kazi ambayo itafanywa na Ofisi ya Msajili wa vitambulisho Zanzibar.

Alisema kwamba vitambulisho hivyo vimelenga kuimarisha usalama, kulinda haki za kiuchumi na kuongeza kasi ya maendeleo ya jamii kwa wananchi wake.

``Lengo kubwa ni kuwatambua Wazanzibari wote waliopo nchini na shughuli zao kwa lengo la kupanga vyema mipango ya maendeleo,`` alisema Waziri Nyanga.

Alisema kwamba vitambulisho hivyo vitasaidia kuwatambua watu walioko Zanzibar ambao wameingia bila ya kufuata utaratibu na kuhakikisha wananchukuliwa hatua za kisheria.

Alisema miongoni mwa matatizo yaliyojitokeza kutokana na kukosekana kwa vitambulisho vya Mzanzibari ni kushindwa kuthibiti vyema wimbi la uhalifu kutokana na kushindwa kuwatambua wale sugu pamoja na kushindwa kugawanya mapato na rasilimali zake kama vile ardhi kwa ajili ya mashamba, viwanja vya kujenga nyumba na hivyo rasilimali hizo kuangukia mikononi mwa watu wasiohusika kupata haki hizo.

``Kutokana na kushindwa kumtambua nani Mzanzibari, serikali hushindwa kutoa huduma kama vile elimu, matibabu na maji bila ya malipo na hivyo serikali hubeba mzigo mkubwa wa kutoa huduma kwa watu wasio Wazanzibari ambao wangesitahiki kuchangia huduma hizo,`` alisema Waziri Nyanga.

Alisema kwamba kwa msingi huo kitambulisho cha Mzanzibari mkaazi ndiyo kitakachotumika katika utoaji wa ajira na leseni za vyombo vya baharini na angani.

Vilevile, alisema vitambulisho hivyo vitatumika kama alama ya Mzanzibari ndani na nje ya nchi na wale ambao ni wageni watakuwa na sifa ya kupewa vitambulisho hivyo baada ya kuishi Zanzibar kwa miaka kumi na kuomba kupewa Uzanzibari ukaazi kupitia Serikali za Mitaa na baadaye Mkuu wa Wilaya.

Kwa habari zaidi, soma hapa:Wabara watengwa Z`bar

Residency permit ndiyo hiyo tena. Mzanzibari mkaazi baada ya miaka kumi! Hata kwa wenzetu haichukui miaka kumi kupata permanent residency!

Inaelekea hata raia wa shirikisho kama E.U. ana haki katika nchi nyingine mwanachama kuliko haki aliyonayo mtanganyika Zanzibar! Yule anapiga kura katika uchaguzi wa manispaa au miji, ana haki ya kugombea udiwani, ana haki ya kuajiriwa popote kama raia wa nchi hiyo na hahitaji passpoti kusafiri baina ya nchi. Sisi tunaosema tumeungana na ni nchi moja, tunawekeana mizengwe yote hii!

Hivi wanaamini kweli kikaratasi kitazuia ujambazi? Mbona tanganyika majambazi yanaingia kila kukicha kutoka Kenya na Rwanda bila matatizo. Wajiangalie kwanza kabla ya kutafuta mchawi nje. Kwa kumbatia biashara ya mihadarati, matokeo yake ndiyo haya. Au wanadhani nani anayewafungulia milango hao majambazi kutoka bara kama si wanao?

Wakati umefika wa kukaa na ku-legitimise huu Muungano wetu. Kwa vile kila siku kuna watu wanaosema wanawakilisha mawazo ya raia wao, basi hao raia waulizwe kama kweli wanautaka Muungano. Raia wa pande zote mbili. Muungano uendelee kama utakubalika na pande zote tu. Pande moja ikikataa, tugawane mali na kila mmoja aangalie ustaarabu wake!

Kwa kuangalia na kujifanya hatusikii tutafikishwa pabaya. Tuwaige Czechoslovakia na si Yugoslavia.

Nashangaa hawazungumzii haki ya mZanzibari aliyehama. Nae akirudi kwao, itabidi akae miaka 10 ndio atambulike kama Mzanzibari Mkaazi? Je Aboud Jumbe na Ali Hassan wameisha poteza uzanzibari kwa kuishi bara?

Isije ikawa waPemba wamepigwa dongo la macho!
 
tumeshabembelezana kiasi cha kutosha, kilichobaki kila mmoja aelekee anakotaka, kama ni mafuta wameshaambiwa hayapo, kama ni karafuu imeshuka bei, hivi tunatafuta nini paleeeeeeeee!
 
Mtoto akililia wembe wacha umkate atakapo pata kidonda ndio akili itamjia. Any way hawa jamaa historia yao ni tofauti na sisi na hata jinsi walivyoupata huo uhuru waliupata kwa shari sasa mbegu ile tunajaribu kuiua kwa njia ya muungano wapo wanaoipandikiza kwa husda zao za kisiasa. Ikumbukwe wakitwangana au wakiuana wakulaumiwa ni Tanzania Bara sio wao na ndio maana inakuwa ngumu. Na sumu hiyo ikishaanza kuingia huku hata kama tutaishinda hoja ya Uzanzibari itakuja hoja ya Udini. Hizi siasa za Uhizbu hazijafa bado Z'bar na zinafadhiliwa na jamaa wa Uajemi kwa kiasi kikubwa kupitia mifuko ya wafanyabiashara wakubwa nchini kwetu. Jamaa hawa wazenji ni wajanja sana kuliko tunavyodhani. Wanaweza kuja kushika rasilimali zetu za kiuchumi na tayari haya yanajionyesha tazama Wapemba sasa hivi ni matajiri wa kutupa lakini utajiri huo wameupatia bara na wapo wengine wa kutisha sasa wataushika uchumi wetu watatuajiri watatunyanyasa halafu watasema Muungano basi. Mgogoro wa kisiasa Z'bar mgogoro wa kidini Tanzania Bara.
 
Binafsi, mimi nina ufahari sana kuhusiana na muungano wetu huu. Ila kama wenzetu wazenji wanadhani sisi wa mrima tunalilia unafuu kutoka kwao basi ni afadhali tuuvunje tu muungano huu kusudi tujipange upya mapema. Dunia hii ina mambo mengi ya kukabiliana nayo kuliko kuwa tunasumbuana na jambo dogo la uvunguni kama hili. Unajua ndiyo maana hata katika ndoa kuna kitu kinaitwa talaka; hata kama mlishakuwa na watoto na mlishavuna mali kwa pamoja, bado talaka inaweza kutolewa tu ili kila mmoja aanze mambo yake upya.
 
Ule mpango wa umeme kwenda zanzibar toka tanga tuuzime...boti za kwenda kwao na kurudi zenye wamiliki bara zisimamishwe...

Harafu tuwaache wakae na kisiwa chao...kama wanafikiri wao ni wa maana sana...dunia ya sasa sio ya kushikamana na misalaba mizito kama hii....hivi kutuona tunaenda kutalii wanafikiri tunapenda sana?

Ndipo utaona na pemba inataka kuwa nchi,zanzibar na unguja..kisha na wao mumo mumo..wanaanza kuvurugana...yaani haita waacha hiyo dhambi..mpaka waishe....

Baadae utasikia tuomba jeshi la la kwenda kusimamia amaini visiwani...

Tuna mambo mengi sana ya kufanya...zaidi ya kushikamana na wale.
 
Wabara watengwa Z`bar

2008-10-21 10:09:30
Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar

Lile chokochoko la kutaka Zanzibar itambuliwe kama nchi kamili sasa limepiga hatua zaidi baada ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kuwasilisha sera ya vitambulisho vya Mzanzibari mkaazi ikilenga kuwaengua wananchi kutoka Tanzania Bara kuruhusiwa kuajiriwa Zanzibar.

Msimamo huo tata uliwekwa bayana jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ, Suleiman Othman Nyanga, alipokuwa akiwasilisha sera ya vitambulisho vya Mzanzibari mkaazi katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea mjini hapa.

Kwa kauli hiyo, wenye vitambulisho vya Uzanzibari ndio watapewa kipaumbele cha ajira ili kudhibiti nafasi za kazi kuchukuliwa na wageni kutoka nje ya Zanzibar, wakiwamo watu kutokaTanzania Bara.

Waziri Nyanga alisema kwamba waajiri wote katika sekta binafsi watatakiwa na Wizara ya Kazi, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na watoto kuhakikisha wanatoa kipaumbele kwa Wazanzibari kabla ya kuwafikiria watu wengine kutoka nje ya Zanzibar.

``Taasisi zisizokuwa za Serikali zitakuwa na majukumu ya kutumia vitambulisho vya Mzanzibari katika kutoa kipaumbele kwa Wazanzibari katika kutoa ajira, mikopo na misaada ya kimaendeleo,`` alisema Waziri Nyanga.

Alisema kwamba mpango huo endapo utatekelezwa itasaidia vijana wengi wa Kizanzibari kunufaika na ajira na hivyo kufanikisha mpango wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini kwa Wazanzibari.

Alisema kwamba Serikali itahakikisha kila Mzanzibari anasajiliwa na kupatiwa kitambulisho hicho na atatakiwa kutembea nacho wakati wote kama alama ya Mzanzibari.

Aidha, alisema kwamba kitambulisho hicho cha Uzanzibari mkaazi pia kitatumika kutoa kipaumbele kwa Wazanzibari wanaohitaji kunufaika na udhamini wa mikopo ya elimu ya juu kupitia mfuko maalum wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Waziri Nyanga alisema kwamba sera hiyo mpya itahakikisha kwamba inadhibiti uingiaji na utokaji wa watu katika maeneo ya Bandari na Uwanja wa Ndege kwa kutumia vitambulisho vya Mzanzibari mkaazi ili kupunguza tatizo la uhalifu na mmonyoko wa maadili Zanzibar.

Waziri huyo alisema kwamba vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi vitatumika katika ugawaji wa ardhi, viwanja na nyumba za serikali ili kuepusha kupatiwa umiliki wa ardhi kwa watu wasiokuwa na sifa kwa mujibu wa sheria ya Zanzibar.

Aliwaeleza Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwamba watumishi wote wa serikali watalazimika kuonyesha vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi kabla ya kupokea mishahara ili kudhibiti vitendo vya wafanyakazi hewa.

Waziri Nyanga alisema kwamba serikali itahakikisha wanatoa vitambulisho maalum kwa wageni wanaoishi kwa ruhusa maalum za kazi ambayo itafanywa na Ofisi ya Msajili wa vitambulisho Zanzibar.

Alisema kwamba vitambulisho hivyo vimelenga kuimarisha usalama, kulinda haki za kiuchumi na kuongeza kasi ya maendeleo ya jamii kwa wananchi wake.

``Lengo kubwa ni kuwatambua Wazanzibari wote waliopo nchini na shughuli zao kwa lengo la kupanga vyema mipango ya maendeleo,`` alisema Waziri Nyanga.

Alisema kwamba vitambulisho hivyo vitasaidia kuwatambua watu walioko Zanzibar ambao wameingia bila ya kufuata utaratibu na kuhakikisha wananchukuliwa hatua za kisheria.

Alisema miongoni mwa matatizo yaliyojitokeza kutokana na kukosekana kwa vitambulisho vya Mzanzibari ni kushindwa kuthibiti vyema wimbi la uhalifu kutokana na kushindwa kuwatambua wale sugu pamoja na kushindwa kugawanya mapato na rasilimali zake kama vile ardhi kwa ajili ya mashamba, viwanja vya kujenga nyumba na hivyo rasilimali hizo kuangukia mikononi mwa watu wasiohusika kupata haki hizo.

``Kutokana na kushindwa kumtambua nani Mzanzibari, serikali hushindwa kutoa huduma kama vile elimu, matibabu na maji bila ya malipo na hivyo serikali hubeba mzigo mkubwa wa kutoa huduma kwa watu wasio Wazanzibari ambao wangesitahiki kuchangia huduma hizo,`` alisema Waziri Nyanga.

Alisema kwamba kwa msingi huo kitambulisho cha Mzanzibari mkaazi ndiyo kitakachotumika katika utoaji wa ajira na leseni za vyombo vya baharini na angani.

Vilevile, alisema vitambulisho hivyo vitatumika kama alama ya Mzanzibari ndani na nje ya nchi na wale ambao ni wageni watakuwa na sifa ya kupewa vitambulisho hivyo baada ya kuishi Zanzibar kwa miaka kumi na kuomba kupewa Uzanzibari ukaazi kupitia Serikali za Mitaa na baadaye Mkuu wa Wilaya.

Wakichangia sera hiyo, Wajumbe wa Kambi ya Upinzani ya Chama cha Wananchi (CUF) walisema ili kukabiliana na vitendo vya uhalifu wa kutumia silaha na ukahaba Zanzibar ni vyema SMZ ikarejesha utaratibu wa watu wenye asili ya Tanzania Bara kuingia kwa hati maalum za kusafiria.

Wawakilishi waliochangia suala hilo ni Mwakilishi wa Jimbo la Gando, Said Ali Mbarouk, Mwakilishi wa Wawi, Soud Yusuf Mgeni na Mwakilishi wa Jimbo la Chakechake, Ali Omar, ambao walisema hivi sasa Zanzibar inakabiliwa na tatizo kubwa la uhalifu na biashara ya ukahaba kwa vile hakuna udhibiti wa watu wanaoingia na kutoka Zanzibar.

Hatua hii ya kuwatenga Watanzania kutoka bara ni mwendelezo wa Zanzibar kujitangaza kuwa nchi huru baada ya kufanikiwa kupata wimbo wa Zanzibar, bendera na hivi karibuni waliibua hoja nzito kuhusu rasilimali za nchi yakiwamo mafuta na madini.

Wazanzibari bila kujali itikadi zao, wameapa kwamba endapo mafuta yatapatikana kamwe hayawezi kuwa mali ya Muungano. Hivi karibuni Wazanzibari walianza kudai gawio kutoka benki Kuu ya Tanzania (BoT), na Waziri Kiongozi wiki hii atatoa tamko la SMZ kuhusu hisa zao BoT.

Mambo mengine ambayo yanaashiria kusukwasukuwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliofikiwa mwaka 1964, ni kutaka kutolewa wazi hati ya Muungano ili kubainisha ni mambo yapi Mwalimu Nyerere na Abeid Karume waliafikiana wakati wa kuundwa kwa taifa la Tanzania.

SOURCE: Nipashe
 
Hakuna kosa wazanzibari kudai paasport kwani kila mtu anaangali interest zake. Lazima tukumbuke muungano ni wa nchi mbili. Muungano haukuwa wa kuimeza Zanzibar. Zanzibar ina kila sura ya kuwa ni nchi kwa hivo tunapozungumzia suala la muungano, hatuzngumzi kama zanzibari ni mkoa kama Mara. Sababu ya kero la Muungano ni kuwa wenzetu mumesahau kuwa paliunganishwa nchi sio mikoa.
Matatizo ni kuwa kuanzai 1995 pasi ya kwenda na kurudi iliondoshwa na ujambazi umezidi Zanzibar. Ndani ya wiki mbili zilizopita, watu 13 wameuawa zanzibar hala hao wauwaji wamekimbilia bara na hawajulikani wamepotelea wapi. Ikiwa patakuwa na udhibiti wa aina fulani itakuwa rahisi kuwatafuta wahalifu wanao kimbilia bara au visiwani kujificha.
sasa hivi tuna serikali mbili (yaani ya bara na visiwani) na NIA ni kwenda kwenye serikali moja. Sisi wazanzibari hatuwezi kukubali kupoteza "IDENTITY" yetu. Sisi tuna historia ndefu na kubwa hapa duniani na kuipoteza Zanzibar kwa kisingiio cha muungano ni kama kuwaua wazanzibari wote.
Jengine, muungano wenyewe pia hautambuliki unaanza wapi na unaishia wapi. Hakuna makaratasi ya mikataba kwa ufupi ni USANII mkubwa huu mungano. Mikataba ya kimataifa huwa ina makubaliano halafu wahusika wanatia "seal" au sinature zao. Mkataba wetu ulisainiwa na NANI?. Nyinyi ndugu zangu mumeona waraka wowote ulio tiwa saini ya NYERERE na KARUME?. Hakuna na kwa kuwa hakuna, mumetukalia KIKOLONI.
Munaweza muka very emotional on this issue but remember, FACTS are FACTS. Hayo mengine tunaweza kuyazungumzia lakini tukubalini kuwa koloni la Tanganyika ni Zanzibar.

Nani aliwaambia kuwa mkiwa mmeungana ni lazima mpoteze IDENTITY yenu? Wascot mpaka keshokutwa wanajivunia uscot wao. Wacatalania nao hivyo hivyo dhidi ya uhispania. Lakini wote hawa wanakubali kuwa nchi yao ni moja, Great Britain na Spain respectively. Hayo mnayodai nyinyi ndio yanayotokea Belgium. Nchi haitawaliki.

Mnatutukana na kutuambia kuwa tumewakalia kikoloni wakati kwa miaka minne nchi iliongozwa na mZanzibari. Kama kweli tumewakalia kiukoloni tungemruhusu vipi? Hivi karibuni mPemba karibu aingie kwenye kinyang'anyiro lakini ni nyinyi wenyewe mkamuanguasha mZanzibari mwenzetu kwa upuuzi wenu wa siasa za kale ( ati muarabu). Sisi hatukua na noma kumpa ubalozi, uwaziri wa ulinzi na hata uwaziri mkuu! Nyinyi jee? Hampendani wenyewe, mtatupenda sisi?
 
Back
Top Bottom