KipimaPembe
JF-Expert Member
- Aug 5, 2007
- 1,285
- 698
Hilo nalo ni neno, Mkuu...Yah ni kweli yapo.... mafuta ya nazi!
Angalia 1st post kuna attachmentWana JF, wapi naweza kupata huo mkataba wa mungano, kati ya Tanganyika na unguja ?
Kila nikiangalia sherehe za muungano hususani zile za mwaka 1964 ambazo huonyeshwa na vituo vya television karibu vyote kila tunapoazimisha sikukuu hiyo, huwa nashindwa kupata jibu kama kweli Karume aliridhia muungano huu au la!
miaka 43 tangu kuungana baina ya Tanganyika na Zanzibar
kuna matatizo mengi yamejitokeza tokea muungano huu kuasisiwa
wazanzibari kwa upande wao wanahisi kuwa muungano unawanyanyasa na kuwabigija kimaendeleo na kiuchumi na na mengi tu na kwa upande wa pili wa shilingi kuna wenye hisia kuwa wazanzibari wanapendelewa sana na Tanganyika imeumizwa sana kuingia kwenye muungano huu.
hivi sasa tukikarabia miaka 43 ya muungano wetu tumo tukijiandaa kuingia kwenye shirikisho la afrika mashariki
jee ni vipi tutaweza kupunguza kero zilizopo na kuhakikisha kila upande wa jamhuri yetu hauhisi kuwa unaburuzwa au kunyanyaswa.
Si kuna serikali ya Mapinduzi Zanzibar; Je imesaidia nini katika kuwa na uhuru wa kuzungumza mambo yao na hatimaye kuchangia kwenye serikali ya JMT.Suluhisho hapa ni Watanganyika kuunda Serikali yao. na kuwa na serikali ya shirikisho.
hapo kila nchi itakua huru kuzungumzia mambo yake na kuchangia kwenye shirikisho.
zaidi ni kuwa zanzibar wataendelea kudhurumiwa haki zao na bara katika nyanja zote za kiuchumi hususan misaada, michezo na hata kisiasa