Mheshimiwa Gaijin , lazima nikiri kuwa uyaelezayo ni sahihi. Na nafurahi kuwa unaeleza Pinda Kachemcha na kuwatonesha Wazanzibari. Hii ni hatari. Sasa hivi lao ni moja -Wana Lugha moja ukiachilia mbali tofauti zao za CUF na CCM au Pemba na Unguja.
 
Kwani hiyo gas inamsaidia vipi mwana nchi wa Tanzania Bara??

Kama kodi inaiingia kwenye serekali ya muungano basi ndiyo haswa ilitakiwa kuwa maana ndio serikali ya wote.yani Tz bara Na visiwani .Na kama wanataka iende kwenye serikali ya mapinduzi basi huo ni upendeleo maana serikali ya mapinduzi si serikali ya wote.

Mimi naona wazanzibar wana miss kwa kuifanya serikali ya muungano kua serikali ya bara ,Wao waelewe Kodi ikipata serikali ya muungano wao na wabara kwa pamoja wanafaidika ndio maana wamo akina Shein,Ghasia na wengine.

Gas najua wanaitumia TANESCO kuzarisha umeme hivi Zanzabar wanatumia umeme kutoka wapi? Ama wao mpaka mshiko tu ndio wataona wanafaidika.
 
Inafurahisha kidogo., Kidogo kidogo tu tutafika. Nafarijika unaelewa kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni ya wote na siyo ya WaBara tu. Jee kivitendo iko hivyo?
 
Last edited:
..yachimbwe kwa ruhusa ya nani?

..halafu,zoezi la kuchimba mafuta si la siku moja.

Kama yapo wangekuja wenye mafuta yao ( Americans ) hao wanajipa ruhusa wenyewe tu...

Yes, zoezi la kuchimba mafuta sio la siku moja ndio maana bado exploration inafanyika pale kwa kuwa kuna potential na kama ingethibitika yapo mchakato mzima wa kuchimba ungekuwa ushaanza. Kinachofanyika sasa ni hiyo exploration
 
Inafurahisha kidogo., Kidogo kidogo tu tutafika. Nafarijika unaelewa kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni ya wote na siyo ya WaBara tu. Jee kivitendo iko hivyo?

Tena kivitendo heri na wazanzibar wakipiga kelele wanapozwa kwa kuhofia muungano.Wabara serikali ile haiwajari kabisa .

Nyie msiangalie Dar es salaam ndio mkazani hiyo ni BARA nenda bara kwenyewe uone mambo kitakachokutoa huko ni machozi tu.
 
..hii habari hapa chini inaweza kusaidia kidogo.

..pia itasaidia kama tukielewa kwamba mkondo wa bahari na mpaka kati ya Tanganyika na ZNZ ni mwembamba mno.

..kwa msingi huo kunaweza kutokea utata katika matumizi ya rasilimali zinazopatikana baharini.


 

Mmh. Haya.
Hivi kwanini tulienda vita Comoro? And who sponsored it? Tumeshapata jibu? Nauliza tu, not connected to anything I may know.
 

..mbishi kama jina lako!

..sasa we unasemaje? kuna mafuta au hakuna?

..tusizunguke kichaka.
 
Zanzibar wanasema hivi wakati tunaishi pamoja chini ya Muungano tangu mwaka 1964, tena ulioasisiwa na baba wa rais wa sasa wa Zanzibar. Watu wengi wa Zanzibar wana sili ya bara, na kuna wazanzibar wengi sana wanaishi na ama kufanya kazi au kuendesha biashara bara. Je itakapokuwa Muungano wa nchi za Afrika mashariki ambapo tutashirikiana na watu wa kutoka Turkana tutaambiana nini?
 
Last edited by a moderator:
while the latter asked why the constitution cannot be changed so as to allow Zanzibar to become a member of the Organisation of the Islamic Conference (OIC).

Nilikuambieni mapema raha na haja ya muzanzibar(waislamu) ni kuona zenj inakaliwa koo vizuri na himaya ya mwarabu.

Fuatilia historia vizuri,hakuna mbunge mkrsito alie wahi kuhoji kwanini wakristo(Tanganyika) wanafungwa kujiunga na Umoja wa Kikristo duniani?Ukweli ni kwamba wakristo wamekaa na kutambua umuhimu wa MUUNGANO wetu,wakaamua kufanikisha maswala yao kupitia asasi zao za kidini,na si kuchomeka moja kwa moja ndani ya chombo cha nchi kama bunge!!

Viongozi wetu acheni woga wa kutengwa na misikiti yenu,waaambieni watu wenu ukweli,wanachemka ovyoooooooooo.
 
Kutakuwa na kikao maalum kesho Zanzibar. Kikao hicho kitahudhuriwa na viongozi wa CCM Bara na viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Kikao hicho kina muelekeo wa kuzungumzia masuala ya muungano.

Je, tutarajie chochote kipya?
 
Kutakuwa na kikao maalum kesho Zanzibar. Kikao hicho kitahudhuriwa na viongozi wa CCM Bara na viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Kikao hicho kina muelekeo wa kuzungumzia masuala ya muungano.

Je, tutarajie chochote kipya?
Mjadala wa ZNZ ni nchi au la unaweka muungano katika hatari...hii ni hatua ya kuepusha mmegeko usitokee
 

Hivi Zanzibari kuna watu millioni ngapi vile? Na bara wana watu milioni ngapi? Tukiwaweka hawa katika mizani ya wanaotaka vipimo vya usawa ni kipimo cha upande gani kitakachodidimia chini na upande gani kitakachoruka juu?
 
Nafikiri ni kosa kuweka mafuta na gas kama source of Energy (under Minerals and Energy) and not Natural Resources.

Wakati tunafahamu kwamba oil and gas are part of Natural resources - inakua ni sawa na kula na kipofu pale tunaposema hivi viwili vitolewe!

Kama Serikali ya Muungano ipo kwa masilahi ya Tanganyika na Zanzibar waseme vyote vilovyomo kwenye natural resource ni sehemu ya muungano na kuoneshwe vipi sehemu mbili zinanufaika na hilo.

Lakini hadi sasa hakuna kinachoonekanwa zaidi ya Wabunge kutoka Zanzibar kukaa Bungeni ndo sehemu yao ya manufaa Zanzibar inapata kutoka kwenye Muungano.

Mainland sizani kama ilikua na inalengo zuri; ukitizama huko nyuma wakati wote kabla na baada ya vita vya Idd Amin; Kila ambapo uchumi wa mainland ukididimia ulikua unaivuta znz bila ya hata kuweko na sababu.

Na yote haya alikua Nyerere ndio fundi mkuu; alipomuona Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi anafanya vizuri ZNZ - akaona hawafai wazanzibari - akamuweka tanganyika.

Siyo hilo tu, uporomokaji wa Shilingi ambao umeiathiri znz kwakiasi kikubwa - huko mwanzo znz ilikua ina fanya biashara vizuri sana kupitia nazi na karafuu - znz serikali ilikua inaumia pale ilipokua inatakiwa ifidie malipo kila ambapo shilingi inaporomoka - hatujasikia lolote kutoka serikali ya muungano kuangalia hili - zaidi bank of Tanzania ambao ndio wamekua kama IMF wa zanzibar kwenye Tanganyika kuinyonya na kuiua Zanzibar (ukoloni Mamboleo wa Tanganyika).

Leo hii wameshaona Zanzibar inaweza kujikomboa kupitiza mafuta - wao wanasema na hichi kiwe chini ya muungano! Kwa hilo tu bora usikuwepo huo muungano - sioni faida yake kwa zanzibar.

Muungano upo tu kwakuikandamiza Zanzibar; kama wanahisi uwepo ( hao mainland) kutahitajika kulipa fidia kwa yote tuliopoteza kwa zaidi ya miaka 40!
 
kwi kwi kwi kwiiiii
kuna mzee mwenzangu nimemuuliza hilo swali je zanzibar ni nchi au sio nchi?
akanijibu zanzibar ni kisiwa...
 
Nachelea kutaraji chochote cha maana. Vikao vya Sisiemu siku hizi vimekosa mvuto, havina maamuzi yenye maslahi, kwa ufupi ni butu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…