Hakuna nchi ya Zanzibar.........
Someni katiba yetu (na ndiyo aliyoinukuu Mhe. Pinda).
"1. Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano."

Sasa wewe na huyo Pinda nyote inaonyesha mna matatizo huoni katika hiyo mistari kuna kiunganishi, halafu mwisho kuna neno Muungano ,Tanzania ni nchi moja lakini Tanganyika na Zanzibar ni nchi mbili kila moja inasheherekea siku ya UHURU wake japo wazenji wao tarehe yao wameipa mgongo kutokana na tabia za uhafidhina ,sasa hapo ipi iliyokuwa haipo naona hao ndio wanaotakiwa wawe na msimamo mkali kule Zanzibar wakati wowote zikiwasanifu wanaweza kutangaza mgogoro wa Muungano na hapo ulipofikia patawekwa frozen mpaka wananchi waulizwe kwani makelele yamekuwa mengi ,Je WaTanganyika si mtaanza kulana nyama.

Hebu nieleze kama sasa hivi itatokea Tanganyika kurudishiwa hadhi yake kama Nchi (Sasa hivi haipo ila Zanzibar ipo na kila kitu chake) WaTanganyika mtafanya nini ? Hakuna litakalofanyika kutakuwepo na mtafaruku mkubwa wa nguo kuchanika kwani haiwezekani kwa mafisadi Kuunda Serikali kwa kutumia Chama chao CCM ni lazima ufanywe Uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi Tanganyika chama kitakachoshinda ndicho kitakachounda serikali ama sivyo , ndani ya CCM pande la Zanzibar CCM litakuwa halipo katika kutumika kuwaekea waTanganyika kiongozi asiepata kura nyingi (Inajulika wazi kura za CCM Zanzibar zinaelemea upande mmoja tu na hapo ndipo upande mwengine unapogalagazwa chini ) .Hivyo machafuko yataanza ndani ya CCM na kugawika mapande mapande hivyo ,na kuenea kwa mgawanyiko huo kwa mikoa mingine ambapo wananchi watakuwa huru zaidi bila ya kubanwa na mbinu za serikali ya Muungano
Hivyo kuibwaga CCM ni lazima idaiwe Tanganyika otherwise watakuwa wakijiuzulu na kuwekwa wengine.Na ndio hata kule Butiama Wahafidhina walikuwa na ubabe kuwambia wabara kama mnataka kutekeleza mwafaka basi chukueni Tanganyika yenu ,wanajua fika wakichukua Tanganyika ndio mwisho wa CCM bara.
Na ndio mpaka leo iwavyo na iwe lakini CCM ni lazima ishinde Zanzibar tumeona majeshi jinsi yanavyopelekwa Zanzibar ,tumeona jinsi polisi walivyomwagwa Pemba na mamluki kibao yote ni kuilinda CCM na utawala wa Tanganyika na sio Tanzania kama inavyofikiriwa na wengi.
Hivyo natoa mwito kwa vyama vya upinzani kuidai Tanganyika kwa nguvu zao zote ,kama alivyosimamia Rev.Mtikila basi vyama vya upinzani vilikuwa vimuunge mkono na kueneza propaganda ya hali ya juu ili Tanganyika irudishiwe mamlaka yake ya ndani kama ilivyo Zanzibar ,kwani kumbukumbu zinaonyesha Mh.Kikwete alikuwa mstari wa mbele katika kuidai Tanganyika na 100% alikwisha fanikiwa kilichomkwamisha ni yeye kuwemo ndani ya CCM ,just baada ya kufanikiwa walikuwa waruke na kutua kwenye Chama kingine ,lakini walibakia baada ya kuambiwa tukimeguka basi CCM tumekwisha.
Shime vyama vya upinzani kuing'oa CCM kupitia mlango wa Tanganyika Huru.
 
""Hakuna Mpasuko wa kisiasa bali kuna mpasuko wa Wanasiasa Zanzibar""

Hadidu za zerejea katika misemo ya baba wa taifa imeeleza mambo mengi kuhusu huu mpasuko wa kisiasa Zanzibar.kuna maneno kama,.bila CCM imara nchi itayumba au upinzani wa kweli utatoka baina ya wana CCM wenyewe.kwa upeo wangu mdogo katika siasa za Tanzania nimeona nukuu hizi za mwalimu kama zilikuwa zinalenga huu mpasuko wa kisiasa wa Zanzibar,kwani kinachotokea sasa hivi ni kutokuwapo na uimara katika chama cha mapinduzi na kuwepo na makundi yanayokinzana lakini bado yanatukuza ule usemi wa zidumu fikra za mwenyekiti wa CCM,Toka serikali ya kwanza ya CCM “bila kuingilia sana enzi za TANU”bado wanachama wa CCM hawajapewa uhuru wa kuweza kukikosoa chombo kimojawapo cha chama ama labda kukishauri,ninaposema chombo muhimu namaanisha vyombo muhimu kama kamati za siasa za kuanzia ngazi ya shina hadi mkutano mkuu.vitu vinavyojadiliwa kwenye mkutano wa siasa wa shina maamuzi yake yote yanategemea mwenyewekiti wa chama cha mapinduzi wa taifa kitu ambacho kinaonyesha ni jinsi gani CCM haiwezi kuwa chama chenye maamuzi yasiyokuwa na chembe chembe ya upendeleo kutoka kwa mwenyekiti,ndio usemi wa ndio mzee unaposharadishwa hapa.kama vyombo hivi vya CCM vingepewa uwezo wa kutoa maamuzi makubwa kuanzia ngazi zake za chini kusingekuwapo na kushindaka kupata suluhisho la mpasuko wa kisiasa Zanzibar.tuache kuongelea nini chanzo cha mgogoro kwa sasa kwani hautatusaidia na wala tusiendelee kukumbushana ni makubaliano gani yamefikiwa toka muafaka wa kwanza hadi leo hii mazungumzo yanapoendelea ambapo pande mbili zinaendelea kukinzana,CUF wanasema mazungumzo yamekwisha wenzetu CCM wanasema bado.hiyo yote kwasasa inatupotezea muda sisi wapenda amani na wafuatiliaji wa masuala yanayohusu amani na umoja wa nchi.viongozi wa CCM kuanzia ngazi zote waachane na uongozi wa mababe na vitisho vya kunyan’ganyana uanachama na uongozi.viongozi wa CCM waache kuitisha vikao vinavyojadili umoja na amani ya nchi yetu yenye sifa katika kila mipaka ya dunia na kuishia kutumia mabavu katika kutoa maamuzi ambayo hapo baadae tutakuja kuwalaumu wao.ifike kipindi tuwe na CCM imara ambayo mwalimu aliongelea,tuwe na CCM yenye kutoa maamuzi thabiti ya bila kuogopana au kushikana uchawi ndio CCM ambayo mwalimu aliita upinzani wa kweli.kwa mtazamo wangu hakuna haja ya kufufua vyama vingi ambavyo hatuoni mwisho wake zaidi ya kugombania ruzuku.ila tuwe na CCM imara yenye viongozi thabiti na walio tayari kukosolewa.nchi yangu Tanzania haitayumba na hakuta kuwa na mpasuko Zanzibar.kwani chanzo cha mpasuko wa kisiasa Zanzibar ni matokeo ya misingi mibovu ya uongozi ambayo CCM iliyojiwekea toka mwanzoni,kungekuwa na msingi mzuri kusingekuwa na uoga wa kuwa na tume huru ya uchaguzi Zanzibar,kusingekuwa na uoga wa kuwa na daftari la kudumu lisilokuwa na mizengwe Zanzibar,bali kungekuwa na uchaguzi huru na wa haki wenye tafsiri ya ushindi wa kimbunga kwa CCM,sitataka kujitumbukiza katika mjadala wa kitaifa ya uundwaji wa serikali Zanzibar,kwani kunawaojadili kuwepo na serikali ya mseto kabla ya uchaguzi na kuna wenyewe msimamo wa kuwepo kwa serikali ya mseto baada a uchaguzi,ila ningependa kusema tu uoga wa CCM ya kuwa na serikali ya mseto kabla ya uchaguzi ni kielelezo tosha cha ni jinsi gani chama cha mapinduzi kisivyokuwa na uongozi imara unaoamini juu ya sera zake.kwani sioni sababu ya kuendelea kuvuruga mazungumzo na kuhatarisha amani wakati suala la serikali ya mseto linatekelezeka.nasema sitaki kuangia ndani zaidi kwani bado katika upande wa viongozi wetu wa chama cha mapinduzi wanasema mazungumzo hayajaisha ila natoa maoni kama mwanachama hai wa chama cha mapinduzi kuwa sera za ndio mwenyekiti zimepitwa na wakati katika suala la mpasuko wa kisiasa Zanzibar.mwisho nanukuu msemo wa rais mstaafu alhaji ali Hassan mwinyi aliosema”kuna msemo wa wahabeshi unaosema usimlaumu mungu kwa kumumba chui ila mshukuru hakumuumba mwenyewe mabawa”ni naweza kusema tuuenzi muungano tusije baadae tukaja kuvurugana na kusababisha amani kupotea Tanzania.Mungu ibariki Tanzania,Mungu ubariki muungano wetu.
 
Date::7/8/2008
Mwanasheria Mkuu Zanzibar apingana na Waziri Mkuu Tanzania
Na Salma Said, Zanzibar

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Mwananchi

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema Zanzibar ni nchi na ina mamlaka kamili ya kikatiba kinyume na ilivyoelezwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuwa si nchi bali ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tamko hilo limetolewa wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Iddi Pandu Hassan baada ya kujitokeza mjadala mkali kutoka kwa wajumbe wa Chama cHA Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF) kutaka serikali itoe kauli yake.

Amesema kimsingi Waziri Mkuu ameteleza kwa kushindwa kutafsiri vizuri baina ya neno taifa (nation) nchi (state) na country kutoka katika kiingereza kwenda kiswahili.

''Mheshimiwa Spika napenda kuwatoa wasiwasi wawakilishi na wananchi wa Zanzibar kuwa Zanzibar ni nchi kwa mujibu wa katiba, mwenzetu Waziri Mkuu ameteleza ulimi,'' alisema.

Alisema kwamba baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar serikali ya Tanganyika iliingizwa katika serikali ya muungano, lakini serikali ya Zanzibar ilibakia ikiwa na mamlaka yake kama nchi inayojitegemea bila ya kuwa na utaifa.

Alisema kimsingi utaifa wa Zanzibar ulikufa kama wa Tanganyika pale waasisi wa muungano walipoamua kuunganisha Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

''Waziri Mkuu kateleza kidogo kibinaadamu, lakini anafahamu kuwa Zanzibar ni nchi isipokuwa tafsiri ya maneno ya Kiingereza kwenda Kiswahili hajayatafsiri vizuri baina ya nation na state,'' aliongeza Mwanasheria Mkuu ambaye alikuwa akipigiwa makofi na wawakilishi.

Hata hivyo, alisema kauli ya Waziri Mkuu imeleta mtafaruku mkubwa kwa wajumbe wa Baraza la wawakilishi na wananchi na ndio maana wajumbe saba kutoka CCM na CUF wametaka serikali kutoa kauli yake.

Mwanasheria Mkuu alitoa maelezo hayo kufuatia baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuibua mjadala kuhusu suala hilo, wakidai kuwa Zanzibar ni nchi kwa mujibu wa katiba ya visiwa hivyo, tofauti na maelezo yaliyotolewa hivi karibuni na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Wawakilishi hapo pia walitaka yafanywe marekebisho ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzani ili kuruhusu Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wakichangia maoni jana kwenye bajeti ya Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba na Utawala Bora, wawakilishi hao walisema kwamba, hakuna nchi inayoitwa Tanzania, isipokuwa ipo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyotokana na muungano wa iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika.

Akiunga mkono mjadala huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma, alisema kuna watu wanaichezea Zanzibar kwa kusema kwamba siyo nchi, lakini ukweli ni kwamba Zanzibar ni nchi kama zilivyo nchi nyingine.

Akizungumzia suala la uteuzi wa nafasi mbili kutoka kambi ya upinzani, ambazo zilipaswa kuteuliwa na Rais wa Zanzibar alisema kwamba CUF ndicho kilichochelewesha nafasi hizo kutokana na kutomtambua Rais wa Zanzibar.

Alisema kwamba kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar nafasi hizo, Rais huteuwa kwa kushauriana na kiongozi wa kambi ya upinzani kutoka baraza la wawakilishi, lakini hadi sasa ameshindwa kufika Ikulu kushauriana naye.

''Kama kuvunja katiba viongozi wa CUF ndio wanaovunja katiba kwa vile hadi sasa hawamtambui rais pia kiongozi wa upinzani hajaenda kushauriana naye,'' alisema mwanasheria huyo huku akipigiwa makofi na wajumbe CCM.

Mwanasheria huyo alisema kwamba kifungu cha 66 cha katiba ya Zanzibar kilifanyiwa marekebisho ili kutoa nafasi kwa Rais kutumia nafasi zake kumi za uteuzi kuwanufaisha na wapinzani ili kukuza demokrasia zaidi badala ya kuchagua wajumbe wote kutoka chama kimoja.

Chama cha CUF kilitangaza msimamo wa kutoitambua Serikali ya Mapinduzi Zanzibar baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2005 kwa madai ya uchaguzi haukuwa huru na haki.
 
tusipoteze muda katika hili watanzania bara na visiwani. kila tunapokuwa na utata wa kisheria mahakama pekee ndio yenye nafasi ya kutoa tafsiri jadidi na hili mahakama ya rufaa tanzania imeshalitolea uamuzi katika kesi ya uhaini zanzibar. sasa hawa wanaoleta tena huu mjadala watafute hiyo hukumu wasome na waelewe.
 
Mkisikia Wahafidhina ndio hao ,wameweza kumziba mdomo Kikwete na kumtoa kapa watashindwa na kuwaumbua magoigoi wengine.
Dawa ya Wahafidhina ni kwa Uchaguzi unaokuja tu,polisi majeshi Usalama wakae kando wawache wanangangari wafanye vitu vyao pale wahafidhina watakapojaribu kuweka ngumu.
Hawa jamaa wanahifadhiwa na vyombo vya Dola Vya Tanzania lakini kama vyombo hivi vitaamua kukaa kando kuacha kutumiwa na Wahafidhina na kutazama na kumtazama anaevunja sheria ndie achukuliwe hatua kali basi Wahafidhina jeuri yao ingekwisha kuwekwa kando.
 
Naomba watu warejee maoni tuliyotoa kuhusu umakini wa Pinda alipoteuliwa kuwa waziri mkuu; ninaamini mnaweza sasa ku-vindicate kwa kile tulichokuwa tunakisema kuhusu huyu mteule wa JK.
 
hata Membe Kwenye Sullivan Summit Ali Acknowledge Zanzibar Kama Nchi Iliyoshiriki
 
Nilishasema Zanzibar ni Country/Nchi... but not a sovereign state!
 
Kasheshe,
Mimi mkuu bado nakubaliana na Pinda kwa kiasi kikubwa sana. Unajua hili neno NCHI lina tafsiri ngumu zaidi inategemea na mtu umeelewa vipi. Kikubwa sio neno lenyewe isipokuwa kile kinachoombwa ama kujielezea wakati neno lenyewe kutumika...NCHI inaweza kuwa Country/ State/Nation, na kadhalika..inategemea na wewe unaelezea kitu gani. Binafsi navyofahamu hata hiyo Country/State zina territorial sovereign...kwa hiyo bado zina mamlaka makubwa ya geograghic territorial ktk eneo lake.
Serikali ya Zanzibar ina mamlaka (sovereignity) ktk visiwa vyake viwili na wanaweza kabisa kujikata toka ktk Muungano..Bara vilevile tunao Uhuru wetu (sovereign) tatizo ama kinachowachanganya watu ni Muundo wa serikali kuu..
Kama nilivyosema siku zote haya ndio matatizo ya ELIMU ya kuiga, Kila kinachozungumzwa na mwanasheria mkuu ni ktk kutazama sheria zilizoandikwa na Muingereza.. Tunashindwa kujielezea sisi wenyewe kama nchi kwa lugha yetu kwa sababu tunajariobu kutafsiri toka kiingereza hata kama swala lenyewe halifanani na mazingira ya muundo wa Muingereza.
Kwa mfano, neno ndoa linaweza tafsirika tofauti lakini matumizi ya jina hayana maana yanatengua ndoa. Wapo wanawake wanaotumia majina ya mabwana zao (surname) wakapoteza kabisa ubin wao (Tanganyika) na wengine huendelea kutumia majina ya U bin wao lakini bado hii haipotoshi maana ya muungano wa hawa watu wawili kuwa tofauti na wale waliooana wakitumia majina tofauti. Sasa huwezi kusema mwanamke anapoolewa hupoteza Uke wake ukitumia mifano ya majina, laa bado ana Uhuru wake kama mwanamke isipokuwa kafungwa ktk maswala yanayohusiana na ndoa..
Na pia huwezi kutumia vigezo vya kutolala kitanda kimoja kudai Ukapela wa mwanaume mhusika kudai haupo ktk ndoa hivyo unadai uhuru wa kufanya mambo ambayo yanakutoa ktk ndoa.(hili ndio swali aliloulizwa Pinda)...
Sidhani kama Pinda alikuwa na maana kuwa Zanzibar sio nchi (country) na kwamba haina madaraka ya territorial sovereign akimaanisha kama state moja ndani ya Muungano.. Zanzibar kama States za Nigeria, USA na nchi nyinginezo ni tofauti kimatamshi ya NCHI na nchi kama Uingereza ambaye Scotland, Wales, Ireland na UK zimejitenga sana kiasi kwamba jina la nchi (nation) halitumiki kabisa..Mara ngapi tumetumia neno Great Britain katika mazungumzo ama kuelezea kitu kinachohusiana na GB tusijikute tukisema UK ama Uingereza. Kwa mfano, leo hii ktk kiswahili kweli tunaweza kutofautisha kati ya Great Britain na Uingereza kama nchi ktk mazungumzo?..Mimi sijawahi kuita nchi hiyo nje ya Uingereza iwe kitaifa ama nchi..

Mimi nadhani ipo haja kubwa sana ya kutazama upya Muungano wetu kama ni ule unaofanana na Marekani au Uingereza kwa sababu kuna mambo kibao yamezidi ama yamepungua ktk mifumo yote miiwili ya serikali za Muungano..Yawezekana pia mfumo wetu ni unique sio lazima ufanane na ule wa wazungu..Pamoja na yote hayo nilichoelewa mimi swali aliloulizwa Pinda linahusiana na Federal government (nation). Muuliza swali alitumia vigezo vya bunge la state ya Zanzibar, madaraka ya ki- territorial kuulizia swala la mamlaka ya Federal...
Ndipo Pinda kwa kiswahili kigumu alisema Zanzibar sio nchi akiwa na maana a Nation! ila ni state (nchi) ndani ya Muungano. Na huyu Mwanasheria mkuu kaelewa kwamba Pinda anapinga kuwa Zanzibar sio nchi kwa maana ya Country/state...
Unless tuseme kuwa Pinda kapotoka kufikiria NCHI ni sawa na TAIFA..
Ukisoma kwa makini utaona kwamba maelezo yake yote yalikuwa yakielemea upande wa TAIFA kama ndio nchi..Ndivyo nilivyoelewa mimi!
 
Hata MEREMETA alisema hivyo hivyo sasa he has to be very coutious kwenye kauli zake.
 
Zanzibar ilikuwa koloni la muingereza. Ikawa nchi huru. Ikachotwa tena ikawa koloni la Tanganyika kwa jina la Tanzania. Msishangae huu ndio ukweli! Kama ni nchi ishindweje kujiunga na OIC au inakuwaje mambo yake yaamuliwe Dodoma na Butiama. Inanikumbusha huko nyuma wakati wa ukoloni wa muingereza mambo yake yalizungumzwa na kuamuliwa Lancaster house London. Leo!!!!! Dodoma. Nini tofauti?
 
Zanzibar ni mkoa unaojiendesha wenyewe ila inatawaliwa na Tanganyika na wao wanataka kuitawala Pemba ,mkubwa anamla mdogo ,Waunguja ndio mambo hayo msizinge shari ,kubalini tu kama ni mkoa ,mkijidai sana jamaa watazima tena umeme muanze kunya kwenye mifuko ya Rambo yaani mumeweka rekodi katika genune book.Haijapata kutokea dunia karibu ya wakazi wa mji mzima wanatumia mifuko kama choo kwa muda wa mwezi mzima.
 
Jaji Augustino Ramadhani alitoa opinion kuhusu kama Zanzibar ni nchi au siyo katika kesi iliyoletwa kama ya uhaini. Kama tunaweza kupata nakala ya Kiswahili ya hukumu hiyo tunaweza kupata ufafanuzi wa kimahakama,.
 

Lakini mwiba
Taarab siilikuwa henu henu?
kidogo nikuulize mwiba ni watu gani wenye uwezo wa generetor? ninatumai wkereketwa kwani wao ndio hawakutumia hivyo vyombo
 
Naomba watu warejee maoni tuliyotoa kuhusu umakini wa Pinda alipoteuliwa kuwa waziri mkuu; ninaamini mnaweza sasa ku-vindicate kwa kile tulichokuwa tunakisema kuhusu huyu mteule wa JK.

Wote tu ndugu yangu, huyo Kikwete na Pinda aliyekuwa mbele hajulikani. Nchi yetu kwa sasa ina pengo kubwa sana la viongozi na sijui kama tutaweza kulirekebisha hili katika uchaguzi ujao 2010.
 
mkijidai sana jamaa watazima tena umeme muanze kunya kwenye mifuko ya Rambo yaani mumeweka rekodi katika genune book.Haijapata kutokea dunia karibu ya wakazi wa mji mzima wanatumia mifuko kama choo kwa muda wa mwezi mzima.

Nimetahayari na kufedheheshwa sana na haya Matamshi yako.
 
Naomba watu warejee maoni tuliyotoa kuhusu umakini wa Pinda alipoteuliwa kuwa waziri mkuu; ninaamini mnaweza sasa ku-vindicate kwa kile tulichokuwa tunakisema kuhusu huyu mteule wa JK.


Nilikuwa mmoja kati ya watu waliounga mkono sana uteuzi wa Bw Mizengo Kayanda Peter Pinda. Lakini sasa nimekuwa mmoja kati ya watu wanaoquestion uwezo wake na uzalendo wake kwa taifa. Toka alipotoa taarifa kuhusu mafisadi, EPA+Richmond, nikaona tuliyemdhania ndiye kumbe siye.
Lakini ni kheri PM asiye mbinafsi na mwizi, kuliko aliye fisadi.
 
What difference does the choice of words of Rt.Hon Pinda make to the status-quo?

Kuna vitu vya maana zaidi vya maendeleo vya kujadiliwa na kufanyiwa kazi na sio haya maneno ya Pinda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…