Mwinyi Mndengereko.
..hakuna haja ya kuanzisha serikali ya Tanganyika.
..masuala ya Tanganyika yanashughulikiwa na serikali ya Muungano.
..kama Zanzibar hawako tayari kuvunja SMZ na masuala yote yashughulikiwe na serikali ya Muungano basi wachukue hatua za kujitoa ktk Muungano.
NB:
..msimamo wangu mimi huu Muungano uvunjwe tu.
kwa taarifa yako "vijisenti" vilivyowekezwa hapo ni sehemu ya faida ya pesa za dakaa, wazenj bwana ruti zao "umangani", " masteti" na london, hakuna atakae pata presha, wote walikuwa huku huku visiwani ufisadi tu wa SMT kuiharibia zanzibar biashara ndo vimewasukuma huko, na nyinyi mlikuwa mkija huku kuchukua vitu na kuviuza huko,na mkaona gere komandoo alipofanya bandari huru, sasa achilieni muone kama zanzibar haitafika 2025, kama singapore.
Nkazahau,
Fed. gov. unayozungumzia kwa Visiwani na Bara..hizo 97% ya pesa kuendesha Fed. Gov. zitatoka bara!
Maana ukiangalia idadi ya watu: 97% ya Watanzania wanatoaka Bara na 03% ndo wanatoka visiwani!
Na kwa hiyo hata mawaziri atatoka tu mmoja au may be wawili, Wabunge yaani watakuwa 03% ya wabunge wa sasa yaani Visiwani watatoa tu Wabunge kama 10 wakati Bara watatoa zaido ya 300!
Bado tuko pale2: je hiyo serikali ya 3 nani ataiharamia? kama ni Bara: basi mfumo wa sasa bado una faida zaidi Visiwani!
Wakati watanzania leo wanadhimisha miaka 45 ya Muungano wa Tanyanyika na Zanzibar, Kiongozi Mwandamizi kutoka Ofisi ya Waziri Kiongozi Zanzibar, Enzi Talib Aboud amesema wakati umefika Serikali ya Tanganyika ikarejeshwa.
Hayo ameyaeleza katika mada yake iliyowasilishwa katika kongamano la kitaifa kwa niaba yake na Mwanasheria Ali Omar ambalo limewashirikisha wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya Zanzibar, viongozi mashuhuri wasomi, na viongozi wa vyama vya siasa wakiwemo wa CCM na CUF.
Aboud alisema kwamba serikali ya Tanganyika irejeshwe ili iweze kusimamia mambo ambayo hayamo katika orodha ya muungano kwa upande wa Tanzania bara ili kuwa na mfumo kama unaotumika Zanzibar.
Amesema tangu kufikiwa kwa Muungano serikali ya Zanzibar imekuwa na katiba na serikali yake ambayo inasimamia mambo ya ndani ya Zanzibar ambayo hayamo katika orodha ya mambo ya Muungano.
kwa kutumia katiba ya Tanganyika iundwe serikali ya Tanganyika inayoshughulikia mambo yake ambayo sio ya Muuungano alisema Enzi katika mada yake hiyo.
Alisema kwamba uchumi wa Zanzibar umekuwa ukififia kutokana na vikwazo mbali mbali vilivyomo katika mfumo wa muungano na kushauri Zanzibar ipate haki zake zote za misaada, utambulisho wake wa kidola na uwakilishi wake katika jumuiya za kimataifa ili iweze kukuza uchumi na kuinua kipato cha wananchi wake.
Vile vile alisema mbali na kurejeshwa na serikali ya Tanganyika pia katiba ya Tanganyika inapaswa kuwepo ili iweze kusimamia mambo ya ndani ya Tanganyika na mambo ya Muungano yashughulikiwe na serikali ya Muungano.
Aboud ambaye ni Mwadhishi wa habari mkongwe aliewahi kufanya kazi katiak vyombo vya habari kadhaa ya Tanzania Bara na kukamata nafasi za juu za serikali ya Zanzibar na ndani ya Chama CCM alisema kwamba wakati umefika mkataba wa awali wa muungano ukapelekwa katika baraza la wawakilishi ili wajumbe wapata nafasi ya kuridhia mkataba huo.
Baraza la kutunga sheria la Zanzibar kwa sasa ambao ni baraza la wawakilishi lipewe nafasi ya kuridhia mkataba huu ili kuupa uhalali wa kisheria kwa upande wa Zanzibar alisema Kiongozi huyo.
Alisema mkataba huo wa Muungano baada ya kufikiwa mwaka 1964 uliridhiwa na upande mmoja wa muungano lakini baraza la kutunga sheria wakati huo Zanzibar (Baraza la Mapinduzi) halikupewa nafasi ya kuridhia
Kiongozi huyo mwandamizi amesema kwamba orodha ya mambo ya muungano hivi sasa imeongezeka kutoka 11 hadi 38 na kuzua mjadala mrefu kutoka pande mbili za muungano kwa vile umefuta baadhi ya mambo ya msingi yaliokuwemo awali katika orodha ya mambo ya muungano.
Hakuna awezae kubisha kwamba tokea kuasisiwa kwake muungano huu umejengeka kutokana na khofu, kutiliana shaka na kutoaminiana baina ya pande mbili zinazounda ambapo wakati mwengine hupelekea hata kutishia uhai wa muungano wenyewe alisema Aboud katika mada yake.
Kiongozi huyo mwandamizi wa SMZ alikumbusha historia ya Rais wa awamu ya pili Aboud Jumbe Mwinyi alipolazimishwa kujiuzulu pamoja na aliyekuwa Waziri Kiongozi wake Maalim Seif Shariff Hamad na wenzake sita waliokuwa na msimamo wa kutaka kuitishwa kura ya maoni kuhusu Muungano.
Hata hivyo alisema kwamba nafasi bado ipo ya kutosha ya kutatua kero za muungano lakini lazima mijadala yake ifanyike kwa uwazi na kuweka mbele maslahi ya taifa hasa katika maeneo ya kiuchumi na misingi ya kuendeleza muungano wenyewe.
Kongamano hilo limefuatia maandamano yalizuwiwa kuunga mkono suala la mafuta na gesi asilia kuondolewa katika orodha ya mambo ya muungano kama ilivyopendekezwa na wajumbe wa baraza la wawakilishi Zanzibar.
Mapema juzi Mkuu wa Polisi wilaya ya Mjini, Mkadam Khamis Mkadam alisema suala la mafuta na gesi asilia ni suala la kikatiba na linapaswa kujadiliwa na mabaraza ya kutunga sheria na sio jumuiya au taasisi nyengine hivyo jeshi la polisi haliwezi kuruhusu kufanyika kwa maandamano hayo.
Wakishangia mada katika kongamano hilo lililoandaliwa na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) baadhi ya washiriki walisema tatizo kubwa linaloukabili muungano ni kuwa wananchi hawajashirikishwa kabla ya kufikiwa muungano huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini wa UPDP Haji Othman Haji alisema kwamba muungano ulifikiwa kwa mamuzi ya Nyerere na Karume lakini wananchi hawakupewa muda wa kutosha wa kufikiria na kuamua katika suala hilo.
Tatizo kubwa linalokabili muungano wetu wananchi hatukupata nafasi ya kutosha kuamua kwa vile ilikuwa ni makubaliano ya viongozi wawili kwa niaba ya wananchi wao alisema kiongozi huyo.
Professa Abdul Sharif ambaye ni mtafiti wa mambo ya historia alisema wananchi katika taifa wamegawanyika kutokana na mitizamo tofauti kuhsuu muungano ambapo wapo wanaofikiria muungano uvunje na uundwe upya ili kuwepo na muungano wenye mashahi ya kiuchumi badala ya kisiasa pekee.
Kwa upande wa Ali Mohammed Said alisema wananchi wajadili uhalali wa muungano wenyewe badala ya kujadili kero za muungano kwa kile alichodai kuwa ufumbuzi wa mambo ya muungano ni kurudi kuangalia mfumo wa muungano.
Awali Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar Ustadh Farid Hadi aliwataka wananchi wa Zanzibar kuondoa woga na kujadili kwa uwazi matatizo yanayoukabili muungano kwa maslahi ya wananchi wake na vizazi vijavyo.
Watu waondoshe khofu wawe huru kujadili ikiwa wewe mzee wa miaka 70 au 65 sijui unaogopa nini kwa vile umekuwepo miaka mingi lakini umeshindwa kuelezea ukweli juu ya muungano alieleza Ustadh huyo.
Kongamano hilo limefungwa na Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Juma Duni Haji ambapo mada tatu zimewasilishwa ikiwemo Athari za Muungano kwa Uchumi wa Zanzibar, Athari za Muungano kwa Utamaduni wa Zanzibar na Zanzibar katika Muungano ambapo awali Naibu Waziri Kiongozi Ali Juma Shamhuna alitarajiwa kulifungua lakini hakuhudhuria kutokana na kukabiliwa na majukumu mengine ya kikazi.
safi sana Karume
kilichobaki tugawane kila mmoja kivyake
Dunia ya leo naamini ZNZ wanaweza kusuyrvive tuu bila matatizo na sie tukaendelea kubaki na MAFISADI wtu
SIJUI TUNANGANGANIA NINI
Sherehe kubwa kama hizo Rais analala mpaka saa 2 abubuhi kama si uhuni nini?
Naona umeishiwa Hoja kwani CUF pia walikwambieni mkatae SHIRIKISHO LA AFRIKA MASHARIKI? Kwani kwenu Muungano si sawa na Ibada kila ukiifanya sana ndio utapata pepo zaidi? Basi ipelekeni nchi shirikisho la Afrika Mashariki huko hilo Limuuungano litakuwa kubwa zaidi.
..kama CUF wako serious hawataki Muungano basi ni vizuri hizi hoja zao wakazizungumzia ndani ya Bunge la Muungano.
..sasa hivi kuna kikao cha Bunge kinaendelea sasa tunasubiri kusikia CUF wakileta hoja ya kuvunja Muungano, au kuunda serikali ya Tanganyika.
jamani mbona hii hadithi iko upande mmoja tu? Je inamaanisha ni wazanzibari tu wanaokerwa na muungano? Azimio la G 55 linamaana gani? Nadhani mpaka tutakapokuwa wakweli na kuona mitizamo na hisi ya Tanzania na zanzibar ndipo tutaweza kutatua tatizo hili. Maana mjadala wetu bado unarudia makosa yale yale ya kikatiba ya kusahau Tanganyika.
Wakishangia mada katika kongamano hilo lililoandaliwa na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) baadhi ya washiriki walisema tatizo kubwa linaloukabili muungano ni kuwa wananchi hawajashirikishwa kabla ya kufikiwa muungano huo.
wazanzibar tumechoka na muungano
na hivi sasa tumeletewa ukiristo na wakiristo ndio wenye nguvu katika utawala wa zanzibar.
nasie wazanzibar eti tumebakia wazanzibar 99% kumbe uongo sasa imekuwa wazanzibar 60% wakiristo 40% kutoka bara.
kama tunavyojua zanzibar hakuna wakiristo wala hakuna mkiristo sasa karume ndio katujazia na kuiaribu nchi.
Junius,
Mkuu wangu huu ni mwaka wa 7 toka nimetoa suggestion ya referendum kwa viongozi wa CUF bara na visiwani..Nilimwandikia in personal, Sharrif Hamad (2003) kuhusiana na hili na hakunijibu pengine yawezekana hakupata ujumbe wangu..
Kwa nini viongozi wote wanacheza mchezo wa siasa mahala ambapo wazi waamuzi wa Muungano ni wananchi wenyewe?.. Kama kweli wananchi wa Zanzibar wanataka Muungano ufe, Referendum ndio mwamuzi na ikumbukwe tu kwamba Bara na Visiwani hapatakalika!..
Leo hii kuna Wapemba na Wakomoro kibao bara, Wabara wapo Visiwani wote wana enjoy uraia wao kwa sababu ya Muungano wa watu na sio nchi wala vyama..Muungano Ukivunjika tu kuweni tayari kwa yote yatokanayo na kuvunjika kwa Muungano huu, kwani Mapinduzi ya mwaka 1964 yalifanywa na wahuni wakuli wabeba mizigo bandarini walioweka rekord ya dunia ktk Mapinduzi ya haraka!.
Katika siku kama ya leo (Muungano) utaona clip ya marehemu Mwl Nyerere kwenye tv mbalimbali, akichanganya udongo kuashiria muungano wa Tanganyika na Zanzibar (au zanzibar na Tanganyika).
Swali langu ni; udongo huo ni wa wapi?? Dar na Zanzibar?; Butiama na Zanzibar? Butiama Unguja? Songea na Zanzibar? Rukwa Na Pemba?? Bagamoyo na kusini unguja?! oohps!!
I am confunsed, naombeni jibu.
hee, Mbona mchanganyaji ni mmoja? au Karume hakuwafiki?