Buchanan,
Kwani nani kasema kajitu toka bara ina maana ya Makamba? Kwani haiwezi kuwa JK? Hapa tatizo ni lugha? Nadhani hii lugha haijamtukana wala kumdhalilisha yeyote, inajaribu kutoa muonekano wa mtu ambaye hana maamuzi yoyote ya maana... na ndiyo maana maamuzi yote katika mazungumzo yaliyofikiwa katika mchakato wa CUF na CCM iliyohusisha wabara hazijafanikiwa including JK mwenyewe ambaye ktk hotuba yake alisema mpasuko ni kipaumbele lakini alishindwa kupiga hatua kama rais na kama mwenyekiti wa CCM. Sasa kama wazanzibari wamekutana na kupiga hatua si lazima wao ndiyo waonekane watu kwa sababu wamefikia maamuzi? Watu ambao hawana maamuzi kama akina Makamba lazima wasemwe vijitu.....
 
Usemayo sawa. Lakini rekebisha hiyo dosari kwanza huko juu. Kwani SMT siyo Serikali ya Maendeleo ya Tanganyika, bali ni Serikali ya Muungano wa Tanzania. Haiombwi msaada kufanya kitu Zanzibar bali huwa inatekeleza wajibu wake kwa Watanzania walioko kule (Wazanzibari)
 
Naona watu wana vichwa vitukutu kweli, na hili limefanywa kwa makusudi kufifisha mipaka baina ya Tanganyika na SMT.

Tukumbuke jamani tumeungana, lakini Zanzibar haikupoteza mamlaka yake na serekali yake.Sasa wewe unapolazimisha lazima maoni yako yasikilizwe na kufuatwa, bado yatakuwa maoni kweli?Mie naona kulazimisha maoni yako yasikilizwe ni kuamrisha na sio maoni.

Sasa Bunge tukufu la Zanzibar kesho linaingia uwanjani, na haya yote yatajulikana kama Karume ataendelea au atabaki.Na pia tutapata kujua kama SMZ ni koloni la mtanganyika au ni nchi yenye mamlaka yake yenyewe.

Sasa tusiandikie mate na kalamu ipo, subirini mchezo kuanzia kesho.
 

Huja nielewa kaka/dada. Namaanisha hivi. Sasa hivi kuna baadhi ya watu wanasema "Zanzibar isiingiliwe". Sasa kuki tokea tatizo kule nani ataombwa msaada? Maana hauwezi kusema mtu "asikuingilie" lakini kukusaidia iwe wajibu am I right? Mtoto hawezi kudai mzazi asiingilie maisha yake lakini the same time ategemee mzazi huyo huyo awajibike pindi chochote kitakapo mkuta(nime tumia msemo huu kujaribu kueleweka zaidi). As it stands ni wajibu wa SMT kwa Zanzibar lakini si ndiyo huo wajibu sasa hivi wanadai unaingilia Zanzibar? I hope nimeeleweka.
 

Nani kalazimishwa maoni yake yasikilizwe? Jukwaani hapa kila mtu ana uhuru wa kuandika maoni yake. Mwingine ana haki ya kusoma au kuto kusoma, kukubaliana au kuto kukubaliana. JF siyo Bunge kwa hiyo maoni yetu hapa siyo lazima yaje kuwa sheria kwa hiyo usiogope πŸ™‚
 

Hujaeleweka soma tena mkataba wa muungano, utajua ni mambo gani wajibu wa muungano na mambo gani Zanzibar au SMZ inaweza kufanya maamuzi yake na kusema hapo musituingilie kwenye maamuzi yetu ya ndani kwa kisingizio cha muungano.

Na ndio maana kukawa na NEC na ZEC.Sasa ZEC inadili na chaguzi za visiwani chini ya SMZ, NEC inadili na chaguzi za SMT rais na wabunge.

Sasa ndugu yangu kuna ugumu gani kusema NEC isiingilie masuala ya ZEC??ZEC ikisema hakuna uchaguzi wa Zanzibar, basi mchezo ndio huo.
 
MwanaFA1 upo right kabsa, suala la zenji linahusu pande zote mbili na kamwe halipaswi kuachiwa wazenji waamue wenyewe. Wanaosema hivyo wako gizani au umevuta shuka wakati kumepambazuka, hatuombei mabaya yatokee zenji ili tuone kama watasolve wenyewe....!
 

I agree kuna mambo ya Muungano na pia mambo ambayo Zanzibar ina autonomy. Lakini katiba pia inasema chochote kinacho tokea Zanzibar amabacho kina affect taifa zima basi hiyo inaingia kwenye jurisdiction ya SMT. Kwa maana hiyo SMT ina kila haki ya kufuatilia yanayo tokea huko ili iact chochote kikitokea. Mazungumzo na makubaliano ya Seif na Karume mpaka sasa hivi hayaja wekwa bayana. Sasa tunajuaje kwamba baadhi ya vitu haviingii kwenye list ya vitu vya Muungano? Unless wewe Mr. Froasty uorodheshe makubaliano yao tujue once & for all kwamba yes yote waliyo kubaliana na kuplan kufanya ipo kweye autonomy ya Zanzibar.

Food for thought. Seif kasema Karume aongezewe muda wa uraisi seti? Je hiyo ya kubadilisha katiba ipo kwenye list ya mambo ambayo Zanzibar ina takiwa kujiamulia yenyewe?
 
Waigereza wanasema "the evil is in the details!". Kimsingi mapendekezo ya CUF ni mazuri kijuu juu lakini ukienda kiundani zaidi kuna maswali mengi kuliko majibu katika mapendekezo ya CUF. Kutaka uchaguzi usogezwe mbele kwa kisingizio cha Karume " kulea maridhiano" kinamnufaisha nani zaidi kati ya CUF na CCM? Ni wazi jambo hili likipitishwa litaleta mtafaruku mkubwa Visiwani hususan katika CCM maana mtu kama Gharib Bilal atasubiri hadi lini wakati 2005 CCM kupitia kwa Rais Mkapa ilimpoza kwa kumwambia ampishe Karume miaka 5 na baadaye atapewa nafasi. Issue hii ni " Hot Potato".
 
Wazanzibari na watanganyika walikubaliana wenyewe kwa hiari yao kuhusu muungano.

Je sasa wakisema hatutaki mtuingilie na mambo yetu na tunataka tuamue mambo yetu wenyewe MABAYA MAZURI mtawalazimisha?


Kwanza hio ishara yakusema hatutaki mtuingilie imeshaonyesha kwamba HAWAUTAKI MUUNGANO.

Mkumbuke pia kwamba Zanzibar ilikuwepo kabla ya muungano nawalikua wanaamua mambo yao wenyewe.
 
\


Ya kweli haya ua ndiyo kufungana kamba hapa.
 


Hivi huo mkataba uko wapi. Mzee tunaomba utuletee tuusome na sisi.
 

I agree kuna mambo ya Muungano na pia mambo ambayo Zanzibar ina autonomy. Lakini katiba pia inasema chochote kinacho tokea Zanzibar amabacho kina affect taifa zima basi hiyo inaingia kwenye jurisdiction ya SMT.


Hiyo katiba ni yenu Tanganyika sisi haituhusu.


Unless wewe Mr. Froasty uorodheshe makubaliano yao tujue once & for all kwamba yes yote waliyo kubaliana na kuplan kufanya ipo kweye autonomy ya Zanzibar.
Sasa kumbe unapiga kelele hata hujuwi watu wamekubaliana nini, wao wenyewe washasema hakuna makubaliano yoyote...na hivyo hakuna haja ya kujadili kitu ambacho hakipo.

Sisi wazanzibari tunajua kama hakuna makubaliano yoyote, Seif na Karume sio Zanzibar hilo ujue kwanza.Sasa mambo yote yataamuliwa na bunge la Zanzibar hapo Maisara...bunge letu tukufu la jamhuri ya watu wa Zanzibar πŸ˜€

Hadi sasa hoja ya mseto na mafuta zitakuwemo, sasa hoja ya kupeleka mbele uchaguzi kwa miaka 2 nitakuachia wewe utege sikio na hiyo serekali yako ya Tanganyika.

Lakini ninavyojua mimi maamuzi ya uchaguzi wa visiwani hayamo kwenye mambo ya muungano....atleast according to the contract.
 


Mwafaka haupo kunufaisha chama chochote au mtu kama Gharib Bilal mwafaka upo kwa manufaa ya wazanzibar wote akiwemo huyo Bilal hata hivyo urais si wa kuahidiwa kama unavyosema kwani wapi waliandikishana?

Kuna miafaka kama miwili hivi tumeshuhudia ikishindikana na ukiangalia kwa undani zaidi haikufanikiwa kutokana na viongozi hasa wa CCM-bara kujali maslahi ya chama zaidi ya wazanzibar wenyewe. Viongozi wa bara walikuwa na wako radhi kuona watu wakiuana Zanzibar kwa uhasama wa kisiasa kuliko kuona chama chao kikifa.

Hawafurahii wanapoona karibu mwanga utokeze Zanzibar ndio sababu wanakuja na vimaneno maneno kwa kisingizio cha kulinda katiba, busara haitumiki tena inakuwa imefishwa na maslahi binafsi na wivu zaidi.

Msekwa, Makamba, na wengine chonde chonde msilete visingizio mbalimbali historia itawaumbua acheni wivu wa kijinga kama kuna wazanzibar wameamua yaishe waachiwe wenyewe sisi huku bara tuendelee kuitana wehu hadi tutakapoona ni upuuzi.
 

Maelezo yako hayana tofauti na kauli ya Seif anapomwita Makamba (soma Majira/Tanzania Daima la juzi, ametajwa Makamba na si JK kama unavyodai) "kajitu toka bara!" Kama "kuzika tofauti zetu" ndio huko basi hapa moto umefunikwa na majivu tu na ukiyakanyaga utaelewa kuna moto au la! Ukitaka kujua kama Zanzibar ni sehemu ya Muungano soma Ibara ya 1 ya Katiba ya Zanzibar, 1984. Labda utuambie kama Ibara hiyo nako ni batili au inazungumzia Muungano upi! Hiyo habari ya kusaini (ratification) inaweza kufanyika kwa maandishi au acquiscence, kitu ambacho naamini Zanzibar ilifanya!
 
Sasa nafikiria kurudi kwenye maada ya thread hii kuwa Tanganyika ina haki ya kuingilia mambo ya Zanzibar? Wakati nimetoa nyaraka hapo juu ya mkataba wa muungano ambao hauna saini ya Karume wala Baraza la Mapinduzi ambavyo ndio vyombo vya sheria huko Zanzibar kwa wakati huo.Hii inaashiria kuwa Zanzibar na wananchi wake hawakukubali muungano, bali wametawaliwa na Tanganyika kwa nguvu.Kwa hiyo kila kitu ni batili!

Kama muungano wenyewe ni batili, hii ni wazi kuwa Tanganyika haina haki ya kuingilia mambo ya nchi nyengine.Laa kama muungano wenyewe munaweza kuuhalalisha kinguvu nguvu kama munavyofanya kila siku.Basi wananchi wa Tanganyika endeleeni kustahamili masumbwi ya migogoro ya kikatiba.

Sie kesho tukimaliza kunywa kahwa, tunaendelea kutengeneza sheria ya nishati ya gesi na mafuta asilia.Nyie na katiba zenu sijuwi mutafanya nini?Pinda sijamsikia siku hizi, vipi kaambiwa na JK asisieme kitu kuhusiana na muungano?

Tukimaliza hilo la futa, tunajadili la mseto mara baada kupata mapumziko ya kahawa na tende...hatuna haraka tunabofya moja baada ya jengine.Si munajua kama jeshi lenu ni kubwa?Sie hatupigani vita, mumeleta jeshi visiwani na sie tunatumia vita yetu hii ya mshikamano πŸ˜€

Tukimailza vitu hivyo viwili, tunavuta pumzi na kutizama kama uchaguzi ufutwe au uendelee.Mambo swafi safari hii....MSHIKAMANO OYEE!!
 
Hiyo habari ya kusaini (ratification) inaweza kufanyika kwa maandishi au acquiscence, kitu ambacho naamini Zanzibar ilifanya!

Wewe sio yesu kristo kama ukiamini tuu ndio watu wote wataamini.Tuletee ushahidi wa vyombo vyetu kukubali muungano.

Kama huna ushahidi basi hakuna cha kujadili, tuendelee na huo ushahidi niliotoa mimi hapo juu.

P:S
**Na wapi imesema kuwa serekali ya Tanganyika ifutwe na itumie jina la Tanzania?Ina maana hii serekali ya Tanganyika ipo bado?
 
Jaribu kuweka aya kwenye bandiko, ili liweze kusomeka...
 

Ibara ya 1 ya Katiba ya Zanzibar, 1984 ni batili au sahihi? Hiyo habari ya Yesu hapa si mahali pake, kama unataka tufungue thread kwenye Jukwa la Dini ili tuhabarishane! Ukianza kuruka hoja na kulazimisha mambo na pia kuleta yasiyohusika (Yesu Kristo) hutaeleweka ndugu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…