Mkuu ni kweli suala la mafuta limeibuka hivi karibuni lakini suala la Wanzazibar kutaka mambo yawekwe sawa limeanza siku nyingi toka enzi za Mwalimu ila wamekua wakinyamazishwa kwa vitisho. Hata Wabara wengi hawaridhishwi na jinsi muungano ulivyo ndio maana ikaibuka G55 enzi za Mzee Ruksa na viongozi wengi walikua wanaunga mkono sema woga wao hawakuweza kutetea walichokiamini mbele ya Mwalimu.
 
Mimi sijui nani mume nani mke. Ila ninachojua ni kuwa ukiangalia muungano Tanzania na Zanzibar na jitihada za kuutaka usimegeke, unapata picha inayofanana na mume na mke ndani ya ndoa ambapo mume kwa sababu ya hadhi hataki ndoa ivunjike japo anajua imejaa migogoro. Na mke naye anatishia kwa kutikisa kibiriti kwa kujidai kuwa hata akiachwa bado atajimudu kujikimu. Kweli sijui.

Au inawezekana wenzetu wa Kisiwani wanataka muungano ukivunjika tu pale pale wanatangaza muungano wao na Sultan Qaboos wa Oman? Cant this happen? Iwapo kisiwa cha Reunion bado ni sovereignty ya France itakuwa ajabu kwa Oman na Zanzibar? Au ninaota jamani. Hili haliwezekani kweli? Na likitokea ni dhahiri geopolitics za Afrika Mashariki na SADC zitabadilika. Am I dreaming?
 
So what is the problem with that? wakiungana na Oman nini kinachokukera wewe Mtanganyika?

Mimi unajua argument nyingi za waTanganyika zinanichefua sana, utafikiri zanzibar ni mali yenu..mnawaamulia hata marafiki...gosh mawazo ya kikoloni na kijinga..

Bana ye wazanzibar embu ondoeni aibu hii chukueni zanzibar yenu, labda wataongea kwa heshima.
 

Wewe upo duniani lakini?Hicho kikao kilifanyika badala ya Karume kugomea kuja huko Bara.Hivyo Msekwa, Mwinyi wote ilibidi wafanye kikao cha dharura kuenda Zanzibar.

Msekwa amefanya kikao cha siri na Karume kumpatia mikwala...sasa hapa sijuwi wewe unatokea sayari gani?
 


Wekeni wazi masuala ya makubaliano yenu, kama hamna copy ya mkataba halisi - basi kaeni chini muangalie kipi mtashare na kipi hapana

Ila mtaonekana watu wa ajabu kuanza kujiuliza na kuuchokonoa muungano baadaya ya miaka yote hiyo.
 

hakua mzanzibari hata mmoja anaetaka muungano...huu muungano unalazimishwa na bara. ndio maana hata serekali tatu bara hawataki...lakini wazanzibar wakotayari...huu muungano wa kulazimisha hauna mpango wowote
 

kwa taarifa yako. Zanzibar imekua masikini baada ya muungano...uliza kabla ya muungano zanzibar ilikua wapi. mimi sioni fahari kuwa na muungano amboa hauna manufaa kwa mzanzibar wala mtanganyika. miaka 46 ya uhuru bado watu wanahangaika na tatizo la umeme na maji? tanzania sio nchi masikini lakini watu kama nyinyi ndio mnaitia umaskini...kwahiya zanzibar ikiwa kivyake itasonga mbele haraka. na kuwaacha bara kuendelea kutawawila na mafisadi
 

kwa taarifa yako...hakuna hata mzanzibari mmoja anaetaka muungano...kabla ya wewe kuzaliwa ,watu wanataka uvunjike. kabla ya muungano zanzibar ilikua mbali sana, sasa imerudishwa kuwa msikini. bara ndio wanaotaka muungano.
ndio maana hata serikali tatu hawataki. sasa wanzanzibar wamesha amka...sooner or later they will be free... free zanzibar
 
Wekeni wazi masuala ya makubaliano yenu, kama hamna copy ya mkataba halisi - basi kaeni chini muangalie kipi mtashare na kipi hapana

Ila mtaonekana watu wa ajabu kuanza kujiuliza na kuuchokonoa muungano baadaya ya miaka yote hiyo.

wewe muulize kila mzanzibar unae mjua , atakwabia hataki muungano. huu muungano unalazimishwa na bara.

na kama utavujika leo, basi zanzibar kutakua na holiday. huu sio muungano ni mateso.wakati umefika na nyinyi watanganyika amkeni.
 

zanzibar +muungano=umaskini, njaa, shida ,tabu na mateso
tanganyika +muungano=??? somebody help me please...
 
Mijadala mingi inayohusu kuvunjwa ama kutovunjwa kwa Muungano wa TZ (Tanganyika na Zanzibar), hakutaji faida na hasara za Muungano huo kwa wakati huu wa sasa, tukiacha historia ya kuanzishwa kwake. Ningeomba wanaJF tujadili kwa kuainisha hizo faida na hasara ili tuelewe umuhimu wa kuwepo ama kutokuwepo kwa Muungano wetu.

Nawasilisha....
 

Ni faida tuu hakuna hasara hata moja itakayopatikana.Mfumo wa muungano uliopo ni wa bei rahisi, lakini hautendi haki.

Kuendeleza muungano ambao utatenda haki ni gharama tuu, itakubidi uweke serekali 3 ambapo gharama za uendeshaji nchi zitapanda.

Kuvunja ni sawa na kusema tumebaki mfumo wa sasa wa serekali mbili, lakini utakuwa hauna kelele za mmoja kukandamizwa au kuonewa.

Hivyo uvunjike tuu!
 
Yaani wabongo mmefulia kabisa au mnabisha ,wait for this feb and c !!
 

sam,
kukumbuka kama kabla ya huu muungano ,kama zanzibar ilikua nchi, na itaendelea kuwa nchi...huwo mfano wa kuwa dar es salaam kuwa ina watu wengi zaidi au kidogo sio muhimu hapa...dar es salaam ni mkoa wa tanganyika kabla ya muungano. na sasa ni mkoa wa tanzania bara. zanzibar kama nchi ilitoa hazina yake wakati wa kuanzisha banki kuu ( BoT) .mkoa wa dar es salaam walitoa nini?
mimi naunga mkono muungano uvunjwe, baadae tuulizwe wa nanchi kama tunataka muungano .na kama tunataka ni muungano wa aina gani. chakushangaza wazanzibari zaidi ya asilimia 90% hawataki huu muungano uliyopo sasa, na kama lazima uwepo wanataka uwe na serikali tatu. chakujiuliza ni nani analazimisha huu muungano? kwa mtazamo wangu jibu ni tanganyika. sasa sielewi kama bado nyerere anaongoza hii nchi pamoja na kwaba amefariki au kuna siri kubwa ambayo viongozi wa tanganyika hawaja iweka wazi, au vipi? kama kweli huu muungano unaleta kero huku tanganyika basi uamuzi utoke huku ,kwani zanzibar naona wako tayari,kuwa na nchi yao kama ilivyokua zamani ...people's republic of zanzibar ( jamuhuri ya watu wa zanzibar) ...kwa ufupi huu muungano ndio nakwamisha maendeleo ya zanzibar na tanganyika.
 
Mawazo ya Nyerere na Karume ilikuwa nimuungano wa Serikali mbili kuelekea serikali moja Sasa wazo la serikali ya tatu lililetwa na G55 nao mwalimu akawazima kwa hoja nzito Sasa kwanini tusiendlee na mawazo ya kuwa na serikali moja badala ya kuvunja muungano au kuunda serikali ya tatu
Hii ni akili iliyopogoka na kuvaa miwani ya giza isiyoweza kuonambele Manufaa ya kuwa nguvu za pamoja munaona zilivyo na manufaa pote duniani ona America ona ulaya na hata latin america wanafikilia kuwa pamoja ili wawe na sauti moja kwa manufaa ya wananchi wao na sasa upuuzi unaanza tena , bora tuwe na serikali moja na mapato ya taifa yatumike kwa manufaa ya nchi nzima
Mfano wa kuiga ni wenzetu wa America kila state ilipata uhuru wake tofauti na state nyingine lakini wakati ulipofika walipigana na kuungana moja baada ya nyingine na sasa munawaona wako wapi
Sisi Watanzania tunashindwa kuunganisha vijiji viwili vyenye ndugu wa tumbo moja kwani huko zanzibar ni akina nani walioko huko Wamatumbi,wamakonge;wazaramo ,wahehe.wanyamwezi,wasukuma waha wazigua ,wasambaa pamoja na washihiri koko nini zaidi
Jamani acheni upuuzi wa mawazo finyu Pelekeni hoja bugeni ya kujadili njia mwafaka ya kuunda serikali moja kama waasisi walivyo kuwa wanatarajia
 
Si Muafaka kuvunja Muungano. Nazani cha muhimu kuondoa kero. na kuangalia Mapungufu
 
Muungano kama muungano hauna ubaya wowote tatizo ni malengo na tunaotakiwa kuuendeleza pamoja na masuala ya ubinafsi tuliyonayo. Hatuwezi kufikia malengo ya muungano ulio makini kama kero ambazo watu wanaziona ndani ya muungano hazishughulikiwi ipasavyo.
 
tuache hizo......hawa jamaa tukiwaachia tu hawachelewi kuanza kujitolea mhanga kwa hiyo watatuangamiza wabara wote.......................tuendelee tu kuwabeba japo sote tunajua hatupati faida yoyote zaidi ya kuingia hasara
 
Nimevutiwa na Gwaride linaloendelea hapo uwanjani hivi sasa pongezi kwa majeshi ya Tanzania ni wakakamavu ,Gwaride zuri wamependeza sana,kweli mnastahiri pongezi ,hivi nasikia sikia huu muungano hauhitajiki tena?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…