Kila mara utasikia eti kamati ya serikali ya muungano na ile ya serikali ya mapinduzi ya zanzibar zimekaa kujadili na hatimaye kuondoa baadhi ya kero za muungano.
Swali hapa ni kuwa zanzibar wanawakilishwa kikamilifu na kamati yao je Tanganyika tunawakilishwa na nani? Kwani ukisema kamati ya serikali ya muungano tayari zamziba wamo na wanafaidi matunda ya serikali ya Tanzania na SMZ pia, hapa watanganyika tunanyonywa na wazanzibari.
Kwa mantiki hiyo hebu ziwekwe wazi hizo zinazoitwa kero za muungano ili wote tuzijue!
..Tanganyika inatoa umeme wa bure, na kulipa mishahara ya watumishi wa SMZ.
Mwiba,
Mkuu swala la mgao wa mapato nadhani ni gumu sana kutokana na mabadiliko mengi yaliyofanywa kikatiba hasa tunapozungumzia kwamba Zanzibar sio nchi ila ni chanya ya kitu kimoja. Ifahamike tu kwamba mgao wa mapato hauwezi kulingana ama kufananishwa na vyeo au nyadhifa za uongozi ktk Jamhuri ya Muungano. Maadam tanganyika haipo wala haina rais wake haina maana hata mgao wa fedha utakuwa na matatizo.
It is simple, what U bring in ndio asilimia ya kile utakachogawiwa kama vile shareholder. Swala kubwa la kujiuliza ni sehemu ngapi ya asilimia Zanzibar na bara wanachangia mfuko wa Taifa kutokana na mapato yanayokusanywa. Sasa sielewi kama ndio utaratibu unaotumika lakini inatakiwa kila upande ukusanye kima cha asilimia toka makusanyo yote kodi na ushuru kuingia mfuko wa Taifa, kwa mfano asilimia 5 au 10 ya kila Tax nchini ni fungu la serikali ya Muungano.
Kama hatufanyi hivyo basi ndio maana swala hili limekuwa sugu na linawashinda kulitatua kwani huwezi kugawana kila senti iliyopatikana na kupanga uuwiano wa maendeleo ya sehemu hizi ambao haupo wala haiwezekani kugawana sawa.
Kwa hiyo, matumizi yoyote yanayotarajia kuboresha huduma za muungano zitawezeshwa na fungu hili ikiwa ni pamoja na wizara ambazo ni za Muungano..Kinachosumbua ni pale bara wanapochukulia muungano wetu na Zanzibar ni kama ndoa baina ya mume na mke kwa asili za kiafrika yaani Zanzibar ni wanawake tu watagawiwa tunachotaka kuwapa, Lakini pia Zanzibar haiwezi kudai mgao wa mapato (50/50) kama vile hii ni hukumu ya taraka baina ya mume na mke!. Swala la Utanganyika na Uzanzibar halina nafasi ktk mgao wa pato la Muungano isipokuwa mchango wa kila sehemu ktk mfuko huo utaweza kutoa picha ya mgao..
Hapo sasa!...Good point nadhani kiini cha tatizo ni kwamba je huo muungano ulianzaje maana kama ilivyo ndoa lazima ijulikane parties ndani ya ndoa walianza vp
Ingelikuwa Tanganyika ina uwezo wa kuisadia nchi nyengine nadhani usingizi tungekuwa hatupati huko visiwani.Ni ukweli usio pingika kuwa Tanganyika ni moja ya sehemu zenye ufukara wa kutupwa.Hapo sina lengo la kukejeli bali huo ndio ukweli wa mambo.
Ndugu yangu Zanzibar sio mzigo katika muungano.Kama ingelikuwa mzigo wakati hio Tanganyika yenyewe ni mzigo tayari...basi nadhani mzigo huo wa visiwa ungelikwisha tupwa kitambo tokea babu yenu Nyerere hajafariki.
Mwenye macho haambiwi tazama, wazanzibari hawataki muungano hata kuuona maana ndio uliowatia ukara.Ving'ang'anizi ni Bara.Hilo linathibitika kila unapokaribia uchaguzi, majeshi pamoja na usalama huongezwa visiwani kuliko sehemu nyengine yoyote.Hii si bure, bali ni kuonesha kama Zanzibar si mzigo.Na kwa wema gani mulionao, hata mubebe mizigo isiowahusu!
Hapo sasa!...
Wazanzibari wepi hawataki Muungano? Mbona akina Nahodha, Shamhuna, Karume, etc wanausifia Muungano kupita maelezo?Ingelikuwa Tanganyika ina uwezo wa kuisadia nchi nyengine nadhani usingizi tungekuwa hatupati huko visiwani.Ni ukweli usio pingika kuwa Tanganyika ni moja ya sehemu zenye ufukara wa kutupwa.Hapo sina lengo la kukejeli bali huo ndio ukweli wa mambo.
Ndugu yangu Zanzibar sio mzigo katika muungano.Kama ingelikuwa mzigo wakati hio Tanganyika yenyewe ni mzigo tayari...basi nadhani mzigo huo wa visiwa ungelikwisha tupwa kitambo tokea babu yenu Nyerere hajafariki.
Mwenye macho haambiwi tazama, wazanzibari hawataki muungano hata kuuona maana ndio uliowatia ukara.Ving'ang'anizi ni Bara.Hilo linathibitika kila unapokaribia uchaguzi, majeshi pamoja na usalama huongezwa visiwani kuliko sehemu nyengine yoyote.Hii si bure, bali ni kuonesha kama Zanzibar si mzigo.Na kwa wema gani mulionao, hata mubebe mizigo isiowahusu!
Wazanzibari wepi hawataki Muungano? Mbona akina Nahodha, Shamhuna, Karume, etc wanausifia Muungano kupita maelezo?
Mwiba, choko choko mchokoe pweza, binadamu huta muweza!, hata kuku ukimchambua sana, utashindwa kumla! Hapa wataka tena kuuchoka Muungano halafu mkiambiwa ukweli, hamweshi kulia lia.......Alihoji ni jambo gani linalokwamisha utekelezaji wa matakwa hayo ya kikatiba ya kila upande kuchangia mfuko wa pamoja wa Muungano.
Awali, Mkullo akisoma hotuba ya bajeti yake kwa mwaka 2010/2011, alisema serikali ya Muungano na ya Zanzibar zimeendelea na uchambuzi wa taarifa mbalimbali za tume hiyo kuhusu vigezo vya kugawana mapato na kuchangia gharama za Muungano kwa ajili ya kuyafanyia maamuzi.