MZAHA WA CUF KUWA 'CHAMA TAWALA' NA 'CHAMA CHA UPINZANI' KWA WAKATI MMOJA KWA KIPINDI KILE KILE NDANI YA TAIFA MOJA!!!




22.JPG

525 × 700 - David Kafulila, Kigoma Kusini. Mkutano

Ni gharama kubwa sana kwetu sisi wapigakura kuchagua baadhi ya vijana wasiokua na msimamo thabiti kwenda bungeni kutuwakilisha.

Nilimtaza huyu Ndugu Kafulila kwa uchungu mkubwa sana jinsi alivyokua anaongea bungeni kutaka kulazimisha ndoa ya kisiasa kati ya CHADEMA na CUF wakati anafahamu fika kwamba CUF ni chama tawala ndani ya mipaka yetu hii ya Tanzania kwa mujibu wa mwafaka wake na CCM.

Mtu asitfute njia ya mkato wa kutafuta CHADEMA kusaidia kusafisha uchafu wa utawal wa kisheria na kidemokrsia kama ambavyo CCM na CUF walivyojisababishia kwa MWAFAKA WA MAKAMBA kule Visiwani na sasa Mwafaka huo ulivyowaletea mikanganyiko ndani ya bunge la Muungano na hata kutishia kuvunja muungano wetu misingi ya kisheria itakapolazimika kuzingatiwa.

Kwa mtaji wa kitendo tu cha bunge letu tukufu kule Dodoma ITAKAPOSHAWISHIKA KULAZIMISHA KUBADILISHWA KWA KANUNI YA BUNGE inayozungumzia sifa na muundo wa chama rasmi cha Upinzani bungeni basi moja kwa moja tangu hapo tujue kwamba taifa letu litakua limeingia moja kwa moja KATIKA MGOGORO WA KIKATIBA ambayo matokea yake huenda yasipendeze sana kwa wengi wwetu.

Hakika mara baada ya CCM kulazimisha ndoa kati ya CUF na CHADEMA huku bara wakati wakijua kwamba kula Zanzibar ndoa ni kati ya CUF na CCM basi naona kuna uwezekano mkubwa wa WA KUZUKA KWA MISURURU YA KESI JUU YA MGOGORO WA KIKATIBA NA KUHITAJIKA KWEPO KWA MAHAKAMA YA KIKATIBA NCHINI AU WATU NA VIKUNDI VISIVYOAFIKI HIYO HALI KULAZIMIKA KWENDA MAHAKAMA YA KIMATAIFA KUTAFUTA HAKI ILI KUNUSURU MUUNGANO WETU TANZANIA.

Mhe Kafulila, ulichukua angalau muda wako kuyafikiria haya kabla ya kuanza na mazungumzo yako kule bungeni???????????? Jamani tusipende kuleta majibu rahisi sana kwa swala ngumu kama hili.

Mwafaka wa Zanzibar ulikua na nia nzuri kwa kutulete utulivu kule visiwani lakini kwa kuwa wahusika huenda walikosa ushauri mzuri kisheria na matokeo ya utekelezaji wa mwafaka wenyewe ndani ya muungano wetu hasa kwa vyama vingine ambavyo havikuhushishwa kwenye mwafaka huo ndio leo hii imetufikisha hapa.

Nakumbuka sana Mhe James Mbatia alilipigia sana kelele wakati ule akitaka vyama vyote vya upinzani vihusishwa lakini kwa bahati maya sana hakusikilizwa na CCM. Inamaana Mbatia hakumpa briefing mbunge wake Kafulila juu ya ukwel huo???

Kwa mantiki hii hata mtu akilazimisha kubadilisha kanuni za mchezo bungeni wakati timu tayari ziko uwanjani tayari kucheza, jamba ambalo kwanza si la kawaida na ni ukiukwaji mkubwa wa misingi ya demokrasia ya vyama vingi ndani ya himaya ya nchi za jumuiya ya madola, pamoja na yote CUF bado haingii kisheria ndani ya kambi ya upinzani mpaka kwanza ama:

(1) CUF kijivue kutoka ndani ya mwafaka na CCM kule visiwani.

(2) au Serikali itangaze wazi kwamba kwa mwafaka wa CCM na CUF basi tayari walishavunja Muungano wetu na Zanzibar ili Watanzania tujue kabisaa kwamba kumbe mpaka sasa hatuna muungano ndipo CUF ipate kukubalika Bara kama chama cha upinzani bila kutupa jicho kwamba kule Visiwani chama hiki kimekaeje bungeni huko.

(3) Na kama hoja namba mbili ndio ukweli wa mambo ulivyo nchini mwetu basi kabla CUF haijavuka sakafu la bunge letu la muungano kule Dodoma kuja upande wa upinzani, kwa maana ya kwamba yanayoendelea bunge la Zanzibar sasa ionekane kana kwamba haituhusu huku Bara, basi kwanza ni sharti wabunge wote wa Zanzibar waondoke bungeni hapo bila kujali chama kilichomleta hapo bungeni.

Watanzania tuliowengi sana hatupendi hata kidogo tunu letu 'Muungano' kuvunjwa na mtu yeyote lakini mantiki hoja yenyewe inatuelekeza hivyo kwamba CUF kuingia kambi ya upinzani huku bara basi maana yake Muungano ulishavunja na wabunge wote kutoka Visiwani ni sharti waondoke bungeni Dodoma.
 
Muungano wetu unaelekea kuwa wa serikali moja kwa faida ya nchi zetu sote..
 
Muungano uliopo sasa ni sawa na ndoa ambayo watu wanaishi kwa mazoea tu, lakini upendo kamili kati ya wanandoa haupo.
Wanaogopa tu kuachana kwa kuchelea labda matatizo ya watoto, jinsi ya kugawana mali n.k
Hivyi ndivyo muungano wetu ulivyo.

Ni mara nyingi huku ughaibuni nikisema natokea Tanzania, kuna watu wa nchi nyingine wananiuliza Tanzania Tanzania or Tanzania Zanzibar? Of course huwa nawambia Tanzania ipo moja tu. Lakini najua kabisa kuwa Tanzania hapa ziko mbili.
 
Acheni upumbavu.. Russia fights to defend its union and its territory. Eti mnataka kuiachia Zanzibar, China and Taiwan. UK and Nothern Ireland and Falklands Islands... Sisi utnataka gawana..ili iweje? Tanzania ina matatizo mengi lakini muungano si moja yapo..
 

Lugha ya namna hii (red font) inaendana na mtu ambaye haoni matatizo ya muungano.
No further comments!
 
Katika hili msimamo wangu nikwamba tuwe na serikai tatu. Wazanzibari walizoea kulia eti tunawanyonya lakini wao ni wanyonyanyi wakubwa wakodi na jasho la watanganyika,. hebu fikiria

(a) Kodi zote za serikali zinazokusanywa Zbar zinatumika huko. Hii ina maana kuwa hela za kuendesha serikali ya muungano zote zinatoka bara.

(b) Zbar kuna wafanyakazi wa muungano wanaotoa huduma kwa SMZ na watu wake bure. Yaani wafanyakazi hao na nyenzo wanazozitumia vinagharimikiwa na Watz bara

(c) Zbar ida idadi ndogo ya watu kuliko hata DSM lakini wana wabunge takribani 50 katika bunge la muungano. Wabunge hawa wanalipwa na kodi za watanganyika licha yakwamba hakuna uwiano wa uwakilishi kieneo

(d) JK aliahidi kujenga hospital kubwa Zbar licha ya kuwa Swala la Afya halikokwenye muungano. Hii ina maana kuwa atatumia fedha za watanganyika



WALE WAZANZIBARI WALIOZOEA KULIA KUWA TUNAWANYONYA WAELEZE WANANYONYWA VP?
 

eleza maslahi tunayopaswa kuyatetea/kuyalinda katika muungano huu na si kutukana.
 
Tatizo la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni tatizo la muda mrefu sana na Ufumbuzi wake ni Wananchi wenyewe wa Tanganyika na Zanzibar wapewe nafasi ya

kupiga kura ya maoni na kuamuwa je Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uwepo au kutokuwepo kwa huo

Muungano? Kwa Maoni yangu Kuna mambo mengi ya kuyaangalia kwa ndani zaidi katika Nchi yetu haswa ukiangalia mambo ya Uchumi wa Nchi yetu bado ni Mchanga sana umasikini, Maradhi, njaa, ukosefu wa ajira, Ufisadi, Ujambazi, na hali mbaya ya Uchumi wa Nchi yetu haya kwetu ni Matatizo Makubwa na yamekuwa kama ni Maradhi na kama hayo Maradhi

yamekuwa Maradhi Sugu. Tuyatafutie dawa jamani tusiangalie Mambo tu ya Kuvunja Muungano,tuangalie mpaka sasa tumetokea wapi na tunakwenda wapi?Hatuna Maji Masafi hatuna Umeme wa kutosha hatuna Barabara nzuri haswa Mikoani ukitoka Mji

Mkuu wa Dares-Salaam mikoa mingine basi balaa tupu miji yetu ya mikoani inatia aibu sana sijuwi viongozi wa Nchi yetu wakisafiri kwenda nje ya nchi hawaoni Maendeleo ya Nchi wanakokwenda?Nchi yetu inatia aibu kwa Watalii wanaokuja hapo

kwetu basi ukiwa DAR ndio kuzuri na kuliko baki kama upo Porini? Tujadili maswala ya kuendeleza Nchi yetu sio kurudi nyuma Wazungu wa Ulaya Wanaungana kuufanya Ulaya kuwa na nguvu kama bara la Amerika sisi bado tunafikiria kuuvunja Muungano

tunarudi nyuma baada ya kwenda mbele? huo ni ujinga wa hali ya juu sana tuache Chuki na fikira mbovu za huyu Mtu wa Bara mimi ni Mtu wa Vsiwani tuache hisia zetu potufu

tuijenge kwanza nchi yetu ili tuweze kuondokana na hayo Maradhi Sugu niliyoytaja hapo juu. Kwa Mawazo yangu Hao Wanaotaka kuuvunja Muungano wetu hao ndio maaduwi wetu Wakubwa MAPAMBANO BADO YANAENDELEA.
 
Tuesday, 01 March 2011 20:42

Na Awadh Ali Said

FEBRUARI 9, gazeti moja la kila wiki lilitoa makala iliyosema “Muungano wa Tanzania sasa umekuwa dhaifu zaidi’’ iliyoandikwa na Tundu Lissu.

Mwandishi amejaribu kujenga hoja inayotoa taswira kuwa Muungano wa Tanzania umezidi kuwa dhaifu kutokana na Mabadiliko ya Kumi ya Katiba ya Zanzibar ya 1984 ambayo yeye anaamini kuwa mabadiliko hayo
“yamemong’onyoa misingi karibu yote ya muungano … yamebadili sura ya muungano wenyewe, mipaka yake na muundo wake” na kwamba anakhofu kuwa mabadiliko hayo “yanaweza kuwa chanzo kikuu cha kubomoka kwa Muungano na hata tishio kwa usalama wa mipaka ya Taifa”.

Hoja ya kwanza ni kuwa Mabadiliko ya Kumi ya Katiba ya Zanzibar yaliitangaza Zanzibar ‘‘kuwa nchi yenye mipaka kamili.” Anaendela kueleza kuwa “Rais anajua kuwa kabla ya mabadiliko hayo kufanyika, Zanzibar haikuwa nchi na wala mipaka yake haikutajwa.” Anaegemeza hayo akirudia kifungu cha kwanza cha Katiba ya Zanzibar 1984 (kabla ya marekebisho) kinachosema ‘‘ Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”

Katika hoja hii ya kwanza kuna mambo mawili; la kwanza kuwa Mabadiliko hayo ya kumi ndio yaliyoitangaza Zanzibar kuwa nchi, na la pili ni kuwa mabadiliko hayo ndiyo yaliyobainisha mipaka ya Zanzibar ambayo mwanzo haikutajwa. Yote mawili katika hoja hii siyo ya kweli. Tuanze na la kwanza la Zanzibar kuwa nchi.
Zanzibar ilikuwa na Katiba yake ya kwanza mwaka 1979 ambayo baadaye ilifutwa na kuandikwa upya mwaka 1984, na hadi leo hii Zanzibar inaongozwa na Katiba yake hiyo ya 1984 ambayo imeshafanyiwa marekebisho mara 10. Sasa tujiulize je, Katiba ya Zanzibar ya 1984 haikutaja Zanzibar kama nchi ila baada ya hayo marekebisho ya kumi yanayolalamikiwa?
Ni kweli Katiba ya Zanzibar ya 1984 kabla ya marekebisho ya kumi ilieleza katika kifungu cha 1 kuwa “ Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.” Lakini ukiwacha kifungu hicho cha kwanza vifungu kadhaa wa kadhaa au tuseme katiba yote ya Zanzibar (kabla ya hayo marekebisho ya kumi) yakiitaja Zanzibar kuwa ni nchi. Angalia vifungu (baadhi tu) ili tuweke sawa hili:

(9)(i) Zanzibar itakuwa ni NCHI ya kidemokrasia na haki za kijamii.

(9)(2)(a) Mamlaka ya kuendesha NCHI ni ya wananchi wenyewe …

Pia vipo vifungu kadhaa katika Katiba ya Zanzibar vinavyoeleza kina ubaga kwamba Zanzibar ni nchi ambayo ina dhamana kwa wananchi wake.

Msingi mkuu katika kanuni za kutafsiri sheria (Statutory Interpretation ) ni kuwa ili uweze kupata tafsiri sahihi kwa waraka wowote (iwe ni Katiba, Sheria, Mkataba n.k.) ni kuwa unatakiwa uusome waraka wote ndipo uweze kufahamu maana, tafsiri au dhamira inayopatikana kwa ujumla katika waraka huo kuhusiana na jambo husika. Sio kuchopoa kifungu kimoja tu ukaegemeza hoja yako hapo hapo tu.

Lakini bila ya kuangalia vifungu vyengine vya katiba hiyo ya kabla ya marekebisho ya 10,tuangalie hicho kifungu kimoja tu, cha kwanza, kama alivyofanya mwandishi kinachosema ‘‘Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano” Sasa tujiulize Zanzibar kama sehemu ya Jamhuri Ya Muungano inasimama katika utambulisho upi? Sawa ni sehemu ya Jamhuri, lakini utambulisho wake ni upi? Ni sehemu kama Mkoa, Wilaya, Tarafa, Jimbo, Kata au kitongoji?

Zanzibar ina katiba yake, ina Rais wake, ina Mahkama zake, ina mawaziri wake, ina Baraza lake la kutunga sheria, ina watu wake (tena wana ID zao), ina bendera yake, ina wimbo wake wa Taifa, ina Mamlaka yake ya Serikali za mitaa, ina magereza yake (vyuo vya mafunzo), ina vikosi vyake vya ulinzi, ina mapato yake na bajeti yake n.k. Je, kuna Mkoa au Wilaya yenye yote hayo? Na yote hayo yapo kabla ya hayo mabadiliko ya kumi ya katiba ya Zanzibar. Hivyo hakuna ukweli wowote kuwa Zanzibar imetangazwa kuwa ni nchi kwa mabadiliko ya 10 ya katiba ya Zanzibar 1984.

Mwandishi anasema:

“Rais anajua kuwa kabla ya mabadiliko hayo kufanyika, Zanzibar haikuwa nchi na wala mipaka yake haikutajwa”. Je, ni kweli mipaka ya Zanzibar haikutajwa kabla ya marekebisho ya 10 ya Katiba ya Zanzibar ? Tuangalie katiba ya Zanzibar 1984 kabla ya mabadiliko ya 10 kifungu cha 2(i) kinasemaje:

2(i) “Eneo la Zanzibar ni eneo lote la visiwa vya Unguja na Pemba na visiwa vidogo vidogo vilivyoizunguka na bahari yake ambayo kabla ya Muungano ikiitwa Jamhuri ya watu wa Zanzibar.”

Na baada ya marekebisho ya kumi kifungu hicho kinaendelea kuwapo kama kilivyo kuhusiana na suala la mipaka.

“1) Zanzibar ni nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogo vidogo vilivyoizunguka bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya watu wa Zanzibar”.

Hoja ya pili ya mwandishi ni kuwa marekebisho haya yanadhoofisha Muungano kwa vile yameondoa mamlaka ya kuigawa Zanzibar katika mikoa kutoka mikononi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na kuweka mamlaka hayo kwa Rais wa Zanzibar. Hili ni kweli limefanyika katika marekebisho ya 10 ya Katiba ya Zanzibar. Lakini tujiulize ni kwa nini limefanyika? Inaeleweka wazi kuwa ni Rais wa Zanzibar ambaye kipindi chote tokea huo Muungano wa Tanzania uasisiwe 1964, ndiye anayeigawa Zanzibar katika mikoa na wilaya.

Hakuna kumbukumbu inayoonyesha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano amewahi kuigawa Zanzibar katika Mikoa au Wilaya. Sasa kwa takriban miaka 47 mamlaka hayo yalikuwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano kikatiba lakini kiutendaji na kiutekelezaji aliyekuwa anatekeleza mamlaka hayo ni Rais wa Zanzibar; hivyo hiyo ilikuwa ni kasoro na ilistahiki kurekebishwa, na ndicho kilichofanyika. Haiwezekani tukadumisha vifungu ndani ya katiba ambavyo vinaonekana ni pambo tu. Hili litoshe kuonyesha mkanganyiko uliomo katika katiba zetu.

Hoja ya tatu ya mwandishi ni kuwa mabadiliko ya kumi yamepunguza mamlaka ya Mahakama ya Rufani ya Tanzania. Anasema:

“Mabadiliko ya katiba yaliyofanyiwa yamekiuka katiba kwa kuinyang’anya Mahakama ya Rufani ya Tanzania mamlaka ya kusikiliza rufani zote zinazotoka katika Mahakama Kuu ya Zanzibar”

Kwa ufupi haijawahi kutokea kwa Mahakama ya Rufani kuwa na mamlaka ya kusikiliza rufaa zote zinazotoka katika Mahakama Kuu ya Zanzibar tokea ianzishwe.

Hoja ya nne ya mwandishi ni kuwa mabadikilo ya 10 ya katiba ya Zanzibar yamekiuka katiba ya Jamhuri ya Muungano na kudhoofisha Muungano kwa vile sasa Zanzibar “imehalalisha uwepo wa vikosi vya Jeshi vya SMZ vinavyoviita Idara maalum” Ama kuhusu hili la “Vikosi vya kijeshi” kama alivyoviita mwandishi au ‘‘Idara Maalum” kama vinavyoitwa na katiba ya Zanzibar, hata kabla ya hayo mabadiliko ya kumi inaeleza kuwepo kwa Idara Maalum na ambazo ni Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU), Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM), Chuo cha Mafunzo na kifungu hichi hakikubadilishwa hata nukta.
Hizi ni Idara kongwe zipo Zanzibar na wala hazijaundwa na mabadiliko ya kumi na hayo mabadiliko ya kumi hata hayakugusa chochote kuhusu Idara hizi. Sijui haya yametokea wapi?

Mwisho nikubaliane na mwandishi kuwa Muungano wa Tanzania umezidi na unazidi kuwa dhaifu kila uchao na sababu za hayo zipo na ziko wazi lakini kamwe sio mabadiliko ya 10 ya katiba ya Zanzibar.

Samahani: Makala ya Hoja kutoka Zanzibar ya Ally Saleh, wiki hii hatukuweza kuitoa kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu.
 
Sijaona sehemu ikizungumzia uwepo au utambulisho wa MAKAMU WA KWANZA NA WA PILI WA RAIS WA ZNZ.
Je navyo vilikuwepo tangu 1984???
Kwenye Muungano hao makamu wa ZnZ wametamkwa wapi ktk katiba ya muungano??
Nikirudi nitachambua maelezo yako mengine
 
Wana JF, nadhani ni muhimu kuwasikiliza hawa jamaa hasa tunapoelekea kuwa na katiba mpya. Nilichokisikia kutoka kwa wachangiaji kinaonyesha ufinyu mdogo sana wa kuchambua mambo,na hapa naona suala la mjadala wa katiba mpya litakuwa gumu. Hii ni summary ya majadiliano kama nilvyoyasakia.
Waznz anasema kuna haja ya kuwa na katiba mpya kwani iliyopo haikuwashirikisha Wananchi. Katiba ya sasa imemeza mambo mengi muhimu ndani ya Tanganyika. Wanataka muungano uvunjwe ili wajiunge na EA, na wawe na waziri wao atakayewawezesha kuomba misaada. Wanashangaa kwanini mkuu wa majeshi na Polisi hawachaguliwi kwa zamu kutoka Bara na Visiwani. Waznz wanashauri nchi yao ipewe uhuru wa kujiamulia mambo ili kuwadhibiti Watanganyika wasiingie visiwani kwani Znz ni kisiwa na kipewe heshima stahiki. Wanauliza kama muungano wetu ni mzuri kwanini Kenya na Uganda hawajajiunga? Yupo aliyeshauri tujadili muungano kabla ya katiba na mwingine ameshauri Wznz waingie barabarani kama Egypt ili muungano uvunjike.
Wakili maarufu ame challenge hoja za Mh Warioba, akisema kuwa kwa WZNZ kugombea nafasi za udiwani na ubunge huku bara ili hali wabara hawana nafasi hiyo viwani si sula la tija kwa Wznz.Kwa ujumla wanataka mgawanyo wa madaraka na uchumi uwe nusu kwa nusu.

Licha ya mada nzuri iliyowasilishwa na Prof. Shivji yenye mada 'Je tunahitaji katiba mpya?' wengi waliondoka nje ya mada na kuushambulia muungano kikamilifu. Hakuna hata mmoja aliye eleza faida za muungano kiuchumi, kisiasa au kiutamaduni japo chache zaidi ya laana juu ya muungano.
 
Waondoke tunamhitaji mama yetu TANGANYIKA tume-mmiss sana, huyu ndiyo mkombozi wetu alitupatia ardhi yetu toka kwa mkoloni.Baba aliamua kumtelekeza mama yetu Tanganyika tunamtaka mama yetuuuuuuuu.Na huyu ataletwa na peoples poweeeeeeeeeeeeeeeer chini ya Rais bora afrika mashariki Dr.W.P.Slaa
 
Waondoke. We are better off without them.

If you guys you are better off without us. Kwanini mnaukumbatia muungano na hata kujidhalilisha kwa kuuwa utaifa wenu wa Tanganyika.

Acheni kiherehere chenu.
 

Kwanini msiandamane kwanza kurejesha utaifa wenu wa Tanganyika na serikali yake mliyo iua kwa ajili ya kiherehere chenu cha Muungano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…