Naam hivyo ndivyo ninavyoamini na Mwiba ana uhuru wa maoni yake. Tunatawaliwa kwa vile kama ni muungano basi kusingekuwa na kuburuzana na kuzuwiana katika uhuru wa kujiamulia ya maslaha yetu. Na kibaya zaidi tunapotishiwa na DOLA. Ninachoshindwa ni jina la kuuita ukoloni huu.
 
Kama huna jina basi ni kwamba hakuna UKOLONI ila tamaa yako ya kupewa unaibu Waziri.
 

Kwanza,sidhani kama inawezekana kuelewa mantiki ya anachoongea kwa kuhoji uprofesa wake (wa jadi au kitaaluma).Labda ungetusaidia kwa kupingana na hoja yake nawe ukaja na hoja mbadala.

Lakini pengine nifafanue nilivyomwelewa mie (mwanafunzi wake wa zamani):kwamba Zanzibar isijidanganye kwamba iwapo mafuta yatapatikana itamudu kujiendesha yenyewe (na hapo anaungana nawe kutambua kuwa znz ni sehemu ya Muungano).Kwa lugha nyepesi,surival ya znz kwa kiasi kikubwa inategemea uwepo kwake ktk muungano.

Binafsi nashangazwa sana na hawa wazenji.Mafuta yenyewe hayajaanza hata kuchimbwa tayari wanaleta longolongo.Na yakianza kuchimbwa (na tu-assume Bara hawatakuwa na haki) then itakuwa mafuta ni ya Wapemba au mafuta ni ya waunguja.....yaleyale lowahi kutuusia Mwalimu.Sintoshangaa huko mbeleni wakaanza kutunishiana misuli wenyewe kwa wenyewe hususan kwenye location ya hayo mafuta yenyewe.

Porojo haziwezi kuchimba mafuta.Na hata ukifika wakati wa kuchimba,bado italazimu yachimbwe na kampuni ya kigeni,yalkasafishwe huko,nk....
 

Towa ruhusa watu wakushangae wewe kwa kumuona mtu akizungumzia kilicho chake. Mafuta ni ya Wazanzibari sasa unataka nani awasemee, Profesa Baregu?
Kipi kinachokushangaza , kwani hujawahi kutegemea mtoto akiwa tumboni, hukuwahi kufurahia siku uliyoambiwa kesho yake uanze kazi? That is natural kwa binaadamu, kuweka tamaa kwa kile kilichotowa matumaini.
Kuhusu huyo Profesa wako na kauli yake inafaa aulizwe kuwa jeenyie Watanganyika mtavunja Muungano kwa kukosa mafuta ya Zanzibar? Mbona ni miaka karibu hamsini sasa na hakukuwa na hayo mafuta. Halafu wapi Baraza la wawakilishi lilisema kuwa kutokana na kupatikana kwa Mafuta basi tuvunje Muungano?
Hivyo kunataka uprofesa kufahamu neno KUONDOWA SUALA LA MAFUTA KATIKA MAMBO YA MUUNGANO? Nafikiri hata mtu aliekosa kusomeshwa na Baregu angefahamu juu ya mtu na chake na kuondowa kitu miongoni mwa jumla ya vitu vyengine. Kama uwezo wa kuendesha basi hilo lisiwatie hofu wenzetu kwani hata nyie kwa kupitia TPDC mlitafuta watu kuyachimba hayo mafuta. Wanachotaka Wazanzibari ni kuwa hiyo ruhusa ya kuwapa hao mliowapa kabla inatolewa na muhusika hasa, Zanzibar
 
Leave prof alone. ALinifundisha International relations pale mlimani. Jamaa ni kichwa! inawezekana hawamwelewi, wamwite awape lecture ya mahusiano ya kimataifa. Ndo taabu ya ukilaza!!
 
A renowned CCM cadre from Mkunazini in Zanzibar, Baraka Mohammed Shamte, said that the main problem with the current generation of Zanzibaris is that they did not experience the evils of regimes that existed prior to the Revolution. He said that people were now moving away from the tenets of TANU and Afro-Shirazi Party.

``In the past, leaders were groomed before ascending to positions of authority. Right now, a young person joins the party today, tomorrow he holds a major party position, and within no time he is a minister.

We get problems like the Band of Tanzania scam because we are no longer grooming our leaders, who are more inclined to forget the poor and embrace the rich,`` noted Shamte.

Contacted for his views on the same issue, Prof Mwesiga Baregu of the University of Dar es Salaam said the achievements of the Revolution were manifested to an extent by removing classes, and Arab master and African slave mentality.

``Although this problem may in a way be seen in the differences between CCM and CUF, that mentality is no longer socially accepted in Zanzibar,`` noted Prof Baregu.

He said there was a possibility that some ``bankrupt`` politicians could still exploit that mentality for their own ends.

The political science professor said the political stalemate in Zanzibar could end with having a Constitution that reflected a social contract.

Source: Guardian
 
Mwanataaluma mashuhuri katika Kitivo cha Sayansi na Siasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Mwesiga Baregu ameonya wanasiasa kuacha kuiingiza nchi kwenye migogoro kwa kisingio cha kutumia rasilimali za asili.

Profesa Baregu alisema tofauti zinazojitokeza sasa katika tafsiri za mali za Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano si tu kuangalia vizuri katiba zote mbili, lakini ni muhimu kuangalia kwenye Mkataba wa Muungano kuliandikwa nini na kulikuwa na nia gani.

"Maana ukiangalia katika hili, Serikali ya Muungano haijaonyesha umakini wowote katika kulinda na kuvuna rasilimali na jamii zetu zifaidi. Ukiangalia dhahabu inavuja, uvunaji mkubwa wa almasi faida yake haionekani.

"Kabla hatujaanza kugombana nani ni mwenyewe, tuangalie taratibu za sheria, lakini pia tusijiingize katika mkumbo wa kuchimba mafuta huku mwenye mali asifaidike. Wataalamu waangalie makubaliano na Katiba watoe maoni yao na tusiende katika njia ya kulipukiana ambayo haina tija.

"Tusinyosheane vidole wakati kitu hakijaonekana na taratibu zipo. Tuwe na utaratibu wa kushughulikia matatizo yetu kama vile tunavyoshughulikia mwafaka wa CCM (Chama Cha Mapinduzi) na CUF (Chama cha Wananchi) na tusijiingize katika tofauti bila kukusudia.

“Na pengine haya yanachochewa si na sisi wenyewe bali ni kwa maslahi ya watu wengine wanataka kutukosanisha…tutumie ukomavu katika kuyakabili haya, tuache kupiga kelele na kutunisha misuli,” anaonya.

Profesa Baregu anashauri suala hili lisipelekwe bungeni kabla ya kujadiliwa na Serikali na kutaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Muungano na wa SMZ wakutana mara moja kuzungumzia tatizo lililojitokeza.

"Bungeni usiende mjadala usio na mwelekeo, wanasheria wakuu wanapaswa kuzungumza...na mahakamani wanapeleka nini? Kinachotakiwa hapa ni Serikali na Rais (Jakaya Kikwete) waonyeshe ukomavu wao katika kuongoza. Na hatima yake hili litahitaji Katiba ya Jamhuri ya Muungano na ile ya Zanzibar ziangaliwe upya ili kuondoa migogoro ya kila mara na hapa si tena kuendelea kufichana fichana, kuwepo na uwazi na kutafuta ukweli uko wapi na suluhisho ni nini," alisema Profesa Baregu.

Chanzo: Rai
 
Profesa Baregu ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, katika masuala ya Siasa na Jamii. Na yeye kama walivyokuwa watoa mada wengine anapewa dakika thelathini ili azungumzie mchango wa Mwalimu katika suala zima la kuwa na Afrika iliyo moja.

Profesa Baregu mwenyewe hayuko hapa ukumbini, tunaambiwa amekwenda kwenye msiba huko Bukoba. Lakini amekataa katakata kuleta ile samahani yetu tuliyoizoea, “Samahani sikuweza kufika wa sababu zisizoweza kuzuilika”. Baregu amemtuma Bashiru Ali, mhadhiri msaidizi hapa Chuoni, kutoa hotuba kwa niaba yake. Hapajaharibika kitu, hebu tusikilize Profesa alikuwa ameandaa nini.


Bashiru anasema Profesa aliandaa mada kwa kikoloni lakini ana hakika angelikuwepo mwenyewe angelitumia Kiswahili, kwa mantiki hiyo Bashiru anatuahidi kutumia Kiswahili, watu wanapiga makofi.

Mada ya Porfesa Baregu inaaza kwa kusema, Mwalimu alipokwenda wa Pan-Africanism amabo ulifanyika Afrika, Ghana, kwa mara ya kwanza, mwaka 1963, kuzungumzia juu ya Afrika kuungana alitoa wito kwamba kuungana kule kusiwe kwa haraka bali Waafrika wapewe kwanza nafasi ya kutafakari na hata watakapomaliza kutafakari muungano uanzie kanda moja hadi nyingine na si kuunganishwa kwa nchi zote za Afrika kwa wakati mmoja.

Kwa upande wa pili, rafiki yake sana Mwalimu, hayati Nkrumah yeye alipingana na Mwalimu. Hoja ya Nkrumah ilikuwa kwamba hakuna muda wa kusubiri zaidi kwani kwa kufanya hivyo, mabeberu watazidi kutumaliza. Mvutano ukawa mkubwa na mwisho wa yote kukawa na kundi linaloungana na hoja ya Mwalimu na lingine likiungana na Nkrumah. Kura zikapigwa na kundi la Mwalimu likaibuka na ushindi.

Baregu anasema, tukitazama leo hakuna anayebisha kuwa hoja ya Mwalimu ilikuwa na uzito zaidi kwani hadi sasa imekuwa vigumu kwa Afrika yote kuungana bali muungano uliodumu kwa muda mrefu zaidi katika Afrika nzima ni ule wa Tanganyika na Zanzibar. Baregu anasema yote hii ni kwa sababu Mwalimu alianza kwa hatua.

Baregu anauliza, je tunajifunza nini sasa tunaposikia kelele za Jumuiya ya Afrika Mashariki kila kukicha? Baregu anasema, watu wanazidi kukosea kumtafsiri Mwalimu kwani katika maadhimisho ya miaka 40 ya uhuru wa Ghana ambako Mwalimu alialikwa, Mwalimu alisema, “Na atemewe mate yule asemaye Afrika na ibaki tenge…” Kutokana na msemo huo, Baregu anasema, ni wazi basi kuwa mawazo ya Mwalimu kuhusu uharaka wa kuungana kwa Afrika ulikwishabadilika siku nyingi. Anasema Mwalimu alishagundua kuwa bila kasi ya kueleweka ya kuungana kwa Afrika basi nguvu ya utandawazi ingelifunika na kulidhoofisha bara.

Baregu anasema alichokuwa anapinga Mwalimu katika mwaka ule wa 1963 kuhusu swala zima la kuungana kwa haraka ni kwa sababu zilizotolewa, kwamba hazikuwa na uzito wa kutosha kufanya Afrika iungane. Mwalimu alisema, “Hatuwezi kuungana ati kwa sababu tu tunapendana sana, hatuwezi kuungana kwa sababu tu historia zetu zinafanana, na hatuwezi kuungana tu kwa sababu kuna mfadhili anataka tufanye hivyo.” Bali, mwaka 1997 Accra, Ghana Mwalimu aliona sababu ya msingi kwa Afrika kuungana kwa haraka, sababu hiyo haikuwa nyingine bali kasi ya mfumo kandamizi wa utandawazi.

Mwalimu akasema, “Muungano kwa sasa ni lazima kwa sababu dola za Kiafrika hazina nguvu ya kutosha, chumi za nchi za Afrika ni dhaifu kwani mfumo wa viwanda uko nyang’anyang’a, hivyo ni lazima tuungane kwa haraka. Ila ni lazima tuwe tunaelewa kuwa tunaungana ili tuwe wazalishaji na si walaji tu, tunaungana ili tuwe na dira inayotuonyesha tuko wapi na tunakwenda wapi na dira hii ndio itakayotujengea kujiamini mbele za jamii za watu wengine. Na mwisho kabisa, ni lazima tuungane sasa ili kurejesha dhana ya mapamabano dhidi ya ubeberu, mapambano ambayo kwa sasa yamelala usingizi wa pono”

Kwa Mantiki hiyo, Baregu anamaliza kwa kusema, ni wazi kabisa kuwa kwa kuogopa kuingia kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki, viongozi wa Tanzania wanataabika kuitafsiri vizuri hoja ya Mwalimu katika swala zima la Afrika iliyo moja ambayo itaanza na muungano wa kikanda. Bashiru anamaliza kumwakilisha Profesa Baregu na kuteremka jukwaani. Watu wamepiga makofi, amemwakilisha vyema Profesa. Ngwe ya kwanza ya ratiba ya leo imekwisha hivyo watu wanakwenda nje kupumzika kidogo halafu warudi kwa ajili ya majadiliano. Hadi baadae kidogo

Chanzo: Mwenyemacho
 
Profesa Mwesiga Baregu wa Sayansi ya Jamii, Idara ya Siasa ya UDSM, alisema kitendo cha CCM kutaka suala la Mwafaka kupigiwa kura ya maoni na wananchi baada ya kukaa nalo kwa miaka miwili sasa, ni uhuni unaoweza kulipeleka taifa katika migogoro.

�CCM wanafanya uhuni na huu ni mchezo mbaya sana kwa sababu yaliyoharibika Kenya yalitokana na wananchi kukosa imani na serikali kutokana na uhuni wa aina hiyo,� alisema Profesa Baregu.

Alisema tabia ya Serikali ya CCM kuanzisha michakato mizito ya kitaifa na kufanya ghiliba za makusudi kisha kuiacha kwenye utata, ni ufisadi wa kisiasa na hatari kwa uhai wake na maendeleo ya taifa.

�Tofauti na ufisadi wa uchumi ambao bado unazungumzwa, kitendo hicho ni ufisadi wa kisiasa na kama serikali haisimamii haki, haistahili kuaminiwa wala kuheshimika na matokeo hayo yote ni watu kuchukua sheria mkononi,� alisema.

Alisema uamuzi wa Halmashauri Kuu ya CCM kurudisha mjadala wa mwafaka kwa Wananchi wa Zanzibar wakati wajumbe wake ni viongozi wa CUF na CCM Taifa ni ujanja wa kuukataa mwafaka.

�Uamuzi huo unaondoa imani na dhamira njema ya CCM kuhusu mwafaka. Kwa nini hatima ya mazungumzo hayo yakafanywe na Wazanzibari tu wakati walioshiriki ni makatibu Wakuu wa vyama vyenye wanachama Bara na Zanzibar?� alihoji Baregu.

Profesa Baregu alisema kama kuna umuhimu kura za maoni ziendeshwe kuhusiana na kutungwa kwa katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba ya Zanzibar badala ya kupoteza fedha nyingi kuendesha kura za maoni kuhusu mwafaka tena katika mazingira ambayo jamii inafahamu kuwa CCM inaukataa.
 
Na Asha Bani

PROFESA Mwesiga Baregu, ni mwanasiasa na mchumi mwenye shahada mbalimbali za elimu ya juu nchini na nchi za nje, ambaye amejitoa mhanga katika kugombea ubunge wa Afrika Mashariki.


Profesa Baregu, ni mgombea wa nafasi hiyo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambacho kilimpitisha kutokana na kumuona anafaa na kwamba hakuna mgombea katika vyama vingine vya sisa ambaye anafanana au kuwa na elimu na umaarufu kama alionao Profesa Baregu katika masuala ya siasa na uchumi.


Hata hivyo kuna sababu ya kuhoji kwa nini Profesa Baregu agombee ubunge wa Afrika Mashariki? Katika mahojiano yake na Tanzania Daima, Profesa Baregu anabainisha kuwa ana sababu nyingi zilizomfanya agombee nafasi hii na akishinda atahakikisha Tanzania inang’ara na kupeperusha bendera katika Afrika Mashariki.


“Sifa nilizonazo katika elimu, katika uwezo wa kufahamu jambo na kulitatua, nina uhakika hakuna mgombea katika chama chochote ambaye anasifa kama hii, hivyo nina uwezo wa kuongoza,” alisema Profesa Baregu.


Anasema mbali na kuwa na elimu, atahakikisha anakuwa na nguvu katika muungano huo na kuiwezesha Tanzania kuwika katika medani ya uchumi na biashara, ambapo uchumi wa Tanzania utapanda na kutambulika kuliko ilivyokuwa hivi sasa, ukilinganisha na nchi za Afrika Mashariki.


“Ikiwa tulifanikiwa na kuupa nguvu muungano wa Tanganyika na Zanzibar hadi ulipo hapa sasa na kuitwa Tanzania, na hadi leo unaendelea kuwapo ingawa kuna migogoro ya hapa na pale, lakini Mwalimu Nyerere alijitahidi kuuimarisha na viongozi wetu wanajitahidi kuuimarisha ili usije kuvunjika, ndivyo itakavyokuwa EAC,” alisema.


Anasema atahakikisha muungano hautaweza kuvunjika tena kama ilivyotokea awali, mwaka 1977, ambapo muungano huo ulidumu kwa muda wa miaka 10 tangu kuanzishwa.


“Kuvunjika kwa Muungano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Tanzania tayari tumejifunza mengi na vya kutosha, na kama kulikuwa na udhaifu au upungufu katika nchi yetu kwa sasa, nitakuwa katika mstari wa mbele kukabili na kuyasawazisha matatizo hayo ili umoja huo usiweze kuvunjika tena, na kinachotakiwa ni kuwa imara kwa umoja huo,” alisema Baregu.


“Tunaweza kuwa viongozi wa EAC endapo tukijiamini na kuacha kuwa wafuasi, na mimi ni mtaalamu pekee wa kusuluhisha migogoro na ninawahakikishia Tanzania itakuwa makao makuu ya usuluhishi, kwa kuwa ni nchi ya amani na yenye utulivu,” anasema Baregu.


Baregu anasema atakuwa kama silaha na chachu ya kuleta maendeleo katika jumuiya hiyo, kwa kuwa anapenda kupata mawazo ya watu kutoka sehemu mbalimbali ili kufanikisha malengo yake aliyojiwekea katika kuimarisha umoja huo.


Baregu anasema kugombea nafasi hiyo ni sawa na kujitoa mhanga, kwa kuwa Bunge la Chama Cha Mapinduzi (CCM) limepitisha wagombea 24.


Katika wagombea 24, kambi ya upinzani kupitia CHADEMA kuna mgombea mmoja ambaye ni yeye Baregu, na Chama cha United Democratic (UDP), kinawakilishwa na Fortunatus Masha.


Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Novemba 2, ndani ya Bunge ili kumpata mwakilishi wa Bunge la Afrika Mashariki.


Profesa Baregu anasema endapo akichaguliwa katika nafasi hiyo atahakikisha anafanya maajabu, kwa kuhakikisha anaunganisha Tanzania, Kenya na Uganda kuwa kitu kimoja katika masuala mbalimbali yakiwamo ya kijamii na kiuchumi.


Profesa Baregu alizaliwa Februari 23, mwaka 1944, katika Kijiji cha Maruku, mkoani Kagera, ameoa na hadi sasa ana watoto saba.


Ana shahada mbalimbali alizozipata katika vyuo vya hapa nchini na nje ya nchi, hasa shahada za uchumi na mambo ya siasa.


Mwaka 1964 alipata elimu ya juu katika Chuo cha Makerere nchini Uganda, ambapo alisoma na kupata Shahada ya Ukutubi. Anasema chuo hicho ni maarufu zaidi kwa kutoa viongozi hapa nchini kama Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.


Mwaka 1998-2002, alisoma katika Chuo cha Senior Reseach Fellow - Afrika Kusini, na kozi kama hiyo pia aliisoma akiwa nchini Zimbabwe.


Kuanzia mwaka 1988 hadi 1994, alikuwa profesa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika masuala ya Sayansi ya Siasa. Mwaka 1982 -1988, alikuwa Senior Lecturer in Political Science katika chuo kikuu hicho hicho cha Dar es Salaam.


Mwaka 1992-1994, alikuwa member Committee of vice-Chancellors and Principal, wa Tanzania.


Mwaka huo huo alikuwa mhariri katika kitengo cha mambo ya Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


Mwaka 1989-1991, alikuwa mratibu nchini Afrika Kusini, na alikuwa msuluhishi katika migogoro ya kisiasa nchini humo.


Mwaka 1989-1991, alikuwa mratibu katika uchunguzi wa masuala ya miradi katika Idara ya Sayansi na Siasa nchini Namibia. Aidha, anasema kuwa mratibu wa mambo ya siasa na katika kamati ya kusuluhisha


migogoro mara kwa mara katika Afrika, kumemfanya awe mzoefu wa kufanya maamuzi katika mchakato wa mtandao wa siasa.


Mwaka 1988 -1991, alikuwa Mhariri Mkuu wa jarida la The Dar Graduate, ambalo lilikuwa linaandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwa wakati huo na ni mtunzi mzuri wa vitabu mbalimbali vinavyoelezea masuala ya siasa na uchumi.


Aliwahi kuwa na nyadhifa mbalimbali katika chuo kikuu na ni mtu ambaye walikuwa wanamthamini sana hasa kwa kazi zake katika chuo hicho na chuo chochote, na ndivyo ilivyo hadi sasa mchango wake kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni mkubwa.
 
MTAALAMU wa mambo ya siasa Profesa Mwesiga Baregu ameonya juu ya hatima ya muungano wa khofu badala ya matarajio.

Amesema, kuwa na aina hiyo ya muungano inazifanya serikali ziwe legelege zikitawaliwa zaidi na unafiki.

Prof. Baregu aliyasema hayo wiki hii katika mahojiano maarufu yanayorushwa na kituo kimoja cha televisheni Jijini kila jumatatu.

"Dola zijenge misingi ya kuwawezesha raia kudhibiti serikali badala serikali kudhibiti raia", alisisitiza Profesa huyo wa sayansi ya siasa.

Aidha alitahadharisha juu ya hatari ya kuendelea kuukumbatia mshikamano uliojengwa kwa msingi wa mchanga badala ya zege.

Kuhusu viongozi wa serikali kutokuwa wavumilivu wanapokosolewa, alisema kwa muda mrefu hapa nchini ulijengwa utamaduni wa "uwenzetu" ambapo wananchi na viongozi walidumu kupongezana na kusifiana.

"Kutoka kwa mwenzako hujifunzi, mnadumaa wote", alisisitiza Prof. Baregu.

Aidha alikosoa utaratibu uliokuwepo enzi za awamu ya kwanza ambapo ilisisitizwa kudumishwa fikra za mtu mmoja.

"Zidumu fikra za mtu fulani maana yake zidumae fikra za jamii", alionya

Kuhusu marekebisho ya katiba Prof. Baregu alisema Tanzania haijawa na katiba kama mkataba kati ya watawala na watawaliwa hivyo inahitaji Katiba ya aina hiyo.

Maelezo ya Profesa Baregu yamekuja wakati wananchi wakiibana serikali ya Rais Mkapa katika masuala kadhaa ya kisiasa.

Miongoni mwa mambo yanayoendelea kuhojiwa na wananchi wengi hivi sasa ni aina ya muungano iliyorithishwa kwao na marais waasisi wa Tanganyika na Zanzibar.

Masuala mengine ni pamoja na kutokuwepo tume huru ya uchaguzi, kuporwa kwa mamlaka ya raia kuwajibisha serikali halikadhalika viongozi wa juu wa serikali kutokuwa tayari kukosolewa au kusikiliza malalamiko ya wananchi.

Chanzo: An-nuur
 
Kama huna jina basi ni kwamba hakuna UKOLONI ila tamaa yako ya kupewa unaibu Waziri.

Wakuu hivi Zanzibar kumbe inatawaliwa na Tanzania bara?
Kwa hiyo wao wanashindwa au watashindwa kuyasisimamia hayo mafuta?
Mnataka wezi wanao fyonza dhahabu kiulaini huku bara waje wajinufaishe na mafuta nayo?
Ukweli wa mambo waZanzibari wamewashtukia wa bara ndo maana nao wanamsimamo wao....mbona karafuu hang'ang'anii ziwe za muungano?
 
UTANGULIZI

Tamko hili linatoa taarifa ya timu ya kampeni ya mgombea ubunge wa Afrika Mashariki kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kuhusu mapungufu, mafanikio, mapendekezo na mwelekeo kuhusiana na mchakato wa uchaguzi husika.

Novemba pili mwaka 2006 wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walichagua kwa niaba ya watanzania wabunge wa kuiwakilisha nchi yetu kwenye bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki.

Mchakato wa uchaguzi huu ulianza rasmi mapema mwezi Septemba baada ya katibu wa bunge kutangaza nafasi kuwa wazi na kupeleka barua kwa vyama kuteua wagombea.

CHADEMA kilishiriki katika uchaguzi huo toka mwanzo mpaka mwisho wa mchakato wa uchaguzi huu.

CHADEMA ilianza kwa kutangaza kwa uwazi kwa wanachama wake katika ngazi mbalimbali kujitokeza kugombea nafasi za ubunge wa Afrika Mashariki kwa tiketi ya CHADEMA. Wanachama mbalimbali walijitokeza kuomba na kamati kuu iliketi Oktoba 27 mwaka huu kufanya uteuzi wa wagombea ambapo wagombea wawili waliteuliwa mmoja katika kundi la wanawake na mmoja katika kundi la vyama vya upinzani. Mgombea wa kundi la wanawake alijitoa katika hatua za awali kabla ya jina lake kuwasilishwa kwa msimamizi wa uchaguzi.

Hivyo CHADEMA iliwasilisha jina la mgombea mmoja katika kundi C la vyama vya upinzani Profesa Mwesiga Baregu. Timu ya kampeni iliundwa kwa ajili ya kuratibu kampeni za mgombea wa CHADEMA katika uchaguzi huo.

Lifuatalo ni tamko la timu ya kampeni za mgombea wa Afrika ya Mashariki kwa tiketi ya CHADEMA kuhusu uchaguzi huo.


MAPUNGUFU:

Uchaguzi wa Bunge la Afrika ya Mashariki 2006 HAUKUWA HURU WALA WA HAKI kutokana na mapungufu yafuatayo ya msingi:

1. UFISADI NA SHINIKIZO/MAELEKEZO KWA WAPIGA KURA: Kampeni zilitawaliwa na mapungufu mawili makubwa: Mosi, palikuwa na ufisadi katika kampeni hususani katika makundi yaliyogombewa na wagombea wa Chama cha Mapinduzi(CCM) pekee. Katika lugha rahisi ufisadi unaweza kutafsiriwa kama uozo wa kimaadili ambao unajumuisha rushwa ya fedha, matumizi mabaya ya madaraka nakadhalika. Katika kundi hili la wagombea yalisikika malalamiko toka kwa wagombea mbalimbali kwamba wapo waliokuwa wakitumia rushwa ya fedha, wengine wakitumia sababu za kuwa na ndugu zao ama watu wa karibu yao walioko katika utawala na hivyo kampeni kujikita katika siasa za makundi na kambi mbalimbali. Takribani nusu ya wagombea walioshinda wana undugu na watu mbalimbali katika utawala ama baba, kaka, wanandoa nakadhalika. Pia palikuwa na malalamiko ya kuwepo kwa kampeni za kuchafuana hususani kupitia jumbe za simu za mkono.(SMS). Lakini katika hali ya kushangaza na pengine yenye kuleta hisia za kulindana wagombea hao hao walihutubia na kutangaza kwamba mchakato mzima ulikuwa wa kidemokrasia. Kwa upande wa kundi C la upinzani hali ilikuwa mbaya zaidi, kwa ujumla wapiga kura ambao pia ni wabunge wa jamhuri ya Muungano wengi wao walipiga kura kwa shinikizo na maelekezo. Usiku wa kuamkia siku ya kupiga kura wabunge wa CCM walikutana kama kamati ya chama chao(party caucus). Vyanzo vya kuaminika vimedokeza kwamba kupitia kikao hicho aliyekuwa Mwenyekiti wa Kikao Mheshimiwa Edward Lowasa ambaye pia ni Waziri Mkuu alitoa maelekezo kwamba imeamuliwa kura zote za wabunge wa CCM apewe mgombea wa UDP Dk. Fortunatus Masha. Vyanzo mbalimbali vinaeleza kuwa hoja hii ilizua mjadala huku wachache wakiipinga waziwazi lakini mwisho shinikizo na maelekezo hayo yalibadili upepo wa uchaguzi. Sababu za kufikia uamuzi huu zilizotolewa ni pamoja na hisia kwamba Profesa Baregu angekuwa na msimamo usiyoyumbishwa katika masuala fulani fulani na kwa upande mwingine hofu kwamba kumpa fursa hiyo ingekuwa ni kama kuijenga CHADEMA kisiasa. Kwa ujumla ufisadi na shinikizo vilifanya wengi ya wabunge wapige kura si kwa kuzingatia zaidi uwezo wa wagombea na maslahi ya taifa na hivyo kufanya uchaguzi kutokuwa huru na wa haki hususani katika kundi la vyama vya upinzani.

Chanzo: Tovuti ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
 
Hivi haya mafuta ya ZNZ yako wapi na yalipatikana lini??? Mimi sioni sababu ya kutoana macho kwa kitu kisichokuwepo. Last year consultant alisema hakuna mafuta ZNZ, sasa badala ya kuutumia huo muda kujadili mambo mengine ya maendeleo wao bado wanagombania mfuta yasiyokuwepo. Unless I am missing something, the last time I follwed the topic on ZNZ oil report I remeber it said that there was no potential of oil reserves in both Pemba nad Unguja. Sasa hii story ya mafuta oh, mafuta ah, mimi nashindwa kuilewa. Hizo nguvu wangezihamishia kwenye madini nafikiri sasa tungekuwa tunafaidika zaidi badala ya kupata 3 % loyality.
 

BARAKA SHAMTE of all persons? Hapa dada yangu hapana kitu, tafadhali tafuta profile yake itasum up everything.
 

Wewe ni mzalendo wa kupigiwa mfano Mmungu akuwezeshe uendele na mawazo hayo hayo .serekali ya Tanzania inasema nchi ni changa kipatao chake ni kidogo kwa hiyo inahitaji misada ili kujiendesha na inawataka wanachi wawe wastahamilivu na hali ya maisha.
 
Hebu nisaidieni kuelewa; kuna haja gani ya kujadili hilo swala la mafuta? Nilifikiri mali asili na utalii wa nchi hii viko wazi jinsi gani viwe managed? Na kama ilikuwa haijulikani tangu awali basi ni wazi lazima lijadiliwe tukubaliane yawe treated namna gani. Je kuna mali asili ya Zanzibar na Tanganyika au yote ni ya Tanzania? Hivi vitu lazima viwe wazi vinginevyo watu watajiona kama vile wako kwenye kutawala au kutawaliwa. Wanaotaka kuyamiliki obviasli ni wabinafsi, in a wei wanajitoa kwenye 'umoja' kwa njia isiyokubalika na ndicho prof. anachozungumzia.

Mimi naona Pof Baregu yuko makini sana.
 

Swala la mali ya asili yetu iko mismanaged ndiyo maana serikali inishia na 3 % Mafisadi kwa kuwatumia the so called wawekezaji wanapata 97 %. Actually wazanzanzibari wana haki ya kupigania umiliki wa mali yao ili isije wakatapeliwa kama ilivyo sasa. Tatizo langu ni kwamba watu wanapigania mali isiyokuwepo (mafuta) wakati mali iliyopo (madini) wameshindwa kui-manage!!!!!!!
 

Mwenye macho haambiwi tazama! Mafuta hakuna Zanzibar lakini kwa tamaa zao wanangangana nayo. Nini kitapotea kwa kuwaambia sawa chukueni hayo mafuta. Basi!!.
Kwanini iwe issue na iwe tishio kwa Muungano? Tishio lilikuwa lile la kudai kuwa Zanzibar ni nchi pengine lingekuwa tishio kwa Muungano lakini la upande mmoja kudai haki yake si tishio bali ni nyenzo muhimu kwa Muungano. Isitoshe upande mmoja unaendelea kuvuna chake bila kugawana na upande mwengine. Sasa tabu iko wapi hapa, Muungano upo pale pale wala hauna mtikishiko wowote kwani pande zote si za Waungwana? Waungwana wanakuwa na kauli moja. tumia chako nitunie changu Basi.
 
Sasa wanasema tunauza mbuzi!

Mbuzi yupo ktk gunia!!!

Fungua basi gunia mbuzi tumwone???

Je kuna mafuta kweli????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…