Wapewe tu nchi yao kama yetu mafisadi wamemaliza basi afadhali wachukue yao mapema kabla haijaingiliwa kisha wakaanza kutuambia siri za usalama wa taifa.

Na Maalim seif amemchallenge Karume afanye hivyo. Anasema yeye (,aalim seif)aliwahi kumsikia Karume original akisema kuwa muungano ni kama koti, likikubana unalivua. sasa anasema kwa kuwa muungano umeshaonekana kuwabana wazanzibari, kwa kuwa karume original alishindwa kulivua koti, basi karume mtoto afanye hivyo
 

Mpita Njia,

Sina uhakika zaidi ila nafikiri sababu nyingi tunazozitumia kuulinda muungano zinaweza kuwa ni za kipindi kile 1964. kama muungano ungekuwa up to date na issue pamoja na maslahi ya both sides sidhani kungekuwa na matatizo yote haya. Ni sawa na kumkataza mtoto kwenda kuchenza nje bila kumpa option yoyote au alternative.
 

...Zanzibar ni nchi iliyomo ndani ya Jamhuri ya Muungano (wa nchi mbili, Zanzibar na ' " ? " ', kumradhi... iliyokuwa Tanganyika!).

Zanzibar miaka ya tisini, hata kwa mbara bila hati ya uhamiaji hapakuingilika.

 
kama nilivyosema katika topiki fulani kiboko wa Chama Cha Mafisadi T & Co(Wahafidhina) ni CUF na nilisema Pinda na Pandu watanyofoana lakini hawatakuwa na jawabu la kuwaelewesha wanachi na kila mmoja hana ubavu wa kusema watabaki kuvutana ,Pinda anaogopa kusema Zanzibar ni nchi na Pandu anaogopa kusema Zanzibar si Nchi nikawawekea pingamizi hapa kuwa anaeweza kusema Zanzibar ni Nchi ni CUF peke yake na si mwengine ila ni yule yule Jogoo wa kupigana Maalim Seif ambae leo hii amewaweka wananchi wa Zanzibar kiti moto pamoja na serikali ya Wahafidhina ambao kwa njia wanazozijua wao waliisikiliza hotuba ya Maalim Seif kuanzia mwanzo hadi mwisho huku habari za ndani zinasema wengine walikuwa wakibubujika na machozi na wengine kutokwa na kijasho chembamba kwa jinsi Mh.Seif alivyozamisha mashambulizi hadi ndani ya mioyo ya WaZanzibari na kuwachoma vibaya sana aidha ameiweka serikali ya Muungano katika hali ngumu vilevile kuibua hisia za Watanganyika waliolala katika mwevuli wa CCM kuwa hawa si viongozi wanaomjali mwananchi wa kawaida ni lazima waamke kuidai Tanganyika yao na wawe proud kuwa ni WaTanganyika kama alivyosema anakuwa proud kuwa Mzanzibar.
Maalim Seif ameweka historia nyengine kwa kuwataka wahafidhina watangaze mgogoro wa Katiba (Hili sio jambo kubwa kwani ni kuweka sawa baadhi ya mambo kama hayo ya Zanzibar ni nchi au ni sehemu ).
Kwa kweli umati uliohudhuria ni wa kuikatisha tamaa CCM na ni kuweka uwazi uliomachoni kuwa CCM haiwezi kushinda kwa kura Zanzibar hata ifanye kitu gani , na vile vile ameitangazia tena CCM & Co kuwa wasiweke tamaa ya kushinda Zanzibar lazima wafanye zaidi ya alivyofanya Mugabe.
Na kwa taarifa yenu baada ya Kikwete kuheshimiwa sana na CUF sasa asubiri kuvuliwa nguo kwa maana ile heshima aliyokuwa akiekewa imeshapita mipaka na CUF wameona ikiwa hathaminiwi ndani ya Chama chake ya nini wao kumuekea heshima ,hivyo hawatomvunjia heshima lakini sasa watakula sahani mbali mbali kama Kikwete amevaa ngozi ya Kondoo basi wataipiga kibiriti na kuwasha manyoya yote ,ile heshima ambayo anaipata kutokana na cheo chake itashuka katika muda mfupi tu ,na hii imetokana na hadaa anayoichukua juu ya kushughulikia matatizo ya Chama chake kule Zanzibar.
Kikwete anaheshimika kama Raisi wa Tanzania na sio kama mwanachama wa CCM hivyo matatizo yale alitoa kauli ya kuyatatua kama Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Nchi mbili hizi ,hivyo ikiwa nchi ya upande wa pili inaona Raisi hafuatilii matatizo yanayowakuta WaZanzibar kila wakati wa Uchaguzi mtu huyo hafai kupewa heshima kama Rais wa Nchi mbili hizo atahesabika kama adui wa WaZanzibari kama alivyokuwa Mkapa na akina Nyerere na hilo WaZanzibari wanaliweza kama watu wa Tanga walivyokuwa wanamchukia Nyerere ,ambae alimaliza utawala wake hajapita Tanga zaidi ya miaka kumi na tano.
CUF wamefufua ,matumaini ya WaZanzibari na kwa kweli watu wamefarijika sana kama Tanganyika wanamwona Waziri Mkuu hafai kwa jinsi anavyojichanganya basi WaZanzibari wanamwona hana maana wala hajui anachokisema zaidi ya kutegemea mistari ya katiba ya Chama chake ambayo inatumika kama katiba ya Nchi.
Katiba ya Tanzania ni katiba iliyotungwa chini ya mfumo wa Chama kimoja hivyo ilitungwa kukidhi mahitaji ya uongozi wa nchi Chini ya Chama kimoja ,mawazo na maazimio yalitokana na uongozi wa Chama kimoja hivyo katiba hiyo ilitokana na Chama kimoja ambacho ni CCM hivyo hakuna shaka hiyo ni Katiba yao na si katiba ya WaTanzania katika mfumo wa vyama vingi.
Vyama vya upinzani vinayo haki ya kutoitambua KATIBA hiyo na tupo mbioni kulitangaza hilo.
 
Tanganyika ni nchi ambayo haipo na Zanziba si nchi lakini ipo
Tanganyika ipo ila Zanzibar ndio haipo labda niongezee kumaanisha WaTanganyika hawapo ila WaZanzibari wapo.
WaTanganyika wanashiondwa kujitetea wanawawacha wachache wanatumbua mali ya Taifa kwa nafasi ,mafisadi hawawezi kudhibitiwa kwa kulitumia Bunge bali wanaweza kudhibitiwa kwa kuwatumia WaTanganyika chini ya Tanganyika na sio Tanzania.
Mafisadi wanaitumia Zanzibar kupitia mawakala wao wahafidhina kujihalalishia ushindi wa kuongoza Tanzania ,wahafidhina wamepachikwa na mafisadi waliopita hivyo watabakia madarakani wao na maswahiba zao wajao ,tumeona wameondoka akina Mkapa wamefika akina Kikwete ,akina Kikwete wanawalinda akina Mkapa au sivyo ? lakini kama WaTanganyika wangekuwepo mafisadi wangekosa kuwapachika wahafidhina ambao wanawasaidia ndani ya mtandao wao kupata mrithi wa huyu ni mwenzetu.
 
Zanzibar ni taifa (nation) na sio nchi/jamuhuri (state).

Ni taifa kwa sababu kuu mbili: Ina mipaka inayotambulika,
Ina watu wanao share historia, lugha na utamaduni moja.

Sio nchi kwa sababu zifuatazo:

Haina jeshi lake peke yake, haina fedha yake peke yake, haina uhuru wa kutunga sheria zihusuzo mambo yote bila kuingiliwa, nk.

Same applies to Tanganyika/Tanzania bara.
 

Kufuatana na maelezo yako, Je, Tanganyika ni taifa na ni wapi inatambulika hivyo. Na huko kuingiliwa kunakujaje na ni nani anaingilia. Natamani Field Marshal Okelo angefufuka aikomboe upya Zanzibar.
 

Tanganyika au Tanzania bara haipo katika huu mjadala. Hiyo ondoa.

Mjadala ni Tanzania na Zanzibar.

Zanzibar sio Nchi wala sio Taifa.

Kuna nchi moja. Na Taifa moja. Na Dola moja.

Tanzania ni nchi moja. Ni Taifa moja. Ni Dola moja.

Maneno 'State,' 'Nation,' 'Country,' 'Sovereignty' na mengine ya kizungu, hayatakiwi kuingia katika mjadala kwa sababu Katiba halali ya Tanzania ni ile ya Kiswahili.

Haya niliyoyasema hapo sio maoni yangu. Ni tafsiri ya Katiba iliyoamuliwa na jopo la Ramadhani (J.A.), Kisanga (J.A), na Lugakingira (J.A) wa Mahakama ya Rufaa.

Katika mfumo wa Sheria za Kiingereza tuliourithi, Common Law, maamuzi ya mahakama katika kutafsiri sheria ndio yanakuwa sheria ya mwisho, ama sheria mpya, Stare Decisis.

Baada ya kusema kuna nchi moja, Taifa moja na Dola moja, ambayo ni Tanzania, Majaji ikabidi waeleze sasa Zanzibar ni nini?

Hitimisho lao, Zanzibar ni Serikali tu.

Tofauti ni nini? Serikali ambayo sio Taifa, sio Nchi, na sio Dola, haiwezi kujiamulia mambo kivyake, kama vile, pamoja na mengine, kusaini treaty. Pia, haiwezi kujiunga na vyombo ambavyo vinataka members ambao ni Nchi au Taifa, au Dola. Haina Amiri Jeshi wa kuipeleka vitani kisheriai. Haiwezi kufanyiwa Haini.

Ndio maana Zanzibar ilijitoa UN na IOC mwaka 1964 na 1993. Ndio maana Zanzibar sio member wa AU. Ndio maana hakuna haini dhidi ya Zanzibar.

Kwa hiyo, tunaweza tukajadili Zanzibar inatakiwa iwe nini, au ingependeza iwe nini, au Pinda na Pandu wanasema Oxford Dictionary inasema Zanzibar ni nini. Lakini hakuna mabishano kuhusu Zanzibar ni nini.

Zanzibar sio Nchi wala sio Taifa. Kwa mujibu wa Mahakama ya Rufaa.
_______________________________________

Reference: S.M.Z. vs. Machano Khamis Ali & Others (Criminal Application No. 8 of 2000) [2000] TZCA 1 (21 November 2000); Session Case No. 7 of 1999

Link: http://www.saflii.org/tz/cases/TZCA/2000/1.html
 
MgonjwaUkimwi,
Hapo awali niliuliza swali kuhusiana na tafsiri ya TAIFA na NCHI sikupata jibu zaidi ya maelezo ya MG kwa lugha ya Kidhungu (kiingereza)..
Ikiwa Zanzibar ni Taifa kwa nini tunaita bendera ya serikali ya Muungano kama Bendera ya Taifa!..pia tuna wimbo wa Taifa, sijaona tukisema bendera ya nchi Tanzania ama wimbo wa nchi Tanzania..
Huoni kama ni matumizi mabaya ya hili neno toka ktk Katiba ambayo inasema Zanzibar sio nchi... hali matumizi ya neno Taifa yametumika ktk kueleza maswala ya jamhuri ya muungano?
 
Nani anazo zile ARTICLES za kwanza kabisa za Muungano atuwekee hapa. Ukitaka kujua Maalim Seif haifai Zanzibar wala Tanzania angalia anayoyasema sasa. Amesahau kabisa kwamba bila Muungano Zanzibar haipo.
 
maana ya kuweko dhana ya usulihishi imekuja katika mambo kama haya, ni pale wawili kila mmoja anapoona kuwa anadhulumiwa. Muungano wa Tanzania kama unawagfaidia wote basi mmoja anafaidika zaidi na mmoja huyo huyo anaumia kidogo kuliko mwengine. Ni kawaida ya binaadamu kupiga kelele pale anapoumia na kusifia pale anapofaidi.
Hii ni hali halisi ya Muungano wetu Zanzibar INAFAIDIKA kwa kiasi kidogo naINAUMIA kiasi kikubwa na Muungano. Si kulaumu kwa kuvutia kwako lakini nakupa changamoto moja KAMA KWELI MUUNGANO HUU UNATUFAIDIA SOTE SAWA SAWA KWA NINI HATUPEWI ILE NAFASI AMBAYO CCM ILIITOWA KWA KULETA MUAFAKA WA ZANZIBAR?
Tupewe fursa wananchi wa pande zote tuujadili na kuamua namna ya Muungano huo. Iwapo tunaenda kimabavu mabavu nina wasiwasi kuwa Muungano huu unawafaidia wote kwani nini haja ya kutishana na uhaini na vyenginevyo eti mwananchi ametowa maoni yake ?
 
Zanzibar imetekwa nyara na waTanganyika nao wametekwa Nyara ,Wazanzibari wamo katika kujipapatua WaTanganyika hawajui waanze wapi maana mafisadi wamewazunguuka na ni wao kwa wao wanalindana.

WaZanzibari wanasema Shujaa wao ameshatoa kitabu kwa Mh.Pinda na waheshimiwa wengine wasioijua Zanzibar kama ni Nchi ambao wanafananisha nyasi na ukoka,sasa wanasema kama Karume ni Raisi wa Zanzibar basi wanasubiri zamu yake nae ahitimishe kazi ya kumshangaa Mh.Pinda.
Wamezidi kusema kwa hili hakuna CUF wala CCM kuna WaZanzibari sasa washitakiwe kama ni mahaini wote Unguja na Pemba.
 
Mheshimiwa Pinda alinukuu katiba , hivyo Zanzibar si nchi japo ina serikali yake. Nionavyo suala la Muungano lijadiliwe kwa wanannchi kutoa maoni yao mfumo upi bora. Kama Zanzibar wanataka kuwa nchi basi mfumo wa Serikali tatu ndo muafaka yaani Tanganyika, Zanzibar na ile ya Muungano lakini pia kuna njia nyingine ya kuwa na Serikali moja tu. Nakumbuka maneno ya Mwl. Nyerere baada ya purukushani za G55 alisema huu ni muundo wa serikali mbili wenye lengo la muda mrefu kueleke serikali moja!!
 
Kuna habari kuwa hasira za Mheshimiwa Kikwete juu ya wahafidhina zinazidi kila siku na kwa jinsi anavyotumia zana zake katika kuwazamisha wahafidhina baada ya kuwakatia umeme kwa muda wa mwezi ,sasa amezua jipya ambalo ndio limewafanya wahafidhina wajifiche kwa kuvaa mabuibui mbele ya macho ya WaZanzibar ,Mheshimiwa Kikwete akiwa wala hana habari wala haoni ,lakini anasikia na anajua linalotokea lakini amezidi kugandamiza na kuwatazama wahafidhina ambao walimdhalilisha anataka awasikie wakidai warudishiwe ASP yao.
Pinda ambae alibeba bango la kujibu suali la papo kwa papo japo si papo kwa papo ,habari kutoka ndani zinasema suali liliandaliwa na jibu lake la mkato nalo pia liliandaliwa ,jawabu ambalo wahafidhina walilivamia na kuulizana wenyewe kwa wenyewe ndani ya ukumbi wao na mpaka kufikia AG wao kujaribu kusema kuwa Zanzibar ni Nchi kabla ya jua kuchwa Mh.Pinda aligandamiza tena kwa kusema ana ushahidi wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na akina Kaka kazi wa Mh. Kikwete wakazidi kuwaumiza wahafidhina kwa kuwaambia kuwa Zanzibar si nchi ila ni sehemu ya Tanzania kama ilivyo Mtwara na Shinyanga,(kumbuka hayo ni malumbano kati ya kundi la Mh.Kikwete ambalo lilitolewa kamasi kule Butiama na Wahafidhina ambao walidai warudishiwe ASP yao)
Pia kuna habari nyengine huenda ikawa zimeshatoka kwenye magazeti ambazo zinasema madai ya wahafidhina kuidai gawio BOT hayana msingi na Zanzibar hawahusiki kugaiwa chochote ,tayari wahafidhina hawajui pa kukamata kwani sasa picha na Mh.Kikwete haziendi sawa ,hivyo tusubiri malumbano.
Kuna mengine ambayo yametayarishwa kuwadhibiti wahafidhina wasiweze kufurukuta.
 
MgonjwaUkimwi,
Hapo awali niliuliza swali kuhusiana na tafsiri ya TAIFA na NCHI sikupata jibu zaidi ya maelezo ya MG kwa lugha ya Kidhungu (kiingereza)..

Mkandara, kwa uelewa wangu nilishatofautisha maneno haya mawili kwenye posting yangu ya awali na nikasema, nchi ni Tanzania. Tanganyika na Zanzibar ni mataifa yanayofanya nchi (Tanzania). Na nikatoa vigezo vya nchi na vigezo vya Taifa.



Makandara uko sahihi 100%, matumizi mabaya ya maneno haya yanaharibu dhana yake halisi, uku wengine wakiyatumia kwa ajenda za kisiasa.

Mstari unaougawa TAIFA na NCHI ni mwembamba mno na hivyo kuchochea mchanganyo wa matumizi ya maneno haya. Ila kuchanganya huku kamwe hakuondoi ukweli kwamba TAIFA na NCHI/DOLA ni vitu viwili tofauti, na kwamba Zanzibar, kadhalika Tanganyika, sio NCHI kwa sababu haina vitu vikuu 3: Jeshi, fedha, na maamuzi yasiyoingiliwa.

Sasa vitu kama bendera, nyimbo, mavazi, lugha, nk ni nothing but political identities za utaifa, sio nchi (kwa maana ya dola). Sijaona bendera ya serikali ya Tz, ila bendera ya taifa. Sijasikia wimbo wa serikali ya Tz, ila nimesikia wimbo wa Taifa. Sijaona vazi la serikali, bali la Taifa. Sijaona fedha ya taifa, bali fedha ya nchi, sijaona jeshi la Taifa, bali jeshi la nchi.

Sasa wengi wetu tunachanganya TAIFA, NCHI, na SERIKALI. Lakini ileweke kwamba kuwapo kwa serikali ndani ya Taifa la Zanzibar hakuifanyi Zanzibar kuwa nchi kwasababu serikali ya Zanzibar haina (i) jeshi lake, (ii) fedha yake, na (iii) haiwezi kufanya maamuzi huru yasiyoingiliwa kama yale ya kujiunga na jumuhia ya nchi za kiislamu, jumuhia ya nchi za Africa mashariki, au kujiamulia kuvamia nchi au kwenda vitani.

Kwa maana hii, Zanzibar sio nchi/dola bali ni taifa. sasa tutakesha kubishana na kuingiza siasa za u-Zanzibar na u-Tanganyika lakini ukweli unabaki pale pale kwamba Zanzibar sio nchi.
 

Huwezi kufananisha na system ya USA kwani wao ni Federal na sisi ni Republic.
Hata hivyo nakubaliana kwenye kuangalia katiba ama tupewe tu Tanganyika na wao wakishaonja joto watajuwa la kufanya.
 
Wiki ijayo nataka nikatembee nchini Zanzibar, sijui ofisi za balozi zao naweza kuzipataje wakuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…