Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Mwinyi Mndengereko.

Naona unaenda mbali sasa, karibu 99% ya wazanzibari (ukimuhesabu mpaka sultani aliepinduliwa 1964) wana damu ya ki Afrika kama sio ya kindengereko basi ni ya kimanyema, kimakondo, kizigua, kinyamwezi, kizaramu etc hivyo hii haimaanishi kuwa mndengereko si mzanzibari, ukisema mzanzibari ina maana pana sana yakhe 🙂
 
..hakuna haja ya kuanzisha serikali ya Tanganyika.

..masuala ya Tanganyika yanashughulikiwa na serikali ya Muungano.

..kama Zanzibar hawako tayari kuvunja SMZ na masuala yote yashughulikiwe na serikali ya Muungano basi wachukue hatua za kujitoa ktk Muungano.

NB:

..msimamo wangu mimi huu Muungano uvunjwe tu.

Jee, Nchi zikiungana zinakuwa na Serikali ngapi?, hapa kwetu kuna serikali mtoto lakini baba hajulikani na mama hajulikani! si ajabu hii. Serikali baba ni ipi? Serikali mtoto (Tanzania), Serikali mama ni ipi?

Ukitatuwa utata huo utaweza kutatua utata wa utatu!

Bila kuwa na Serikali mbili tofauti (Tanganyika (mama au baba) na Zanzibar mama au baba) halafu zikatatuwa matizo yaliyokuwepo (zikazaa mtoto) na kuunda Serikali moja (nazo zikafa), ambae ni Tanzania, hakuna cha kutatuwa.
 
Dar Es Salaam,
tatizo kubwa lipo ktk CCM chama hiki ni kimoja na hakiwezi kuwa na mfumo huo Visiwani kwani hukjo kuna Baraza la Mapinduzi ambao kwa kila kitu wanatofautiana na CCM bara.. isipokuwa wanabebana tu.
 
hali ya maisha imekua ngumu sana kwasababu ya muungano. kwasababu msisahau kama zanzibar ni sehemu ya biashara tangu enzi hizo. hakuna viwanda kama bara. sasa zile sekta zote za biashara zimeuliwa kutokana na system ya muungano. wazanzibar wanakufa njaa kwahiyo hawataki. huko bara endeleni kufuga mafisadi.
 
kwa taarifa yako "vijisenti" vilivyowekezwa hapo ni sehemu ya faida ya pesa za dakaa, wazenj bwana ruti zao "umangani", " masteti" na london, hakuna atakae pata presha, wote walikuwa huku huku visiwani ufisadi tu wa SMT kuiharibia zanzibar biashara ndo vimewasukuma huko, na nyinyi mlikuwa mkija huku kuchukua vitu na kuviuza huko,na mkaona gere komandoo alipofanya bandari huru, sasa achilieni muone kama zanzibar haitafika 2025, kama singapore.


Umangani!!! utakutana na popo bawa London nako huweziongea kitu .wachakudanganya kadamnasi .sisi tumehamia india china kuchukua wenyewe!!!! na hao mabwana umangani tunakutana nao wananunua huko huko .ujinga kufika kurudi weka maboya.wakati ni huu!!! anza wewe mie namalizia!!! kuutwa kuona wabara wa shamba.imepitwa na wakati kujenga inchi kwa kwenda mbele.umangani simali kitu.maisha ya megeuka.vitu kede kede.wamanga wakiwa likizo wako huku telee!!! umechelewa umelala wapi?nanyinyi mpaka leo mnachukua hatuwasemi .wewe unamatatizo utakaa kusifia wenzako mpaka lini??????? fanyakazi kwabidii .singapore.unayo mikononi.umangani.pia.london jibidishe maendeleo utayaona.lakini kama ni taarabu !!!!!!!!!!! oho!!!! utalaumu hata akitawala babu yako!!!!!!!! upokee ushauri wa bure1!!!!!!!!!!
 
wazanzibar tumechoka na muungano

wazanzibar tumechoka na muungano. historia ya zanzibar waliokuja kuua watu 1964 ni kutoka bara waliotumwa na nyerere na kumuweka karume ambaye hakuzaliwa mwera na kuharibiwa historia yetu na kupandikiziwa wabara kama wazenj.

jumbe naye mbara akapewa urais na nyerere baada nyerere kumuua karume na kusema aliuliwa na waarabu.
hivi majuzi amani karume alisema suala ya muungano zanzibar wasikilizwe wazanzibar halisi na wakati wazanzibar halisi ndio wamechoshwa na muungano huo.

yeye karume pamoja na wazee wake wote wawili sio wazenj baba yake ni mtumwa aliyekimbia ngome kongwe akalelewa na wazenj kwa kuonewa huruma na mama yake ni mtumwa aliyezaliwa kwa kuingiliwa na waarabu na hii ipo wazi.

makamo wa rais muungano ni mnafiki anayetetea tumbo lake mwenyewe na wala hana msaada wowote katika zanzibar anaouchangia.
pamoja na mawaziri waliochaguliwa kutoka zanzibar katika muungano hawana mchango wowote.

misaada ya kitaifa inayoifikia tz zanzibar hainufaiki chochote. huku ndio kuonewa na kuibiwa.

hivi sasa kuna serikali za muungano 2.

1... muungano wa tz na

2...muungano wa smz na haya sio siri kwani kuna wazanzibar, wazanzibara na wahamiaji katika smz.

tulichoomba ni serikali 3'/

1.tanganyika
2.zanzibar.
3. muungano

na hivi sasa tumeletewa ukiristo na wakiristo ndio wenye nguvu katika utawala wa zanzibar.
nasie wazanzibar eti tumebakia wazanzibar 99% kumbe uongo sasa imekuwa wazanzibar 60% wakiristo 40% kutoka bara.
kama tunavyojua zanzibar hakuna wakiristo wala hakuna mkiristo sasa karume ndio katujazia na kuiaribu nchi.

tukienda kwenye YouTube - Broadcast Yourself. alafu uandike zanzibar 1964 hapo ndipo mutopooona wabara walivyotufanya.

waliwaua wazee wetu pamoja na waarabu na waliingia kila nyumba na kuwaua wanaume wote na hili linajulika.

lakini walituziba midomo kwa kutuua na kuibadilisha historia,
ndio ukaona kila kabla ya uchaguzi wabara huja zanzibar na kupiga watu na kuua na hili linajulika.

sie kama wazenj hatutaki muungano na wala hatutaki udugu na wabara na walio zenj wanaoji wazanzibara warudi makwao

tushachoka na ujanja na wizi na kutuharibia nchi yetu
 
Nkazahau,

Fed. gov. unayozungumzia kwa Visiwani na Bara..hizo 97% ya pesa kuendesha Fed. Gov. zitatoka bara!

Maana ukiangalia idadi ya watu: 97% ya Watanzania wanatoaka Bara na 03% ndo wanatoka visiwani!

Na kwa hiyo hata mawaziri atatoka tu mmoja au may be wawili, Wabunge yaani watakuwa 03% ya wabunge wa sasa yaani Visiwani watatoa tu Wabunge kama 10 wakati Bara watatoa zaido ya 300!

Bado tuko pale2: je hiyo serikali ya 3 nani ataiharamia? kama ni Bara: basi mfumo wa sasa bado una faida zaidi Visiwani!

Fairness itakuja kwenye federal taxes zikiwa sawa nchi nzima, of course kama una watu wengi basi utalipa pesa nyingi lakini kumbuka pia kuwa serikali ya Muungano itatumia hizi pesa kufanyia shughuli zake zaidi kwenye watu wengi, kama Jeshi na polisi basi at least 90% wapo Tanganyika (huu ni mfano tu), hutegemei Zanzibar kulipa 50% ya gharama za serikali za muungano wakati inatumia let say 5% ya gharama hizo - right?.

Sasa kwa unavyotaka wewe hakutokuwa na haki hata kama tutakuwa na serikali 25 za kila mkoa na moja ya muungano. Kama Tanganyika ina watu 97% pia itakuwa na 97% uwakilishi kwenye bunge ambayo inamaanisha kuwa watakuwa na sauti zaidi kwenye maamuzi ya kimuungano (still not fair), katiba itaamua zaidi kuhusu mambo mengine lakini zanzibar haiwezi kutegemea kuwa na wabunge wengi kama ilivyo sasa (hii ni fact).
Kuwa na serikali za Tanganyika na Zanzibar zenye mamlaka fulani kutapunguza hii fikra ya kujihisi kuwa sehemu moja inaiamulia sehemu nyengine mambo yake au inabebwa au inabeba. Ingawaje kwa kiasi fulani itakuwa hivyo lakini haitokuwa kama sasa lakini ni mwanzo unaohitajika.
 
Wakati watanzania leo wanadhimisha miaka 45 ya Muungano wa Tanyanyika na Zanzibar, Kiongozi Mwandamizi kutoka Ofisi ya Waziri Kiongozi Zanzibar, Enzi Talib Aboud amesema wakati umefika Serikali ya Tanganyika ikarejeshwa.

Hayo ameyaeleza katika mada yake iliyowasilishwa katika kongamano la kitaifa kwa niaba yake na Mwanasheria Ali Omar ambalo limewashirikisha wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya Zanzibar, viongozi mashuhuri wasomi, na viongozi wa vyama vya siasa wakiwemo wa CCM na CUF.

Aboud alisema kwamba serikali ya Tanganyika irejeshwe ili iweze kusimamia mambo ambayo hayamo katika orodha ya muungano kwa upande wa Tanzania bara ili kuwa na mfumo kama unaotumika Zanzibar.

Amesema tangu kufikiwa kwa Muungano serikali ya Zanzibar imekuwa na katiba na serikali yake ambayo inasimamia mambo ya ndani ya Zanzibar ambayo hayamo katika orodha ya mambo ya Muungano.

“kwa kutumia katiba ya Tanganyika iundwe serikali ya Tanganyika inayoshughulikia mambo yake ambayo sio ya Muuungano” alisema Enzi katika mada yake hiyo.

Alisema kwamba uchumi wa Zanzibar umekuwa ukififia kutokana na vikwazo mbali mbali vilivyomo katika mfumo wa muungano na kushauri Zanzibar ipate haki zake zote za misaada, utambulisho wake wa kidola na uwakilishi wake katika jumuiya za kimataifa ili iweze kukuza uchumi na kuinua kipato cha wananchi wake.

Vile vile alisema mbali na kurejeshwa na serikali ya Tanganyika pia katiba ya Tanganyika inapaswa kuwepo ili iweze kusimamia mambo ya ndani ya Tanganyika na mambo ya Muungano yashughulikiwe na serikali ya Muungano.

Aboud ambaye ni Mwadhishi wa habari mkongwe aliewahi kufanya kazi katiak vyombo vya habari kadhaa ya Tanzania Bara na kukamata nafasi za juu za serikali ya Zanzibar na ndani ya Chama CCM alisema kwamba wakati umefika mkataba wa awali wa muungano ukapelekwa katika baraza la wawakilishi ili wajumbe wapata nafasi ya kuridhia mkataba huo.

“Baraza la kutunga sheria la Zanzibar kwa sasa ambao ni baraza la wawakilishi lipewe nafasi ya kuridhia mkataba huu ili kuupa uhalali wa kisheria kwa upande wa Zanzibar” alisema Kiongozi huyo.

Alisema mkataba huo wa Muungano baada ya kufikiwa mwaka 1964 uliridhiwa na upande mmoja wa muungano lakini baraza la kutunga sheria wakati huo Zanzibar (Baraza la Mapinduzi) halikupewa nafasi ya kuridhia

Kiongozi huyo mwandamizi amesema kwamba orodha ya mambo ya muungano hivi sasa imeongezeka kutoka 11 hadi 38 na kuzua mjadala mrefu kutoka pande mbili za muungano kwa vile umefuta baadhi ya mambo ya msingi yaliokuwemo awali katika orodha ya mambo ya muungano.

“Hakuna awezae kubisha kwamba tokea kuasisiwa kwake muungano huu umejengeka kutokana na khofu, kutiliana shaka na kutoaminiana baina ya pande mbili zinazounda ambapo wakati mwengine hupelekea hata kutishia uhai wa muungano wenyewe” alisema Aboud katika mada yake.

Kiongozi huyo mwandamizi wa SMZ alikumbusha historia ya Rais wa awamu ya pili Aboud Jumbe Mwinyi alipolazimishwa kujiuzulu pamoja na aliyekuwa Waziri Kiongozi wake Maalim Seif Shariff Hamad na wenzake sita waliokuwa na msimamo wa kutaka kuitishwa kura ya maoni kuhusu Muungano.

Hata hivyo alisema kwamba nafasi bado ipo ya kutosha ya kutatua kero za muungano lakini lazima mijadala yake ifanyike kwa uwazi na kuweka mbele maslahi ya taifa hasa katika maeneo ya kiuchumi na misingi ya kuendeleza muungano wenyewe.

Kongamano hilo limefuatia maandamano yalizuwiwa kuunga mkono suala la mafuta na gesi asilia kuondolewa katika orodha ya mambo ya muungano kama ilivyopendekezwa na wajumbe wa baraza la wawakilishi Zanzibar.

Mapema juzi Mkuu wa Polisi wilaya ya Mjini, Mkadam Khamis Mkadam alisema suala la mafuta na gesi asilia ni suala la kikatiba na linapaswa kujadiliwa na mabaraza ya kutunga sheria na sio jumuiya au taasisi nyengine hivyo jeshi la polisi haliwezi kuruhusu kufanyika kwa maandamano hayo.

Wakishangia mada katika kongamano hilo lililoandaliwa na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) baadhi ya washiriki walisema tatizo kubwa linaloukabili muungano ni kuwa wananchi hawajashirikishwa kabla ya kufikiwa muungano huo.

Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini wa UPDP Haji Othman Haji alisema kwamba muungano ulifikiwa kwa mamuzi ya Nyerere na Karume lakini wananchi hawakupewa muda wa kutosha wa kufikiria na kuamua katika suala hilo.

“Tatizo kubwa linalokabili muungano wetu wananchi hatukupata nafasi ya kutosha kuamua kwa vile ilikuwa ni makubaliano ya viongozi wawili kwa niaba ya wananchi wao” alisema kiongozi huyo.

Professa Abdul Sharif ambaye ni mtafiti wa mambo ya historia alisema wananchi katika taifa wamegawanyika kutokana na mitizamo tofauti kuhsuu muungano ambapo wapo wanaofikiria muungano uvunje na uundwe upya ili kuwepo na muungano wenye mashahi ya kiuchumi badala ya kisiasa pekee.

Kwa upande wa Ali Mohammed Said alisema wananchi wajadili uhalali wa muungano wenyewe badala ya kujadili kero za muungano kwa kile alichodai kuwa ufumbuzi wa mambo ya muungano ni kurudi kuangalia mfumo wa muungano.

Awali Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar Ustadh Farid Hadi aliwataka wananchi wa Zanzibar kuondoa woga na kujadili kwa uwazi matatizo yanayoukabili muungano kwa maslahi ya wananchi wake na vizazi vijavyo.

“Watu waondoshe khofu wawe huru kujadili ikiwa wewe mzee wa miaka 70 au 65 sijui unaogopa nini kwa vile umekuwepo miaka mingi lakini umeshindwa kuelezea ukweli juu ya muungano” alieleza Ustadh huyo.

Kongamano hilo limefungwa na Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Juma Duni Haji ambapo mada tatu zimewasilishwa ikiwemo Athari za Muungano kwa Uchumi wa Zanzibar, Athari za Muungano kwa Utamaduni wa Zanzibar na Zanzibar katika Muungano ambapo awali Naibu Waziri Kiongozi Ali Juma Shamhuna alitarajiwa kulifungua lakini hakuhudhuria kutokana na kukabiliwa na majukumu mengine ya kikazi.

tatizo zanziba kuna mchanganyiko wa watu wengi watumwa ambao ndio akina karume ambao wao wanataka kutambulika kama wazanzibar.

na tukienda mwera tukiiuliza midoriani yote ni mdoriani kani uliomzaa karume hatupati jibu.
ndipo pale wazanzibar walipopiga kelele kuhusu muungano karume akasema waulizwe wazanzibar wa kweli kwani sie sio wazanzibar.

kuna wale waliokuja kwa mauaji walioletwa na nyerere hawakuwaua wazanzibar peke yao waliwachanganya na waarabu. tunajua karume yeye hakushiriki kwenye mauaji hayo lakini aliyajua kwani yeye na nyerere ndio waliopanga hata mkewe karume alikuri kwenye tvz 2001 mwaka

kuna wale waliokuja kwa mwenge
na kuna wale waliokija kwa ukiristo

sie wazanzibar tunasema hatutaki muungano na mzanzibar yeyote mutakayemsikia eti anataka muungano huyo sie ukimtizama baba ukiruka babu basi siye au hata baba pia siye mzanzibar

historia ya zanzibar imefanywa kama biblia.

tunachosema hatutaki muungano kila mmoja na kwao mutuone kama tutakufa na njaa.

hawa watu wamejazana zanzibar na wale watumwa imekuwa kuwabatiza vizazi eti kila mzanziba mtumwa.

hakuna mtumwa anajulikana
mzanzibar anajulikana

wauaji wanajulikana

waliokuja kwa mwenge wanajulika.
na waliokuja kwa ukiristo wanajulikana
 
safi sana Karume

kilichobaki tugawane kila mmoja kivyake

Dunia ya leo naamini ZNZ wanaweza kusuyrvive tuu bila matatizo na sie tukaendelea kubaki na MAFISADI wtu

SIJUI TUNANGANGANIA NINI

Sherehe kubwa kama hizo Rais analala mpaka saa 2 abubuhi kama si uhuni nini?

Ulitaka kusema "TUNANG'ANG'ANIA" au huu ni msamiati mpya kwenye kiswahili? Heshima mbele mkuu!!
 
Naona umeishiwa Hoja kwani CUF pia walikwambieni mkatae SHIRIKISHO LA AFRIKA MASHARIKI? Kwani kwenu Muungano si sawa na Ibada kila ukiifanya sana ndio utapata pepo zaidi? Basi ipelekeni nchi shirikisho la Afrika Mashariki huko hilo Limuuungano litakuwa kubwa zaidi.

eti yule kafiri aliyepewa ubunge kutokea zanzibar katika afrika mashariki anatokea wapi?
 
ikingie
YouTube - Broadcast Yourself.

zanzibar 1964 part 1

hapo ndio mutawaona watanganyika waliotumwa na nyerere walivyowasabaratisha wazanzibar na waislam.

na leo zanzibar kumejaa makafiri tukumbukeni mwaka 1964 wanajzana tena na kila uchaguzi wanatuletea majeshi watupige
 
..kama CUF wako serious hawataki Muungano basi ni vizuri hizi hoja zao wakazizungumzia ndani ya Bunge la Muungano.

..sasa hivi kuna kikao cha Bunge kinaendelea sasa tunasubiri kusikia CUF wakileta hoja ya kuvunja Muungano, au kuunda serikali ya Tanganyika.

ndio spika wa bunge ai kikwete?
 
jamani mbona hii hadithi iko upande mmoja tu? Je inamaanisha ni wazanzibari tu wanaokerwa na muungano? Azimio la G 55 linamaana gani? Nadhani mpaka tutakapokuwa wakweli na kuona mitizamo na hisi ya Tanzania na zanzibar ndipo tutaweza kutatua tatizo hili. Maana mjadala wetu bado unarudia makosa yale yale ya kikatiba ya kusahau Tanganyika.


Hao wanaobisha wanafanya hivyo for the sake ya kubisha tu.Inashangaza kuwa hawa watu hawana msimamo, pale Zanzibar waliposema wao ni nchi kulikuwa na kauli za na wao wapatiwe Tanganyika yao na hata kuwakumbuka G55. Sasa kwa kuwa kauli imetoka Zanzibar wanabisha.Hawajulikani nini wanataka isipokuwa linalokuja akilini ni kuwa labda wanataka kutawala wenzao na ni tabia ya watawala kungangania.
 


Wakishangia mada katika kongamano hilo lililoandaliwa na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) baadhi ya washiriki walisema tatizo kubwa linaloukabili muungano ni kuwa wananchi hawajashirikishwa kabla ya kufikiwa muungano huo.


Mwiba!
Mmh! Sikujua Jumuiya ya Uamsho ina malengo zaidi ya kuamsha waumini kuhusu mambo ya dini!
Au swala la Muungano limeshakuwa la kidini huko Zanzibar?
Au hii Jumuiya imebadili malengo?
 
wazanzibar tumechoka na muungano

na hivi sasa tumeletewa ukiristo na wakiristo ndio wenye nguvu katika utawala wa zanzibar.
nasie wazanzibar eti tumebakia wazanzibar 99% kumbe uongo sasa imekuwa wazanzibar 60% wakiristo 40% kutoka bara.
kama tunavyojua zanzibar hakuna wakiristo wala hakuna mkiristo sasa karume ndio katujazia na kuiaribu nchi.


Mchungajimakini!

Unapoandika punguza jazba

- Ni kweli kuwa wakristo ndio wenye nguvu katika utawala wa Zanzibar?

- Je ni kweli Zanzibar kuna Wakristo 40% na Wazanzibar 60%?

-Na hapo unamaana gani Wazanzibar wote ni waislam au wabara wote ni wakristo?

- Una uhakika kwamba wanaotoka bara kuja Zanzibar ni Wakristo tu au ndio ubaguzi wenyewe?
 
"For a long time Zenj wamekuwa wakitutake for a ride kwa udogo wao na sasa wanataka kingi.
Ni vyema muungano ukafilia mbali ili wenzetu warudi 1964.
Ila wajue kwamba
Ubaguzi wa rangi zanzibar upo
Ubaguzi wa kiitikadi usio na mfano Zbar upo
Matatizo ya kisiasa kati ya waliopindua na waliopinduliwa 1964 bado yapo
Umaskini uliokithiri ( kama huku bara ) Zbar uko

Kabla hamjatoka katika muungano yatatueni hayo la sivyo vibaraka wa sultani watakapokuja kwenu wabara itabidi tushirikiane nao tu".




Nadhani huelewi kuwa Zanzibar ilikuwa nchi kamili kabla ya 1964 na iliweza kujiendesha kiuchumi bila matatizo yoyote yale, vile vile kama unaweza angalia GDP au statistics zozote za kimaendeleo na kiuchimi za Zanzibar na Tanganyika kabla ya Muungano na ilivyo hivi sasa utaona ni nani anadhurika zaidi na huu muungano. Matatizo yote unayowatisha waZanzibari yapo pia Tanganyika na sehemu nyengine duniani na musione kuwa nyinyi ni wakombozi wa Zanzibar.

Unapozungumza kubebwa kwa serikali ya Zanzibar kumbuka pia kuwa serikali ya Zanzibar ilianza kufilisika wakati wa vita vya Kagera na mara baada ya vita wakati Nyerere alipotangaza miezi 18 ijayo itakuwa ya taabu, ukweli ni kwamba Nyerere alikuwa akibadilisha pesa Zanzibar, akichukua pesa za kigeni toka Zanzibar na kutupa pesa za madafu kwa exchange rate ambayo anaijua mwenyewe. Jumbe akienda baraza la mawaziri na kuwaambia tu ametoa kiasi fulani kuwapa bara bila ushauri wa mtu yoyote yule, sio kuwa tukihitaji pesa za madafu lakini tuliamini umoja na kuwasaidia wenzetu wala hatukusema kuwa tunawabeba hadi leo, leo tumefilisika mumesahau mpaka fadhila eti munatubeba na kutusimanga, sijui ni watu wa aina gani ndugu zetu nyinyi, kutusaidia hamutaki mpaka mutusimange tukitaka kutafuta misaada kwengine munanuna na kutuzuia, mfano OIC.

Hizi siasa za kisultani zimemalizika tangia 1964, hivi bado unafikiri kuna muarabu ambaye atataka kuja kutawala Zanzibar leo? afanalek!!!!!
 
Last edited:
Junius,
Mkuu wangu huu ni mwaka wa 7 toka nimetoa suggestion ya referendum kwa viongozi wa CUF bara na visiwani..Nilimwandikia in personal, Sharrif Hamad (2003) kuhusiana na hili na hakunijibu pengine yawezekana hakupata ujumbe wangu..

Kwa nini viongozi wote wanacheza mchezo wa siasa mahala ambapo wazi waamuzi wa Muungano ni wananchi wenyewe?.. Kama kweli wananchi wa Zanzibar wanataka Muungano ufe, Referendum ndio mwamuzi na ikumbukwe tu kwamba Bara na Visiwani hapatakalika!..

Leo hii kuna Wapemba na Wakomoro kibao bara, Wabara wapo Visiwani wote wana enjoy uraia wao kwa sababu ya Muungano wa watu na sio nchi wala vyama..Muungano Ukivunjika tu kuweni tayari kwa yote yatokanayo na kuvunjika kwa Muungano huu, kwani Mapinduzi ya mwaka 1964 yalifanywa na wahuni wakuli wabeba mizigo bandarini walioweka rekord ya dunia ktk Mapinduzi ya haraka!.

Hili suala la kuvunja Muungano ni silaha ya mwisho inayotumiwa na Watanganyika katika kutaka kuendeleza unyanysaji juu ya Wazanzibari. Hapana pahala ambapo Wazanzibari wamesema kuwa wanataka kuvunja Muungano na hii inathibitishwa na mada zinazozungumzwa kwa kipindi sasa.

Hivyo kusema kitu fulani kitolewe katika orodha kwa vile kulifanyika kimakosa ni sawa na kusema tuvunje Muungano?

Hivyo kusema kuwa kuwe na Serikali itakayokuwa kwa dhati ikishughulikia mambo ya nchi zote na hilo litawezekana kwa kuwepo serikali ya Tanganyika jambo litakaloweka mipaka kati ya shughuli za Muungano na zile za Tanganyika kwani hivi sasa hali hiyo inaumiza upande mwengine na pengine kubebesha mzigo upande mwengine Ni SAWA NA KUSEMA TUVUNJE MUUNGANO?

Hivyo kusema kuwa Zanzibar inajitambua kua ni nchi ndani ya muungano wa nchi mbili ni sawa na KUSEMA TUVUNJE MUUNGANO?

Imekuwa tabia ya upande wa Tanganyika kujibu hoja hizi kwa hisia ya kuvunja Muungano na katika hali ya kutoelewana yeyote atakuwa tayari kukabili chochote ili apate msingi wa haki yaani kujiamulia mambo yake hivyo kama kupata haki hiyo hakuna la kufanywa isipokuwa kuvunjwa kwa Muungano basi na iwe hivyo.

Zanzibar ilishakuwepo kabla ya Mapinduzi na kwa namna ambayo inaishi kivyake ndani ya Muungano huu haitokuwa tabu sana kama wanavyohisi upande mwengine, kujiendea kivyake na amini itakuwa kwa ari na kasi mpya ya kweli siyo ile ya bandia ya wanamtandao.
 
Katika siku kama ya leo (Muungano) utaona clip ya marehemu Mwl Nyerere kwenye tv mbalimbali, akichanganya udongo kuashiria muungano wa Tanganyika na Zanzibar (au zanzibar na Tanganyika).

Swali langu ni; udongo huo ni wa wapi?? Dar na Zanzibar?; Butiama na Zanzibar? Butiama Unguja? Songea na Zanzibar? Rukwa Na Pemba?? Bagamoyo na kusini unguja?! oohps!!
I am confunsed, naombeni jibu.

ule udongo haukutoka zanzibar.

ila walivyokwisha mazungumzo alimtuma mtu ende nje wakachoke udongo hata ukitizama vile vyombo vilivyotumika kubebea udogo au mchanga vyote ni vya bara.

engekuwa kimoja kutoka zenj basi chombo kimoja chengekuwa mkoba wa ukili au pakacha.

sasa jiuze mwenzewe janja ya njani?
 
hee, Mbona mchanganyaji ni mmoja? au Karume hakuwafiki?


mchanga wake mwenyewe ule usijiulize tizama hata vifaa vilivyobebewa mchanga ni kutoka bara .

karume yeye alikuwa akimtizama tu kwa jinsi ile alivyopewa ukubwa wa bure

engekuwa kaja nao karume basi engebebea mkoba wa ukili

nyerere kachota nje ikulu kwakwe
 
Back
Top Bottom