Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Na huu walioutumia ndo utaratibu wa kuondoa mambo kwenye muungano? Nilidhani vikao vilivyokaa kuyaingiza haya mambo kwenye muungano ndo vyenye uwezo wa kuyatoa!

Kwa hiyo wenyewe wanaweza wakakaa na kuamua kuwa suala hili na lile hatutaki liwemo tena kwenye muungano. Nadhani hii ni flexible enough kuwawezesha kufanya kile ambacho kinalinda maslahi yao. Na ikiwa utaratibu ni rahisi namna hii sitarajii tena kusikia kelele za wapemba na waunguja kuwa muungano hivi au muungano vile. Watakua wanachukua hatua kama hizi au wakae kimya!

Kwa hili nawapongeza, wamekuwa practical na proactive badala ya ulalamishi tuliouzoea.
 
Hayo ni mawazo yako kwamba Mh. Karume alishuhudi kuchanganya udongo bila kukubali. cha muhimu ni ukweli ambao haupingiki kwamba udongo ulichanganywa na ukatumika kupandia mti.
 
Karume aliridhia na nadhani ndio maana akashiriki sherehe za kuchanganya udongo wa Zanzibar na ule wa Tanganyika
 
Hakika kwa wakti ule mwaka 1964 aliridhika na hiyo inatokana kutokana mazingira na upepo wa kisiasa wa miaka hiyo. Lakin sasa mimi ikiwa pamoja na wa znz wengi hatuoni manufaaa yake kiuchumi labda kijammii kuna manufaa kidogo.

Nashauri kama upo uwezekano ipigwe kura ya maoni kuangalia kama muungano huo kama ulivyo sasa unafaa au la
 
Ukweli ni kwamba kuwepo au kutokuwepo mafuta hakutakuwa na manufaa kwa wananchi kawa hakuna viongozi wenye wenye vision ya kuendeleza nchi. Ni bora yabaki huko huko zanzibar kwani hatujasikia serious corruption cases kama huku bara

Sana sana pato la nchi likiongezeka ni kununua magari zaidi ya kifahari na kutimiza anasa za viongozi wetu. Je wananchi wa Nigeria wananufaika na mafuta yao?
 
Hayo mafuta yamepatikana au ni ule mchezo wa "tukiokota shilingi milioni moja, mimi nikizichukua nitakupa laki mbili" ukifuatiwa na ugomvi wa watu wawili juu ya kiasi cha kugawana, hali kwamba mnaweza msiokote hata senti katika kutembea kwenu kote.
 
Mimi naona KWANINI WATANGANYIKA MSISIMAME KIDETE KUDAI SERIKALI yenu ili kuondoa zogo looooote hili.


Haya sasa WADANGANYIKA daini serikali yenu ili muwe na sauti nayo
 
Wana JF, wapi naweza kupata huo mkataba wa mungano, kati ya Tanganyika na unguja ?
Angalia 1st post kuna attachment

Kila nikiangalia sherehe za muungano hususani zile za mwaka 1964 ambazo huonyeshwa na vituo vya television karibu vyote kila tunapoazimisha sikukuu hiyo, huwa nashindwa kupata jibu kama kweli Karume aliridhia muungano huu au la!

Asingetia saini kama inavyoonekana kwenye 1st post
 
miaka 43 tangu kuungana baina ya Tanganyika na Zanzibar
kuna matatizo mengi yamejitokeza tokea muungano huu kuasisiwa
wazanzibari kwa upande wao wanahisi kuwa muungano unawanyanyasa na kuwabigija kimaendeleo na kiuchumi na na mengi tu na kwa upande wa pili wa shilingi kuna wenye hisia kuwa wazanzibari wanapendelewa sana na Tanganyika imeumizwa sana kuingia kwenye muungano huu.

hivi sasa tukikarabia miaka 43 ya muungano wetu tumo tukijiandaa kuingia kwenye shirikisho la afrika mashariki

jee ni vipi tutaweza kupunguza kero zilizopo na kuhakikisha kila upande wa jamhuri yetu hauhisi kuwa unaburuzwa au kunyanyaswa.

Suluhisho hapa ni Watanganyika kuunda Serikali yao. na kuwa na serikali ya shirikisho.

hapo kila nchi itakua huru kuzungumzia mambo yake na kuchangia kwenye shirikisho.

zaidi ni kuwa zanzibar wataendelea kudhurumiwa haki zao na bara katika nyanja zote za kiuchumi hususan misaada, michezo na hata kisiasa
 
Hakika kuna mengi yamesemwa na yanaendelea kusemwa.

sasa waungwana kwa ihsani zenu naomba tujadili hapa bila kugombana kubainisha faida wanazopata wa Zanzibari kutokana na huu muungano na hasara gani anazopata Mtanganyika.

Tupembue kwa kina kuona kwanini waTanganika wanalazimisha muungano?.


Mimi kama mchumi naona Kuna maonevu makubwa sana kwa zanzibar hususan katika nanja hii a uchumi katika misaada na mikopo ya nje.

nakaribisha mjadala.
Tujue kwanini watanganyika hawataki kunda Serikali yao ya Tanganyika?
 
Heri ikiwa ni nia ya kweli na ya dhati kwa BWZ na BMZ na nitawapa big up kwa kuweka mbele maslahi ya wazanzibar,,,,, lkn hofu yangu kuwa isije kuwa ni mchezo m-baya wa ccm kuelekea uchaguzi mkuu unaokuja kama wanavofanya kwa suala la mahakama ya kadhi,nahisi kama kuna ka-element flani hivi ya babaisha-*****... CCM HAWAAMINIKI HATA CHEMBE
 
mmmm this thread sounds like kisiwa ni chao maji na samaki ni vyetu!!
 
Last edited:
Kama wakitaka wajitenge kwa sababu ya mafuta itakuwa heri kabisa. Watakapoanza kuchapana mikwaju basi wataweza kutia akili.
 
Wanasiasa wa zanzibar nadhani nao wanafuata upepo wa wanasisa wa Tanzania bara kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2010.Tumesika misemo mingi katika kikao cha bunge Dodoma,wabunge wanajitahidi kubuni misamiati mingi ili ijekuwasaidia mara uchaguzi mkuu utakapowadia.

Mambo ya mafuta ni suala la muungano kuliondoa au kutoliodoa nilazima bunge la JMT lihusiswe si baraza la wawakilishi.Kulipeleka suala la mafuta kwenye kikao cha baraza la wawakilishi kwa kweli ni aina ya propaganda za wanasiasa wanaotaka kuifadhi nafasi zao za kisiasa kwa kutumia uelewa mdogo wa wananchi.

Naomba mwenye chanzo cha uhakika atuletee uthibitisho kama kweli mafuta yapo Zanzibar.Isije kuwa ni hadithi za kufikirika mnatuletea hapa jamvini.Nakumbuka kuna mtaalamu nadhani kutoka UK alishawaambia wawakilishi hakuna mafuta Zanzibar kidogo atolewa macho kwa kusema ukweli.
 
Suluhisho hapa ni Watanganyika kuunda Serikali yao. na kuwa na serikali ya shirikisho.

hapo kila nchi itakua huru kuzungumzia mambo yake na kuchangia kwenye shirikisho.

zaidi ni kuwa zanzibar wataendelea kudhurumiwa haki zao na bara katika nyanja zote za kiuchumi hususan misaada, michezo na hata kisiasa
Si kuna serikali ya Mapinduzi Zanzibar; Je imesaidia nini katika kuwa na uhuru wa kuzungumza mambo yao na hatimaye kuchangia kwenye serikali ya JMT.
 
Back
Top Bottom