Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Hakuna haja ya kuandika sana na kumsema ovyo mpiganiaji haki wa WaZanzibari ,huyu ni sawa na mpiganiaji wa ukombozi wa Wananchi wake ambao wamewahi kutokea hapa duniani ,kuna aina nyingi za mapambano wako wanaoona maneno ya mezani hayafai ni bora msituni na wako wanaoona maneno yote yawepo mezani.Seif .
Kusema Seif ni mpigania haki za Wazenj, ni kituko cha mwaka, labda awe mpigania haki ya tumbo lake hapo nitakuelewa...

Seif hana tofauti yoyote na mafisadi wa sasa katika nchi hii, pengine tofauti ni kwa kuwa yeye hana serikali....
 
Huko Nyuma nilishawahi kumlinganisha na Marehemu. Jonas Savimbi... ambaye alivyoondoka tu... it took hardly less than 10 days... vita ya miaka zaidi ya 25 ya Angola ikaisha...Ingawa siku zote tuliambia tatizo ilikuwa la chama chake cha UNITA, kumbe ilikuwa yeye mwenyewe Savimbi.

Na leo hii Maalimu Seif akisema siasa basi, au hagombei tena, au uongozi wa siasa basi... Muafaka Zanzibar utapatikana same day/week/month or maximum same year. Kwani Tatizo sio CUF, tatizo ni Maalim Seif mwenyewe.

Siijui vizuri hii ishu, lakini this one comment inaonekana ku-make a lot of sense, anyways sielewi sababu za Maalim na CUF kukataa kura za maoni, lakini angejaribu kuupa a chance, maana ninaamini kuwa next time CCM watampa no choice kabisaa, na atalazimika kubeba the worst, maana inategemea ni nani atachukua urais huko,

Lakini still, I am lost na hii ishu ya muafaka in general.
 
nimekaaa na kufikiria upya kuhusu suala la kwetu na nimekuja na haya huenda ya kutusaidia.


moja ss ccm tunaamini wazi kuwa wenzetu cuf wanabagua wazanzibari na hili wamelirithi kwa muda mrefu kutoka vyama vilivyopigania uhuru.

wao wanaamini kuna wazanzibari na wazanzibara au majina mengine wakavirondo. wakati ule wa uhuru vyama vyao vilikuwa vikiwaita magozi na wao wanaamini sio wazanzibari na hawastahiki kuwa na nafasi yeyote zanzibar.


na afro shirazi ikifatiwa na ccm wao wanaamini waafrika wote ni ndugu na waliopo zanzibar ndio kwao bila ya kujali kama umetoka bara, kenya au nyasa land .


karume(mkubwa) alipoingia alijitahidi kuhakikisha jambo hili analimaliza kabisa na mikakati yetu wakati ule tuliimairisha sana kwa vijana.


tulihakikisha vijana wanaishi na kushirikiana kwa umoja na nguvu na kujifagharisha uzanzibari wao, sio ukabila wao au sehemu aliotoka na kwa msingi huu tulilazimisha watu waowane ili ifike siku huna sababu ya kumchukia mwengine. nyote mmechanganyika hakuna mwarabu wala muhindi wala mmakonde.


tulianzisha kwa makusudi mchango wa kielimu wapemba wanakuja unguja na kusoma boarding skuli na wenzao wa unguja na waunguja wanaenda pemba kusoma na wenzao wapemba na wengi walisoma hivyo na kuamini kuwa wao ndugu na kuoleana pasipo na kutumia nguvu tena.


ila baadae wachafuzi wakaingia kwenye system kwa makusudi wakaendeleza vitendo vya kibaguzi wakawafanya watu waanze kuangalia nyuma baada ya kusonga mbele.

mambo yakawa mabaya zaidi na chuki zikazidi kupandikizwa mpaka sasa tatizo si wabara na wazanzibar tu, likahamia baina ya wapemba na waunguja na likapelekwa baina ya wapemba wa kusini na wa kaskazini.

hali imekuwa mbaya sana, watu hawaaminiani kabisa kabisa, imefika pahala wazanzibari kufanya kazi pamoja ni suali zito na gumu, imekuwa aibu ofisini kabla ya kupata huduma unataka kujua mtoa huduma ni wa upande gani na matokeo yatayotolewa kutokana na huduma ulioomba utajaji kwa upande wa yule mtu nimenyimwa kwa kuwa mm na kwa kuwa yy.


tukija sasa hali hii na kuanza serikali ya mseto moja kwa moja ni hatari maana hali haijatulia nnaamini kila failure italazimishwa ionekane inatokana na watu fulani na kila success italazimishwa ionekane ya upande fulani.


suluhisho nilionalo ni kuunda serikali ya kitaifa kama zilivyo wakati wa nyuma kabla ya vyama vingi, chama kiwe kimoja kitachoshinda iwe ccm au cuf lkn rais awe muunguja au mpemba na waziri kiongozi awe upande mwengine na mawaziri na ngazi nyengine ziende hivyo.

ccm tulitegwa tukaingia ss siasa yetu sio wabaguzi lakini wenzetu waliendeleza na ss tukaamua kuwafata, hili ni kosa na limetutia doa. tunapaswa kujirekebisha.

tuweke mazingira mazuri ya tume ili hawa wenzetu wasipate pa kutolea lawama lkn kutawala pamoja tusiliunge mkono.

na wala kuwabagua tusiwabague, wanatumia udhaifu wetu huo kuhalalisha madai yao
 
Kusema Seif ni mpigania haki za Wazenj, ni kituko cha mwaka, labda awe mpigania haki ya tumbo lake hapo nitakuelewa...Seif hana tofauti yoyote na mafisadi wa sasa katika nchi hii, pengine tofauti ni kwa kuwa yeye hana serikali....

Unaweza kuwa na muelekeo wa aina hiyo ikiwa tu mawazo yako yanapingana na akili yako na hakuna coordination kati yao.
Fahamu tu East Timo wana kiongozi ambae ameweza kuwakomboa kutoka kwa utawala mkuu ,kutokana na ukandamizwaji waliokuwa wakifanyiwa leo hii wapo huru ,hata katika Nigeria wako akina Calonel Emeka Ojokwu ambae aliendeleza mapambano dhidi ya serikali kuu kwa kutumia mtutu kama umewahi kusikia Jimbo la Biafra na mambo yao bado yanaendela mpaka kieleweke ndio ukasikia maengeneer wanaokwenda Nigeria kuchimba hazina ya huko huuliwa kila wanapoanza mazoea na wakazi.I don't feel any responsible at all for Mr Seif Sharif he did the best he could to resolve the Zanzibar Issues.And still on the move !!!
 
Siijui vizuri hii ishu, lakini this one comment inaonekana ku-make a lot of sense, anyways sielewi sababu za Maalim na CUF kukataa kura za maoni, lakini angejaribu kuupa a chance, maana ninaamini kuwa next time CCM watampa no choice kabisaa, na atalazimika kubeba the worst, maana inategemea ni nani atachukua urais huko,Lakini still, I am lost na hii ishu ya muafaka in general.

Kuna hatari ya watu hapa kujadili kwa kuelemea upande mmoja wakifuata mrengo wa chama akipendacho mimi sipo huko nipo katika misingi ya haki za binadamu.
Niliwahi kusema CCM walikuwa na haki ya kuyakataa au kuyakubali,walichokifanya CCM ni kuongeza jambo jingine ambalo ni jipya,taarifa za ndani zinasema yote yaliokuwa yakijadiliwa yakifikishwa kwa Mh.Kikwete na Karume na wao wakitoa michango yao,kilichotakiwa kufanywa na CCM na CUF ni kuyakubali au kuyakataa na sio kuongeza jambo jipya na kulirudisha ili lianze kujadiliwa upya hapo ndipo CCM walipo vaa mkenge na hawawezi kutoka kwa hapo kwani muafaka umekuwa locked,ndio maana ya kumalizika na kurudishwa kwa vyama vyao ili viwatangazie wateja kama wao ndio viongozi wakuu.Kama viongozi wenu tumekubaliana hili na lile.Hili la kura ya maoni CCM walikuwa nalo lakini walilificha na kuliweka kiporo ili kuipiku CUF kama walivyoonekana katika maandishi yao,kwa ilivyo walitakiwa walilete kwenye kamati na kujadiliwa ,sio unaliweka ili liwe kikwazo cha baadae kama ilivyotokea.
Tumeona Kamati ya Richmond ,na hata hapa JF iliwekwa ,imefikishwa Bungeni imesomwa na hatua zimechukuliwa na bado na bado nyengine zitafuata.
Sasa Chiligati anawaomba CUF warudi haraka kumaliza mazungumzo,sijui jambo gani lililomfanya aharakize hivyo,wakati mmoja wao alisema kama hawatorudi ndio muafaka umekufa,CUF wameshasema kama ni kujadili jambo jipya hawako tayari na msiwategemee kwa hilo,muafaka umeshafungwa rasmi haya ni mambo ambayo yamejadiliwa kwa muda wa miezi kumi na nne tofauti na Kenya ambako hayakufika hata mwezi , na huenda ikawa pia ni tofauti na Zimbabwe.
CUF wamesema hawana wakati wa kuwadanganya wananchi na kuwafanyia usanii na uhuni wakimaanisha mifano ya kushughulikia ufisadi kuwa watu wameshatiwa hatiani bado wanapewa madaraka bungeni,Balali na kundi lake wameshaonekana kufanya ubadhirifu bado hawajachukuliwa hatua zozote,Mkapa kufanya Biashara akiwa serikalini tena Raisi wa Nchi ,hakuna lolote limefanywa,huu ni usani wa uhuni ambao CUF umesema unafanywa dhidi ya wananchi na Chama kilichoko madarakani ,CUF hawana sera hizo.
Narudia kusema CCM wanayo haki ya kuyakubali au kuyakataa kama wenzao wa CUF ,kwa yale yaliokubaliwa na Kamati yao ya pamoja na si vinginevyo kuzidisha au kupunguza,madai yote yatoke ndani ya makubaliano.
 
..mimi NJIA WANAYOTUMIA CUF KUDAI HAKI NAONA INA WALAKINI..SIKUBALIANI NA HILI LA SEIF NA TIMU YAKE KUTEGEMEA ZAIDI ZIARA ZA NJE ,KUWEKA SHINIKIZO.....VITA VYA KWELI VYA HOJA VIPIGANWE ZANZIBAR NA PEMBA ...MIKUTANO YA HADHARA,MIGOMO....[YA AMANI]....ETS VITASAIDIA ZAIDI....TATIZO LA CUF HALINA TOFAUTI SANA NA LA ODM AMABAKO KENYE KUNA JAMII ZINAHISI KUNYIMWA UTAWALA...SIKUMUONA HATA SIKU MOJA RAILA AKIENDA NJE KWA KIPINDI CHOTE CHA MGOGORO..ALIPIGANA NDANI...ZAIDI NJE ALIWATUMA WAJUMBE WAKE WA KAMATI KUU KUFANYA KAMAPENI YA KIMATAIFA.....

STRATEGY REVIEW FOR CUF PLEASE!!
 
Mtu wa Pwani:
Nakuuliza tena una uhakika mimi ni mbaguzi wa kidini?
Hivi kwanini viongozi wa vyama na serikali ya hapa zanzibar wooote ni waislamu?Hili limefanyika na waislamu,then unaacha kukemea ushenzi huu,na kuniita mimi mbaguzi wa kidini.
Hivi huwa unakaa na kufikiria kabla ya kukosoa watu?hivi ni kwanini mnapinga politics za BUSH zidi ya waislamu wenzenu huko uarabuni?so mnataka na sisi tuwaachie wakristo wenzetu waingie ktk gharama zisizo na maslahi kwao?embu nikuulize wewe mnafiki,wakristo watafaidika vipi na kuisaidia serikali ya zanzibar?wakati hata mjumbe wa shina mkristo hapa zenj hakuna.
Naomba ujicheck kwanza,usitake tufunue na yasiyofunuliwa hapa.
Br. Gen. (Retired) Adam Mwakanjuki ni Mkiristo (anasali kila ,Jumapili) hivi sasa ni Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi katika SErikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Bw. Joseph Meza ni Mkiristo (anas ali kila Jumapili) Hivi sasa yeye ni Katibu Mkuu katika Wizara ya Biashara,Utalii,na Uwekezaji.
 
..mimi NJIA WANAYOTUMIA CUF KUDAI HAKI NAONA INA WALAKINI..SIKUBALIANI NA HILI LA SEIF NA TIMU YAKE KUTEGEMEA ZAIDI ZIARA ZA NJE ,KUWEKA SHINIKIZO.....VITA VYA KWELI VYA HOJA VIPIGANWE ZANZIBAR NA PEMBA ...MIKUTANO YA HADHARA,MIGOMO....[YA AMANI]....ETS VITASAIDIA ZAIDI....TATIZO LA CUF HALINA TOFAUTI SANA NA LA ODM AMABAKO KENYE KUNA JAMII ZINAHISI KUNYIMWA UTAWALA...SIKUMUONA HATA SIKU MOJA RAILA AKIENDA NJE KWA KIPINDI CHOTE CHA MGOGORO..ALIPIGANA NDANI...ZAIDI NJE ALIWATUMA WAJUMBE WAKE WA KAMATI KUU KUFANYA KAMAPENI YA KIMATAIFA.....

STRATEGY REVIEW FOR CUF PLEASE!!

Ndugu yangu Michael,
Mie nakubaliana kwa 100% na njia ya kudai haki kwa Maandamano na migomo. Lakini ni lazima tukubali kuwa kuna watu wengi watakufa kwani CCM haitakubali, na kama kawaida yao watatumia dola. Sasa naona ni busara kabla hujamua maisha ya watu yapotee, ni vizuri kuhahakisha njia zote sawia za amani umezi-apply.
Watanzania hatukawii kuja hapa na kuanza kusema, Oooh CUF ni chama cha fujo kwa nini waliamua kufanya maandamano/ migomo wakati wamezuiwa.
 
Kwa kukumbushana tu, CuF imewahi kufanya yafuatayo:-
  • Kupaka vinyesi katika shule
  • Kuweka vinyesi vya binadamu katika visima vya maji
  • Kulipua mtambo wa ugawaji umeme Zanzibar(kidatu)
  • Kutoa talaka kwa wake zao ambao ni ccm
  • kugoma kushiriki katika shughuli za maziko
  • kugoma kushiriki katika shughuli za arusi
  • Na pengine kuanzisha hadithi za popo bawa 😀
 
Jamani hii thread imakaa vibaya kwa mtizamo wangu, jamaa anaistigate coup de tat hii inaweza kusabababisha umwagikaji wa damu hata za wasio na makosa....Wanzazibara watumie kupiga kura kuwaondoa hao akina Shamhuma, Zimbambwe wameonyesha nyia kumtoa jimbi, pamoja na kuiba kura imeshindikana...sauti za wengi ni sauti ya MUNGU

..kwahiyo iondolewe? kwakuwa inachochea uhaini?halafu,mapinduzi yale hayakumwaga damu zisizo hatia?

..wazanzibar watajua wenyewe nini cha kufanya!kama wanaona sawa,itakuwa sawa! kama wanaona mizengwe,basi kutakuwa na mizengwe!

..enzi za kuburuzana zimepita!watu watakula wakitakacho,wasichokitaka kitatupwa jalalani.
 
Kwa kukumbushana tu, CuF imewahi kufanya yafuatayo:-
  • Kupaka vinyesi katika shule
  • Kuweka vinyesi vya binadamu katika visima vya maji
  • Kulipua mtambo wa ugawaji umeme Zanzibar(kidatu)
  • Kutoa talaka kwa wake zao ambao ni ccm
  • kugoma kushiriki katika shughuli za maziko
  • kugoma kushiriki katika shughuli za arusi
  • Na pengine kuanzisha hadithi za popo bawa
  • 😀

enough said, CHADEMA mbona siwasikii siku hizi ! kelele zao zimeishia wapi ?
 
Br. Gen. (Retired) Adam Mwakanjuki ni Mkiristo (anasali kila ,Jumapili) hivi sasa ni Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi katika SErikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Bw. Joseph Meza ni Mkiristo (anas ali kila Jumapili) Hivi sasa yeye ni Katibu Mkuu katika Wizara ya Biashara,Utalii,na Uwekezaji.


Wawili tu katika serikali nzima?
 
Kwa kukumbushana tu, CuF imewahi kufanya yafuatayo:-
  • Kupaka vinyesi katika shule
  • Kuweka vinyesi vya binadamu katika visima vya maji
  • Kulipua mtambo wa ugawaji umeme Zanzibar(kidatu)
  • Kutoa talaka kwa wake zao ambao ni ccm
  • kugoma kushiriki katika shughuli za maziko
  • kugoma kushiriki katika shughuli za arusi
  • Na pengine kuanzisha hadithi za popo bawa 😀

Naona umesahau ulikusudia CuF na sio CUF hiyo ya mwanzo ni Chama cha ufisadi kwa wingi utapata Chama cha mafisadi CCM).
Kupaka vinyesi wanajulikana kwa majina ni CCM wakiongozwa na jamaa aitwae Edi CCM mkereketwa wakati wa Salmini ,huyu kidogo hawapatani na Karume wanasema ni ndumila kuwili.
Kulipuwa mitambo ya umeme wanajulikana ni CCM ndio waliolipua na kurusha mabomu kwenye mahoteli na majumba Wanajulikana ni CCM maana nakumbuka walitoka mbwa wa polisi na ripoti yao imetiwa kapuni kwani ni wenyewe kwa wenyewe ,guruneti lilorushwa ndani ya nyumba pemba waliorusha ni CCM na kumripwa mwenzao ambae alitibiwa muhimbili ,wamejulikana kama ni wao.
Kutaka kumuua Seif Sharif na kumsingizia amepora silaha ,mwanamke aliepewa au aliechukua jukumu lile alichelewa na kuwahiwa na walinzi wa CUF alipokuwa akipewa amri ya haya muuwe au mpige ,hapa CUF walikuwepo kwenye maskani yao wakikutana wakubwa na wadogo ili kuweka gumzo la siku halafu watu wajiendee zao kulala ,jamaa hawa wa CCM waliokuja kutimiza haja yao ya kutaka kuua au kumuua Maalim Seif walipofika walitoa sababu za kwa nini mnafanya mkutano au kwa nini mumekusanyika hapa wakati wakiuliza ulizia ndipo kati yao aliposikika akisema haya mmalize nafasi ndio hii hapo ndipo alipowahiwa na kuchezea kisago cha mbwa koko ,hadi hii leo bado anauguza kipigo ,inasemekana huwa anasema kuwa alikuwa tayari kumfyetua maali Seif. Jina la mwanamke huyu nitaliulizia kwa wazenji walio karibu nae.
Tatizo hapa ni kuwa security ya CUF ni kali na imepenya ndani ya CCM Zanzibar hivyo kila wanalolifanya basi linajulikana sasa CCM wametupa vikaratasi kuwataka eti Wapemba warudi kwao.
 
sidhani kama maalim seif ameenda kuishitaki CCM kwa maslahi yake binafsi kwasababu kuu mbili zifuatazo.
1. Maslahi yake yamesha kamilika siku nyingi na kama ingekuwa anayoyafanya ni kwa ajili ya maslahi yake basi angekuwa hana ulazima tena. Si analipwa stahili zake kama waziri kiongozi mstaafu?
2.Kama mtasoma ile taarifa ya seif "aenda ulaya" kuna paragraph moja inasema alikuwa ahudhurie ule mkutano kabla hata CCM hawajawapiku CUF sasa iweje leo hii watu wanga'ang'anie kidedea Seif kaenda ulaya kushitaki!Seif anataka maslahi yake?yapi zaidi ya hayo aliyopewa?(Kulipwa stahili zake?)
Kuweni wapembuzi wa mambo msikubali kulishwa pumba!
 
Kutokana na maneni yaliyowahi kusemwa na mmoja wa wakilishi ndani ya baraza wakati fulani wa mchakato wa Muafaka wa 1 au wa 2 "Sisi tumeipata nchii kwa mapinduzi watu wamekufa iweje leo hii tuitoe nchi hii kwa karatasi?" huyu ni mtu akiethubutu kusema ukweli.
Wale wote mnaodai kuwa mapinduzi si njia sahihi kuwaondoa kina Karume ila kwa njia ya KURA hampo sahihi kwani wameshasema hawatatoa nchi kwa karatasi pengine wanataka watakao take over wafanye kama wao walivyofanya! Mengi yamefichika kwenye yale mapinduzi watu walikufa wengi sana wengi wao hawakuwa na hatia! ni mapinduzi hayo ambayo ni sababu ya mpasuko uliopo mpaka sasa ila wanasiasa hawataki "ku point out" mapinduzi yalifanywa bila ridhaa ya wananchi leo iweje mfanye kura ya maoni kwa ajili ya serikali ya mseto? Set up ya mwafaka ilikuwa mapinduzi tosha bila ya mtu kutokwa damu although watu wamekufa 2001 jan 26 na 27.
Naomaba nimalizie kwa kusema kuna vitu vina kera sana sometimes najiona kama mie sipo katika ulimwengu huu mtu anakazania watu wasilete chokochoko damu ikamwagika hivi nani anaesababisha haya yote kama si hao CCM? pili mnao nga'nga'ania watu wachukue madaraka kwa kupitia sanduku la kura hamjui hiyo mbinu imeshindikana zanzibar mara tatu?hii inanisukuma kuamini kuwa wale wote wanaosema njia ya CUF kuchukua ni kungojea 2010 utakapofanyika uchaguzi ni watu ambao pengine mbongo zao zimeganda mtu mwenye akili timamu hawezi kusema maneno haya. Ifahamike kuwa mgogoro wa CUF na CCM sababu au chanzo chake ni zaguzi zilizofanyika!
Jamani tunapojadili ni bora mtu awe anajua hata kidogo historia ya kitu anachotaka kuchangia tusikurupuke na kujisemea "mwerevu husikiliza zaidi na kuongea kidogo mpumbavu huongea zaidi na kusikiliza kidogo"
Kama hujui soma wenzenu wanavyochangia usipo post hakuna neno au na nyie namngangania mfike post 2000?
Naomba kutoa hoja
 
sokomoko
Uchaguzi visiwani sio njia ya mbadalaya kuondoa matatizo,ubaguzi,chukibinafsiza kijinga ambazo hata hawa watoto wetu tukiwaelezea sababu kubwa za watu kuishi namna kamaile wanashungaa sana
uchaguzi wowote kwa zanzibar ni ongezeko la chuki nauhasama ambao unapangwa kwa makusudi kabisa na hao wanaoitwa wahafidhina kwa njia ya wao kuendelea kuwapo katika madaraka na kuwarisisha watoto wao, kwa mfano kama utasikia mtotowa mwiyi anataka nayeye kuwa raisi karume mwengine naye pia utasikia pia mtoto wa shamuhuna na weeengi ambao wanaufikiria na kuota nao siku moja wataitwa muheshimwa au mtukufu rais,
Lakini pamoja na yoote hayo serikali ya muunga ndio inayo fanya yooote hayo kwa ajili ya kuilinda ccm bara.
kama tutakubali au kukataa chaguzi zoote za zanzibar ccm inashidnwa sasa ili ccm iweze kuedelea kutala basi nlazima visiwani ishinde ndipo uwongo wao wataulazimasha ukubalike kwa wale ambao hawaoni mbali kaziyao nikuskilza redio tu,
Lakini hakuna usiku ambao hauna mchana na hakuna mchana ambao hauna usiku.
 
1.Sifagilii mapinduzi ya mtutu

2. Kupindua Zanzibar katika set up ya sasa ni upunguani, utapindua Zanzibar na kuacha bara unafikiri itakuwa nini kama si mbio za sakafuni?

3.Naamini katika uhuru wa kujieleza kwa hiyo kila kitu kinaruhusiwa kama tupo ndani ya sheria.Tatizo swala la mapinduzi huwa linachukuliwa vingine kabisa hata kuweza kuwapa the powers that be uwezo wa ku suspend "civil liberties" chache tulizo nazo kwa kutumia clauses za sedition na national security.

Tusiwape msemo, wanaotaka kupindua seriously hawaongelei hilo kwenye internet boards, wanaoongelea hilo katika internet boards hawawezi kuwa serious kuhusu kupindua.

Kasheshe za uhaini waulize The Ngaizas,Banyikwas,McGhee and that Lakha lawyer kama wao au familia zao wapo watakuelezea.

Heshima mbele mkuu, kama nimekupata vema naomba nikuunge mkono kuwa mapinduzi yanahitajia sana Zanzibar hivi sasa lakini si mapinduzi ya mtutu kama wengine wanavyodhani.
Tunatakiwa kufanya mapinduzi kwanza kwenye fikra za wanajamii, ambao ndio wapiga kura. waeleweshwe kuwa kunachotokea hakiwaathiri CUF au CCM peke yao, athari zake ndizo zinazowasababisha waishi maisha mabaya.
Hawa wakishaelewa ndio watafanya mapinduzi kupitia sanduku la kura. Inabidi wakati wanalishwa propaganda za kisiasa, wengine wawe busy kuwaelewesha kuwa propaganda hizo ni kwa manufaa ya watu wachache na wao wala hawamo kwenye list ya watu hao.
Kwamba ustawi wao haukustahili kuwa kama ulivyo leo, wanachotakiwa ni kuchagua kizuri ili kiwaondoe hapo walipo na kuwafikisha kwenye eneo ambako watakuwa wakifaidi uchumi wa nchi yao wao wenyewe.
Kama kuna mtu anang'angania mapinduzi ya mtutu, huyo atakuwa hafikirii mbali
 
Back
Top Bottom