Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Mkuu sidhani kama kuna anayeogopa mabadiliko bali wazanzibar ndiyo wanataka mabadiliko kwa kuwa huko kwao kumegundulika mafuta. Mbona kipindi kile hizi chokochoko hazikuwepo? Hawa jamaa ni wabinafsi sana.

Lakini yote heri kama wanataka usawa na uwekwe ili kila mmoja ajue mipaka yake. Hawa jamaa wamebebwa sana, lakini hawaridhiki siku hizi hata kazi hawafanyi KARAFUU iko wapi siku hizi? Wanabebwa na utalii. Wanaota mafuta tu.

Mkuu ni kweli suala la mafuta limeibuka hivi karibuni lakini suala la Wanzazibar kutaka mambo yawekwe sawa limeanza siku nyingi toka enzi za Mwalimu ila wamekua wakinyamazishwa kwa vitisho. Hata Wabara wengi hawaridhishwi na jinsi muungano ulivyo ndio maana ikaibuka G55 enzi za Mzee Ruksa na viongozi wengi walikua wanaunga mkono sema woga wao hawakuweza kutetea walichokiamini mbele ya Mwalimu.
 
Mimi sijui nani mume nani mke. Ila ninachojua ni kuwa ukiangalia muungano Tanzania na Zanzibar na jitihada za kuutaka usimegeke, unapata picha inayofanana na mume na mke ndani ya ndoa ambapo mume kwa sababu ya hadhi hataki ndoa ivunjike japo anajua imejaa migogoro. Na mke naye anatishia kwa kutikisa kibiriti kwa kujidai kuwa hata akiachwa bado atajimudu kujikimu. Kweli sijui.

Au inawezekana wenzetu wa Kisiwani wanataka muungano ukivunjika tu pale pale wanatangaza muungano wao na Sultan Qaboos wa Oman? Cant this happen? Iwapo kisiwa cha Reunion bado ni sovereignty ya France itakuwa ajabu kwa Oman na Zanzibar? Au ninaota jamani. Hili haliwezekani kweli? Na likitokea ni dhahiri geopolitics za Afrika Mashariki na SADC zitabadilika. Am I dreaming?
 
So what is the problem with that? wakiungana na Oman nini kinachokukera wewe Mtanganyika?

Mimi unajua argument nyingi za waTanganyika zinanichefua sana, utafikiri zanzibar ni mali yenu..mnawaamulia hata marafiki...gosh mawazo ya kikoloni na kijinga..

Bana ye wazanzibar embu ondoeni aibu hii chukueni zanzibar yenu, labda wataongea kwa heshima.
 
Mimi siwaelewi kabisa Wazanzibari! CCM Zanzibar walikutana wenyewe na kuamua kwamba Karume hataongezewa muda na kwa upande wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (mseto?) walidai kwamba maamuzi ya Butiama yazingatiwe na hakuna mtu yeyote toka bara aliyehudhuria vikao hivyo wala kuwaamulia mambo yao!

Wewe upo duniani lakini?Hicho kikao kilifanyika badala ya Karume kugomea kuja huko Bara.Hivyo Msekwa, Mwinyi wote ilibidi wafanye kikao cha dharura kuenda Zanzibar.

Msekwa amefanya kikao cha siri na Karume kumpatia mikwala...sasa hapa sijuwi wewe unatokea sayari gani?
 
Nimevumilia vya kutosha nikidhani kama kuna mtu anayekerwa na fumbuzi wa matatizo ya muungano yaliyotolea kwenye kikao cha pamoja kati ya Mh. Lowassa na Mh. Nahodha.

Kitu kinachonitisha ni kwamba yale mambo waliowaamulia wananchi yatapelekwa bungeni october kwa ajili ya "constitutional reforms".
Kwa upande wangu sikubaliana na ufumbuzi waliofikia kwa 100%
Check this out:

1) mineral and oil exploration be co-opted into the national debate on the future of the political federation.

-debate is good but mineral and oil exploration should not be political.

2)Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) should have an equal number of representatives from either side.

-Equal number kwa vigezo gani? Idadi ya watu? Tuelezene mlivyokuja na hiyo soultion equal number of people.

3)consultant on the distribution of wealth generated through mining and oil extraction be hired to advise the Union government on how it can be shared equitably.

-Please kama ni hivyo na huo muungano hatuutaki. For what?

4)It was decided that 50 per cent of the income would be used to finance the operations of the authority and the other 50 per cent be distributed on the basis of 60 per cent for the Mainland and 40 per cent for Zanzibar.

-Hivi hizo hesabu mnafanyaje? How did you come up with 60%, ardhi, watu,?????

Najua watanzania hawataki kuongelea muungano wakiogopa mizimu ya Mwalimu. Kwa upande wangu kuna mambo mawili tu hapa ambayo yanaweza kuleta ufumbuzi wa kudumu kwanza kuuvunja muungana na Zanzibar ikawa nchi kama ilivyo Kenya na tutaendelea kushirikian nao kama tunavyoshirikiana na Kenya, au Zanzibar uwe mkoa. zanzibar kuna watu wasiozidi 3 mil wakati mkoa wa Dar tu una watu 4 mil. Hapo utajiuliza ni kivitu tugawane nusu kwa nusu?

Kama watu hamtaki kuongela hili sual basi mwezi October linaingia kwenye katiba.

i477_usainiwamkataba.jpg

Mkataba wa makubaliano ya kuanzisha muungano wa Tanganyika na Zanzibar ukisainiwa mwaka 1964.

Mkataba wenyewe (uliosainiwa) umeambatanishwa kama attachment.

Mkuu ni kweli suala la mafuta limeibuka hivi karibuni lakini suala la Wanzazibar kutaka mambo yawekwe sawa limeanza siku nyingi toka enzi za Mwalimu ila wamekua wakinyamazishwa kwa vitisho. Hata Wabara wengi hawaridhishwi na jinsi muungano ulivyo ndio maana ikaibuka G55 enzi za Mzee Ruksa na viongozi wengi walikua wanaunga mkono sema woga wao hawakuweza kutetea walichokiamini mbele ya Mwalimu.

Wekeni wazi masuala ya makubaliano yenu, kama hamna copy ya mkataba halisi - basi kaeni chini muangalie kipi mtashare na kipi hapana

Ila mtaonekana watu wa ajabu kuanza kujiuliza na kuuchokonoa muungano baadaya ya miaka yote hiyo.
 
Hili suala hata mimi niliwahi kusema si suala la Lowassa na Vuai!

Hivi CCM na viongozi wake ni lini watakubaliana kuwa watanzania wana mawazo nao wanaweza kuchangia?

Kuhusu muungano ninakubaliana na wewe ni vema tuuvunje kwanza au iundwe serikali moja hata ukisoma kitabu cha Mwalimu uongozi na ... alishauri serikali moja kwa sababu alisema muundo wa muungano ni serilaki mbili kuelekea serkali moja baadaye. Lakini zanzibar cini ya CUF na CCM wenye we huko wanataka serikali tatu ili waendelee kutunyonya zaidi!!

Sawa haya ya (Lowaasa na Vuai )yakipelekwa bungeni yakapitishwa yatakuwa mabaya zaidi kuliko hata ya Nyerere na Karume . Hawa watu wa bara wataumia zaidi lakini hao hao wa bara wamekuwa kama

walinyweshwa dawa kuhuu muungano hawataki kabisa kuungolea!!!

Hapa ndipo huwa ninakubaliana na Mtikila!

hakua mzanzibari hata mmoja anaetaka muungano...huu muungano unalazimishwa na bara. ndio maana hata serekali tatu bara hawataki...lakini wazanzibar wakotayari...huu muungano wa kulazimisha hauna mpango wowote
 
Mimi sijui nani mume nani mke. Ila ninachojua ni kuwa ukiangalia muungano Tanzania na Zanzibar na jitihada za kuutaka usimegeke, unapata picha inayofanana na mume na mke ndani ya ndoa ambapo mume kwa sababu ya hadhi hataki ndoa ivunjike japo anajua imejaa migogoro. Na mke naye anatishia kwa kutikisa kibiriti kwa kujidai kuwa hata akiachwa bado atajimudu kujikimu. Kweli sijui.

Au inawezekana wenzetu wa Kisiwani wanataka muungano ukivunjika tu pale pale wanatangaza muungano wao na Sultan Qaboos wa Oman? Cant this happen? Iwapo kisiwa cha Reunion bado ni sovereignty ya France itakuwa ajabu kwa Oman na Zanzibar? Au ninaota jamani. Hili haliwezekani kweli? Na likitokea ni dhahiri geopolitics za Afrika Mashariki na SADC zitabadilika. Am I dreaming?

kwa taarifa yako. Zanzibar imekua masikini baada ya muungano...uliza kabla ya muungano zanzibar ilikua wapi. mimi sioni fahari kuwa na muungano amboa hauna manufaa kwa mzanzibar wala mtanganyika. miaka 46 ya uhuru bado watu wanahangaika na tatizo la umeme na maji? tanzania sio nchi masikini lakini watu kama nyinyi ndio mnaitia umaskini...kwahiya zanzibar ikiwa kivyake itasonga mbele haraka. na kuwaacha bara kuendelea kutawawila na mafisadi
 
Mkuu sidhani kama kuna anayeogopa mabadiliko bali wazanzibar ndiyo wanataka mabadiliko kwa kuwa huko kwao kumegundulika mafuta. Mbona kipindi kile hizi chokochoko hazikuwepo? Hawa jamaa ni wabinafsi sana.

Lakini yote heri kama wanataka usawa na uwekwe ili kila mmoja ajue mipaka yake. Hawa jamaa wamebebwa sana, lakini hawaridhiki siku hizi hata kazi hawafanyi KARAFUU iko wapi siku hizi? Wanabebwa na utalii. Wanaota mafuta tu.

kwa taarifa yako...hakuna hata mzanzibari mmoja anaetaka muungano...kabla ya wewe kuzaliwa ,watu wanataka uvunjike. kabla ya muungano zanzibar ilikua mbali sana, sasa imerudishwa kuwa msikini. bara ndio wanaotaka muungano.
ndio maana hata serikali tatu hawataki. sasa wanzanzibar wamesha amka...sooner or later they will be free... free zanzibar
 
Wekeni wazi masuala ya makubaliano yenu, kama hamna copy ya mkataba halisi - basi kaeni chini muangalie kipi mtashare na kipi hapana

Ila mtaonekana watu wa ajabu kuanza kujiuliza na kuuchokonoa muungano baadaya ya miaka yote hiyo.

wewe muulize kila mzanzibar unae mjua , atakwabia hataki muungano. huu muungano unalazimishwa na bara.

na kama utavujika leo, basi zanzibar kutakua na holiday. huu sio muungano ni mateso.wakati umefika na nyinyi watanganyika amkeni.
 
Mkuu sidhani kama kuna anayeogopa mabadiliko bali wazanzibar ndiyo wanataka mabadiliko kwa kuwa huko kwao kumegundulika mafuta. Mbona kipindi kile hizi chokochoko hazikuwepo? Hawa jamaa ni wabinafsi sana.

Lakini yote heri kama wanataka usawa na uwekwe ili kila mmoja ajue mipaka yake. Hawa jamaa wamebebwa sana, lakini hawaridhiki siku hizi hata kazi hawafanyi KARAFUU iko wapi siku hizi? Wanabebwa na utalii. Wanaota mafuta tu.

zanzibar +muungano=umaskini, njaa, shida ,tabu na mateso
tanganyika +muungano=??? somebody help me please...
 
Mijadala mingi inayohusu kuvunjwa ama kutovunjwa kwa Muungano wa TZ (Tanganyika na Zanzibar), hakutaji faida na hasara za Muungano huo kwa wakati huu wa sasa, tukiacha historia ya kuanzishwa kwake. Ningeomba wanaJF tujadili kwa kuainisha hizo faida na hasara ili tuelewe umuhimu wa kuwepo ama kutokuwepo kwa Muungano wetu.

Nawasilisha....
 
Ni faida tuu hakuna hasara hata moja itakayopatikana.Mfumo wa muungano uliopo ni wa bei rahisi, lakini hautendi haki.

Kuendeleza muungano ambao utatenda haki ni gharama tuu, itakubidi uweke serekali 3 ambapo gharama za uendeshaji nchi zitapanda.

Kuvunja ni sawa na kusema tumebaki mfumo wa sasa wa serekali mbili, lakini utakuwa hauna kelele za mmoja kukandamizwa au kuonewa.

Hivyo uvunjike tuu!
 
Yaani wabongo mmefulia kabisa au mnabisha ,wait for this feb and c !!
 
Mzee Mkandara,
Mimi naamini hakuna kitu kitachotutengenisha kati yenu na Zanzibar kijamii, sisi ni wamoja na tunashirikiana vizuri sana kijamii. Muungano wa kiuchumi na kisiasa unaturudisha nyuma sana kimaendeleo. Ni kitu ambacho hakiingii akilini kwa nini Zanzibar iwe na serikali yake ndani yamuungano wakati Dar es Salaam ambayo wakati wake ni mara mbili ya wakazi wa visiwani na bado wanataka wachukua 40% for what. Kama hawataki Zanzibar uwe mkoa basi muungano wa kisisa na uchumi ufe, ni gharama kubwa kwa serikali ya Muungano.

sam,
kukumbuka kama kabla ya huu muungano ,kama zanzibar ilikua nchi, na itaendelea kuwa nchi...huwo mfano wa kuwa dar es salaam kuwa ina watu wengi zaidi au kidogo sio muhimu hapa...dar es salaam ni mkoa wa tanganyika kabla ya muungano. na sasa ni mkoa wa tanzania bara. zanzibar kama nchi ilitoa hazina yake wakati wa kuanzisha banki kuu ( BoT) .mkoa wa dar es salaam walitoa nini?
mimi naunga mkono muungano uvunjwe, baadae tuulizwe wa nanchi kama tunataka muungano .na kama tunataka ni muungano wa aina gani. chakushangaza wazanzibari zaidi ya asilimia 90% hawataki huu muungano uliyopo sasa, na kama lazima uwepo wanataka uwe na serikali tatu. chakujiuliza ni nani analazimisha huu muungano? kwa mtazamo wangu jibu ni tanganyika. sasa sielewi kama bado nyerere anaongoza hii nchi pamoja na kwaba amefariki au kuna siri kubwa ambayo viongozi wa tanganyika hawaja iweka wazi, au vipi? kama kweli huu muungano unaleta kero huku tanganyika basi uamuzi utoke huku ,kwani zanzibar naona wako tayari,kuwa na nchi yao kama ilivyokua zamani ...people's republic of zanzibar ( jamuhuri ya watu wa zanzibar) ...kwa ufupi huu muungano ndio nakwamisha maendeleo ya zanzibar na tanganyika.
 
Mawazo ya Nyerere na Karume ilikuwa nimuungano wa Serikali mbili kuelekea serikali moja Sasa wazo la serikali ya tatu lililetwa na G55 nao mwalimu akawazima kwa hoja nzito Sasa kwanini tusiendlee na mawazo ya kuwa na serikali moja badala ya kuvunja muungano au kuunda serikali ya tatu
Hii ni akili iliyopogoka na kuvaa miwani ya giza isiyoweza kuonambele Manufaa ya kuwa nguvu za pamoja munaona zilivyo na manufaa pote duniani ona America ona ulaya na hata latin america wanafikilia kuwa pamoja ili wawe na sauti moja kwa manufaa ya wananchi wao na sasa upuuzi unaanza tena , bora tuwe na serikali moja na mapato ya taifa yatumike kwa manufaa ya nchi nzima
Mfano wa kuiga ni wenzetu wa America kila state ilipata uhuru wake tofauti na state nyingine lakini wakati ulipofika walipigana na kuungana moja baada ya nyingine na sasa munawaona wako wapi
Sisi Watanzania tunashindwa kuunganisha vijiji viwili vyenye ndugu wa tumbo moja kwani huko zanzibar ni akina nani walioko huko Wamatumbi,wamakonge;wazaramo ,wahehe.wanyamwezi,wasukuma waha wazigua ,wasambaa pamoja na washihiri koko nini zaidi
Jamani acheni upuuzi wa mawazo finyu Pelekeni hoja bugeni ya kujadili njia mwafaka ya kuunda serikali moja kama waasisi walivyo kuwa wanatarajia
 
Muungano kama muungano hauna ubaya wowote tatizo ni malengo na tunaotakiwa kuuendeleza pamoja na masuala ya ubinafsi tuliyonayo. Hatuwezi kufikia malengo ya muungano ulio makini kama kero ambazo watu wanaziona ndani ya muungano hazishughulikiwi ipasavyo.
 
tuache hizo......hawa jamaa tukiwaachia tu hawachelewi kuanza kujitolea mhanga kwa hiyo watatuangamiza wabara wote.......................tuendelee tu kuwabeba japo sote tunajua hatupati faida yoyote zaidi ya kuingia hasara
 
Nimevutiwa na Gwaride linaloendelea hapo uwanjani hivi sasa pongezi kwa majeshi ya Tanzania ni wakakamavu ,Gwaride zuri wamependeza sana,kweli mnastahiri pongezi ,hivi nasikia sikia huu muungano hauhitajiki tena?
 
Back
Top Bottom