Jaribu kuweka aya kwenye bandiko, ili liweze kusomeka...
Mie personally, taifa langu likipotea na kufanywa mkoa basi niko tayari kujifunga bomu na kujiripua sehemu yoyote ya Dar 😀
Mara baada ya mwafaka kati ya Karume na Seif kumekuwa na kauli mbali mbali zinazojichanganya kuhusu Karume kugombea tena au kuongezewa muda ili "alee" makubaliano yake na Seif! Hilo ni jambo jema sana kwa mustakabali wa visiwa hivyo.
Hata hivyo kumekuwa na kauli zinazotaka kuwa mambo ya Zanzibar yasiingiliwe, waachiwe wenyewe, watayamaliza. Mimi kwa upande wangu niko tofauti na kauli hizo.
Kwa kuwa Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama Ibara ya 1 ya Katiba ya Zanzibar, 1984 inavyosema na kwa kuwa suala la Ulinzi na Usalama ni la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ipo haja ya kujua na kutoa maoni kwa kile kinachoendelea huko, si kwa kuwalazimisha wafanye tunayotaka bali kutoa maoni kama wafanyavyo observers wengine kwenye masuala mbalimbali! Mbona Jumuiya ya Kimataifa na hata JK mwenyewe alitoa pongezi kwa mwafaka wa Seif na Karume? Hizo pongezi sio maoni kwamba mlichokifanya ni kizuri? Mbona hatukusikia malalamiko kwamba tunaingiliwa?
Hakuna anayependa Wazanzibari wauane au kuchukiana. Ndio maana Wazanzibari wengi wanaishi Tanzania Bara na hakuna anayewabughudhi wala kuwachukia! Wazanzibari wengine wameajiriwa kwenye Taasisi ambazo si za Muungano na wanaishi vizuri na Wabara. Sijazungumzia wale ambao wameoana na Wabara na hakuna unyanyapaa wowote!
Sasa hizi kauli za akina Seif anapodai kuwa "kajitu toka Bara" (akimaanisha Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba) kuhoji mambo ya Zanzibar hazionyeshi nia njema na zinawafanya watu kuanza kuhoji kulikoni!
Kwani hakuna lugha ya kistaarabu ya kutamka, hata kama kweli Wazanzibari wameingiliwa? Hizi ni kauli za "kusahau yaliyopita na kujenga mapya" kweli? Hapa watu wataendelea kuhoji maana Seif mwenyewe ndiye anayejenga mazingira hayo ya "kutaka kuhojiwa!"
Otherwise, mimi naona kuwa maamuzi ya kuwa na uchaguzi au la wanayo Wazanzibari wenyewe hata kama watu hawatapenda, ila wasikilize maoni ya watu wengine, ndio maana ya demokrasia, si kutoa kauli za chuki, hakutajenga, kutabomoa!
Binafsi huwa nawashangaa sana wabara wenzangu. Kuna ugumu gani kuwaachia wazanzibari wajiamulie mambo yao? Wenyewe wameamua kupatana baada ya kuona ugomvi wao hauwasaidii chochote zaidi ya kuendelea 'kupokea instructions' kutoka 'Dar es Salaam'!
Aya = paragraphs?
sasa mkuu,MrFroat, Nakubaliana na wewe kwa hili kuwa amani ya Zanzibar ndio priority no.1, hata ikibidi uchaguzi usogezwe.
Kwa vile maridhiano ya Karume na Seif ni dhima, muda uliopo kati ya sasa na October, unatosha kuyafanya yote hayo na kufanya uchaguzi huru na wa haki.
Pia naungana na wale wote wanaoshauri mambo ya Wanzibari, waachieni wenyewe, ila hili la kuahirisha uchaguzi au kuuzogeza mbele sio lenu, hata sisi bara tukifanya uchaguzi wetu tarehe ile ile, kuanzia rais wetu, bunge letu, serikali yetu, vyote vitakosa uhalali 'legitimacy' bila kura ya Mzanzibari.
Kama Baraza litakapokuta na kupitisha kwa kauli moja kusogeza mbele uchaguzi, Bara italazimisha uchaguzi wa rais na wabunge wa Bunge la Muungano uendelee, jee unajua kitakachotokea ni nini?.
Hivi nyinyi Wazanzibari hamjifunzi tuu na kilichomkuta Jumbe alipotaka kuikomboa Zanzibar toka mkoloni Tanzania?. Hamjifunzi tuu Salmini alipotaka badili katiba kuongeza kipindi cha urais, sasa hizi kelele za kutaka kusogeza uchaguzi, zitawatokea puani.
Dawa ya kuimarisha Muungano wetu, ni kufanya serikali moja, Zanzibar na Pemba itageuka mikoa, kelele na chokochoko zote kuhusu muungano zitaisha, si mnaona kisiwa cha Mafia kilivyotulia?. Nacho kilikuwa himaya ya Sultani na sehemu ya Zanzibar, pamoja na Kilwa, Lamu mpaka Mombasa enzi hizo.
Acha ugumu wa kuelewa! Kesho wazenj wakikaa kwenye Baraza la Wawakilishi na kuamua kumwongezea Karume aongoze mpaka atakapokufa kuna mtu atawakataza? Mbona wazenj wanapoajiriwa katika Taasisi ambazo si za Muungano hatusemi kuwa wanaingilia mambo ya Bara? Mtu toka Bara akipiga chafya tu eti "unaingilia mambo ya Wazanzibari!"
Kama na wewe utaweza kujibu errors zote katika mfumo wa muungano basi tutakuwa even.Ibara ya 1 ya Katiba ya Zanzibar, 1984 ni batili au sahihi? Hiyo habari ya Yesu hapa si mahali pake, kama unataka tufungue thread kwenye Jukwa la Dini ili tuhabarishane! Ukianza kuruka hoja na kulazimisha mambo na pia kuleta yasiyohusika (Yesu Kristo) hutaeleweka ndugu!
Utakavyopenda wewe, lakini nchi itakuwa haikaliki.Sasa hivi tunaacha kwanza hiyo SMZ, lakini ikifutwa tuu hiyo kazi itakuja mikononi mwetu wananchi.Al Qaeda, Taleban au Al..?
Kama na wewe utaweza kujibu errors zote katika mfumo wa muungano basi tutakuwa even.
Obviously, huu muungano una makosa mengi na unahitajika ufanyiwe ukarabati.
Sasa kaka zangu na dada zangu kutoka Tanganyika kaeni kando na acheni kutoa comments na critics kwa kulazimisha lazima tuende kwenye uchaguzi ili mupate nafasi ya kumueka kibaraka mwengine.Hiyo nafasi haipo safari hii, maana mukipewa nafasi ya kueka kibaraka na futa letu limeenda harijojo.
Ndio nikasema mutakula harufu tuu, tutakula mseto na futa letu huko huko jikoni huko kwenu itakuja harufu tuu...kama mulivyofanya kwenye madini na vitu vyengine.
Hapo kwenye bluu nenda pole pole! Kwenye nyekundu umenisikitisha kidogo. Kama dhana yako ya 'kuingilia mambo' ndio hiyo basi huu mjadala hauna maana.
Binafsi huwa nawashangaa sana wabara wenzangu. Kuna ugumu gani kuwaachia wazanzibari wajiamulie mambo yao? Wenyewe wameamua kupatana baada ya kuona ugomvi wao hauwasaidii chochote zaidi ya kuendelea 'kupokea instructions' kutoka 'Dar es Salaam'!
Sasa naona tumeshaanza kuwa pamoja: Kwamba Muungano upo lakini una kasoro, suala sasa ni kurekebisha. Mwanzoni ulidai Muungano ni batili huku ukijua kwamba Rais wa Zanzibar anapoapa hutaja kwamba "Zanzibar ni Sehemu ya Jamhuri ya Muungano" na ndivyo ilivyo Katiba ya Zanzibar, 1984, Ibara ya 1! Na hayo mafuta unayodai mtayala yako sehemu gani? Na kama yapo na mkifanikiwa ninyi sisi tuchukie, kama unavyodai, kwa sababu gani? Attitude za chuki, kama unazotoa hazijengi ndugu MrFroasty, zinabomoa! Change your attitude, a simple advice!
Kwa mtazamo wangu uchaguzi wa JK hauna tatizo lolote, na wala sio unaoleta vugu vugu huko visiwani.Hivyo huo unaweza kuendelea bila ya matatizo, kwani hauhitaji hata ZANID hata Mmasai alie Zanzibar anaruhusa ya kuchagua rais wa TZ.Je?Baraza la wawakilishi litaongezewa muda?
Je?uchaguzi wa wabunge wa upande wa Zanzibar utafanyika? kama utafanyika utafanywa katika mazingira gani?
Hakuna attitude huo ndio ukweli kuwa Tanganyika chini ya CCM inapenda kuzorotesha kila chenye kheri na Zanzibar.
JK badala ya kuweka mjadala wa kero za muungano ndani ya bunge ametuletea Pinda ambae anaendelea kutonyesha vidonda vya wazanzibari.
Sasa sisi tuseme nini?Ubabe mupunguze, mtanganyika hata akitoa mfano wa muungano basi atasema ni sawa na ndoa...na Zanzibar itakuwa ndio jike
Unaeleweka sana Ndugu yangu. SMT kinarani ni JK. Katika hotuba zao mbali mbali wote Karume na Maalim wamemshukuru JK kwa kuonesha kuwaunga mkono na wamemuomba (Kiheshima-lakini ni wajibu wake) msaada wake wa dhati katika kufanikisha dhamira zao. Wanaoingilia ni watu kama Msekwa na Makamba (watu wa CCM Bara hao) ni kweli unaweza kusema hayawahusu hao kwani CCM ina watu wenye nafasi kama za kwao kwa ajili ya kuhudumia wanaCCM Zanzibar (Makamo Mwenyekiti CCM Zanzibar -Karume, Na Naibu Katibu Mkuu wa CCM -Zanzibar, Feruzi)Huja nielewa kaka/dada. Namaanisha hivi. Sasa hivi kuna baadhi ya watu wanasema "Zanzibar isiingiliwe". Sasa kuki tokea tatizo kule nani ataombwa msaada? Maana hauwezi kusema mtu "asikuingilie" lakini kukusaidia iwe wajibu am I right? Mtoto hawezi kudai mzazi asiingilie maisha yake lakini the same time ategemee mzazi huyo huyo awajibike pindi chochote kitakapo mkuta(nime tumia msemo huu kujaribu kueleweka zaidi). As it stands ni wajibu wa SMT kwa Zanzibar lakini si ndiyo huo wajibu sasa hivi wanadai unaingilia Zanzibar? I hope nimeeleweka.