Habari njema hizi kwa wale wanyonge wa kizanzibari kupata watu wa kuwatetea.Mulizani mutakuwa mukiwapiga bakora tuu na wao kulia bila ya mtetesi?

Ukimtesa mnyonge hupata wahisani, na kwa Zanzibar wahisani wanaweza kuwa wa aina hii Alshabab, Alqaida au Al-Taliban.Kwa hiyo kosa ni lenu Tanganyika, na hata muungano ukivunjika kosa pia ni lenu.

Mie ilinisikitisha sana kuona video pale Youtube wazanzibari wakipigwa bakora na watanganyika...halafu nyie mukifurahi kabisa huku mukipata Larger.

Hakuna hata kiongozi mmoja wa muungano aliekemea mauji ya 2001, watu wanafanyiwa kila aina ya unyama huko Pemba na Unguja, watu wanaporwa hadi kwenye video za Youtube tunaona watu waporwa pesa mifuko, huku wakipigishwa vichura na kutiwa maji machafu!...Wengine binti zao wamelawitiwa...basi ni uchafu mtupu!

Mie wala siingii majonzi nikiona Alqaeda au Alshabab wakisaidia ndugu zao wa kiislamu...ni sawa kabisa!
 


,,,,,,,Aaaah this is too much sasa!!,hizi ni hasira au???
 
Mimi nilisema haya mambo tuende mbele turudi nyuma, wazanzibar wamefikia hatua wamesema imetosha. sisi bara tulifanya nini kuzuia wasiuane mbali na kupeleka majeshi kuwachalaza bakora?

Hata kama ni muungano lazima kuna mambo muhimu lazima wafikie muafaka wenyewe, washaelewana na hawatarudi nyuma kamwe. CCM wamefanya nini kutafuta mwafaka kwa miaka yote hiyo? wanaosema katiba kuchezewa ndiyo wananichafua mimi zaidi, katiba ni nini zaidi ya damu za watu?

Watu wamepoteza ndugu zao watoto wao sasa wamefikia hatua wamalize tofauti zao nyinyi tena mnathubutu kusema eti urafiki wao ( maalim na karume) usivunje katiba yetu.

We mtu wa bara una katiba kule? katiba yako ya tanganyika ipo wapi? sasa baraza lao likiamua YES, tia mguu kule waambie hayo unayoona yanakufaa ili uone kitakachokupata, lazima serikali ya mseto miaka miwili hivi then tunaenda uchaguzi wa rais.

Huwezi kuwa rais wa upande mmoja, then unajiita rais wa zanzibar, unahutubia mkutano huku unalindwa na mapolisi - unatawala watu au?

Hata ningekuwa mimi Rais wa Zanzibar nisingekubali kuondoka niache kazi hii ambayo ilicheleweshwa tu na siasa na ajabu ajabu za ccm

Narudi akusema hongera Karume na Maalim - Mwendo Mdundo....
 
Re: Tanganyika ka England, Zanzibar ka Scotland ktk Muungano, tujifunze
MrFroasty,
hoja zako zina uzito mwingi bila ushabiki.
Tumeona juzi serikali ya Scotland ilimwachia mlibya aliyetuhumiwa kulipua ndege, serikali ya Scotland ikamwachia on 'compassionate grounds'. suala hilo lilileta maoni tofauti ndani ya United Kingdom, lakini serikali ya Scotland iliitetea uamuzi wake kwa vifungu vya sheria hata swahiba wao mkuu Marekani wakakubali hoja za kisheria.

Sasa na sie huku Tanzania, tunapitia mkondo huo huo wa kisheria kuwa Zanzibar inaweza kufanya baadhi ya maamuzi kupitia Baraza la Wawakilishi na maamuzi hayo ya baraza la Wawakilishi inabidi yaheshimiwe.

Katika Muungano kuna baadhi ya mambo yataleta maoni mengi na tofauti, lakini mradi sheria na makubaliano ya hati ya Muungano yanaruhusu, inabidi kutambua hali hiyo na kuiheshimu.

tuanaona ktk United Kingdom, England ni kama Tanganyika na Scotland ni kama Zanzibar. Scotland bunge lao lina mambo mengi ambayo kisheria wanauwezo wa kujiamulia mambo kufuatana na makubaliano ya United Kingdom. England ni kama Tanganyika, ilijifanya ni nchi kubwa,Ufalme upo London(makazi makuu), bunge la United Kingdom lipo London, Serikali ya United Kingdom ipo London n.k hivyo mambo yake England hayako waziwazi kwa vile ni sehemu kubwa ya United Kingdom.

Hivyo suala ni kuzoea masuala mazito yanapojitokeza kutokukimbilia kutoa kauli ambazo hazizingatii hati za muungano, sheria na udugu wetu.
 
Katika Peku peku zangu za kufuatilia Kikao nyeti ambacho taarifa zilizoliwa hapa jamvingi kingefanyika leo, nakutana na haya wanayosema wenzenu wa upande wa pili katika Jamvi lao linaolojulikana kama "Mz.Net -ZNZ katika Zama za Ukweli na Uwazi, ebu gusa hapa: http://www.mzalendo.net/mahojiano-ya-sio-rasmi-na-jaji-mkuu-wa-zanzibar-juu-ya-mapinduzi


MIYE MMEISHIA KUJICHEKEA TU ATIIII, MANAKE...., LOH, NGOJA NKAJIPATIE "MIJIBIA" YANGU, NKAJILALIE NSIJE LETA BALAA HAPA TENA!.

LOL
 
Kaaz kwelikweli.
Hawa watu wameshaamua, hakuna cha kuwa'stopisha kwa sasa.
Tutasikia kila lugha sasa kutoka huko!
 
Kaaz kwelikweli.
Hawa watu wameshaamua, hakuna cha kuwa'stopisha kwa sasa.
Tutasikia kila lugha sasa kutoka huko!


Oh, Baba awasamehe, kwa maana hawajui walitendalo.

Namkemea vikali huyo mtu aliekwenda kuwaomba na kuwabembeleza wakubali kujiunga na "Wadanganyika" ili tuwe nchi ya "Two in One" na kuunda Serikali mbili zenye mihilimi tofauti kila upande kama pande mbili za "chapati".

· "Tanzania Vs Tanzania Zanzibar)
· "Katiba ya Jamhuri ya Muungano" Vs Katiba ya Zanzibar
· Sheria za Tanzania Vs Sheria za Zanzibar
· "Jamhuri ya Muungano" Vs "Serikali ya Mapinduzi Zaanzibar".
· "Bunge" Vs "Baraza la Wawakilishi"
· "Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" Vs "Rais wa SMZ"
· " Baraza la Mawaziri" Vs "Baraza la Mapinduzi"
· "Mwenyekiti wa Chama" Vs "Makamu Mwwenyekiti"
· " Mahakama Kuu Vs "Mahakama Kuu ya Zanzibar"
· "Mwanasheria Mkuu" Vs Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar"
· "Waziri Mkuu Vs Waziri Kiongozi"
· "Spika wa Bunge" Vs "Spika wa Baraza la Wawakilishi"
· Tume ya Uchaguzi ya Tanzania (NEC) Vs Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC)

AU





Tulikusudia kuwa Taifa moja lenye Serikali moja yenye mshikamano tukiwa na:
  • Mwenyekiti mmoja wa Chama
  • Katibu Mmoja wa chama
  • Makamu mmoja wa Rais
  • Amiri Jeshi mmoja
  • Mkuu mmoja wa Majeshi na Polisi nk
  • Mwenyekiti mmoja wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
  • Msajili moja wa vyama vya siasa
  • Maamlaka moja ya Mapato
  • Waziri Mmoja wa Mambo ya Nje.
  • Hati za iana moja za kusafiria
  • Taratibu sawa za Bandari, usafiri wa anga, posta na simu.
  • sarafu moja na masuala ya fedha sawa
  • Leseni za viwanda
  • Elimu ya juu sawa .
  • Baraza moja la Mitihani
  • Ulinagnifu wa Takwimu
  • Mahakama ya moja ya Rufani
AU tulitaka iwe:

  • TFF ≥ ZFA
  • Mgambo ≤ KMKM
  • Mahakama ya Kadhi = Mahakama Kuu
  • Tanesco = ZECO
 
AU tulitaka iwe:


  • TFF ≥ ZFA
  • Mgambo ≤ KMKM
  • Mahakama ya Kadhi = Mahakama Kuu
  • Tanesco = ZECO


Hapo kwenye Nyekundu mkuu, kuna tofauti za wazi kama hivi:

BARA .........................ZENJI
1.MGUU UPANDE!................ MGUU KANDO!
2.MGUU SAWA!....................MGUU REJESHA!
3.MWILI LEGEZA!.................MWILI MDEBWEDO!

Hizo peke yake zinatosha kuonyesha kwamba kweli tulilazimishana hii maneno ya Muungano..! huh!
 
Hongera wa Zenj kwa kumjua Adui yenu!, kilichobaki sasa ni kumshughulikia na kumvua KOTI alilojivisha na kujita Tanzania kumbe ni TANGANYIKA KINACHOTAKIWA NI MUUNGANO SIO UKOLONI HUU WA WATANGANYIKA
 
hakuna lolote kwa wazanzibar ni vema kuwaachia tu hakuna jipya hao hawawezi kujiendesha hata siku moja wamewakumbuka wajomba zao waarabu tu, hapo patakuwa kama kisiwa cha Mayote + Ufaransa.... visiwani Comores
 
Hapa ndipo akina "Ngombale" wa CCM walipojitia kitanzi kwenye MOU iliyofikiwa na CUF tarehe 29 Aprili 2009 wakidhani upinzani ni CUF peke yake hapa nchini na wamekuwa wazito kuyatekeleza wanayofikia kwa matshi yao.

 

Attachments

Hongera wa Zenj kwa kumjua Adui yenu!, kilichobaki sasa ni kumshughulikia na kumvua KOTI alilojivisha na kujita Tanzania kumbe ni TANGANYIKA KINACHOTAKIWA NI MUUNGANO SIO UKOLONI HUU WA WATANGANYIKA


Mawazo finyu hayo, Mkishamaliza na hao unaowaita Watanganyika haitachukua muda, mtaanza muunguja na mpemba, na kwa wale mliokwisha bahatika kuishi unguja na pemba, Waunguja wanaaamini mpemba hawezi watawala hakuna mpepmba anaweza kuwa rais, wapemba wanaamini waunguja wamewaonea kwa miaka mingi, na ilikhali chakula na karafuu nyingi inatoka pemba, Wazanzibari Muungano ndo unawafanya mjiite Zanzibar Bila huu muungano hakuna na wala halitakuwepo taifa la watu wa Zanzibar, TIME WILL TELL
 



Haya ndo mawazo finyu manayodanganywa na CCM eti amani, amani Tanzania kuna amani, utulivu hakuna ukabila, uzembe mtupu!!!!

Naamini kabisa Zanzibar wakijitenga baada ya miaka kumi Tanganyika wataenda kuomba misaada Zanzibar, I bet you, na tusubiri!!!
 
Hamadi ameshindwa kutumiza malengo yake kwa sababu ya muungano.Akifanikiwa na hiki kinachoendelea , Unguja haitakuwa na nguvu tena ya kumzuia kutimiza lengo lake ya Pemba kama nchi.
 


wewe unaongea Zanzibar au pemba waijua, kuwa objective na comments zako, naona unasukumwa saana na hisia ,,pole
 
..
Sidhani choko choko kama kamahizo zina nafasi tena! Wazenj wametambua adui wao ni yule anaewaimbia wimbo wa WAPEMBA NA WAUNGUJA. Ili afanikishe malengo yake.
 
Ni wakati sasa wa kuacha siasa na kufanya mambo katika uhalisia wake! Muungano wowote hata uwe mzuri kiasi gani kama hauna maridhiano ya kweli hauwezi kufika kokote. Sometimes waswahili husema mtoto akililia wembe mpe! Hivyo kama ni kweli bara wana huruma sana na watu wa Zanzibar ni vyema pia wakawaheshimu na mawazo yao waliyo nayo sasa.

Binafsi sioni ubaya wowote kama nia ni njema Zanzibar waachwe wafanye mambo yao watakavyo na kama kuna majuto mbele na bara wana nia njema na Zanzibar, watakapo kiri kwamba wamechemsha waruhusiwe kurudi kwenye muungano, kuliko ilivyo hivi sasa ambapo inaonekana kwamba hakuna anaye faidika na muungano huu ki uchumi, kikubwa ndani ya muungano huu ni siasa tu hauna chochote ndani yake.

Hata bara wananchi wa kawaida wanaona kama Zanzibar wanadekezwa sana katika muungano, hivyo kama umefika wakati maslahi ya muungano huu yamekwisha ni bora zanzibar wakaachiwa njia yao.
 
kusema ukweli wazanzibar wakijitoa kwenye muungano, amani yao itakuwa ya kuisikia kwenye bomba maana hata hao waunguja na wapemba bado wanamsuguano.
wakishamalizana na wabara wataanza kuonyeshana wao kwa wao kwamaba ni nani anahaki au anastahili zanzibar kuliko mwingine.
Time will tell
 
yamekuhusu vipi wewe matatizo ya znz walipo uwawa watu mbona tanganyika mlikaa kimya na nyinyi ndio mnao utaka huo muungano wakati wazenji hawana haja nao nini mumewasaidia nyinyi mnapenda kuoa wanauana na kumalizana ndio furaha yenu wache waondoe tafauti zao kazi yenu kutia fitna tu wameshakustukieni kuwa hamuwatakii mema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…