Jamani Hata Mie Nisingependa Kukutana Na Mwanakijiji,inv Mac Ambao Hawanitambui Kama Ni Mwana Jf ......mwacheni Aseme Yaliyopo Moyoni
Chukulia Uko Nafasi Ya Karume Unakwenda Kwake Kama Nani?????????
 
Ila twende mbele kurudi na nyuma, Seif naye longolongo sana. Kama yeye kweli amekomaa kisiasa awamu ijayo awaachie wengine maana naona kama anatuzuga uchaguzi ukishapita ndio anajidai kujitutumua. Seif ni CCM mtupu.
 
ili niamini kweli CUF ni chama kisicho cha kibaguzi kimsimamishe JUma Duni. lkn siku zote mgombea awe huyo huyo utadhani imeandikwa bila yeye zanzibar haitoendela
lol
 
Hapa Tuangalie Ukweli Halisi Hawa Watu Ni Ccm Kama Sio Basi Ni Walafi Wenye Macho Na Akili Nafuikiri Mnaona Embu Angalia
Cuf------seif Shariff Hamad
Naibu Yuleyule

Tlp
Anaegombea Uraisi Mrema
Naibu Yuleyule

Chadema
Uraisi Mbowe
Naibu Yuleyule

Nccr
Came Shit

Hawa Watu Tusiwalee Kama Kweli Tuko Makini
Aiwezekani Kila Mwaka Wanatgombea Wao...hivi Vyama Vya Kuangalia Sana
Samahanini Wanamageuzi Wenzangu Nimesema Kwa Amani Sikuwa Nimelewa Ila Ni Mawazo Tu
 

inaonekana umelewa au mawazo yako ni mgando..

Mbowe amegombea uraisi kwa mara ya kwanza mwaka 2005...

Rudi kwenye baa uwaambie wakurudishie pesa yako maana inaonekana wamekuuzia pombe ya kienyeji.
 
Hivi kumbe Karume hana raha kwa kuwa Seif hamtambui kama Rais ? Mimi nilidhani CUF ndiyo hawamtambui kumbe yeye anaona ni Seif pekee ? Je Duni anamtambua ? Wawakilishi wa CUF wanamtabua ?

Hebu nielewesheni kidogo nini wasi wasi wa Karume .Je anaye omba kuonana na mwenzake ni nani ? Seif ama Karume ?Kama Karume anataka kuonana na Seif sasa analia nini na kutambuliwa naye si amwite tu bila kujali kutambuliwa ?
 
Hawa Watu Tusiwalee Kama Kweli Tuko Makini
Aiwezekani Kila Mwaka Wanatgombea Wao...hivi Vyama Vya Kuangalia Sana

inaonyesha wewe ni Bongo Flava (kizazi kipya)! hata hufahamu vyama vingi vilianza lini na wala hufahamu historia ya hivyo vyama, eti leo hii umewachoka ... utasemaje kwa hawa wafuatao:
- John Samwel Malecela
- Pesambili Mramba
- Kingunge Ngombale Mwiru!
 
Karume ni jambazi wa kura... na ameingia madarakani kwa njia ya wizi wa kura. Sasa Maalim Seif atamwangukiaje jambazi aliyempora? Karume ndie aliyetakiwa aombe msamaha kwa wizi alioufanya
 
inaonekana umelewa au mawazo yako ni mgando..

Mbowe amegombea uraisi kwa mara ya kwanza mwaka 2005...

Rudi kwenye baa uwaambie wakurudishie pesa yako maana inaonekana wamekuuzia pombe ya kienyeji.

...duh!!! astaghafirullah, ha ha ha aaaaaa!!!!
 
sasa Karume akutane na mtu ambaye hamtambua kuwa ni Rais? atakutana naye kama nani?

Mzee MwanaKijiji,


I said and I repeat; Maalimu ni Tatizo kwenye amani ya visiwa vya Zanzibar (Unguja na Pemba)
---> Wakati tunajadili muafaka muliona alivyokuwa anatoa macho kwenye suala la yeye kuwa waziri Kiongozi immediate baada ya muafaka kusainiwa.
---> Sasa hili la kutotambua Rais wa Zanzibar hilo hapo.
---> Na yapo mengi tulishasema.

Mchana Mwema.
 
CUF waja juu

2008-05-20 16:32:06
Na Sharon Sauwa, Mikocheni

Baada ya Rais wa Zanzibar Bwana Amani Karume kutoa masharti ya kukutana na hasimu wake, Maalim Seif Sharif Hamad, chama cha CUF kimekuja juu kikidai kwamba kauli za kiongozi huyo ni kejeli tupu na kwamba piga ua galagaza, hakitamtambua kama rais halali wa visiwa hivyo.

Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Habari wa chama hicho,
Bw. Salum Bimani, ameliambia Alasiri leo asubuhi kuwa, kauli ya Rais Karume kutaka CUF wamtambue kwanza ndiyo akae nao kuzungumzia mgogoro wa kisiasa unaokikabili kisiwa hicho, inaonyesha hana nia ya kumaliza mgogoro huo.

Mwanasiasa huyo amedai kuwa wanao ushahidi ambao unaonyesha Bw. Karume hakushinda katika uchaguzi wa mwaka 2000 na ule wa 2005 na hivyo hata siku moja hawatamtambua kama ni rais.

``Kauli zake hizo ni za kejeli, si za kujenga na hata siku moja hatutamtambua kuwa ni rais kwa sababu vigezo vya kufanya hivyo tunavyo...mwaka 2000 hakushinda wala 2005 hakushinda pia,`` akasema Bw. Bimani.

``Salmin (Rais Mstaafu wa Zanzibar), naye alileta kibri na sasa yuko huko nje, anasikika wapi sasa hivi?, muache huyo Karume naye amalize kipindi chake, historia ndiyo itakayomhukumu,`` akasema Bw. Bimani.

Amesema itafika wakati Zanzibar itakuja kupata rais ambaye atawaunganisha Wapemba na Waunguja na kuwa kitu kimoja.

Ameongeza kuwa wao hawana tatizo la kukutana na rais Karume lakini si kwa masharti aliyoweka yeye.

Jana rais Karume alisema atakuwa tayari kukutana na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, kuzungumzia mpasuko wa kisiasa Zanzibar kwa sharti la kumtambua kuwa yeye ni rais halali wa visiwa hivyo.

Alisema kimsingi yeye amekuwa mstari wa mbele kukaribisha maelewano ili kuendeleza umoja wa kitaifa na ndio maana CCM ikaingia katika mazungumzo ya kutafuta muafaka wa kuondoa tatizo hilo.

Alisema iwapo chama hicho kitatangaza rasmi hadharani kumtambua kama rais halali wa Zanzibar yeye hana tatizo la kukutana nao kuzungumza.

* SOURCE: Alasiri
 
Duh.. lakini hapa kuna vichekesho vya mwaka. Kenya Odinga alisema hamtambui Kibaki kuwa Rais lakini leo hii wanakaa meza moja na mmoja baada ya kutengenezewa cheo (Uwaziri Mkuu) anamuita Kibaki Mr. President. So haya mambo ya never say never ni ya kweli.

Kutomtambua Karume kunafanya mazungumzo yawe rahisi kwa kiasi gani na kwa kiasi gani yanafanya yawe magumu? Endapo kutomtambua kunafanya mazungumzo yawe rahisi basi CUF waendelee na msimamo wao; hata hivyo endapo kumtambua kutarahisha mazungumzo basi CUF hawana budi kufikiria mkakati wao huo.
 


Kasheshe umejificha weeeeeee hatimaye umeamua kujionyesha true rangi yako .Pole sana .Sasa mmeanza kuhamishia matatizo kwa CUF ? Kwani kutolea macho kwenye uongozi kuna kosa gani ? Si kama akina JK na Karime kutolea macho madaraka hata kama wapemba wanakufa wote ?Ama hili hulioni kwamba hata Karatu damu ilimwagika kisa CCM kushinda ?
 
Lets face it, leo hii Seif akipewa ulaji atamtambua na sifa atampa......
Kwa hili nampongeza Karume, unataka tukutane nitambue tutajadili muafaka...its a two way street!!!
 
[
QUOTE=Mtu wa Pwani;200940]ili niamini kweli CUF ni chama kisicho cha kibaguzi kimsimamishe JUma Duni. lkn siku zote mgombea awe huyo huyo utadhani imeandikwa bila yeye zanzibar haitoendela
lol
[/QUOTE]



Hayo si maswala ya kichama? jamani mbona mnataka kuwapangia CUF? mi najua CCM ndiyo mmezoea kupangia baa utitili wa viongozi wenu utakavyokuwa. Kwa vyama vinavyojali demokrasia waache wachague wanayempenda mpaka kifo wakipenda. Hiyo ruksa.
 
sasa Karume akutane na mtu ambaye hamtambua kuwa ni Rais? atakutana naye kama nani?

Akimtambua kuwa Rais, yale mazungumzo yote hayana maana kwa sababu msingi wake ulikuwa ni kusawazisha uwanja wa mapambano katika uchaguzi. Sasa na wewe inabidi tukuulize, kama Seif atamtambua Karume kuwa Rais, kwa nini wafanya mazungumzo ya mwafaka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…