Siijui vizuri hii ishu, lakini this one comment inaonekana ku-make a lot of sense, anyways sielewi sababu za Maalim na CUF kukataa kura za maoni, lakini angejaribu kuupa a chance, maana ninaamini kuwa next time CCM watampa no choice kabisaa, na atalazimika kubeba the worst, maana inategemea ni nani atachukua urais huko,Lakini still, I am lost na hii ishu ya muafaka in general.
Kuna hatari ya watu hapa kujadili kwa kuelemea upande mmoja wakifuata mrengo wa chama akipendacho mimi sipo huko nipo katika misingi ya haki za binadamu.
Niliwahi kusema CCM walikuwa na haki ya kuyakataa au kuyakubali,walichokifanya CCM ni kuongeza jambo jingine ambalo ni jipya,taarifa za ndani zinasema yote yaliokuwa yakijadiliwa yakifikishwa kwa Mh.Kikwete na Karume na wao wakitoa michango yao,kilichotakiwa kufanywa na CCM na CUF ni kuyakubali au kuyakataa na sio kuongeza jambo jipya na kulirudisha ili lianze kujadiliwa upya hapo ndipo CCM walipo vaa mkenge na hawawezi kutoka kwa hapo kwani muafaka umekuwa locked,ndio maana ya kumalizika na kurudishwa kwa vyama vyao ili viwatangazie wateja kama wao ndio viongozi wakuu.Kama viongozi wenu tumekubaliana hili na lile.Hili la kura ya maoni CCM walikuwa nalo lakini walilificha na kuliweka kiporo ili kuipiku CUF kama walivyoonekana katika maandishi yao,kwa ilivyo walitakiwa walilete kwenye kamati na kujadiliwa ,sio unaliweka ili liwe kikwazo cha baadae kama ilivyotokea.
Tumeona Kamati ya Richmond ,na hata hapa JF iliwekwa ,imefikishwa Bungeni imesomwa na hatua zimechukuliwa na bado na bado nyengine zitafuata.
Sasa Chiligati anawaomba CUF warudi haraka kumaliza mazungumzo,sijui jambo gani lililomfanya aharakize hivyo,wakati mmoja wao alisema kama hawatorudi ndio muafaka umekufa,CUF wameshasema kama ni kujadili jambo jipya hawako tayari na msiwategemee kwa hilo,muafaka umeshafungwa rasmi haya ni mambo ambayo yamejadiliwa kwa muda wa miezi kumi na nne tofauti na Kenya ambako hayakufika hata mwezi , na huenda ikawa pia ni tofauti na Zimbabwe.
CUF wamesema hawana wakati wa kuwadanganya wananchi na kuwafanyia usanii na uhuni wakimaanisha mifano ya kushughulikia ufisadi kuwa watu wameshatiwa hatiani bado wanapewa madaraka bungeni,Balali na kundi lake wameshaonekana kufanya ubadhirifu bado hawajachukuliwa hatua zozote,Mkapa kufanya Biashara akiwa serikalini tena Raisi wa Nchi ,hakuna lolote limefanywa,huu ni usani wa uhuni ambao CUF umesema unafanywa dhidi ya wananchi na Chama kilichoko madarakani ,CUF hawana sera hizo.
Narudia kusema CCM wanayo haki ya kuyakubali au kuyakataa kama wenzao wa CUF ,kwa yale yaliokubaliwa na Kamati yao ya pamoja na si vinginevyo kuzidisha au kupunguza,madai yote yatoke ndani ya makubaliano.